Vituko Vya Wakaka Na Wadada
Cheki huyu jamaa alivyoumbuka kwenye harusi
Jamaa mmoja alialikwa ktk harusi. Akafika mlango Wa 1 umeandikwa kulia ni ndugu Wa maharusi, kushoto ni wageni waalikwa, akaenda kushoto maana yy alialikwa. Akakuta mlango wa2 umeandikwa kulia wenye zawadi kushoto wasionazawadi yy hakuwa na zawadi. Mlango Wa 3 umeandikwa kulia wanawake kushoto waume akapita kushoto akajikuta ametokea mtaani
ππππππππ. Tujifunze kutoa wandugu
*hatupendagi ujinga sisi*
πΆπΏπΆπΏπΆπΏπΆπΏπΆπΏπΆπΏπΆπΏ
Duh! Kizungu kigumu, cheki alichojibu huyu
“`Nimetoka interview hapa ya job flani
Wameniuliza “so how far did you go with your education?”, nikawaambia.. “””””I didn’t go very far because our school was just behind our house”””
wameniambia ningojee watanipigia!“`β¦β¦.
π *your prayers plz*
Ungekua wewe ni mwalimu ungemshauri nini huyu mwanafunzi?
Mwalimu aliingia darasani na kuwauliza wanafunzi juu ya ndoto zao za baadae.
MWAL: John we unataka ukiwa mkubwa uwe nani?
JOHN: Nataka niwe daktari wa moyo niwasaidie watanzania wanaougua magonjwa ya moyo.
MWAL: vizuri. Na wewe Rose unataka kuwa nani?
ROSE: Nataka kuwa rubani, niweze kusaidia watu wanapenda kusafiri kw anga.
MWAL: Safi sana Rose. Utakua utakua mfano kwa wasichana wenzio kuwa na bidii kwenye masomo ya sayansi.
MWAL: Na wewe James??
JAMES: mimi nataka kuwa tajiri mkubwa sana. Niwe na nyumba Tanzania, S.Africa, Marekani na Dubai. Niwe na gari 7 za kutembelea. Kila siku nabadilisha. Leo nikipanda hii, siirudii hadi week iishe. Nataka niwe namiliki viwanda, Makampuni, ndege binafsi na mashamba makubwa. Nataka niwe na nguvu serikalini ya kuamua nani awe Rais na nani asiweβ¦β¦”
Akameza mate kisha akaendeleaβ¦.
“Nataka kuwa na walinzi 20 wenye silaha nzito wakinizunguka, na watumishi wakininyenyekea. Nataka kuwa bilionea ninayeogopwa. Lakini pia nataka kuwa na mke mzuuuri sana ambaye nitakuwa natembea nae kila mahali.”
MWAL: ndoto nzuri sn lakini unahitaji bidii sana kutimiza. Haya na wewe Jenny tueleze unataka kuwa nani??
JENNY: Nataka kuwa mke wa James.!!
Watoto wa siku hizi ni shida! Angalia huyu mtoto anachomwambia baba yake
Ka ni wewe?
DOGO: baba mi siendi tena shule inaonekana walimu hawana uhakika na majibu yao.
BABA: Kwanini unasema hivyo?
DOGO: juzi walisema 3+4= 7, jana wakasema 1+6=7, halafu leo wanasema 5+2=7 sasa huoni kama wanatuchanganya.
ungekua wewe ungemjibu nini
Angalia mchezo wa kutuma message mara zikubali mara zikatae.. Lilishakukuta hili???
GARLFREND»»hellow sweetheart
BOYFREND»»hellow darling(SENDING FAILED)
GARLFREND»»kwanin hutaki kujibu sms yangu,au huna mda»??
BOYFRENDΒ»>najitahid kukujibu lakin mtandao unasumbua,imefika??(SENDING FAILED)
GARLFREND»»kama hunipend bhas usinijbu,kama unanipenda kwel bhas nijibu
BOYFREND»»i love you (SENDING FAILED)
GALFREND»»do you lov me????
BOYFREND»»i lov you baby(SENDING FAILED)
GARLFREND»»usiongee na mimi tenaaaaa
BOYFREND»»i love you sweetieeee(SENDING FAILED)
GARLFREND»»unataka mim na wew tuachaneee????
BOYFREND»»nshachoka mie na huu upUmbavu,shenz (MESSAGE SENT)
πππππππππππππππππππππππππππ
BREAKING NEWS: WAZIRI ANASWA KOFI
Mkazi wa Mbagala Kibondemaji, Waziri Salum (23) amejikuta akinaswa makofi baada ya kupishana kauli na jirani yake.
Soma alichokisema mlevi baada ya kukuta watu wakimpiga mwizi
Mlevi mmoja aliona wananchi wakipiga mwizi akawaambia “mwacheni msimpige, hii tabia yenu ya kupiga wezi mtakuja shtukia mnampiga Yesu, maana imeandikwa atakuja kama mwizi!”
Misemo ya kina dada
Misemo ya kina dada
walianza na halohalooo!
Wakaja unalo babu weee!
Ikafuata utajijuuu!
Ikafupishwa utajiJJ!
Mara ghafla kantangazeee!
Haikukaa sana kansajiriii!
Ikatoka nyingine nishiiiiida!
Unaijua iliyotoka Leo?
Heh! Heh! Heeeh! MB zenyewe 8 nikudownload unanini?
Hyuyu daktari ni noma, cheki anachokisema
Kuna Daktari wa Moyo alifariki wakamchongeaa jeneza lenye umbo la Moyo. Ghafla Daktari mwingine akaanza kucheka, watu wakamuuliza “kwanini unacheka unafurahia mwenzako kufariki?” Daktari yule akajibu “hapana mimi ni Daktari wa kutahiri nafikilia nikifa mtanichongea jeneza lenye umbo la β¦.”
Mapenzi Stress tupu
Stress Tupu
Unapokea Sms kwa mpenzi wako anakuambia
“Kuanzia Leo Mimi Na wewe Basi! ????”
Unashtuka ??β¦. Una muuliza kulikoni? ????
Anakujibu: “Sorry Sio Sms yako?”
Hapo Ndo utajua Kwanini Hakuna Mmasai Albino??????
Kilichompata huyu jamaa akiwa anaangalia mpira mechi kali na mke wake
WIFE: Baibie, yule ni nani? Ni Chris Brown??
HUSBAND: Yule ni Theo Walcott
WIFE: ile Yellow Card ni ya nini?
HUSBAND: ile ni ya Onyo, na Red Card inamaanisha mchezaji awache kucheza na atoke inje ya uwanja.
WIFE: Oooooh! Inakaa kama traffic light! Yellow- Ilani na Red – Simama
HUSBAND: Yeah yeah swity! Ndio hivyo.
WIFE: Na je Green Card??
HUSBAND: Aaaah! Hakuna kitu kama hicho.
WIFE: Nataka Arsenal ishinde world cup.
HUSBAND: [kimya]
WIFE: Ni nani yule mzee anakaa kama Mr. Bean??
HUSBAND: Yeees swity, yule ni kocha wa Arsenal, anaitwa Arsene Wenger.
WIFE: Oooooh! inamaanisha yule kocha mwengine ni Chelsea Wenger??
HUSBAND: [Kabadilisha channel]
Huyu mgeni wa huyu jamaa ni shida
Pale unapokuwa umefulia sanaβ¦
Mgeni anakutembelea Maskani kwakoβ¦.Unaamua Kuchukua Ile Sh 600 iliyobaki na kwenda Dukani Kumnunulia Soda Unaondoka na Chupa Mbili Unanunua Fanta Moja kwaajil ya Mgeni na Ile Chupa ya Sprite Unaijaza Maji ili Ukirudi Uweze kumpa Kampani Mgeniβ¦β¦Unafika Seblen Unampa Ile soda ya Fanta Mgeni anakuambia Fanta huwa situmii Nipe hiyo sprite β¦..Bwanaβ¦.Bwana. β¦Bwanaβ¦.Weee ππππππππ
Tabia za Kimama kwa wanaume
1, mwanaume kuoga haraka haraka ili uwahi kuangalia igizo, huo ni UMAMA..π
2, mwanaume kupiga picha umeng’ata Lips na Unapiga na Camera Beauty Plus huo ni UMAMA..π
3, Mwanaume kuangalia tamthilia na Jamai Raja na Maigizo kwenye chanel ya sinema zetu wakati mechi za kombe la dunia zinaendelea, pia nawe ni MMAMAAβ¦ππ
4, Mwanaume kuandika ‘Jomon’ badala ya Jamani, kuandika ‘Pw’ badala ya Poa, kuandika ‘Thatha’ badala ya Sasa, kumwandikia mwanaume mwenzio ‘Mambo my’ Huu ni UDADA, tena UDADA wa CHUO..π
.
5, Mwanaume kunywa soda au Juice na kubakisha, kununua chakula halafu unakibakisha, kubagua bagua chakula na kujamba hovyo hovyo baada ya kushiba, huo nao ni UMAMAA..π
.
6, Mwanaume kumuuliza mwanaume mwenzio anapata faida gani kuangalia Mpira, pia nawe ni MMAMAβ¦
.
ππππππππππ
Tatizo la kukuta nywele kwenye chakula
Hapa ni shida
KUKUTA NYWELE KWENYE CHAKULA SIO TATIZO,TATIZO NI KUWAZA ITAKUWA IMETOKA SEHEMU GANI
π€£π€£π€£π€£π€£π€£π€£π€£
Angalia wanachokifanya Zuzu na msichana chumbani kwenye giza
Zuzu: Mambo Anna!
Anna: Poa!
Zuzu: Kuna kitu nataka nikuonyesheβ¦
Anna: Kitu gan?
Zuzu: Twende chumbani kwako (wakaenda)
Anna: Haya nionyesheβ¦
Zuzu: Funga mlango na madirisha kwanza (akafunga)
Anna: Haya nionyeshe sasa!..
Zuzu: Zima taa kwanza (akazima)
Anna: Mhmβ¦nionyeshe sasa!
Zuzu: Haya njoo hapa kitandaniβ¦
Anna: Ok, nionyeshe!
Zuzu: Ona nimenunua saa ambayo inawaka yenyewe gizani⦠Acha mawazo mabaya ww???
Kama mpezi wako akikuita MAMITO Unatakiwa umjibu hivi
Akina dada mpenzi wako akikuita MAMITO usikubali
na yeye mwite MAFORONYA kama mbwai na iwe mbwaiπ€ͺπ€ͺπ€ͺπ€ͺπ€ͺπ€ͺ
Hizi swaga za huyu jamaa ni shida, Google!
Jamaa alikuwa kwenye daladala pembeni kuna
dada mrembo kakaa. Kamlia timing kwa muda
kisha halafu akamuuliza “Samahani dada
unaitwa Google?”.
Dada: “hapana, kwanini umedhani naitwa
hivyo?”. Jamaa: “Una kila kitu nnachokitafuta
“π
πππππππππ
Mbele ya hela binti usharobaro achia mbali
Boy:- hallow
Dem:- hellow
Boy:- ivi jina lako nani vile
Dem:- am miss precious A. K. A dope girl
Boy:-Okay, nmekutumia 50,000 nimeona Jina tofauti ngoja nipige customer care
Dem:-no no baby usipige Ah ah Hapana baby mi naitwaΒ Andongolile MwakasakafyukaΒ πππππ
Kilichotokea baada ya babu mzee kuibiwa nauli kwenye daladala
Mzee mmoja alipanda Gari Stend;
Wakati wa kugombania Siti,
Akaibiwa Nauli.
Akasimama katikati ya Gari-Akasema; “Jamani Naomba Aliyeniibia Pesa yangu Arudishe Haraka,
Tena Fasta kabla Sijafanya Tukio kama Nililofanya 1977″
Abiria kuskia hivyo wakaogopa.
Ikabidi Mwizi Ajitokeze,
Akarudisha Pesa na Kuomba Msamaha! Mtu Mmoja akauliza,
Mzee,
Kwani 1977 Ulifanya nn?
Si nilienda kwa Miguu mpaka Nyumbani!
Uscheke Peke Yako, wa2mie na wengine ili nao wacheke!
Recent Comments