Vituko Vya Kukuchekesha

Cheki masifa yalivyomponza huyu, Sifa nyingine ni mbaya jamani

Mbongo, Mganda, na Mkenya walikamatwa na makosa Uchina.

Wakaambiwa adhabu ni ama kifo cha moja kwa moja au adhabu nyingine ambayo atakayeifaulu atakuwa huru, atakayeshindwa atauawa.

Basi wao wakaomba wapewe hiyo adhabu nyingine wajaribu bahati yao.

Wakapelekwa msituni wakaambiwa kila mmoja aende kwa njia yake halafu arudi na matunda kumi ya kufanana.

Wakaingia msituni kila mtu njia yake.

… Mganda akarudi wa kwanza na machungwa kumi. Akaambiwa adhabu yake ni kumeza moja moja likiwa zima bila kufumba macho bila kulia wala kucheka wala kujitikisa mpaka yote kumi yaishe. Akameza la kwanza. Safi. Kumeza la pili, akashindwa kuvumilia akafumba macho. Akapigiwa risasi akafa.

Mkenya akaja. Ana vitunda vidogo vidogo kama pili vilaini. Akasomewa masharti. Akaanza kumeza bila kufumba macho wala kulia, wala nini… alipofika cha tisa akashindwa kuvumilia akaangua kicheko! Akapigwa risasi pia akafa.

Wakiwa kuzimu Mganda akamwuliza Mkenya, β€œVipi, mbona ulishindwa kuvumilia wakati kilibaki kitunda kimoja tu?”

Mkenya akamjibu: β€œMkuu, nilishindwa kuzuia kicheko maana nilimwona Mbongo anakuja na matikiti maji!”

Mkalimani alivyoharibu ibada ya leo

Leo nikaamua niingie misa ya asubuhi kwenye kanisa moja la kilokole kulikua na ugeni wa mchungaji kutoka Bulgaria, Mahubiri yameanza saa 1 asubuhi hali ikawa kama hivi:

MCHUNGAJI: My name is Pastor Livingstone
MKALIMANi: Kwa jina naitwa mchungaji Jiwe linaloishi
MCHUNGAJI: We thank God for All goals we set by our hands
MKALIMANI: Tunamshukuru Mungu kwa Magoli yote tuliyoweka kwa Mkono

Hivi navyoongea kanisa halina viti waumini wote tumekimbia nje naona Mkalimani amebaki na kiatu cha kushoto tu.
Sunday joke

Kuna watu makauzu ila huyu kazidi.. Soma hii!

Kakubaliana vizuri na msichana fulani hivi kuwa aibuke gheto, mchizi kajipanga vizuri kabisa…. mara saa nne hivi mdada kasema hana nauli.
Mshkaji kajikunja kamtumia Elfu tano maana mwenye shida alikuwa ni yeye……
Baada ya nusu saa yule dada akamtumia meseji.
“Jamani mpenzi, kumbe baba hatoki nilijua atatoka… sorry bae sitaweza kuja kwa leo… sooo sorry!”
Mshkaji jiii! hajajibu kitu…..

Baada ya muda kidogo meseji ikaingia katika simu ya binti, akajua mchizi kajibu. Mh! kutazama ni meseji kutoka Mpesa.

“CA90F0511 IMETHIBITISHWA Tshs 5000 ILIYOTUMWA KIMAKOSA KATIKA ACCOUNT YAKO IMETOLEWA SALIO LAKO NI Tshs 5”

Halafu ndo ikaingia meseji ya mshkaji.
“BASI POA SIKU NYINGINE KAMA VIPI”

#dada wa watu mashavu yakamshuka… hakuamini kilichotokea…. yaani jamaa keshawapigia Voda na pesa fasta imezuiliwa……

Mke alichomfanyia mme wake kabla ya kwenda safari, Chezea mawaifu walokole wewe!

JAMAA alimuaga mke wake mlokole kuwa anaenda semina ya siku tatu, kumbe anakwenda kwa bi mdogo.

Mke akamwambia mumewe; “Tupige magoti tusali”,

Wakapiga magoti…:
MKE: Eee baba msaidie mume wangu afike salama safari yake.
MUME: Emen…

MKE: Mpe nguvu katika yote atakayoyafanya huko.
MUME: Emen…

MKE: Akitaka kufanya uasherati ashindwe.
MUME: Kimya…

MKE: Akifanya uasherati apatwe na janga baya kwa uwezo wako bwana.
MUME: …….!!

MKE: Yaani akifanya uasherati afie hukohuko kwa mateso makali.
MUME: Maombi gani sasa hayo!!?. Haya basi siendi semina ufurahi wewe.

Chezea mawaifu walokole wewe!

Tofauti ya mwanamke wa Kizaramo, Kitanga, Kihaya, na wa Kichaga

Mwanamke wakizaramo: Unampa hela ana nunua dela anaenda ana msutia jirani, analivaa dela bila nguo ya ndani mbele yako, unazidiwa anakupa kitu fresh unatoka unatabasamu.πŸ€πŸ½πŸ™ŒπŸ½

Mwanamke wa kitanga:
Unampa hela anapika vitu mtaa mzima unasikia harufu ya chakula, chenji inayo baki ananunua kinga ukirudi unakula afu unakula..πŸ‘πŸΌπŸ‘πŸΌπŸ€πŸ½πŸ™ŒπŸ½

Mwanamke wa kihaya:
Unampa hela ukirudi unakuta majirani wote wanataarifa kuwa wew uliacha hela, anakupkia vitu vzuri, usiku anakuhudumia ukimsifia anakuhudumia tena hata mara nne kwa usiku mmoja..we mle sifa tuπŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½πŸ€ΈπŸΎβ€β™€πŸ‘ŒπŸ½.

Mwanamke wa kichaga:
Unampa hela anaenda ananunua dagaa anapika na michuzi mingi mpaka dagaa wanafufuka unakula kwa shida, dagaa wanakula utumbo wako unakufa.. Madaktari wanajitahidi wanakutibu unafufuka. Ukiwa hujapata akili vizuri anakuletea bili ya umeme, anakukumbusha deni la kwa Massawe, anakukumbusha kodi ya nyumba.. *Unashikwa na presha unakufa moja kwa moja*πŸ™ŒπŸ½πŸ˜‚πŸ™†πŸΌβ€β™‚πŸƒπŸΎπŸ€ΈπŸΎβ€β™€

Jinsi ya Kubana matumizi X-mass

Badala yakupika PILAU tutapika TAMBI kwenye Xmas maana tutakua tumeokoa sh.15,000/= Vitunguu swaumu 2000, Vitunguu maji 1000, hiliki 1000, Magome 1000, Michele wa 2000, Soda 3000, Nyama 5000 . Fedha hizi zitatumika kununua mfuko wa cement ili tuanze kujaza kibubu cha ujenzi wa nyumba badala ya kupanga. Karibuni saana maji ya kunywa tumechemsha ndoo nzima.

πŸŽ€βœ¨Marry Xmas & Happy new year.βœ¨πŸŽ€

Kilichompata huyu jamaa mroho wa nyama, Hata kaa arudie tena

Jamaa kaenda kumtembelea rafiki yake Levi, kule sehemu za kwetu, akakaribishwa bonge ya ugali na nyama nyingi tu, wakati anakula akagundua kuwa shemeji yake, mke wa rafiki yake hali nyama;

JAMAA: Aise hili ni bonge ya lanchi hii, lakini Levi mbona sisi tu tunakula nyama shemeji Gulo hagusi kabisa anaishia mchicha tu? Tabia gani hii?
LEVI: Hapana sijamkataza, ila shemeji yako Mngoni halagi nyama ya FISI kama sisi

Shopping Cart
26
    26
    Your Cart
    🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About