Vituko Vya Kileo Tuu
Hii sasa ni kali
Siku izi kujuana kumezidi hata ukienda msibani kama hauna connection hauli msosi
πππππ
Angalia kilichonikuta nilipoenda kwa mganga
Usije ukaenda kwa mganga, mwenzako yamenikuta, yani masharti niliyopewa, acha tu,
yalikua hivi:-
1.Jasho la nyoka.
2.Manyoya ya mende.
3.Sisimizi Shoga.
4.Mbwa mjane.
5.Kuku aliye single.
6.Samaki mwenye miaka miwili bila kuoga
7.Mti wenye ujauzito.
8.Mbavu za Nzi.
9.Nywele za Kiroboto.
10.Mwanya wa Mbu.
Duuh..!! mwanangu kwa hali hii mbona itakula kwako.
Wengine wanasemaga
IGA UFE! Rizik anagawa Mungu tu shetan simuelew!
Mke anamwambia mme wake kuwa angetamani mme wake awe tajiri cheki alichojibiwa
Mke; mme wangu ungekuwa tajiri ningefurahi
Mimi; kwa nini?
Mke; ungekuta na sisi tuna gari nzuri hatutembeu kwa mguu
Mimi; ah wap,unadhani ningekuwa tajiri ningekuwa na wewe?ungekuta natoka na kina wema,zariβ¦
πππ
naona anakusanya nguo zake itakuwa anaenda kufua
Mvua zazua kasheshe! Soma hii..
Baba- : Halloo mke wangu.. yaani ni shida sitaweza kurudi nyumban, daraja limevunjika na kutoka morogoro kurudi dar haiwezekani
MAMA:- Mme wangu morogoro ulienda bila kuniaga! ?
BABA:- Ilikuwa ni ghafla sana mke wangu sikuweza kukwambia
MAMA:- kha! Sasa watoto nani atawaangalia
BABA:- Unasemaje! We uko wapi kwan
MAMA:- Niko bagamoyo na daraja limeondolewa na maji sitaweza kurudi.
BABA:- Unasemaje we mwanamke.. nakwambia nikukute nyumban ndani ya dk 15
Baada ya dk 15 Baba kafika nyumban.
MAMA:- Haya umefkaje kutoka morogoro?
BABA:- Nimepewa lift na helkopta ya Mbowe..
Kama umeipenda shea na rfiki zakoooβ¦..
Bongo usanii mwingi!!!
BONGO USANII UMEZIDI DAAH!!
β¦yani nakupeleka dinner unakula sana vipaja vya kuku na chips yai halafu nakupeleka bar unakunywa sana tu, tukitoka hapo nakupeleka club, Masaa yote hayo hakumbuki kuniambia upo periods hadi mdaa wakwenda kulala ndo beiby nipo kwenye siku zangu!! jamani jamaniβ¦ Hapo ndo unaanza kupiga hesabu pesa iliyopotea bureeππππ
Ndooo maana mabinti wa kibongo ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»
Huyu Jamaa kawaweza polisi kweli
Et jamaa kawekwa jela kwa kosa la kupoteza mamiilion.ya kampun akiwa gerezan babayake alituma barua
Ikisema yan.mwanangu tumapata shida maana shamba halijalimwa na jatujii litalimwaje na msimu ndio huo nataman.ungekuwepo ningepata msaada wa kulimiwa hili shamba
Yule kijana alijibu tafadhal baba usilime hilo shamba maana pesa zote nilizo ibwa nimeficha.huko
Kwakuwa barua zote laxima zipite kwa mkuu wa gereza ndio xiende kwa muhusika kesho yake mzee alikuwa shamba lote limelimwaa na polisi
Akatuma ujumbe tena yule kijana
Nashukulu umepata msaada sasa nazan unaweza ukaendelea kupanda mazao shamban.kwetuπππππ
Angalia huyu jamaa anavyojiona msomi, huyu kamuotea, hapa amekwama
USIJIONE MJUAJI SAAAAβ¦NA.
Jamaa kamaliza chuo anarudi nyumbani kwa wazee, kufika
nyumbani.
kwa furaha waliopata wazazi, mama aliamua
kurosti kuku WAWILI(2) kwa ajili yao.
Mezani jamaa akataka kuwadhihirishia kuwa yeye ni msomi,
akawaambia “hawa kuku unaona wako wawili ila kwa kutumia
sheria za arthematic na geometric kuna kuku watatu mezani”
mama”hee embu tuoneshe mwanangu”
jamaa akachukua kuku ya kwanza akainua juu “ngapi?”
wazazi”moja” akainua wa pili “ngapi?” wazazi “mbili”
akawarudisha akisema”wazee wangu nadhani japo shule
hamkwenda ila mnajua moja+mbili=tatu so tuna kuku watatu
mezani”
baba”mmh kweli mwanangu umesoma. SASA TUFANYE IVI
MIMI NACHUKUA KUKU MOJA NA MAMA YAKO WA PILI WE
UTAKULA UYO WA TATU ULIYOSEMA”
Angalia anachojibu huyu babu. Wazee wengine bwana
Babu: Mjukuu wangu ngoja nikusimulie hadithi ya mimi babu yako kwenye vita ya kagera
Mjukuu: Niambie babu
Babu: Kwenye vita ya kagera tulienda sehemu tukakamatwa wote askari na maadui wakatuambia chagueni kuuliwa au kubakwa.
Mjukuu: Sasa babu wewe ulichagua nn?
Babu: Niliuliwa!!!
Hapa itakuaje?
NAJISIKIA NIMEBOEKAβ¦
SIJUI NIENDE KAMBI YOYOTE YA JESHI NITEREMSHE BENDERA
ALAFU NITOKE MBIOβ¦..
πππππππΎππΎππΎππΎππΎππΎ
Mambo makuu matatu waafrika tusiyoyajua
NIMEKAA NIKAWAZA ππΌ KUWA KUNA MAMBO KAMA MATATU HIVIππ» WAAFRIKA HATUYAJUI π
KAMA TUNGEKUWA TUNAYAJUA HATA HAWA WAMAREKANI,πΊπΈWACHINAπ―π΅ NA HATA WATU WA ULAYA TUNGEKUWAπ½πͺ TUNAWAPITA KIMAENDELEO
MAMBO YENYEWE,,
HATA MIMI SIYAJUI MAANA NA MIMI NI MWAFRIKA ππππ
Breaking news
Breaking news π₯
Watu wasiojulikana wamevamia jengo lisilojulikana na
Kufanya tukio lisilo julikana na kukimbiliaππΏ kusiko julikana na mpaka sasa hakuna kinachojulikana na mimi sijui ninachosema ππ
Alichokisema mwizi baada ya kushinda bahati nasibu
Hapa mtaani kuna mwizi sugu ameshinda mil.10 za bahati nasibu ??.
Alipoulizwa atafanya nini na hela nyingi hizo
Akasema anataka kupanua shughuli zake. Mimi sijamuelewa na sasa hivi watu wameanza kuhama mtaaβ¦
ππ
Mkwe kazua mpya, Hii dunia ina mambo sana
Mama mkwe alimuuliza mkwewe “binti” samahani mbona mtoto hajafanana na mwanangu kabisa?
Binti akajibu, “bila samahani mama huku chini nina njia ya uzazi sio mashine ya photocopy”
mama mkwe hoii!! Chezea Wakwe Wa Bongo wewe.
Jambo la kufanya kama binti alikuachaga zamani na sahizi anakutaka
Kuishi kijijini kunahitaji moyo sana
..unaenda kuoga, unakumbuka kuwa umesahau sabuniβ¦unaenda kuchukua sabuni kurudi bafuni, unakuta ng’ombe amekunywa maji yote..unaamua kufuata mengne,unarudi unakuta mbuzi kala sabuniβ¦ππππ
Hapo sasa akili itakuja
Pale unapo gundua kuwa yule ulie mtukana kwenye bajaji ndio boss anaeenda kukufanyia interviewπ₯π₯π₯π
My freand apo ndo utagundua kwaanini wimbo wa Taifa tokea 1961 ni audio aujatolewa video
ππππππππ
Kilichotokea baada ya polisi wa kibongo kukutana na mwizi mzungu
POLISI KAKAMATA MZUNGU ‘yestaday I saw u at ze maize shop..(jana nilikuona dukani kwa muhindi) when u saw me u started 2 six six.(uliponiona ulianza ku-sitasita) u ran n decided 2 plant a car.(ulikimbia na ukaamua kupanda gari) zen u pot-cry me through ze window.(kisha ukanichungulia dirishani) now sleep down n snake well b4 I cut u a millet.(sasa lala chini kisha nyooka vizuri kabla sijakukata mtama) Chezea lugha wewe..!!!
Huyu jamaa bonge la bwege, ungekua wewe ndiyo rafiki ake ungemwambiaje?
RAFIKI: Vipi mbona leo huna uchangamfu
JAMAA: Wanawake bwana, mwanamke hata umpendeje atakugeuka tu
RAFIKI: Nini tena ndugu yangu? Mbona shemeji mtu fresh sana
JAMAA: Hata mimi nilikuwa najua hivyo, leo nimegundua kumbe ana siri kubwa sana
ananificha, mi naita huu ni usaliti wa ndoa.
RAFIKI: Nini tena?
JAMAA:Nimegundua mke wangu kumbe anafanya biashara ya kitimoto na hajawahi hata kuniambia
RAFIKI: Kitimoto? We umejuaje?
JAMAA: Leo asubuhi nilichelewa kuamka niliamua nijipumzishe kidogo kabla ya kwenda kazini, simu ya mke wangu ikalia, nikaamua kuipokea, kabla hata sijafungua mdomo, nikasikia sauti ya mwanaume mmoja akauliza, βHuyo nguruwe umeshamuondoa?β Hebu we fikiria nilivyoshtuka, yaani mpaka sasa nashindwa kuamini kuwa mke wangu ananizunguka anafanya biashara ya nguruwe hajaniambia hata siku moja
Cheka kidogo na wewe hapa
*Kama mtaani kwenu mambo yamekuwa tait , usikimbilie mtaani kwetu kwani huku yamekuwa dera kabisa*πππππ
Jana nilipeleka viatu kwa fundi sasa hivi nimekutana nae amevivaa namuuliza ananiambia eti ni ROAD TEST” πππ
MAMBO KUMI YA KUFURAHISHA NA HUWEZI KUYAFANYA
1. Huwezi kuosha Macho kwa Sabuni;
2. Huwezi kuhesabu Nywele zako;
3. Huwezi kupumua kwa Pua na huku umetoa Ulimi;
4. Unajaribu kufanya namba 3
6. Umeona inawezekana, sanasana unakuwa Kama Jibwa;
7. Unatabasamu kwa kuwa umejiona Mjinga!
8. Umeruka namba 5;
9. Unahakikisha Kama kweli 5 haipo.
10. Unacheka kwa kuwa nimekubamba!






































































I’m so happy you’re here! π₯³






Recent Comments