Vituko Vya Jumatatu

Alichofanya mke baada ya mme wake kupenda kumchunga sana

Alifanya hivi;
Siku ya kwanza

MUME: Halooo vipi mke wangu salama weye?.
MKE: Salama tu
MUME: Uko wapi?
MKE: Jamani si niko nyumbani
MUME: Mhh kama kweli uko nyumbani washa blender nisikie…..mke­ akawasha blender
MKE: Umesikia?
MUME: Okay haya mi natoka kazini naja

Siku ya pili
MUME: Vipi mko salama huko?
MKE: Tupo kama ulivyotuacha
MUME: kwani uko wapi?
MKE: Niko nyumbani napika
MUME: Washa brender kama kweli uko nyumbani
Mke akawasha blender
MKE: Umesikia?
MUME: Poa ntarudi baada ya masaa mawili

Siku sita baadae mume akaamua kurudi bila kumtaarifu mkewe alipofika home kamkuta mdada wa kazi yuko peke yake.
MUME: We mama yako yuko wapi?
MDADA: Sijui ameondoka na blender toka asubuhi

Huyu jamaa bonge la bwege, ungekua wewe ndiyo rafiki ake ungemwambiaje?

RAFIKI: Vipi mbona leo huna uchangamfu
JAMAA: Wanawake bwana, mwanamke hata umpendeje atakugeuka tu
RAFIKI: Nini tena ndugu yangu? Mbona shemeji mtu fresh sana
JAMAA: Hata mimi nilikuwa najua hivyo, leo nimegundua kumbe ana siri kubwa sana
ananificha, mi naita huu ni usaliti wa ndoa.
RAFIKI: Nini tena?

JAMAA:Nimegundua mke wangu kumbe anafanya biashara ya kitimoto na hajawahi hata kuniambia
RAFIKI: Kitimoto? We umejuaje?
JAMAA: Leo asubuhi nilichelewa kuamka niliamua nijipumzishe kidogo kabla ya kwenda kazini, simu ya mke wangu ikalia, nikaamua kuipokea, kabla hata sijafungua mdomo, nikasikia sauti ya mwanaume mmoja akauliza, “Huyo nguruwe umeshamuondoa?’ Hebu we fikiria nilivyoshtuka, yaani mpaka sasa nashindwa kuamini kuwa mke wangu ananizunguka anafanya biashara ya nguruwe hajaniambia hata siku moja

Misemo 10 bora ya kuchekesha itakayokuacha mdomo wazi

1. Mwanaume hata awe bahili vipi, hawezi kumpa mwanamke mimba nusu.

2. Hata uwe na magari mangapi chooni utaenda kwa miguu.

3. Kama ubinadamu kazi mbona hatupewi mishahara?

4. Ukichanganya wali na choroko unapata mseto, lakini hautibu malaria.

5. Hata njiwa nae ana makinda, lakini hawezi kuwa spika wa Bunge.

6. Hata uwe na haraka vipi kwenda Zenj, huwezi kupanda Jahazi ya Yusuph Mzee.

7. Umeme hauna kiuno lakini unaongoza kwa kukatika.

8. Hata uwe kauzu vipi, huwezi kujamba wakati unatongoza.

9. Hata uwe na imani kali vipi, huwezi kusali wakati unafanya mapenzi.

10. Hata kizibo ni mfuniko lakini hauwezi
kufunika sufuria.

Tofauti ya mwanamke wa Kizaramo, Kitanga, Kihaya, na wa Kichaga

Mwanamke wakizaramo: Unampa hela ana nunua dela anaenda ana msutia jirani, analivaa dela bila nguo ya ndani mbele yako, unazidiwa anakupa kitu fresh unatoka unatabasamu.🤝🏽🙌🏽

Mwanamke wa kitanga:
Unampa hela anapika vitu mtaa mzima unasikia harufu ya chakula, chenji inayo baki ananunua kinga ukirudi unakula afu unakula..👏🏼👏🏼🤝🏽🙌🏽

Mwanamke wa kihaya:
Unampa hela ukirudi unakuta majirani wote wanataarifa kuwa wew uliacha hela, anakupkia vitu vzuri, usiku anakuhudumia ukimsifia anakuhudumia tena hata mara nne kwa usiku mmoja..we mle sifa tu🙌🏽🙌🏽🤸🏾‍♀👌🏽.

Mwanamke wa kichaga:
Unampa hela anaenda ananunua dagaa anapika na michuzi mingi mpaka dagaa wanafufuka unakula kwa shida, dagaa wanakula utumbo wako unakufa.. Madaktari wanajitahidi wanakutibu unafufuka. Ukiwa hujapata akili vizuri anakuletea bili ya umeme, anakukumbusha deni la kwa Massawe, anakukumbusha kodi ya nyumba.. *Unashikwa na presha unakufa moja kwa moja*🙌🏽😂🙆🏼‍♂🏃🏾🤸🏾‍♀

Angalia huyu jamaa alivyoachika na msichana wake kwa kujidai kuongea kingereza na mwishowe kuchanganya maneno

MSICHANA: Mbona jana nimekupigia simu hujapokea?
JAMAA: please beby forget me.
MSichAnA: eeeh unaniambia hivo mimi?
JAMAA: nakuomba sana forget me.
MSICHANA: aya bwana poa maisha mema.

Msichana anakata simu jamaa ndo ananiuliza.”sasa
sijui amekasirikia lipi?” Mi nikamwambia we zuzu
umemwambia AKUSAHAU, dah, kumbe
ningemwambiaje? hahaha, ungemwambia
ForgivE me! au Ungesema Tu NaombA nSameHe.

Sababu za kumuacha mke kama umemchoka

Ukimchoka mkeo, waweza kumtaftia sababu za kumuacha kama hizi

_
1. Missed calls 16? Umeua betri la simu yangu. Kwa hiyo hata mimi unaweza kuniua… It’s Over!!!
_
2. Hata hunieshimu. Mi naongea na wewe lakini we upo bize unavuta pumzi? It’s over!
_
3. Nimekupigia umepokea simu hapohapo. Huna subira. It’s over!!
_

4. Nilikwambia huwa napenda chakula cha moto lakini hujanipashia ice cream. Hunijali. It’s over!
_
5. Nimekupa mayai mawili, moja uchemshe jingine ukaange. We umekaanga ambalo ulitakiwa kuchemsha na umechemsha ulilotakiwa kukaanga. Huniheshimu, It’s over!
_
6. Nimekuita DARLING na wewe ukaniita HONEY. Yani kwa maana nyingine unamuita mama yangu NYUKI. Huheshimu wazazi wangu, fungasha kilicho chako. its over.

😄😂😄😂😄😂😄😂😄

Cheki huyu mwanamke anavyomkomoa mme wake baada ya kumsaliti

MKE: Mbona unanukia pafyumu ya kike?
MUME: Yaa kuna mwanamke tulikuwa tumeminyana ndani ya daladala
MKE: Na lipstiki kwenye shati?
MUME: Tulikumbatiana na wageni toka Zambia walitembelea ofisi yetu
MKE: Na ile kondom iliyotumika kwenye mfuko wa suruali?
MUME: Bwana ee acha maswali ya kijinga mi nalala nina usingizi
MKE: Lazima niulize mie huwa nahakikisha nimeacha kila kitu hukohuko ndio narudi nyumbani
MUME: Umesema nini wewe?
MKE: Bwana ee acha maswali ya kijinga mi nalala nina usingizi. 😄😄

Kuwa na mahusiano na msichana kama huyu ni changamoto, Mabinti bwana!

Binti: Hallow mpenzi, Mambo

Jamaa: Poa baby

Binti:Uko wapi?

Jamaa: Niko town napata lunch

Binti: Wow unarudi saa ngap? Nina njaa dear naomba uniletee msosi

Jamaa: Narudi baada ya nusu saa nikuletee nini?

Binti: Niletee chipsi kuku, soseji, mayai manne ya kukaangwa pembeni, baga, piza, coke take away baridi, mkate wa moto kwenye ile bekari ya wapemba na maji ya kunywa ya kiimanjaro.

Jamaa:Umesahau viti, meza, masufuria, sahani na beseni na vijiko.

Binti: Kwanini dear?

Jamaa: Naona hutaki kula unataka kufungua hoteli!

Shopping Cart
2
    2
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About