Vituko Vya Jumapili

Makonda wana mambo, Kila mtu ni ndugu yao

Hakuna m2 mwenye ndugu wengi kama konda wa daladala.

Utasikia,
“HAYA, DADA HAPO MBELE, MJOMBA KULE MWISHO.
MA-MDOGO UNAENDA?,
NGOJA ASHUKE BIBI.
HAYA SHEMEJI UMEIKUTA YA KUWAH.
Babu njoo ukae!
Baba angu hapo tusogee kidogo,

Shangazi maliza ngazi,
Swaiba geukia mbele,
Kaka hapo shika upande wa pili,
Mdogo wangu mpishe Ma Mkwe akae.
Subiri Shemeji yako apande…

Duh… makonda noma…!!

Kapresha kakiamua kuja kanakujaga tuu, cheki kilichompata huyu mme wa mtu mpenda michepuko

Kimchepuko chako kinakuandikia meseji kama hii…

…Samahani baby kama unavyojua nimeokoka ,nimetubu kanisani lakini nabii kaniambia niwaombe msamaha wote niliowakosea.

Nimemkosea sana mkeo kwa kumwibia mumewe na nimepanga kuja kumwomba msamaha kesho ntakuja na nabii na Mchumba wangu mpya nilie mpata kanisani.

Samahani kwa usumbufu uliojitokeza lakini hilo ni kwa ajili ya utukufu wa bwana!!!

Wako Manka wa Magorofani😅😅

Huyu mchaga kazidi sasa, angalia anavyomfanya huyu mbuzi

Mchaga alinunua mbuzi akamwambia mpishi Nyama nusu ipike pilau na ingine itie kwenye friza. Kichwa fanya supu, miguu fanya mchuzi chukuchuku. Ngozi usitupe tutafanya mswala, utumbo pikia ndizi na mifupa tutawauzia wenye mbwa. Kinyesi kihifadhi kwa mbolea ya bustani.

Mpishi akamuuliza Hutaki na sauti ya mbuzi tufanye ring tone kwenye simu yako? Mchaga akajibu Yesuu! hivi inawezekana? bac fanya hivyo tuwauzie na wengine hiyo ringtone. Chezeya mchaga!

Soma hii, kama wewe ndio mzazi wa huyu msichana ungefanyaje?

Wewe ni mzazi mwanao anasoma kidato cha tatu mkoani umemsafirisha leo kwenda shule baada ya masaa matano ukasikia gari alilo panda mwanao limepata ajali wamekufa watu wote upo ktk harakati za kuandaa msiba,

mwanao anakupigia simu baba/mama mimi mzima sijafa mpenzi wangu ABDUL aliniambia nishuke Chalinze ili niwe nae kwa siku mbili alafu niende shule je, wewe mzazi unge mfanyaje mwanao?

Wabongo ni noma! Angalia huyu mbongo anachokifanya

Basi juzi kati hapa sehemu ndogo ya ukuta wa Ikulu ya Magogoni ilianguka!..
Wakapelekwa contractors watatu ili achaguliwe mmoja atakayejenga vzr na kwa bei nafuu!..
Wakwanza alikuwa MUHINDI, wa pili MCHINA na MBONGO!…

MUHINDI: “ntajenga kwa milioni 90!.., 40 za vifaa, 40 za mafundi na milioni 10 faida yangu”

MCHINA: “mi ntajenga kwa milioni 70!.., 30 za vifaa, 30 za mafundi na milioni 10 faida yangu”

MBONGO kuona vile akamvuta chemba msimamizi wa Magogoni!..
MBONGO: “mi ntajenga kwa milioni 270”

MSIMAMIZI WA MAGOGONI: “we una wazimu nn!.. yaani unathubutu kusema hivyo na unaona wenzako wametaja kiwango kidogo?!.”

MBONGO: “milioni 100 zako, 100 zangu alafu hiyo milioni 70 tunaajiri yule mchina”

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About