Vituko Vya Ijumaa

Analia kilichompata huyu jamaa baada ya kubadili jinsia yake kichawi

Jamaa alimpa ujauzito mwanafunzi akashtakiwa kumbe yule jamaa ana bibi yake mtaalam wamambo yetu ya Jadi…

Jamaa akaongea na bibi yake amuwekee jinsia ya kike ili akashinde Mahakamani na akitoka arudishiwe mambo yake kama kawaida.

Bibi akampachika jamaa jinsia ya kike alipofika mahakamani kuhojiwa akasema mi sijampa ujauzito kwasababu minina jinsia ya kike pia…!
Kwa kuthibitisha akajifunua nguo, basi jamaa akashinda kesi.

Jamaa akawa anarudi Home, lakini wakati anakaribia kufika akaona watu wengi wamejaa home wanalia akauliza kulikoni akaambiwa “Bibi amefariki”!

Vuta picha hapo…!!!

Huyu mchungaji ni noma, cheki alichomwambia pedeshe

Mchungaji kamfuata pedeshe moja maarufu kwa
kumwaga pesa kwenye kumbi za muziki;
MCHUNGAJI: Kijana, tuko katika harakati za
kujenga kanisa, jitafutie nafasi katika ufalme wa
mbingu kwa kuchangia ujenzi huu. Na Mungu
atakubariki zaidi

PEDESHE: Samahani Mchungaji haitakuwa vizuri
mimi kuchangia kanisa, fedha zangu ni haramu,
huwa nazipata kwa utapeli na kuuza madawa ya
kulevya.
MCHUNGAJI: Yote ni heri, pesa yako tutatumia
kwa kujenga eneo la choo we toa tu!!!

Kilichompata sista duu bishoo wakati akijidai kununua pete

Mwanamke mmoja aliingia duka la vito vya thamani, akaona pete moja ya dhahabu nzuri sana amabayo ilikuwa kwenye shelf ya chini, wakati anainama apate kuitazama vizuri kwa bahati mbaya (au nzuri!), shuzi likamtoka- druuuuuu, soni ikamuingia huku akigeuka haraka kuangalia kama kuna yeyote dukani pale ameliskia shuzi lake, macho yakagongana na mwenye duka ambaye alikuwa karibu huku uso ukiwa umejaa tabasamu zito, mwana mama hakuwa na uhakika kama amesikika au hakusikika, akaona atumie nafasi ile kuyeyusha…Akauliza “Hii pete bei gani?” . Jamaa mwenye duka, huku akiangua kicheko, akajibu “Umeiona tu umejamba, je nikikuambia bei yake si utakunya kabisa?”

Kuna watu makauzu ila huyu kazidi.. Soma hii!

Kakubaliana vizuri na msichana fulani hivi kuwa aibuke gheto, mchizi kajipanga vizuri kabisa…. mara saa nne hivi mdada kasema hana nauli.
Mshkaji kajikunja kamtumia Elfu tano maana mwenye shida alikuwa ni yeye……
Baada ya nusu saa yule dada akamtumia meseji.
“Jamani mpenzi, kumbe baba hatoki nilijua atatoka… sorry bae sitaweza kuja kwa leo… sooo sorry!”
Mshkaji jiii! hajajibu kitu…..

Baada ya muda kidogo meseji ikaingia katika simu ya binti, akajua mchizi kajibu. Mh! kutazama ni meseji kutoka Mpesa.

“CA90F0511 IMETHIBITISHWA Tshs 5000 ILIYOTUMWA KIMAKOSA KATIKA ACCOUNT YAKO IMETOLEWA SALIO LAKO NI Tshs 5”

Halafu ndo ikaingia meseji ya mshkaji.
“BASI POA SIKU NYINGINE KAMA VIPI”

#dada wa watu mashavu yakamshuka… hakuamini kilichotokea…. yaani jamaa keshawapigia Voda na pesa fasta imezuiliwa……

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About