Visa Vya Msimu

Angalia huyu jamaa alivyowafanyia watu uhuni bar

Jamaa kaingia Bar;
Jamaa: Muhudumu, nipe kinywaji na mpe kila mtu humu ndani kinywaji, maana wakati napata kinywaji lazima kila mtu apate kinywaji. Haraka sana muhudumu akagawa vinywaji,

Jamaa: Muhudumu nipe supu na kila mtu humu ndani mpe supu maana ninapokunywa supu kila mtu lazima anywe supu. Watu wakapewa supu tena safari hii wakapiga makofi.
Jamaa: Muhudumu nipe bili, na kila mtu humu ndani mpe bili maana wakati nalipa bili yangu kila mtu lazima alipe yake. Zogo lilianzia hapo…….

Kilichotokea baada ya bibi na babu kukumbukia mahaba ya ujanani

Mzee wa miaka 60 alimwambia mkewe, leo nataka tukumbukie enzi zetu kutongozana, mke akajibu sawa, inabidi unisubiri mwembeni saa 1 usiku nitapita, mzee akafika saa 1 alikaa hadi saa 5 usiku, aliporudi nyumbani akamuuliza mkewe kwa hasira; sasa tumepanga nin halafu haujatokea ?
Mke; leo mama alinikataza nictoke nyumbani usiku nijisomee ! Babu hoii…

Hawa wanaume wanaopenda wanawake hovyo barabarani wamepatikana, hawatarudia 😂😂😂

Marafiki wawili (Jose na Ben) walikuwa wanatembea mtaani akatokea mwanamke akarusha busu kwa mmojawapo kupitia dirishani katika jengo la ghorofa tatu.

Wakaanza kujadiliana kama ifuatavyo:

Ben: Muone yule mrembo amenirushia busu

Jose: tafadhali achana na huyo mwanamke, usimjali..

(baadae yule mwanamke akamuashiria aende)

Ben: yule mwanamke ameniita!

Jose: Rafiki yangu, usiende. Nakutafadhalisha.

Ben: Kwa nini unaniambia nisiende Wakati mrembo kama yule ananiita? Huo ni wivu

Jose: Ben, Ninakutafadhalisha tena, usiende, tafadhali usiende kule (akihisi kutotiliwa maanani)

(Rafiki yake alimpuuza na alienda kwa yule mwanamke, mwanamke alishuka kukutana naye na wakapanda juu. Ghafla wakiwa wanataka kuanza taratibu za kula uroda, wakasikia mlio WA gari getini).. 🔊🔊

Lady: _(akiangalia kupitia dirishani)_
Oooh! Yule ni mume wangu!!

Ben: Mama yangu !
Nipo matatani, kweli ? ..!!

Lady: Usiwe na khofu, jifanye kuwa Dobi na anza kupiga pasi hizo nguo

(akimuonyesha lundo la nguo)

(Ben alitumia masaa matano kukamilisha kunyoosha zile nguo kwa sababu yule mume hakutoka tena siku ile)

(Siku iliyofuatia Ben alikwenda kwa Rafiki yake)

Ben: Kaka, unaweza kuamini Jana nimepiga pasi nguo kwa masaa matano???

Jose: Lakini nilikwambia usiende. Nguo zote hizo ulizonyoosha, Nilizifua Mimi Juzi!!
😂😂😂😂😂😂😂😂😂

When an experienced person speaks … 👂you must listen..!

Kichekesho cha mwalimu na wanafunzi

Mtoto: Mwalimu mimi nataka nisome darasa la nne kwani hili la3 halinifai.

Mwalimu: Kwa nini unasema hivyo?

Mtoto: Nina akili…

Basi mwalimu akamueleza mkuu wa shule na mkuu kaitisha interview kwa dogo. Maswali ni haya….

Mwalimu: Kwenye ndege kuna matofali 20 tukitoa moja tukalidondosha chini yatabaki mangapi?

Dogo: Yatabaki 19.

Mwalimu: Nipe hatua za kumuweka tembo kwenye friji.

Dogo: Unafungua friji unamuweka tembo kisha unafunga.

Mwalimu: Nipe hatua za kumuweka nyani kwenye friji.

Dogo: Unafungua friji unamtoa tembo ulemuweka..unamueka nyani kisha unafunga friji.

Mwalimu: Kuna sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa simba, wanyama wote wameenda kasoro mmoja. Ni nani na kwa nini?

Dogo: Ni nyani kwa sababu tumemuweka kwenye friji.

Mwalimu: Bibi kizee amevuka mto unaokuwaga na mamba na viboko wakali, aliwezaje?

Dogo: Aliweza kwani mamba na viboko nao walienda kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa simba.

Mwalimu: Ingawa bibi kizee alivuka mto, baadae alikufa. Unadhani ni kwanini alikufa?

Dogo: Alidondokewa na lile tofali tulotoa kwenye ndege na kutupa chini.

Mwalimu mkuu: Huyu dogo akasome chuo kikuu….
😆😆😆😆😆😆😆😆

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About