Visa Vya Kileo
Alichofanya maasai baada ya kupanda Tax
Baada ya kupanda daladala aina ya DSM kutoka Mbagala chalambe mpaka Mwenge na kulipa sh 500.Masai akachukua tax wakati wa kurudi.walipofika sasa shughuli ilikuwa hivi.
Masai: we dureva? Naulisa Ng’ombe na mbusi ipi ngali?
Dereva: Ni ng’ombe ghali Masai.
Masai: kwanini Ng’ombe ngali?
Dereva: kwa sababu ni mkubwa zaidi ya mbuzi
Masai: umepata..na mbusi na kuku ipi ngali
Dereva: ni mbuzi kwa sababu nae ni mkubwa kuliko kuku.
Masai: Umepata..
Masai: sasa me nimekwenda kule mwenge kwa ngali kubwa nikalitoa sh. 500 hii yko ndogo unasema nikupe 40,000 wewe acha wizi.. Nitakupa 250 Tu..wee acha lbia moraniโฆ!!!
Alichokijibu chizi baada ya kuanguka ghorofani
Chizi kaanguka toka kwenye gorofa fasta watu wakamfuata kumsaidia wakamuulza VP IMEKUAJE?
Chz akajbu: ”HATA CJUI NA MIE NDO NAFIKA SASA HIVI
Sitasahau mwaka huu
Sitasahau mwaka ule ambapo nilipeleka barua ya maombi yangu ya kazi kwenye kampuni moja maarufu. Wakati nasubiri majibu siku moja nikaenda kwa mama ntilie kununua maandazi akanifungia vizuri, kufika nyumbani hamu yote ya maandazi iliniishia pale nilipogundua karatasi iliyofungiwa maandazi ni barua yangu ya kuombea kazi๐๐
Cheki kilichompata huyu dada!!
NDOA inafungwa KANISANI Mchungaji akauliza-Yeyote mwenye Pingamizi La Ndoa hii kufungwa aje Mbele, +++ KIBABU kikasimama na kwenda Mbele,
Bi harusi akaanguka na akazimia ghafla!๐ญ๐ญ๐ญ
Mchungaji- Tuambie Babu Pingamizi Lako!
Babu-Nimeamua kuja mbele,kule nyuma sisikii vizuri! watu hoiiii!!
hata mimi hoiโฆ๐๐๐๐๐๐๐
Angalia hawa vichaa walichokifanya, Vichaa bwana, ni noma!
Vichaa walipanga kutoroka, wakakubaliana wamnyonge mlinzi watoroke!
Walipofika getini wakakuta geti lipo wazi na hakuna mlinzi, wakasema “Turudi mipango yote imevurugikaโฆ
Angalia nilichokifanya baada ya kuumwa na meno
Baada ya kuumwa na Meno nikaamua hivi.
mimi sipeรฑdagi ujinga,,,Nmeumwa na jino moja la chini..nimeng’oa meno yote ya chini ili iwe funzo kwa meno ya juu๐ก๐ก
Cheki kilichotokea stesheni ya treni, mambo mengine ukipaniki inakula kwako kama huyu jamaa
Jamaa Wawili Walifika Stesheni, wakakuta Treni ndo kwanza inaondoka. Wakaanza Kuikimbiza. Mmoja akafanikiwa kupanda akaondokaโฆ
Yule aliyebaki akaanza kucheka sanaa mpaka machozi yakamtoka. Watu wakamuullza, unacheka nini sasa wakati umeachwa? Akawajibu: “kinachonichekesha, yule aliyepanda alikuwa ananisindikiza.
Cheki hawa washikaji wanachokifanya baada ya kuvuta bangi, Bangi si mchezo
Kuna washikaji walikuwa wakivuta bangiโฆ kiberiti kikawaishiaโฆ wakamtuma mwenzao akatafute kingineโฆ bangi lilikuwa limemkoleaโฆ akazungukazunguka hatimaye akarudi palepale kijiweniโฆ
MSHIKAJI:ย oyaaa wanangu eeehโฆ niazimeni kiberiti mwanangu mwenyewe โฆ..
WENZAKE:ย baharia ee subiria kimtindo kuna mwana tumemtuma akatafute kiberiti.
Wanaume ni noma, Angalia huyu alivyomdanganya huyu ๐ง girlfriend wake
Jamaa kamdanganya girlfriend wake kuwa anasomea HOTEL MANAGEMENT. Siku huyo girlfriend akamkuta jamaa anaosha vyombo kwa MAMA NTILIE.
Girlfriend akamuuliza jamaa โbeby vipi mbona uko hapa?โ Jamaa bila woga akajibu โNIPO FIELD.
Wanaume hatupendi ujinga sisi ๐ ๐ ๐
Januari kweli ngumu, soma hii
Januari kweli kiboko
Hii january sabuni za kuogea ni zile za kuoshea vyombo, yani unakutana mjini na mtu ana mchicha shingoniโฆ๐
Kilichompata huyu anayependa kusoma SMS za watu kwenye daladala
Jana nilipanda daladala nikapata seat nikaketi, nikawa nimejiachia ninachati kwenye simu yangu(Smart phone), kukawa na jamaa kasimama pembeni yangu, ye hakupata seat. Sasa akawa anasoma message zangu bila aibu yani anafutilia ninavyochatiโฆ
Basi nikasema ngoja nimtie Adabu mshenzi huyuโฆ. Nikacheck saa yangu yamkononi kisha nikatext:ย “Oya Ben Kwaheri bwana, zimebaki sekunde 30 tu hili bomu๐ฃ lilipukeโฆ najua hatutaonana tena, nitunzie Familia yangu, wambie nawapenda sanaโฆ”ย Yule jamaa akajirusha dirishaniโฆโฆ๐๐
โkwani mi napenda ujinga xx ๐๐๐๐๐๐๐
Mshahara usiobadilika
PAMOJA NA HALI NGUMU YA UCHUMI NCHINI HUWEZI AMINI MSHAHARA WA DHAMBI HAUJABADILIKA HATA KIDOGOโฆBADO NI MAUTI VILEVILE
๐๐๐๐
Huyu ndo mwanamke
Akikuta PESA wakati anafua atapiga kimya kimya, sasa ngoja akute umeacha CONDOM ndo utajua kama umeoa KIPAZA SAUTI ๐๐๐๐๐๐
Ndio maana mimi nafungaga condom na hela kwa pamojaโฆ akivikuta anachukua hela na kuishia kusonya tu.. ๐๐๐๐๐๐๐
Huwa sipendagi ujinga Mimi
๐ก๐ก๐ก๐ก๐ก๐ก
Hili nalo neno kwa wavulana
Hili nalo neno
Demu wako anakuja kwako kasuka nywele za 30,000 na hujampa hata mia,we unakalia kusema waooo waoooo kama king’ora cha ambulance.
Shauri yako we endelea kusema waoooo waooo na atakuwa wao kweli.
๐๐๐๐๐๐๐
Duh! Hii sababu ya huyu mwanaume kulewa ni shida
๐ง: “Mpenzi, nakuomba uache kulewa”
๐จ: “poa, na wewe acha kutumia make up”
๐ง: “Mimi napaka make up ili unione mzuri”
๐จ: “Na mimi nalewa ili nikuone mzuri”
Vodka hatareee๐๐
Cheka kidogo na wewe hapa
*Kama mtaani kwenu mambo yamekuwa tait , usikimbilie mtaani kwetu kwani huku yamekuwa dera kabisa*๐๐๐๐๐
Jana nilipeleka viatu kwa fundi sasa hivi nimekutana nae amevivaa namuuliza ananiambia eti ni ROAD TEST” ๐๐๐
Utani kwa wadada wembamba
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Wadada wembamba hebu nenepeni basi mnatupa tabu kusoma maneno ya kwenye kanga jamanii โฆโฆโฆmnaviringisha kanga mwili mara 3 mpaka maandishii hayaonekanii
๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ
Kifahamu Kidada kimbea kilichofukuzwa kazi
Unafahamu?
Kile kidada kimbea kinachosemaga salio lako halitoshi kimefukuzwa kazi saivi kupiga simu ni bure mjulishe na mwenzako
๐ฒ ๐ฒ


















I’m so happy you’re here! ๐ฅณ



























































Recent Comments