Visa Vya Kileo

Cheki kilichonipata sasa, ungekua wewe ungefanyaje?

Siku moja katika pitapita zangu nikakutana na mtoto mmoja mkali balaa yaani ni mzuri sanaaaa, moyo ukanituma nimuimbishe mtoto akakubali kwamba nitafute siku tukae tuongee vizuri akasema nimpe namba yangu ya simu.

 

Ebwana si akatoa simu hiyo inauzwa laki sita mimi hapa nina kisimu cha tochi tena nimefunga na rababendi
Je, wewe ungeendelea kumtajia namba zako!!!

Kwa nini vitu vunavyoanza na “K” ni vitamu sana?

Zuzu kaniuliza, “Anko, unajua vitu vinavyoanzia na K ni vitamu sana.”
Nikashtuka, “Astaghafilulah we mtoto! Niondolee wehu wako hapa!”

Zuzu akatabasamu. Akaendelea kuongea kabla sijafanikiwa kumzuia. “Kweli kabisa anko. Vitu vinavyoanza na K ni vitamu sana kwa mfano kuku, kalimati, keki, kabab, katleti, kashata, kisheti na karoti.”
Nikashusha pumzi. “Ahaa! Kumbe ndo hivyo, ni kweli!”

Zuzu akanitupia swali. “Kwani we anko ulidhani nini?”

Tofauti ya mke na mchepuko!!!

MKE NA MCHEPUKO.

Mke ni kama Tv na Mchepuko ni kama Simu.
Nyumbani unaangalia Tv lakini ukitoka unatoka na simu.

Mara chache unafurahia Tv lakini Muda mrefu unacheza na simu yako.

Tv ni bure kwa maisha yako yote, lakini Simu kama hujalipia hupati huduma.

Tv ni kubwa nzito na wakati wote ni ya zamani. Lakini simu ni nzuri, nyembamba, na ni rahisi kubeba.

Gharama za huduma za tv ni ndogo sana, Lakini gharama za huduma za Simu ni kubwa na pia ni lazima kuzitimiza.

Tv ina remote lakini Simu haina.

Kitu muhimu zaidi simu ina njia mbili za kuwasiliana unaongea na unasikiliza lakini Tv unalazimika kusikiliza hata kama hutaki au unataka.

Unaweza kununua Tv mara moja na ukatumia kwa kipindi kirefu lakini Simu mara zote unabadilisha inategemea na fasheni.

Ya mwisho na ya kuzingatia

Tv haina Virusi lakini Simu inayo.

KUWA MAKINI.

Angalia huyu mwanafunzi anachomjibu huyu mwalimu wake

1. Ticha:”Punda ni mnyama anaefugwa nyumbani,lakini akiwa mwituni anaitwa pundamilia….Je sungura anayeishi mwituni anaitwaje?”

ZUZU:”Sunguramilia.”

2.Ticha:”Rais wa kwanza wa kenya aliitwa KENYATTA…Je rais wa kwanza wa
Tanzania aliitwaje?”
ZUZU:”TANZANIATTA.”

3. Ticha:”Kuku yuko katika jamii ya NDEGE…Je samaki yuko katika jamii ya nini?”

ZUZU:”MELI.”

4. Ticha:”Coach wa Arsenal anaitwa ARSENE,wa Man-city anaitwa MANCINI….Je wa
Liverpool anaitwaje?

ZUZU:”LIVER.”

5 Ticha:”Ukiwa na mbuzi 10,wezi waje waibe 5,utabaki na nini?”

ZUZU:”Hasira nyingi sana!”

Shopping Cart
2
    2
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About