Vihoja Vya Kuwaadisia

Kauli 10 mbaya za walimu darasani, unakumbuka ipi hapa?

1:Mkimaliza kuongea niambieni niendelee kufundisha

2:Baba yako kauza ng’ombe ili alete ng’ombe mwingine shule

3:Kama unajua kuliko mimi njoo ufundishe wewe

4:Ulikuja peke yako na utaondoka peke yako

5:Hata msiponisikiliza mshahara wangu uko pale pale

6:Baba yako anahangaika kulipa ada wewe unafanya utumbo tu

7:Hata nikeshe nafundisha wengine ni mizigo hawatoki na lolote

8:Tunavisaidia tu kwan vikifanikiwa mbelen hata salam vinatoa?

9:Bichwa kubwa ubongo nukta

10:Wengine hapa wamekuja kukua tu

SHARE NA MARAFIKI ZAKO WAKUMBUKE ENZI ZA SHULE KIDOGO

Baada ya kumkuta mwanamme mwingine chumbani kwake na mke wake cheki huyu anachokifanya

NAKUA(BABA) karudi kazini mwanae mdogo akamuwahi,
DOGO: Baba usiingie ndani kina jini chumbani kwenu
NAKUA: Hakuna kitu kama hicho
DOGO: Kweli baba kuna jini liko kwenye kabati lenu la nguo….

NAKUA kaingia ndani kamkuta mkewe kalala kitandani kajifunika shuka gubigubi hadi kichwani. Kaenda kwenye kabati kufungua mlango , akamkuta rafiki yake wa miaka mingi yuko uchi ndani ya kabati
NAKUA: Aise unajua we fala sana, we rafiki yangu miaka yote hiyo halafu unamtisha mwanangu eti wewe jini, hebu toka huko nenda kwenu kacheze michezo hiyo na mwanao.

Angalia kilichotokea baada ya dogo kupewa ada na kuitumia kubeti

Dogo kampigia simu baba yake;
DOGO: Baba katika zile shilingi laki mbili ulizonipa
nikalipe ada nimetumia shilingi alfu 30 kubeti
BABA : Unasema nini we mpumbavu mshenzi
mkubwa? Nimekukanya mara ngapi kuhusu kubeti?
DOGO : Lakini baba
BABA : Lakini baba nini ngoja urudi utaona
ntakachofanya.
DOGO : Nilitaka kukwambia kuwa nimeshinda
shilingi milioni 3
BABA : Ndio hayo ninayosema wewe mpumbavu
sana kwanini hukutumia laki nzima kubeti? Si
ungepata pesa nyingi zaidi? Ngoja urudi niwataarifu
ndugu zako kuhusu uulivyo na akili za kuamua
haraka mwanangu mpenzi…

😂😂😂😂😂😂😂😂😂

Ufugaji wa nguruwe kazi, Cheki jamaa hawa wake walivyompa mtihani

MWANAHARAKATI: Hawa nguruwe unawalishanini?
.

MFUGAJI: Nawalisha mabaki ya chakula toka migahawa mbalimbali
.
MWANAHARAKATI: Hayo ni makosa unawatesawanyama kwa kuwalisha chakula kichafu. Akapigwa faini… Baada ya siku chache wakaja wanaharakati toka Umoja wa Mataifa
.
MWANAHARAKATI: Hawa nguruwe unawalisha nini?
.

MFUGAJI: Huwa nawaanzia siku na uji wa ulezi, halafu mikate, mchana ugali kwa kabeji na usiku viazi
.
MWANAHARAKATI: Loh watu wanakufa kwa njaa wewe unalisha nguruwe, akapigwa faini….siku chache baadae wakaja wanaharakati wa Mazingira
.
MWANAHARAKATI: Hawa nguruwe unawalisha nini?
.
MFUGAJI: (Kwanza akasita kidogo) Hawa huwa nawapa shilingi alfu tano kila mmoja kila siku halafu wao wenyewe wanaenda kununua chakula wanachokitaka.. .

Cheki hawa washikaji wanachokifanya baada ya kuvuta bangi, Bangi si mchezo

Kuna washikaji walikuwa wakivuta bangi… kiberiti kikawaishia… wakamtuma mwenzao akatafute kingine… bangi lilikuwa limemkolea… akazungukazunguka hatimaye akarudi palepale kijiweni…

MSHIKAJI: oyaaa wanangu eeeh… niazimeni kiberiti mwanangu mwenyewe …..

WENZAKE: baharia ee subiria kimtindo kuna mwana tumemtuma akatafute kiberiti.

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About