Vihoja Vya Kukuburudisha

Angalia nilichokifanya Jana kumkomoa x-wangu

Mwenzenu nilikatiwa umeme jana basi leo si nikaamua kwenda kununua luku ya 10,000. Kufika njiani nikatamani fursana nikaingia kijisupermarket mara sindo nakutana na ex wangu! Mshenzi yule kaniona mimi sijui alikua na mpango wa kununua vocha ya jero eti kabadili kanunua vocha ya buku tano ilimradi nione maisha yake safi tangu tuachane. Mambo ya kijinga spendi kudadeky nimetoa buku kumi nikanunua mipampers nami nijifanye nimeowa nina mtoto halafu huyoo nikashika njia yangu.

Sasa washkaji zangu tafadhalini mwenye mtoto au shida ya pampers naomba anunue kwangu maana leo nalala tena kiza ๐Ÿ™†โ€โ™‚

Makonda wana mambo, Kila mtu ni ndugu yao

Hakuna m2 mwenye ndugu wengi kama konda wa daladala.

Utasikia,
“HAYA, DADA HAPO MBELE, MJOMBA KULE MWISHO.
MA-MDOGO UNAENDA?,
NGOJA ASHUKE BIBI.
HAYA SHEMEJI UMEIKUTA YA KUWAH.
Babu njoo ukae!
Baba angu hapo tusogee kidogo,

Shangazi maliza ngazi,
Swaiba geukia mbele,
Kaka hapo shika upande wa pili,
Mdogo wangu mpishe Ma Mkwe akae.
Subiri Shemeji yako apandeโ€ฆ

Duhโ€ฆ makonda nomaโ€ฆ!!

Hii ndio maana ya Matatizo, usiombee hili likukute

Matatizo ni nini???

`Matatizo ni pale unapokuwa umefika ukweni usiku na haja kubwa ikakubana na hukuwa unajua choo kilipo, ukatoka nje na kujisaidia kwenye majani kumbe ni mboga asubuhi ukasikia mama mkwe anasema kuna mjinga kajisaidia kwenye mboga na kaangusha pochi yake hapohapo haa! Vile unajisachi pochi hamna na kulikuwa na passport,vitambulisho, kadi ya benki, pesa zaidi ya laki 2 na nusu, funguo za nyumba yako, `
๐Ÿค’๐Ÿค’๐Ÿค’๐Ÿค’๐Ÿค’๐Ÿค’๐Ÿค’๐Ÿค’๐Ÿค’

Walahi haya ndo matatizo๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…

Kweli shilingi yaua, Huyu jamaa kapatikana, angalia anachomjibu mke wake,

Jamaa alikuwa anagombana na mkewe,hatimae
akamwambia kwa ukali
“Unajua nimechoka sasa, haya kusanya nguo
zako naโ€ฆโ€ฆ..

Kabla hajamalizia sentensi simu
ya mkewe ikaita, kumbe alikuwa ni baba yake.
Basi mzee akaanza kuongea na binti yake huku
jamaa anasikia

“Aisee mwanangu nimebahatika kuuza ile
nyumba yangu sasa nimeona niwatumie milioni
20 mjaribu kuanzisha mradi na mwenzio.
Haya mwambie yeye nitampigia kesho kama
ana mradi mwingine nimpe hela kidogo”.Baada
ya simu kukatwa mke akamgeukia jamaa
akamuuliza,”eeenhee!!! ulikuwa unasema
umenichoka nikusanye nguo zangu halafu
iweje? Jamaa kwa upole akajibu “Nilikuwa
nasema ukusanye nguo zako na unipe nifue”.

Ameniomba nimfungulie akaunt facebook cheki nilichomjibu

Leo nimechoka zangu alafu shangazi amekuja anataka nimuunganishe facebook. Imebidi nimwambie
lazima awe na picha passport size 4 kwaajili ya kuweka profile picture, barua kutoka kwa afisa mtendaji na Atm card ya nmb bank. Alafu awe na marefa wanne ambao wamekuwa facebook for more than 3 years. Amesema
hataki tena kujiunga fb!

๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Saa ivi niko zangu nimelala naendelea kupunguza uchovu

Angalia hawa wadada walivyoumbuliwa, Huyu kasuku jeuri kweli

Kasuku alisimama mlango wa kuingia supermarket wakapita wanawake watatu akasema nyeupe, nyekundu, kijani. Wale wanawake wakatatizika baada ya mda wakajua ni chupi walizovaa. Wakasema basi kesho tubadilisheni. Siku ya pili wakapita tena kasuku akasema nyeusi, manjano, zambarau. Loh! Wanawake wakastaajabu sana. Wakasema lazima wamshinde yule kasuku kwa hekima. Wakaambiana basi kesho tusivae chupi tuone kama ni kweli anaona mpaka ndani. Siku ilipowadia wakapita mbele ya kasuku akasema- kipilipili, kipara, rastaโ€ฆ

Ziara za kushtukiza zinachekesha sana

Mimi Nimecheka sana
๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

ZIARA ZA KUSHTUKIZA๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€
Mimi ni msomaji mzuri wa magazeti, na msikilizaji mzuri wa redio, huwa naangalia luninga mara chache sana kama nikibahatika kupita mahala kuna luninga. Sasa wiki hii nimesikia mengi kuhusu hizi ziara za kushtukiza za viongozi wetu, nikaona hili ni jambo zuri tena linafaa kuigwa na sisi wananchi wapenda maendeleo. Nikaona nijipange na mimi nifanye ziara kadhaa za kushtukiza katika sehemu mbalimbali zinazonihusu.

Nikaona nianze na ziara ya kushtukiza pale shuleni kwa huyu mwanangu, maana kila siku anakunywa chai na kuondoka na daftari zake na mie sijawahi kwenda shuleni kwao toka nilipomuandikisha shule mwezi Januari. Nilifika shuleni na kumuona mwalimu mkuu, ambae alianza kutetemeka nilipomuambia kuwa nimekuja pale kwa ziara ya kustukiza, sijui alidhani mi ni mmoja wa Mawaziri wapya, maana nilimuona jasho linamtiririka ghafla. Akanikaribisha ofisi yake iliyokuwa na vitabu kila kona, na kuita waalimu wote na kunitambulisha kuwa ni kiongozi nimekuja kwenye ziara ya kustukiza.

Nilipojitambulisha kuwa ni mzazi, waalimu wote nikawaona waanza kupumua kwa raha. Nikawaambia kuwa mimi nina mwanafunzi pale na nilikuja ziara ya kustukiza kujua maendeleo yake. Baada ya mwalimu mkuu kusaka jina la mwanangu nae akanambia, โ€œMzee huyu mtoto hajaja shule mwezi wa tatu sasa, tulijaribu kukutafuta ikashindikana, hatujui yu wapiโ€ Jasho likaanza kunitoka mimi, yule mtoto kila asubuhi nampa nauli anaenda shule, na mara nyingi ananiomba michango kumbe hata shule haji. Niliondoka bila kuaga presha ikiwa juu.

Nikaona niende kwenye genge la mke wangu nae nikamfanyie ziara ya ghafla nimhadithie mambo ya mwanae, nilipofika pale nikakuta kuna mdada mwingine anauza genge. Nikamsalimu, na kumuuliza mwenye genge ntampataje, jibu lake lingeniua kama ningekuwa si mkakamavu, โ€œMume wake kaja kumchukua na gari wameenda kununua shamba Bagamoyoโ€. Nikaondoka nimechanganyikiwa, nikajuwa hapa dawa yangu moja tu, nayo ni Sabrina, mtoto wa Kinyaturu pale ambapo nikipata maudhi huwa naenda kubembelezwa.

Nikatwanga mguu kwa Sabrina nae nikamfanyie ziara ya ghafla ili anipoze moyo. Nilipogonga mlango wa chumba chake akatoka mbaba wa miraba minne, akanisalimia kwa upole, โ€œSalama kaka unasemaje?โ€ Jibu likanitoka โ€œSamahani mie nilimkopesha huyu dada wa chumba hiki vitenge, nilikuja kuuliza kama ameshapata hela yanguโ€ Ziara za kushtukiza zinataka moyo wa chuma jamani

Nilichomfanyia huyu aliyenizingua nilipomuazimisha pasi

๐Ÿ™„๐Ÿ™„๐Ÿ™„๐Ÿ™„๐Ÿ™„๐Ÿ™„
Jana nimeenda kuazima pasi chumba jirani, ili ninyooshe nguo zangu, Jamaa wakaniambia nichukue nguo nikanyooshe room kwao maana hawataki pasi yao itoke.
Sasa leo amekuja mmoja wao kuazima mopper akasafishe room, nimemwambia aje adekie humu humuโ€ฆ

Jamaa ameondoka nadhani atakua ameenda kuchukua maji
๐Ÿค’๐Ÿค’๐Ÿค’

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About