Vichekesho Vya Wajanja

Baada ya kumkuta mwanamme mwingine chumbani kwake na mke wake cheki huyu anachokifanya

NAKUA(BABA) karudi kazini mwanae mdogo akamuwahi,
DOGO: Baba usiingie ndani kina jini chumbani kwenu
NAKUA: Hakuna kitu kama hicho
DOGO: Kweli baba kuna jini liko kwenye kabati lenu la nguo….

NAKUA kaingia ndani kamkuta mkewe kalala kitandani kajifunika shuka gubigubi hadi kichwani. Kaenda kwenye kabati kufungua mlango , akamkuta rafiki yake wa miaka mingi yuko uchi ndani ya kabati
NAKUA: Aise unajua we fala sana, we rafiki yangu miaka yote hiyo halafu unamtisha mwanangu eti wewe jini, hebu toka huko nenda kwenu kacheze michezo hiyo na mwanao.

Alichofanya maasai baada ya kupanda Tax

Baada ya kupanda daladala aina ya DSM kutoka Mbagala chalambe mpaka Mwenge na kulipa sh 500.Masai akachukua tax wakati wa kurudi.walipofika sasa shughuli ilikuwa hivi.

Masai: we dureva? Naulisa Ng’ombe na mbusi ipi ngali?
Dereva: Ni ng’ombe ghali Masai.
Masai: kwanini Ng’ombe ngali?
Dereva: kwa sababu ni mkubwa zaidi ya mbuzi
Masai: umepata..na mbusi na kuku ipi ngali
Dereva: ni mbuzi kwa sababu nae ni mkubwa kuliko kuku.
Masai: Umepata..
Masai: sasa me nimekwenda kule mwenge kwa ngali kubwa nikalitoa sh. 500 hii yko ndogo unasema nikupe 40,000 wewe acha wizi.. Nitakupa 250 Tu..wee acha lbia morani…!!!

Angalia huyu jamaa alivyowafanyia watu uhuni bar

Jamaa kaingia Bar;
Jamaa: Muhudumu, nipe kinywaji na mpe kila mtu humu ndani kinywaji, maana wakati napata kinywaji lazima kila mtu apate kinywaji. Haraka sana muhudumu akagawa vinywaji,

Jamaa: Muhudumu nipe supu na kila mtu humu ndani mpe supu maana ninapokunywa supu kila mtu lazima anywe supu. Watu wakapewa supu tena safari hii wakapiga makofi.
Jamaa: Muhudumu nipe bili, na kila mtu humu ndani mpe bili maana wakati nalipa bili yangu kila mtu lazima alipe yake. Zogo lilianzia hapo…….

Angalia huyu mgeni anachokifanya, wageni wengine ni hatari

Hata kama ni Mgeni this is too much.
Mwenyeji: Karibu mgeni karibu ukae,utapenda chai au soda?
Mgeni: Nipe nianze na soda wakati chai inachemka.
Mwenyeji: Utakunywa fanta au sprite?
Mgeni: Nipe fanta wakati sprite inapoa.
Mwenyeji: Utakunywa na keki au mkate?
Mgeni: Nipe keki mkate nitanywea chai ikishachemka.
Mwenyeji: Utapendelea ndiz au machungwa,
Mgeni: Nipe machungwa ndizi ntakula na wali
mchana.
Chezea mgeni ww.!!!

Ndege ya Tanzania

Kuna maprofesa 40 walipanda AIR TANZANIA ili wasafari. Kabla ndege haijaanza kuondoka, Lilipita tangazo kama ifuatavyo:

Ndugu wasafiri wote, ndege unayotarajia kusafiri nayo imetengenezwa na wanafunzi wa Kitanzania.
Baada ya tangazo maprofesa wote waliteremka isipokuwa mmoja alibaki kwenye kiti chake
Walipomuuliza ni kwanini hakuondoka akajibu kwa haraka na furaha kuwa:
Kama ndege hii imetengenezwa na watanzania, hata kuwaka haitawaka!

Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About