Vichekesho Vya Kuwaadisia
Baada ya kunitumia SMS usiku ikawa hiviβ¦.
Jana usiku kuna Jirani yangu..kanitumia text “mambo vipi?”β¦halafu tunakaa nae mtaa mmoja nikaona nikimjibu ni uharibifu wa hela nikaenda kumgongea mlango saa 7 usiku. Alipofungua nikamjibu “shwari”halafu nikarudi nyumbani kulala zangu..
Sipendagi kuchezea salio..
πππππ
Hakuna siku mbaya maishani kama hii
Hakuna siku mbaya maishan kuona mtu uliyesoma naye darasa moja, anakupita na private car,, afu we umeninginia kwenye daladala,,, tena ulikua unamzid akili πππhapo Ndo utajua kwann gunia na dunia vinatofautiana neno moja
Misemo 17 ya kuchekesha
1) gari la kuvutwa halina overtake
2) kisigino hakikakai mbele
3) wimbo wa taifa haupgwi disko
4) feni haiwashwi beach
5) mshkaki hauchomwi kwa jiko la ges
6) mganga haagiz tembele
7) hata bibi alikuwa bint
8) mke wa mtu sumu,mume wamtu maziwa
9) kipara bila pesa ni kovu
10) mbwa hanenepi migiuu
11) picha ya rais haina bodyguard
12) mjini shule kijiji tuition
13) saa ya ukutani haivaliwi mkonon
14) heshima pesa shkamoo makelele
15) ulinz pesa bastora mzgo
16) kuku ni kuku jogoo mbwembwe
17) kusoma kuelewa kukesha mbwembwe
Jinsi Baba na mtoto wanavyoweza kuwaziana
Duh! Maisha
Ile time unawaza baba angekua MO DWEJI baba ako na ye anawaza mwanangu angekua MBWANA SAMMATA
Ni shetani tu anajaribu kucheza na akili zenu
ππππ
Huyu ndo mwanamke
Akikuta PESA wakati anafua atapiga kimya kimya, sasa ngoja akute umeacha CONDOM ndo utajua kama umeoa KIPAZA SAUTI ππππππ
Ndio maana mimi nafungaga condom na hela kwa pamojaβ¦ akivikuta anachukua hela na kuishia kusonya tu.. πππππππ
Huwa sipendagi ujinga Mimi
π‘π‘π‘π‘π‘π‘
Chezea paka wewe, Angalia kilichomkuta huyu na paka wake
Jamaa alichukua paka wake na kwenda kumtupa
mbal,aliporudi nyumban alimkuta paka
amekwisharudi,jamaa alikasirika sana.
Siku ya 2
akamchukua na kwenda naye zaid ya kilometa 50
akapiga chochoro za kutosha kisha
akamtupa,akaanza safar ya kurud nyumban
baada ya muda akampigia cm mkewe.Vp mke
wangu huyo paka yupo? MKE:Ndio mume wangu
tena ametulia hapa kwan imekuaje? JAMAA:hebu
mpe cm anielekeze njia ya kurud nimepoteaπ³
ππππππππππ
Wanaume ni noma, Angalia huyu alivyomdanganya huyu π§ girlfriend wake
Jamaa kamdanganya girlfriend wake kuwa anasomea HOTEL MANAGEMENT. Siku huyo girlfriend akamkuta jamaa anaosha vyombo kwa MAMA NTILIE.
Girlfriend akamuuliza jamaa βbeby vipi mbona uko hapa?β Jamaa bila woga akajibu βNIPO FIELD.
Wanaume hatupendi ujinga sisi π π π
Mambao ya saluni ni shida, cheki kilichotokea kwa huyu
DADA alienda Salon wakati anasukwa akaingia
MKAKA mtanashati,
DADA akaamua kujaribu bahati yake.
DADA:Mambo? KAKA:Poa.
DADA:Mimi na wewe tunaweza kuongea baade?
KAKA:Kuhusu nini?
DADA:Nimekupenda nataka nikutoe out.
KAKA:Sawa ila nitamwambia nini
MKE wangu?
DADA:Aah ilo sio tatizo mdanganye tu,mwambie unakwenda kumtembelea rafiki yako hospitalini.
KAKA:Mwambie mwenyewe huyo hapo anayekusuka.
Β
Unajua nn kiliendelea?
Biashara ambayo imefeli
*TEACHER*: _nielezee biashara ambayo imefeli kutokana na uzembe
*STUDENT*: Changudoa akipata mimbaβ¦
*TEACHER*: _get Out!!!!!!!!!!!!!!_
ππ
Ameniomba nimfungulie akaunt facebook cheki nilichomjibu
Leo nimechoka zangu alafu shangazi amekuja anataka nimuunganishe facebook. Imebidi nimwambie
lazima awe na picha passport size 4 kwaajili ya kuweka profile picture, barua kutoka kwa afisa mtendaji na Atm card ya nmb bank. Alafu awe na marefa wanne ambao wamekuwa facebook for more than 3 years. Amesema
hataki tena kujiunga fb!
ππππππππππππππ
Saa ivi niko zangu nimelala naendelea kupunguza uchovu
Angalia huyu bibi alichotufanyia kwenye gari
βtulikua kwenye gari kibao ad wengne mlangon likasmimama kituo kimoja kulikua kuna bibi anataka kupandaβ
Konda- bibi twende sit kibao ata utalala
Bibi – oooh sawa mjukuu
Konda – simama tu apo wanashuka mbele
Bibi – akacheka sana tu
Konda- mbona unacheka bibi
Bibi – mjukuu hawa wote hawashuki wanakufa apo mbele
Watu- simamisha gar
Saiv bibi kabaki mwenyewe amelala sit ya nyumaπππ ππ
Angalia kilichotokea baada ya dogo kupewa ada na kuitumia kubeti
Dogo kampigia simu baba yake;
DOGO: Baba katika zile shilingi laki mbili ulizonipa
nikalipe ada nimetumia shilingi alfu 30 kubeti
BABA : Unasema nini we mpumbavu mshenzi
mkubwa? Nimekukanya mara ngapi kuhusu kubeti?
DOGO : Lakini baba
BABA : Lakini baba nini ngoja urudi utaona
ntakachofanya.
DOGO : Nilitaka kukwambia kuwa nimeshinda
shilingi milioni 3
BABA : Ndio hayo ninayosema wewe mpumbavu
sana kwanini hukutumia laki nzima kubeti? Si
ungepata pesa nyingi zaidi? Ngoja urudi niwataarifu
ndugu zako kuhusu uulivyo na akili za kuamua
haraka mwanangu mpenziβ¦
πππππππππ
Ujanja alioutumia msichana wa kazi ili apandishiwe mshahara na mama mwenye nyumba
Msichana wa kazi alitaka mama mwenye nyumba ampandishie mshaharaβ¦.. Mama mwenye nyumba akamwambia msichana ampe sababu tatu za kutaka kupandishiwa mshahara.
Msichana: Napika vizuri kuliko wewe.
Mama: Nani kakuambia?
Msichana: Baba kaniambia.
Mama: ok. Sababu ya pili?
Msichana: Napasi nguo vizuri kuliko wewe
Mama: Nani kakuambia na hili?
Msichana: Baba pia kaniambia
Mama: ok, na sababu ya tatu?
Msichana: Najitahidi kitandani kuliko wewe.
(Hapa mama kaonekana kutaka kujua zaidi na akawa tayari kujiandaa kumrukia akate kichwa cha binti mara moja)
Mama: Mume wangu kakuambia na hili pia?
Msichana: Hapana ni Shamba boy kaniambia mimi najitahidi kitandani kuliko wewe.
Mama: Tafadhali punguza sauti baba yako asisikie. Nitakupandishia mshahara wako mara tatuβ¦β¦.
Wanandoa wa Kijapani wakibishana
*Wanandoa wa Kijapan wakiwa wanabishana hadharani*
*Husband: Takamushi jiku.*
*Wife :hashi jiku mishihe*
*Husband: inamoto kushini hat a pi*
*Wife: jejeta takuna mota shinita*
*Husband: kituya sitina kutara*.
*Wife: totori yatika miniya*
_Uko busy kusoma utadhani unaelewa kijapan kuwaga serious saa zingine_
ππππππ
Cheki huyu kiherehere alivyojibiwa
Za asubuhi?
Nzur sjui huko?
Huku kwema tuu
VP si ulimaliza chuo ww?
Ndio kwani vp?
Mbona hatuoni matunda yake?
Kwani mi nlienda na miche ya mipapai au miembe au umeambiwa TIA, IFM na IAA wanakodisha Mashamba ya nyanya ????????
Hamna sio hvyo umeenda mbali kaka
Kama kilomita ngapi?
Haya yaishe bhanaβ¦
Ukome kwa kiherehere
Nitukane tuu unakumbuka kuna SKU nlkupa buku ya nauli?
Nitajie namba yako ya tgo pesa nkuwekee hyo buku
Kwani mi nimesema unilipe
Utajua mwenyewe ila nakutumia kwenye namba uliyonitext wee si umefanya ujinga mi nafanya upumbavu
Simple lyke dat Viherehere huwa tunawajbu HVOβ¦β¦ππππππππππππππππππππππππππ
Misemo ya kina dada
Misemo ya kina dada
walianza na halohalooo!
Wakaja unalo babu weee!
Ikafuata utajijuuu!
Ikafupishwa utajiJJ!
Mara ghafla kantangazeee!
Haikukaa sana kansajiriii!
Ikatoka nyingine nishiiiiida!
Unaijua iliyotoka Leo?
Heh! Heh! Heeeh! MB zenyewe 8 nikudownload unanini?
Recent Comments