Ujasiriamali: Kujitambua na Kuwa na Mafanikio Katika Maisha

Ushauri wangu kwa leo

Kuna watu wengi sana huwa wanani-challenge ninaposema kwamba ni muhimu sana mtu kuishi katika kusudi la maisha yake. Na moja kati ya hoja zao ni kwamba haya maisha ya sasa mtu akisema aanze kutafuta kusudi la maisha yake atakufa maskini. Hivyo wanaonelea ni bora kufanya chochote kitakachotokea mbele yake ilimradi mwisho wa siku anapata pesa. Yaani anachagua kuwa mtumwa wa Pesa

Kusudi la maisha ya mtu huwa halina ukomo na halibadiliki, kinachobadilika au kufikia ukomo ni malengo ya kuli-ishi kusudi hilo. Kwa hiyo unapopanga malengo yako au unapokuwa na ndoto zako ni lazima uweze kupambanua mwisho wa siku hizo ndoto au hayo malengo yanakwenda kukidhi kiu ya aina gani inayofukuta ndani yako.

Ukifanikiwa kulitambua kusudi la maisha yako na ukafanikiwa kuli-ishi kwa vitendo, ni dhahiri utakuwa maarufu kwenye mazingira yanayohusiana na maisha yako. Mazingira yanayohusiana na maisha yako yapo ndani ya kusudi la maisha yako.

Ni wakati gani mtu anaweza kusema amefanikiwa katika maisha yake? Ni pale ambapo tu mtu anapoweza kutatua tatizo fulani katika jamii; Kugundua uhitaji wa kutimizwa au kukamilishwa kwa jambo fulani katika jamii. Ukiweza kuziba pengo fulani. Ukiweza kupata ufumbuzi wa kukamilishwa kwa hilo jambo kwa faida ya jamii fulani au niseme ukiweza kutatua tatizo hilo hapo unaweza kusema umefanikiwa. Huwezi kutatua tatizo lolote katika jamii kama hujawekeza ndani yako.

Haijalishi ni jambo gani unafanya katika jamii na liko kwenye kiwango kipi ilimradi liko ndani ya mstari wa maisha yako. Kwa mfano, una kamtaji kadogo na unaamua kuanzisha genge la kuuza mahitaji madogo madogo ya nyumbani (hasa jikoni) naamini unakuwa umeanzisha kwa sababu umeona eneo hilo kuna uhitaji wa aina hiyo ya huduma. Wewe unaweza kuwa unafanya tu labda kwa sababu ya shida fulani za maisha lakini wakati huo huo moyo wako unafurahia kile unachokifanya na unajikuta kila siku unabuni mbinu mpya na mikakati wa kuboresha genge lako. Kidogo kidogo unafungua genge lingine sehemu nyingine, na lingine na lingine, nk. Mwishowe unajikuta unatamani kuwa na duka kubwa la vyakula na mahitaji mengine ya kila siku au supermarket. Ukijiona unangโ€™angโ€™ana kwenye โ€œlineโ€ moja ya shughuli (Biashara) basi tambua hilo ndio kusudi lako na ndani yako una zawadi kubwa sana ya kutoka kwa Mungu ya kuhudumia jamii kupitia uuzaji wa mahitaji ya nyumbani.

Lakini ukijiona unatanga tanga leo umefanya shughuli hii kesho umefanya shughuli ile ambazo mwisho wa siku hakuna mahali zinakutana kwa namna yoyote ile japo unapata pesa, basi wewe hujatambua kusudi la maisha yako na usipokuwa makini utakuwa mhangaikaji hadi mwisho.

Ukifanya jambo nje ya kusudi ya maisha yako hutakaa ulifurahie kamwe, litageuka kuwa mateso hata kama linakuingizia pesa nyingi. Unaweza ukawa unafanya kitu nje ya mstari wako wa maisha hata kama kinakulipa mabilioni yaani bado utakuwa kama SAMAKI ALIYETUPWA NJE YA MAJI. Samaki akiwa nje ya maji, zile dakika chache kabla hajafa huwa anahangaika sana na ukimmiminia tone moja la maji kwenye mkia utaona anavyojaribu kutaka kuogelea. Kale katone ka maji kwenye mkia wa samaki akiwa nchi kavu ni sawa na wewe unapokuwa unafanya shughuli nje ya kusudi la maisha yako inyokupa hela nyingi lakini ikatokea katika kuhangaika ukafanya ka-kitu kadogo ambako kako ndani ya kusudi la maisha yako โ€“ moyo waku unakuwa na amani sana na unafurahi sana. Lakini unajikuta huendelei kufanya hilo jambo kwa sababu halikuingizii hela nyingi kwa wakati huo ukilinganisha na lile lingine hivyo unaamua kuendelea kuishi nje ya kusudi la maisha yako ili upate mali za nje na kuunyanyasa moyo wako. Maana yake ni kwamba, kama unafanya shughuli inayokuingizia kipato iliyo nje ya kusudi la maisha yako, hutokaa uache kuhangaika kujaribisha vitu vya aina mbalimbali. Kwa sababu moyo wako hautotosheka wa kuridhika โ€“ HUWEZI KUKATA KIU YA MAJI KWA KUNYWA SODA AU JUISI JAPOKUWA VYOTE NI VIMIMINIKA. . Ndio sababu huwa napenda kusisitiza sana kupata muda kwa ajili ya maisha yako binafsi, hii inakusaidia kujitambua.

Tatizo wengi hatutaki kuanzia chini, tunapadharau huku chini lakini matajiri wakubwa duniani kama unafuatilia historia za maisha yao na jinsi walivyoanza utagundua kwamba walianza wengine wakiwa hawana kitu kabisa. Ukiwa na nidhamu ya maisha hasa kwa kufuata kanuni za maisha, kanuni za biashara/shughuli unayofanya na kanuni za maisha yako binafsi huwezi kuacha kufanikiwa. Mafanikio ni safari. Umaarufu hauji bila kuwa umefanikiwa kwenye jambo fulani hata kama ni ujinga utapata umaarufu kwa wajinga wenzako.

Mafanikio yanaanza kwa wewe kuweza kujitofautisha na maisha yako ya nyuma. Usiruhusu maisha yako ya nyuma kukuwinda na hivyo kuwa kikwazo cha maisha yako unayoyaendea. Usiishi kwa mazoea ya nyuma. Mafanikio ni pale unapoweza kujitambua na kusimama imara katika kanuni za maisha ulizojiwekea na kujitofautisha na watu wengine wote kwa sababu wewe ni wa tofauti, kila binadamu ni wa tofauti ndio mana kila mtu ana nafsi yake mwenyewe hata mkiwa mapacha mmeunganika viungo vya mwili.

MAFANIKIO YANAANZA NAWEWE

Hichi ndicho unatakiwa uwe nacho kulingana na umri wako

20 – 25 =Iwe kama ni kielimu hujafikia malengo yako,sitisha mara moja tafuta kazi/biashara ya kufanya,pigana kufa na kupona ili kama vipi urudi shule kwa pesa yako.

25 – 30 = Hakikisha uwe na angalau na SHUGHULI RASMI kama umeajiliwa au umejiajili.

30 – 35 = Uwe na angalau kama sio nyumba basi kiwanja,tena ujitahidi uwe umeoa/umeolewa kama sio kuishi nae,tena si mbaya ukawa umeshatengeneza familia,kwa maana ya kuwa na watoto kama mungu kakuwezesha.

35 – 40 = Ni umri wa kama kiwanja kiwe kimejengwa, na kama ni tayari basi nenda step nyingine ya kumiliki kama ni Gari au kuongeza nyumba na hakikisha vinaenda sambamba na ongezeko la familia.

40 – 45 = Ni umri wa masahihisho, kama hukuwahi kununua kiwanja au kujenga basi hapa pambana afe kipa afe beki,kama umegundua mkeo hazai fanya mchakato kwingine kama ni mwanaume na kama mwanamke umegundua mumeo ndio mwenye shida basi tafuta nje umletee mtoto. Kifupi ni umri wa masahihisho.Ila kwa wale ambao wameenda vizuri huko nyuma basi hapa kama ni wale watoto wapo kwenye level tofauti za elimu,kwahiyo ni muda wa kuwawekea malengo ya kimasomo watoto wao.

45 -50 = Kwa yule ambaye hakukosea huko nyuma,basi umri huu ni wa kuanza kuwatengenezea mazingira watoto wako,kama ni shuguli zako ni kuanza kuwahusisha,huku wewe ukijiweka pembeni taratibu na kuangalia fulsa za umri wako. Lakini kwa wale waliokosea hapa ni kupitia zile hatua za 35 -40.

50 – 60 = Ni kujiandaa na maisha mapya ya kustaafu au kujiweka mbali na shughuli za shulba.Na kama ulijitenga na msikiti/kanisa huu ndio muda wako.

60 – 70 = kula matunda yako huku ukiangalia misingi ya wanao inaendaje.

70 – 80 = kula matunda.

80 – n.k= unamsikilizia Mungu anasemaje

JITAMBUE : Maisha yako ya kesho hayalingani na maisha yako ya jana, Anza sasa

THERE IS NO FUTURE IN THE PAST.** Ukitaka kufanikiwa usiangalie nyuma yako kunanini na ulishindwa mara ngapi. Siku zote kukaa Chini nakuanza kujuta kwa makosa uliofanya uko nyuma nikupoteza muda, huo muda Utumie kwa kupanga ya kesho.

Bahati nzuri Mungu alitujalia kusahau, ivyo siku zote sahau ya nyuma na waza yale ya mbele yako.

Maisha bora ya mbele hayawezi kuja kama akili yako imebeba kushindwa kwa nyuma.

Binadamu yeyote anayeweza kupoteza muda wake wa leo kwa kulaumu mabaya ya jana, kesho atapoteza muda akilaumu mabaya ya leo.

Tambua ya kuwa, “hakuna awezaye kurudi nyuma na kuanza upya, bali waweza kuanza leo na kutengeneza maisha yako ya kesho”

Kadri unavyofikiria ya nyuma ndivyo unavyochelewa kufika mbele zaidi. Penda zaidi ndoto yako ya kesho kuliko historia yako ya jana,maana hatima yako siku zote iko mbele na sio nyuma.

Siku zote utashindwa kwa kuendekeza mambo yaliopitwa na wakati maana utakuwa unatumia ujuzi uliopitwa na wakati.

“Habari njema ya siku ni leo, na siku nzuri yako ni ya kesho “

Ukiona umesononeka kwa maisha kuwa magumu jua unaumia kwaajili ya maisha yako ya nyuma, maana unawaza jinsi ulivyo shindwa kulipa kodi ya nyumba,ulivyoshindwa kulipa umeme, maji, ada za watoto na ulivyoshindwa kuendesha biashara yako au ulivyoshindwa kuitetea ajira yako. Usipoteze Muda wako kwa kuwaza yaliopita badala yake waza kesho yako itakuwaje.

Waswahili wanasema yaliopita si ndwele, tugange yajayo. Huwezi kubadilisha jana, Bali waweza kubadilisha kesho yako kwa kufanya maamuzi leo.

Usipoteze Muda kwa kugeuza shingo yako kutazama ya nyuma, utajikuta unadumbukia katika shimo la maisha magumu.

“You can’t have a better tomorrow if you are thinking about yesterday all the time “

Maisha yako ya kesho hayalingani na maisha yako ya jana. Anza sasa.

JITAMBUE: Kipi hauna kati ya pesa na muda?

Soma kidogo hapa.. Kuna watu wa aina NNE tunapoongelea pesa na muda.

1. WANA MUDA MWINGI ILA HAWANA PESA

Watu ambao hawana pesa ila wana muda wa bwerere. Hawajui thamani ya muda. Hawa ndo wale ambao hawajui cha kufanya. Anaamka mpaka analala usiku hana specific timetable. Unaweza kumkuta anaenda dukani ukamwambia nisindikize saluni na akakubali. Yupo yupo tu. Unaweza kuta ameingia Facebook hajui hata kwa mini. Basi tu kwa sababu ana bando. Akiperuzi akaona mahali wanaongelea mpira yumo. Akiscroll post za chini akakuta kuna mtu kapost kuhusu UKAWA yumo. Akikuta kuna mtu kapost mtu ana uvimbe mkuuubwa watu wameambiwa wacomment AMEN na yeye huyo anacomment AMEN. Akikuta watu wanaongelea TRUMP na yeye anaingia kucomment. Kundi hili ni kundi lenye watu wengi mno. Watu wa aina hii kufanikiwa ni bahati nasibu. Labda kwa bahati tu akutane na post nzuri kama hii na post zingine nzuri huenda ikamsaidia. Otherwise hawa ndo hawaelewi maisha yanaenda wapi maana hawana kitu fulani specific wanachofanya. Wakisikia tu kuna kitu kiko kama dili hivi wanaenda. Wakikuta kumbe kinahitaji bidii na kujituma wanaondoka. Wanataka maisha mazuri yaje tu yenyewe.

2. WANA PESA ILA HAWANA MUDA

Hili ni kundi la watu wenye shughuli fulani ya kiuchumi. Labda ameajiriwa au amejiajiri. Wako busy kweli kweli. Na ukweli pesa inaonekana. Hawa huwezi kumwambia njoo tuonane akaja hapo hapo. Huyu lazima apange kwanza ratiba zake. Maana yupo busy. Au lazima aombe ruhusa kazini maana hana uhuru na muda wake. Muda wake kamuuzia mtu (mwajiri). Au labda atoroke ndo anaweza kupata muda wa kufanya mambo yake binafsi. Au asubiri weekend ambapo kila ratiba itategemea siku hizo mbili, kama ni ibada, usafi, kutembelea wagonjwa au ndugu kwenda mahali kuona labda kiwanja kinauzwa au kuona ujenzi au mradi wake unaendeleaje nk. Mara nyingi watu wa kundi hili hushindwa kufanya vitu vingi vinavyohusu maendeleo yako binafsi mfano kujisomea, kuhudhuria semina zinazofundisha mambo yanayoweza kuwa na manufaa kwake nk. Sababu ana ratiba iliyobana. Ukiwa na sherehe ukamwomba mchango hashindwi kukuchangia angalau chochote kile lakini muda wa kuja kujumuika na wewe ni vigumu akaupata.
Hili ni kundi ambalo kuna watu wanaitwa MIDDLE CLASS people. Watu wa maisha ya kati. Mambo yako si mabaya sana lakini si kwamba ni mazuri. Wasomi wengi na watafutaji wengi wapo hapa. Afu ndo wanahisi wanajua kila kitu. Na wengi wao huishia kupata changamoto za kifedha na kiafya ukubwani au uzeeni kama stress na maradhi mbali mbali nk. Sababu ya kutokuwa na muda hata wa kuangalia wa kuinvest na kujifunza biashara au ujasiriamali mapema wala kujishughulisha na afya zao, mazoezi, kupumzika vizuri nk kwa kuwa walikuwa busy siku zote. Maisha ya watu hawa middle class mwishoni huja kuwa magumu kwa kuwa hata kuwa na muda na majirani tu ilikuwa ishu. Kwa kuwa wengi wana magari (mengi ni mkopo. Wengine gari la kazini) na kwa kuwa wanaweza kulipa kodi ya nyumba au hata kupata kakiwanja na kuanza kujenga huko Malamba Mawili basi wanaridhika. Hawawezi kuota kumiliki nyumba Masaki au kununua kiwanja Upanga. Kama upo kundi hili lazima uanze kutafuta mbinu mbali mbali za kuyakabili maisha vizuri siku za usoni. Waangalie wastaafu ambao walikuwa busy zamani. Saivi utasikia mgongo, miguu, macho nk vinasumbua. Hawa middle class people ndo ukimkuta social media wengi wao wako critical kwa kila kitu. Maana haoni kama ana shida yoyote.

3. HAWANA MUDA WALA HAWANA PESA

Ulishasikia mtu anaambiwa “busy for nothing”? Ni kitu kama hicho. Yani mtu unakuta labda ni kibarua tu mahali anatumwa kazi asubuhi mpaka jioni. Labda ameajiriwa kazi ya ulinzi, au gereji, au kwenye mradi wa ujenzi anabeba zege au kupaka rangi. Hashindi njaa ni kweli lakini ukweli hana hela. Wala hatamani kuendelea kuwa hivyo. Kuamka alfajiri kulala saa tano usiku. Hela anayopata inatosha kula kwa mama ntilie tu na nauli. Basi. Hawezi kuota hata gari. Hata ya mkopo. Maana hata hakopesheki. Huyu hata muda wa Facebook ni nadra akiingia ni kupitisha macho afu anatoka. Au hata simu ya Facebook hana.

4. WANA MUDA NA WANA PESA

Hapa ndo utakuta wale ambao hana tena shida ya pesa. Pesa iko. Hana tena shida ya muda. Akihitaji kwenda mahali haombi ruhusa wala kuaga mtu labda kumuaga mwenza wake tu. Anaweza kusikia kuna shamba linauzwa mahali na hahitaji kutafuta hela tena ili akalinunue bali anaanza michakato ya kisheria pale pale kununua kama amelipenda. Kuna siku nilienda Morocco Square hapo Kinondoni jirani na Airtel kuna Apartments zinajengwa nikaonana na watu wa NHC waliokuwa wanakagua ujenzi unaendeleaje. Nikawauliza hizo apartments zinauzwaje wakasema kuna za milioni 600 na za milioni 800. Na unatakiwa kulipa cash 10% (yaani aidha milioni 60 au 80 cash) halafu inayobakia unaweza kuimalizia ndani ya miezi 12. Na kuna watanzania kadhaa wamenunua tena kwa hela halali. Hawa wako kundi hili hapa. Hela ipo. Muda upo. Kuna watu walienda kutembea Marekani kibiashara walipokuwa njiani kurudi wakapita mahalinchi nyingine wakakuta kuna mnada wa nyumba kwenye nchi hiyo. Hawakujiuliza mara mbili wakanunua. Kuna wazee fulani wana mtoto wao alikuwa akisoma Canada. Alipograduate wakamuuliza unataka kuishi wapi akasema huku huku Canada wakamnunulia nyumba Canada. Ukisikia hivyo unaanza kuwaza ni mafisadi. Mawazo yako ninkuwa bila ufisadi watu hawanunui nyumba Canada. Kwa taarifa yako Hawa siyo waajiriwa serikalini wala popote ni wafanya biashara.. Kundi la watu kwenye pesa. Na muda. Wanaweza kuamua kesho wakaenda kutembea visiwa vya Comoros. Watu wanaoishi kundi hili wana discipline kubwa ya maisha. Na watu wengi wanatamani kufika kundi hili. Lakini HAWANA discipline ya kujifunza tabia zinazoweza kukufikisha huko.

Swali muhimu tu la kujiuliza tu ni kuwa je, wewe upo kundi lipi.

Una muda mwingi lakini huna hela? = FUKARA

Una hela nyingi lakini huna muda? = MIDDLE CLASS

Huna muda wala huna hela.. Vijisenti unavyopata vinaishia nauli kula kodi ya nyumba nk? = MASKINI

Au una muda mwingi na hela siyo shida tena? = TAJIRI

Wewe ni mshindi: Mambo yakuzingatia ili uweze kushinda chochote katika maisha

Mshindi ni mtu aliyeshinda, Hivyo wewe ni mshindi kwa kuwa umeshinda, kuwa hai leo ni ushindi, kuwa na Mungu mpaka sasa huo ni Ushindi, kuweza kujifunza semina na kufuatilia mafundisho kama haya wewe ni mshindi.
Ebu jiulize ni watu wangapi ulikuwa unawafahamu leo hawapo duniani? Wewe umeshinda Mungu kakuweka duniani ili uendelee kushinda.

KWANINI WEWE NI MSHINDI

Wanasayansi wanasema wakati ujauzito wa binadamu unatungwa kunakua na mamilioni ya mbegu za kiume ambazo zinakua zinatoka ili kwenda kurutubisha yai ili azaliwe mtoto. Na kwa kawaida inatakiwa mbegu moja tu kati ya hizo milioni. Hivyo basi wewe ni mmoja wa pekee kati ya mbegu za kiume millioni moja zilizotoka siku ile ulipotungwa tumboni mwa mama yako.

JIPIGIE MAKOFI SEMA MIMI NI MSHINDI

Kabla hujazaliwa ingewezekana ujauzito wako ukaharibika, Ingewezekana labda ujauzito wako ungetolewa, lakini haikuwa hivyo ukatoka salama. Na ulipozaliwa kuna watoto wengi tunasikia wanafariki wakati wa kujifungua lakini hukuwa wewe. Tunasikia pia magonjwa mbalimbali yanaua watoto lakini hukuwa wewe. Umeyashinda yote hayo hivyo wewe ni MSHINDI usijidharau kwa hali uliyonayo sasa wewe ni mshindi. Kuwepo kwako hai leo ni kwa sababu maalumu.

Umekwenda shule, umekua ,wako waliokufa kwa ajali lakini wewe upo hai bado Mungu ana kusudi na wewe.

Usijidharau nipo hapa Leo kukonyesha jinsi wewe ulivyo wa thamani mbele za Mungu. Wako wenzako wamepitia hatari ngumu na mateso hadi wakafikia kujinyonga, kunywa sumu, kujiua, lakini wewe upo hai. Wewe ni mshindi.
Upo duniani sasa ili uendelee kushinda.

Umezaliwa na uwezo wa kipekee sana ndani yako unaokuwezesha wewe kushinda kila siku na ukiweza kuutambua uwezo huo ushindi ni lazima. Kabla ya kutambua uwezo huo lazima utambue kwanini wewe umezaliwa! Ulizaliwa kwa kusudi gani? Ili uelewe kwanini Mungu amekuacha hai mpaka sasa ni ili ulitimize kusudi lake.

Hayo Yote niliyokwambia yanaweza yasiwe na maana sana kwasababu yameshapita sasa nakwenda kuzungumza namna ya kuendelea kutengeneza ushindi mwingine kila siku kupitia kwenye kusudi lako!

UFANYEJE UENDELEE KUSHINDA?

Haijalishi hali gani unapitia sasa upo hai leo kwa sababu maalumu na ni ili uweze kuendelea kua mshindi kwa kuifanya dunia kuwa mahali bora zaidi kuliko ulivyoikuta. Hii dunia haikua hivi miaka 10 iliyopita ni watu wachache wametumia uwezo Mungu aliweka ndani yao na kuvumbua mambo mengi na ya ajabu tunayoyaona sasa. Ni nafasi yako wewe kutumia nafasi hii ya kuwa hai leo kuifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi naamini wewe una nafasi kubwa sana.

“You were born to win, but to be a winner, you must plan to win, prepare to win, and expect to win.” – Zig Ziglar

Zig Ziglar anasema ulizaliwa kushinda kama tulivyoelezana hapo awali, lakini ili uendelee kua mshindi, lazima ujipange kushinda, ujiandae kushinda, na utarajie kishinda

Timu ya mpira inapochukua kombe sio mwisho wa mchezo wanakwenda kujinoa zaidi ili waweze kushinda tena na tena. Wewe unajiandaa vipi na kuendelea kushinda?
Vipo Vitu vichache vya Muhimu unatakiwa uwe unavifanya ili kushinda kila siku.

(a)Jitambue.

Ili uendelee kushinda kila siku lazima ujitambue wewe ni nani! Najua unatambua kwamba wewe ni jinsia gani. Lakini kujua hivyo tu haitoshi.
Kwanini ulizaliwa mwanamke/mwanaume, mtu mweusi tena Tanzania na sio nchi nyingine?
Ukitambua hivyo lazima ukubali na uanze kufanyia kazi na uendelee kushinda kila siku, Tambua kusudi la wewe kuzaliwa na kwanini ukazaliwa kipindi hiki na sio wakati mwingine.

(b) Usiangalie nyuma.

Haijalishi umepitia maisha ya namna gani umezaliwa kwenye mazingira ya namna gani, wewe jua kusudi la Mungu ndani yako na ulifanyie kazi, haijalishi jana umefanya vibaya kiasi gani, haijalishi pia ulifanya vizuri kiasi gani angalia mbele angalia kule unakokwenda.
Kule unakokwenda kuna maana zaidi ya unakotokea. Pia huwezi kwenda mbele huku umeangalia nyuma utajikwaa. Haijalishi ulikosea mara ngapi, umeua, umeachwa, umefeli, huna kazi, umefukuzwa, una madeni, usiyaangalie hayo.
Kama umeshajitambua liangalie kusudi na songa mbele.
“Adui wa mafanikio yako ya leo ni mafanikio yako ya jana, Adui wa mafanikio yako ya kesho ni mafanikio ya leo”

(c) Jua unapokwenda.

Hakikisha umetambua unapokwenda kama tayari umeshajitambua na umeacha kuangalia nyuma hakikisha sasa unajua unapoelekea. Kuwa na Maono, ndoto kubwa na kua na viongozi wanaokufundisha uelekee kwenye maono yako.Ukijua unapokwenda huwezi kupotea, Ukijua unapokwenda huwezi kufanya mambo ya ajabu ajabu, ukijua unapokwenda huwezi kuchukuliwa na kila mtu hovyo hovyo, Ukijua unapokwenda lazima utajisitiri, Biblia inasema pasipo maono watu huacha kujizuia.
Kama huna maono kulijua kusudi hakuna maana, kama huna maono utadondoka kila siku.

(d)Jifunze Kila Siku.

Umeshajitambua, ukaacha kuangalia nyuma, ukajua unapokwenda kwa kuwa na maono na ndoto kubwa, sasa huwezi kuvifikia vyote hivyo bila kujifunza. Huwezi kwenda kuwa mtu mkuu kwa ufahamu huo ulio nao sasa hivi, Inawezekana umesoma vyuoni una Degree au Masters lakini hiyo haionyeshi vyema kwamba wewe umesoma unajua kila kitu unaweza kuyabeba maono makubwa.
Soma vitabu vya uongozi, vitabu vya kuhamasiha jiendeleze binafsi, Jifunze kwa kupitia watu unaokutana nao kila siku, Jiunge na magroup kama ya whatsapp na ujifunze Makala kama hizi.

USHINDI UTAKUA WAKO KILA SIKU

“adui mkubwa wa kujifunza ni kujua” unapojiona wewe unajua kila kitu umesoma sana huwezi kujifunza kwa mtu mwingine alieko chini yako unakosea sana na hutaweza kufika popote kubali kujifunza kwa kila mtu haijalishi ni nani. Ushindi ni wako Na naamini kabisa kupitia makala hii kutatoka watu wakubwa sana katika Historia ya nchi hii na dunia.

(e) Jitengenezee tabia za Kushinda.

Unajitengenezeaje Tabia za kushinda? Jiambie maneno ya kushinda,huonagi wachezaji huwa wakiwa kwenye mazoezi wanashangilia kama vile tayari wana ushindi?
Jiambie maneno ya kujihamasisha mwenyewe. Mimi ni mshindi nimezaliwa kushinda, Siziogopi changamoto, mimi ni wa thamani, Unaweza kuandika maneno mazuri ya kukuhamasisha ukutani ili unapolala na uamkapo asubuhi uyaone na kuyasoma.
Washindi wana amka mapema. Washindi wanajua ndoto zao vizuri. Hakikisha kile unachokitaka kimekaa kwenye akili yako yaani hata ukishtuliwa usingizini leo unakuwa na uwezo wa kukisema.
Anza kufanyia kazi yale unayojifunza kila siku.

(F) Usiogope Kushindwa.

Usiziangalie changamoto na kukata tamaa. Zitumie changamoto kama shule jifunze kwa kupitia hizo na utaendelea kushinda kila siku.
Changamoto zinakuja kwasababu njia unayoiendea ni nyembamba hujawahi kuipita kabla. Na pia bado uwezo wako haujakuwa vya kutosha tumia changamoto kama njia za kukuza uwezo wako ili siku moja ufikie kule unakotaka ukiwa imara na usitetereke.

(g) Fanya vitu unavyoviogopa.

Usikubali kila siku unafanya vitu vile vile. Hakikisha kila siku kuna kitu kipya umefanya. Hii itakuongezea wewe uwezo wa kushinda na ujasiri wa kupita sehemu za mbele zaidi.
Hakikisha inapokua jioni umeangalia ni vitu gani vipya umefanya. Ni hatua gani umepiga katika malengo yako. Ni kitu gani kipya umejifunza. Usikubali unakutana na mtu anakupita hivi .Hujaongeza kitu chochote kwenye ufahamu wako au yeye hajajifunza kitu kutoka kwako. Wewe una kitu cha pekee sana ndani yako ambacho Mungu kakiweka kwa ajili ya wengine.

(h) Fanya na fuatilia zaidi vitu vinavyoongeza thamani kwako, kwa wengine, kwenye roho yako, kwenye mahusiano yako, kwenye maono na malengo yako na kwenye kusudi lako.

Ukifanya nje ya hapo utakua unapoteza muda bure. usikubali kupoteza siku yako bure. Kumbuka tumepewa masaa 24 tu ya kuishi yatumie vyema masaa hayo.

UKIWEZA KUFUATILIA HAYA USHINDI NI WAKO KILA SIKU, NI MAMBO MADOGO MADOGO UTAPITIA TU NA YANAREKEBIKA.

“Hakuna kiumbe kingine kitakachozaliwa tena kifikiri kama wewe, kitembee kama wewe, kiongee kama wewe, Hakuna tena, wewe ni wa pekee sana usijidharau tumia upekee huo kufanya mambo makubwa katika dunia hii usikubali kuondoka hivi hivi.”

โ€œHamu Yangu Ni Kuona Unafanikiwaโ€.

Mambo ya kufanya mwezi Disemba

Ikiwa leo ni tarehe **1/12 huwezi amini kuwa hakuna tarehe 1 nyingine tutakayoiona ya mwaka huu hivyo sichelei kusema kuwa mwaka umeisha .Lakini mwaka unaishaje??? pengine hili ndilo swali gumu na la muhimu la kujiuliza .Je, Mwaka unaisha ukiwa umefanya nini cha kujipongeza??? .Je mwaka unakaribia kuisha maarifa yako yakiwa yameongozeka kwa kiasi gani???.Haya ni maswali muhimu sana unavyooanza kufikiria juu ya sherehe za mwisho wa mwaka.

Watu waliopiga hatua katika fikra โ€“ yaani, wale waliofanikiwa kutimiza malengo na mipango waliyojiwekea โ€“ wanajikuta katika kipindi cha kipekee ifikapo mwezi huu. Ni wakati ambao wanapaswa kuchukua muda na kutafakari kwa kina juu ya safari yao ya mwaka uliopita. Huu si tu wakati wa kuzingatia mafanikio na mafunzo, bali pia ni kipindi cha kulinganisha matarajio yaliyokuwa yamewekwa dhidi ya yale yaliyotimia.

Kurudi kwenye malengo yaliyowekwa hapo awali ni zoezi la muhimu linaloleta tafakuri juu ya uendelevu na ufanisi wa mikakati iliyotumika. Watu hawa wanaweza kujiuliza maswali kama, je, malengo yalikuwa yanatekelezeka? Je, walikutana na changamoto gani, na walizishinda vipi? Changamoto hizi zinaweza kuwa za ndani kama vile kutunza motisha, au za nje kama vile mabadiliko ya kiuchumi na kijamii yaliyokuwa yameshuhudiwa.

Inawezekana pia walikuwa na malengo ambayo hayakutimia. Katika hili, kuna fursa ya kujifunza na kuchukua hatua za marekebisho. Mwisho wa mwaka ni muda mwafaka wa kutathmini upya na kuweka mikakati mipya, kuondoa yaliyopitwa na wakati na kuja na mawazo mapya yatakayowasukuma mbele zaidi. Uchambuzi wa kina utawasaidia kuweka malengo yanayoweza kutekelezeka kwa mwaka unaofuata pamoja na kutengeneza mpango kazi madhubuti ambao utawaongoza katika hatua zao zijazo.

Kwa kuangalia nyuma na kufanya tathmini yenye unyoofu, waliopiga hatua katika fikra wanaweza kupata msingi imara wa kujenga juu yake. Wanaweza kujitathmini na kujipanga upya, kuchukua mwelekeo wenye nguvu na mpya ambao utawawezesha kutimiza malengo yao yaliyosasishwa na yaliyo wazi zaidi. Kila hatua, kila mafanikio, kila funzo, yote huchangia katika safari yao ya kipekee ya maendeleo binafsi na ya kitaaluma.

Leo nataka nikuekeze mambo muhimu ya kufanya mwezi huu pamoja na kuwa unawaza sikukuu na kusafiri kwenda kwenu .Mambo haya unaweza kuwa hujawahi kufanya lakini ni muhimu sana ukafanya mwaka huu ili mwakani tuone mabadiliko .Mambo hayo ni pamoja na ;

1.Fanya Tathimini (Evaluation)

Tathimini ni kipimo kinachoonesha kushindwa kwako na kufanikiwa kwako .Mwezi huu ni mwezi wa kukaa chini na kurejea kwenye malengo na mikakati uliyokuwa umejiwekea na kuona ni kwa jinsi gani umefanikiwa .Ainisha mambo uliyofanikiwa na ambayo hujafanikiwa .Kwa yale uliyofanikiwa jipongeze kwa kufanikiwa kwa yale ambayo hujafanikiwa jiulize kwanini hayajafanikiwa ili yakupe mbinu na hatua mpya mwaka ujao.

Andika kwa mtindo huu;

SEHEMU A:MAMBO NILIYOFANIKIWA HUU

-Mwaka huu nilifanikiwa kuwapata marafiki wazuri wanaounga mkono maono yangu
-Mwaka huu nilifanikiwa kuanzisha biashara ya genge
-Mwaka huu nilifanikiwa kusoma vitabu viwili

*Jitihidi sana kujipongeza kwa yale uliyofanikiwa na hii ni tabia ya watu waliofanikiwa .Usione umefanya madogo lahasha.*

SEHEMU B:MAMBO AMBAYO SIKUFANIKIWA mwaka huu

-Sikufanikiwa kuhudhuria semina hata moja ya ujasiriamali
-Sikufanikiwa kuboresha ofisi

Kwa yale ambayo hukufanikiwa jiulize kwanini hukufanikisha utagundua wewe ndiye sababu kubwa ya kutoyafanikisha .

2.Anza kuandaa malengo ya mwaka ujao (GOAL SETTING)

_Pasipo maono, watu huacha kujizuia_
~(Biblia)

Ndiyo bila malengo hutafika na utafanya kila kitu bila mpangilio .Huu ndio mwezi kwako ambao unapaswa kuandaa malengo ya mwaka ujao haijalishi hukuwahi kuweka malengo toka unazaliwa .Najua malengo yako yalikuwa yanakaa kichwani mwaka huu amua kuandika kwenye notebook Nzuri .Andika kwa ujasiri mkubwa sana .Malengo yako yafuate kanuni za malengo(yapimike,yawe na ukomo,yawe mahususi na yakufikika ).

Andika kwa mfano huu;

-Kufikia Mei  nitakuwa nimefuga kuku watatu hata kama nyumba yangu ni ndogo .

-Kufikia Agosti   nitakuwa nimehudhuria semina 2 za ujasiriamali

Ukiandika kwa mfumo huo itakusaidia kuyafikia malengo yako maana yamefuata kanuni za malengo.

3. Andaa Bajeti ya mwaka  (Budgeting)

Hii ni sehemu ambayo inaleta shida sana .Na hii ni kwa sababu hata wazazi wetu wametulea bila kutufundisha bajeti.Masomo ya darasani wengi hatufundishwi kuishi kwa bajeti .Lakini Tusilaumu sana kutofundishwa maana lawama ni tabia ya kimaskini tuamue mwakani 2017 kuishi na kutembea na bajeti

Mara nyingi tukiulizwa hela zetu zinaenda wapi huwa hatuna majibu sahihi .Hii ni kwasababu hatuna bajeti .Kwanini bajeti??? .Bajeti hutusaidia kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na yaliyo nje ya bajeti .Bila bajeti sehemu ya kutembea kwa mguu utapanda bodaboda .Bila bajeti utanunua simu ya laki saba wakati unasema huna mtaji wa laki sita.Bajeti itaamua uchangie harusi na kitchen party ngapi kwa mwaka.

Ndiyo lazima tubadilike hata mimi nimeamua hivyo mwaka ujao.Kama una familia kaa na mke wako tengeneza bajeti ya mwaka.Kuna vitu vinaweza kujitokeza njiani na hivyo kumbuka kuweka dharura .

Bajeti iliyopangwa kwa mwaka ujao ni kama ramani inayoonesha njia ya malengo na maelekezo ya kifedha ambayo shirika au mtu binafsi anapaswa kufuata. Inatoa muhtasari wa kina kuhusu matarajio ya mapato na matumizi, na hivyo kumwezesha mtu au shirika kupanga kwa ufanisi zaidi juu ya rasilimali zake. Kuweza kwenda sambamba na bajeti hii, mtu au shirika linahitaji kuelewa vizuri vipaumbele vyake na kuweka mipango thabiti kwa kila sehemu ya matumizi au uwekezaji.

Katika kuhakikisha ufanisi, ni muhimu kwa shirika kuwekeza nguvu katika upangaji wa bajeti ulio sahihi, utafiti wa masoko ili kufahamu mwenendo wa kiuchumi unaoweza kuathiri mapato na matumizi, pamoja na uboreshaji wa mbinu za usimamizi wa fedha. Ufuatiliaji wa mara kwa mara wa bajeti na utathminini wa maendeleo halisi ikilinganishwa na yale yaliyopangwa ni muhimu sana. Nguvu katika kufuatilia na kurekebisha mtiririko wa bajeti inaweza kumaanisha tofauti kati ya kufikia malengo ya kifedha au kukabiliana na upungufu.

Kuwekeza nguvu inamaanisha pia kuwa na nidhamu na ufuatiliaji madhubuti wa matumizi ya kila siku, kujifunza kutokana na takwimu na ripoti za awali za fedha, na kujitayarisha kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza. Mwisho, uwekezaji katika mafunzo kwa wafanyakazi wanaoshughulikia fedha na matumizi inaweza kuongeza ufanisi na kuimarisha uzingatiaji wa bajeti iliyowekwa.

Ilinde ndoto yako

Ndoto ni nini?

Ndoto ni zile ndoto za kiuhalisia ambazo mtu anaweza kuwa nazo akiwa macho na anatumia mawazo yake kutengeneza au kuunda picha ya maisha anayotamani kuishi siku zijazo. Hizi si ndoto ambazo mtu anaota usiku akiwa usingizini, bali ni matakwa ya dhati ambayo yanamfanya mtu ajizatiti na kutia bidii katika mambo anayofanya ili kuyafikia malengo yake.

Kila mtu ana ndoto tofauti ambazo anatamani kuzifikia, na mara nyingi ndoto hizi huwa zinaongoza maisha yake na kumpa dira na mtazamo wa maisha yake ya baadaye. Ndoto hizi zinaweza kuwa kubwa au ndogo, na zinaathiri jinsi mtu anavyochagua kuishi maisha yake ya kila siku, jinsi anavyofanya maamuzi, na hata jinsi anavyoingiliana na watu wengine.

Kwa mfano, mtu mwenye ndoto ya kuwa Rais atajituma katika masuala ya uongozi, atajifunza mambo mbalimbali yanayohusiana na siasa na uongozi wa jamii au nchi. Ataweza pia kujihusisha na harakati mbalimbali za kijamii au kisiasa ili kujenga umaarufu na kuwa na uwezo wa kufikia ndoto yake.

Kwa upande mwingine, mtu anayetamani kuwa mwimbaji bora atajikita katika kuendeleza kipaji chake cha uimbaji, kuhudhuria mashindano ya muziki, na pengine atajitahidi kuwa karibu na watu wengine waliofanikiwa katika tasnia hiyo ili ajifunze mbinu za kufanikiwa.

Wale wenye ndoto za kumiliki vitu kama nyumba za kifahari, magari, au kuwa bilionea, mara nyingi wanajikuta wakihusika katika kufanya kazi kwa juhudi zaidi, kujifunza na kutafuta taarifa juu ya uwekezaji, na kutafuta njia bora za kukuza uchumi wao binafsi.

Ndoto za kutembelea nchi fulani zinaweza kumfanya mtu aweke akiba ya pesa, ajifunze kuhusu tamaduni mbalimbali, na hata kujifunza lugha tofauti ili kujiandaa kwa safari yake. Kwa kufanya hivi, mtu huyo anajiweka katika nafasi nzuri ya kufikia ndoto yake na kuifanya iwe halisi.

Kwa ujumla, ndoto za mchana ni muhimu sana katika kuhamasisha na kutoa motisha kwa mtu kufikia mafanikio makubwa maishani. Zinamfanya mtu kuwa na malengo, azimio la dhati, na muelekeo wa wapi anapenda maisha yake yawe siku za usoni. Ndoto hizi zinapoambatana na mipango mizuri na jitihada za makusudi, mara nyingi huwa na matokeo chanya na kutimia kwa matarajio ya mtu.

Zote hizo ni ndoto ambazo kila mmoja alikua nazo huenda ni kipindi anakua au hata sasa bado anayo.
Kwa bahati mbaya sana watu wengi wamekuwa na ndoto kubwa sana wakiwa wadogo na kuzipoteza walipoanza kuingia kwenye uhalisia wa maisha.

VITU VINAVYOWEZA KUIPOTEZA NDOTO YAKO.

Ugumu wa Maisha.

Maisha yanavyozidi kubadilika na kuwa magumu ndipo baadhi ya watu huanza kuasahu vile vitu ambavyo walikua wanatamani waje kuwa navyo. Maisha yanapokuwa magumu sana wengi huona haiwezekani tena wao kufikia ndoto zao hivyo kukata tamaa kabisa na kuamua kuwa na maisha ya kawaida.
Mtu anaweza kujitazama vile alivyo na kuona yeye hafananii kabisa kuja kuwa Rais wa nchi hii labda kutokana na familia aliyotokea au maisha yanayoendelea sasa hivi.
Nakuomba kama unapitia hali hiyo anza kuikataa kabisa ili usije kupotea.

Marafiki wabaya.

Marafiki na watu unaokuwa nao mara kwa mara wanaweza kuwa sababu kubwa sana kukupoteza kabisa na kukufanya wewe uache kupigania ndoto yako.
Ndoto yako ni ya thamani sana ndio maana inapata upinzani.
Ndio maana utaambiwa haiwezekani. Ndio maana watakucheka ukiwaambia wewe unataka kuwa Rais wa nchi hii au unataka kua Bilionea.
Mara zote watu wanakuhukumu kutokana na hali uliyonayo sasa hivi.
Unaweza kuachwa na Mpenzi wako umpendaye kwa sababu tu yeye anaangalia maisha uliyonayo sasa hivi na hata ukimueleza ndoto zako haamini kutokana na hali yako ya maisha uliyonayo sasa.

Ufanyeje?

Kaa nao mbali wale watu ambao hawana ndoto kama za kwako. Kaa mbali na watu ambao wanafikiri kama kuku. Yaani wao wamejiona kwamba ni maskini na haiwezekani kuwa tajiri labda kuiba tu. Inawezekana ni watu wako wa karibu sana labda kaka, dada, wazazi.
Ufanyeje?
Usikubali kuwasikiliza weka pamba sikioni. Mimi kuna mtu aliniambiaga hizo ni ndoto za mchana haziwezi kutokea kamwe lakini sijakata tamaa naendelea kufanyia kazi ndoto zangu.

UNALINDAJE NDOTO YAKO?

Iandike.

Kama unasema una ndoto lakini bado ipo kichwani bado hujaelewa maana yake. Katafute Notebook nzuri sana ya gharama Huwezi kuandika ndoto ya kuwa Bilionae kwenye note book ya elfu mbili aisee.
Tafuta notebook ya Gharama hata ya 20,000 ili uweze kuitunza vizuri. Andika kila kitu unachokitaka kwenye dunia hii. Hakikisha umeandika kila Kitu na usiache hata kimoja.
Hii ni njia ya kwanza ya kuilinda ndoto yako. Nikikutana na wewe sehemu Uniambie au unionyeshe kilipo kitabu chako cha ndoto. Andika ni Jinsi gani unaweza kupata vile vitu. Ni ujuzi wa namna gani unahitaji ili uweze kufikia ndoto zako. Ni watu wa namna gani unahitaji kuambatana nao ili ufanikiwe kwenye doto zako. Andika ni Baada ya Muda gani utakua umefikia Ndoto zako. Sasa hapa Ni somo jingine kabisa jinsi ya kuandika malengo. Malengo ya muda mfupi na Muda mrefu.

Soma ndoto zako kila siku Asubuhi na kabla ya Kulala.

Soma kila siku namaanisha kila siku asubuhi na jioni. Kwanini usome kila siku ? Unaichora au unaiingiza picha ya ndoto zako ndani ya ubongo wako hii itakufanya chochote utakachokutana nacho kama hakiendani na ndoto yako uweze kukiepuka na kama kinaendana basi uweze kukivuta. Unaposoma inajijenga kwenye akili yako na kutengeneza ukaribu wa wewe kuifikia zaidi.
Soma na tafakari.

Tenga Muda peke yako.

Hakikisha unatenga Muda wa peke yako angalau kila wiki ukiwa peke yako sehemu ambayo haina usumbufu wowote. Sehemu hiyo utakua unaipa akili yako nafasi ya kutafakari juu yako wewe. Jitazame ulivyo sasa halafu jitazame wewe ukiwa umefikia kwenye ile ndoto yako. Kama ni gari basi anza kujiona jinsi unavyoliendesha lile gari la ndoto yako. Kama ni Rais ebu jione ukiwa Ikulu basi Jione ukiongoza majeshi. Kama ni Bilionea anza kuona ukiwa Bilionea utakavyokua. Utakavyoweza kubadilisha maisha ya watu wengi sana Duniani. Ona jinsi dunia inavyofurahia Mungu Kukuumba wewe kwasababu maisha yao yamebadilika. Nashauri hili ufanye angalau lisaa limoja ukiwa peke yako bila simu wala kifaa chochote cha mawasiliano.

Soma Vitabu na Fanyia Kazi ndoto yako Kila siku.

Soma vitabu ambavyo vitakuza ufahamu wako ili wewe uweze kuifkia ndoto yako.
Kama unataka kuwa Rais wa Nchi lazima ujue kua unakwenda kuongoza watu hivyo vitabu gani usome ili ukuze ufahamu wako.
Unataka kuwa Bilionea hutaweza kuwa bilionea na ufahamu ulionao sasa hivi mali zote zinatakiwa ziongozwe na wewe hivyo jijengee tabia ya kujisomea vitu mbalimbali juu ya ile ndoto yako.
Ili ufikie Ubilionea unaanza na hatua moja anza leo kupiga hatua moja moja hadi ufikie kule unakotaka. Usikubali kabisa siku ipite ujafanya chochote juu ya Ndoto yako ni kupoteza fursa.

Kama tunavyojua fursa ya kwanza ni uhai tulionao leo hivyo usitumie vibaya leo siku zote unakuwaga na leo tu. Ukiweza kuipangilia leo vizuri itakufikisha kwenye ndoto yako.

Jipongeze

Kwenye kila hatua unayopiga jipongeze ili kujiongezea hamasa na wewe uweze kusonga mbele. Unaweza kujipa zawadi ndogo ndogo ambazo huwa unazipenda kila unapopiga hatua kuelekea kule unapotaka.

Iseme ndoto yako sehemu yeyote unapokuwa.

Kwanini uiseme kwa sababu una Imani na Imani ni kua na hakika juu ya mambo yasiyoonekana.
Hata Yusuf alianza kuwaambia ndugu zake kwamba anaona ndoto anaona akiwaongoza. Walimkemea lakini hakusita kuendelea kuwaambia.
Hii itakusaidia unapokamilisha iwe ushuhuuda kwamba huyu jamaa alituambiaga anakuja kuwa Rais, Bilionea, Mtu mkuu sana.

Kuwa na ndoto kubwa ni jambo la muhimu sana katika maisha. Mara nyingi, inasemekana kwamba ikiwa una ndoto ambazo hazikutoi usingizi, basi unaelekea katika mwelekeo sahihi. Mara nyingine, watu watakuita mchawi au Freemason wanapoona unafanikiwa. Lakini, kumbuka, maneno hayo hayana msingi kama yanasemwa wakati unapoanza tu kuota ndoto zako kubwa, kama vile kujenga ghorofa au kumiliki gari la kifahari kama BMW, wakati huna chochote.

Watu wanaokatisha tamaa mara nyingi ni wale wale ambao hawawezi kuona mbali kuliko hali yako ya sasa. Hawaelewi kwamba ndoto huenda zaidi ya hali ya sasa. Kama mtoa hamasa Norman Vincent Peale alivyosema, “Panda picha ya mafanikio ya kustaajabisha katika akili yako. Fikiria hili kwa nguvu. Kisha, fanya kazi kwa ujasiri kila siku kufanya picha hiyo kuwa uhalisia.”

Ni muhimu pia kutambua kwamba kuisema ndoto yako, kuiweka wazi mbele ya wengine na kujiamini, kunaweza kukujengea ujasiri. Hiyo ina maana ya kuendelea kutafakari kwa bidii jinsi ya kuifanya ndoto yako iwe kweli. Usemi unasema, “Ujumbe mzito huvunjika moyo pale unapotamkwa.” Hivyo, endelea kuongea kuhusu matarajio yako, mipango yako, na ndoto zako. Hii itakupa nguvu ya kuvumilia nyakati ngumu na kukusaidia kubaki thabiti katika njia yako.

Naamini una kila kitu kinachohitajika kuilinda ndoto yako. Itapasa uwe na nidhamu, uvumilivu, na azma thabiti. Kikubwa zaidi, uwe tayari kujifunza na kukua. Kila hatua unayopiga kuelekea katika ndoto yako, hata ikiwa ni ndogo, ni hatua muhimu.

Kumbuka kwamba hakuna jambo la maana ambalo hutokea usiku mmoja. Mafanikio ya kweli hujengwa kidogokidogo. Kwa hiyo, hata kama unakabiliwa na kejeli au shutuma, usiruhusu hiyo ikuvunje moyo. Kama alivyosema mwanasiasa na mwandishi wa Marekani Adlai Stevenson, “Ni jambo kubwa kuweza kukumbuka wakati umefanikiwa, kwamba kuna wakati pia uliwahi kushindwa, na kwa vipimo vilevile, ukatumia fursa hiyo kukua na kuboresha.”

Hivyo basi, lipokee wazo la mafanikio moyoni mwako, liweke hai katika mazungumzo yako na hatua zako, na kisha, lifanyie kazi kwa ajili ya kesho yenye matumaini. Jitahidi kwa kila njia kuona ndoto yako ikitimia. Jipe moyo na usisahau kusherehekea kila hatua unayopiga kwa mwelekeo chanya.

FURSA HAIJI MARA MBILI: Jinsi unavyoweza kupata faida au hasara ukitumia Nafasi au fursa uliyonayo

Kwenye maisha fursa moja tu inatosha kabisa
kubadilisha hali yako ya sasa na kukuweka kwenye
kiwango kingine kabisa cha mafanikio.Kuna watu
wengi sana ambao waliwahi kufikiria kuwa maisha
yao yatachukua miaka mingi sana kabla
hayajabadilika na kwa mshangao wao walipoanza
kufanya vitu sahihi wakakutana na mabadiliko
makubwa sana katika maisha yao kwa kupitia
fursa moja tu.

Kufanikiwa kwenye maisha ni matokeo ya kujua
mambo sahihi ya kuyafanya.Ni kama ilivyo wakati
unapotaka kufungua mlango
uliofungwa,unachohitaji ni ufunguo sahihi wa
kutumia na sio vinginevyo.
Ili ufanikiwe lazima uwe mtu mwenye bidii na
ambaye unawathamini watu bila kujali hali zao za
sasa.Ili kutoka hapo ulipo na kwenda kule
unakotaka unahitaji watu wa kukuunganisha na
fursa mpya,kukuonyesha njia nzuri ya kufanya
mambo,wa kukurekebisha na watu ambao
unaweza kujifunza kwao.

Mwaka 2012 mmiliki wa kampuni kubwa ya vifaa
vya michezo ya Modell nchini marekani,bwana
Mitchell Modell alifanya tukio la ajabu sana lililotoa
funzo kubwa la mafanikio katika maisha yetu ya
kila siku.Aliamua kujibadilisha mwonekano wake
kwa kunyoa nywele zake zote na kuweka ndevu
nyingi sana za bandia na pia kuvaa hereni sikio
moja.Kisha baada ya hapo alienda kuomba kazi
kwenye kampuni yake na akaanza kufanya kazi ya
daraja la chini kabisa.
Akiwa ameajiriwa bila watu kujua kuwa ndiye
mmiliki alikutana na wafanyakazi wengi sana wa
aina mbalimbali.Kati ya wafanyakazi katika tawi lile
alikuwepo dada mmoja anayeitwa Angel ambaye
alikuwa ana watoto 3 ila hakuwa anakaa na mume
wake na kwa muda wa miaka 2.Lakini pia,Angel na
watoto wake wamekuwa wanaishi kwenye vibanda
kwani hakuweza kulipia pango kwenye nyumba
nzuri ya kuishi.Gharama zote za
chakula,ada,matibabu na mavazi ya watoto yote
ilikuwa juu yake.
Pamoja na hali yake hiyo,Angel alikuwa ni
mfanyakazi anayewahi kazini kila siku na alikuwa
anafanya kazi kwa bidii sana.Hata wakati wengine
walikuwa wanalamika juu ya mshahara,yeye kazi
yake ilikuwa ni kuwatia moyo na kuwahamasisha
wafanye kazi kwa bidii sana akiamini ipo siku
mambo yatakuwa mazuri.Kila wakati Bwana
Mitchell alipokuwa anamkuta Angel,alikuta
anafanya kazi zake kwa umakini na hata akikuta
anaongea na wenzake basi itakuwa ni kuwatia
moyo na kuwapa hamasa na kuwataka waaache
kulalamika.
Wakati Bwana Mitchell akiwa kama mfanyakazi
mpya alihitaji sana msaada wa kufundishwa jinsi
mfumo unavyofanya kazi na mambo mengine.Kila
mmoja alikuwa hayuko tayari kumfundisha,ila
Angel alikuwa tayari kumfundisha na kumsaidia
hata na kazi ambazo alikuwa hawezi kuzifanya
kutokana na ugeni wake.Na kwa sababu ya ukaribu
wake ndipo alipoweza kumfahamu Angel na
kuyajua maisha yake kwa undani.
Baada ya siku kadhaa za kufanya kazi bila mtu
yoyote kujua kuwa ndiye mmiliki,ndipo alipoamua
kufanya kitu kikubwa kwa Angel.Kwanza
alimpandisha cheo na kumfanya kuwa meneja
msaidizi na kisha alimpa zawadi ya dola laki mbili
na hamsini(Takribani shilingi milioni 500 za
kitanzania) ili aweze kupata nyumba nzuri ya
kuishi.
Baada ya tukio hili kutokea wafanyakazi wengi
sana walijilaumu na walitamani sana kupata fursa
upya kama wangejua kuwa yule alikuwa ni mmiliki.
Ndivyo maisha yalivyo na ndivyo safari ya
mafanikio ilivyo.mara zote huwezi kujua ni wakati
gani fursa kubwa inayohusu maisha yako
itakutokea.Kilichomfanya Angel kufanikiwa ni ile
hali ya kuwa ni mtu ambaye hakuruhusu jambo
lolote limzuie kufanya kazi kwa bidii na kwa ufanisi
kila wakati hata kipindi ambacho maisha yake
yalikuwa magumu.
Mara nyingi unaweza kujikuta katika hali ambazo
zinakatisha tamaa na zinakupa uhalali wa kila
namna wa wewe kuwa mtu wa kulalamika na
kukata tamaa.Hebu fikiria mama wa watoto
watatu,analipwa mshahara mdogo lakini bado
anawahi ofisini na huwa halalamiki.Kuna fursa
nyingi kwenye maisha unazikosa kwa sababu ya
malalamiko juu ya hali inayokuzunguka.Kitu cha
msingi unachotakiwa kujua ni kuwa kulalamikia
kitu au mtu hakuwezi kubadilisha hali yako ya sasa
lakini kufanya kwa bidii kunaweza kufungua fursa
nyingi kubwa katika maisha yako.
Inawezekana kazi unayoifanya ni ndogo
ukilinganisha na ndoto kubwa
uliyonayo,inawezekana mshahara unaolipwa sio
mkubwa kama unavyotaka,inawezekana biashara
yako bado haifanyi vizuri kama mipango yako
ilivyo ama hauna mtaji kiwango
unachotaka.Katikati ya hali hii unachotakiwa
kufanya sio kuanza kulalamika na kukata
tamaa,unatakiwa kuwa kama Angel,weka kiwango
kikubwa cha bidii kwani kwa kufanya hivyo
utakuwa unajifungulia milango mikubwa zaidi
katika maisha yako.
Kuanzia leo fanya maazimio katika maisha yako
kuwa utakuwa mtu wa kufanya kwa bidii kile
ambacho unakifanya hata kama itakuwa kwenye
mazingira magumu,kwani kwa kufanya hivyo
utakuwa unajitengenezea fursa kubwa sana mbele
yako.Ukiamua kuishi kwa mtazamo huu,muda
mfupi sana ujao utafanikiwa.
Kitu kingine cha msingi cha kukizingatia hapa ni
kuwa usidharau watu katika maisha yako.Kati ya
mafumbo makubwa ambayo Mungu ameyafumba
ni kuhusu hatima za watu ambao tunakutana nao
kila siku katika maisha yetu.Hakuna kitu kibaya
kama kumdharau mtu eti kwa sababu anaonekana
kwa wakati huo hawezi kukusaidia
chochote.Jifunze kumuheshimu na kumthamini
kila mtu.
Ilil ufanikiwe katika maisha yako jifunze kuishi
kama Angel,jifunze kuwa na bidii ya kazi hata
katika mazingira magumu lakini pia jifunze
kuthamini kila mtu ambaye unakutana naye-
Kuanzia mdada wa kazi
nyumbani,mlinzi,mfagizi,kondakta wa daladala
hadi dereva wako.Kila mtu ni muhimu na ana
mchango katika maisha yako.Kanuni ya maisha
inasema-โ€œHusiana na watu kama wewe unavyotaka
watu wengine wahusiane na wewe piaโ€. Kuanzia leo
ishi na kila mtu kama โ€œMitshell wakoโ€ wa
kukuunganisha na fursa kubwa uliyokuwa
unaisubiria.
Sina shaka kuwa fursa yako kubwa iko njiani
inakuja,usikate tamaa.
Kumbuka kuwa ndoto Yako Inawezekana,
See You AT The Top.
ยฉJoel Nanauka

Kwa ushauri huu jitambue upate mafanikio

Ukiona unalala masaa 9 wakati Donald Trump analala manne tu. Afu unaamka huna nauli na bado kesho unalala masaa manane tena.. Ujue unashabikia mafanikio.

Ukiona Bill Gates anasoma kitabu kimoja kwa wiki. Na wewe unasoma kimoja kwa miezi sita ujue nod maana kuna tofauti ya Bill Gates na wewe.

Ukiona unasema utakuwa successful siku moja afu huna DAILY GOALS. Yani hujui ukiamka ufanye nini na jioni utapimaje kama kweli umekifanya ujue hujaelewa vizuri maana ya kuwa successful.

Hard Work beats talent.

You must sleep less and work harder until you get what you want.

Elimu tuu haitoshi kukunufaisha maishani na kukupa mafanikio

EMBU SOMA HII KWA MAKINI SJUI NI KWELI? USIMAINDI LAKINI MAANA ITAKUGUSA TUU. MAFANIKIO YA MAISHA SIO ELIMU TU, UTHUBUTU, KUJIAMINI NA UJASIRI WA MAAMUZI
โœ๐ŸฝUkichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana elimu ndogo ama hawakusoma kabisa.

๐Ÿ‘‰๐ŸพKatika miji na maeneo yote; wenye majengo ya maana, wenye makampuni makubwa, wenye utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka makubwa ni wale wa “darasa la sabaโ€ au wale ambao hawakuingia darasani kabisa

๐Ÿ™‡๐Ÿฝ๐Ÿ“š Wasomi wengi wana maisha ya kawaida yaani yale ya kiwango cha kubadilisha mboga, wakijitahidi sana wanaishia kujenga nyumba za kuishi ๐Ÿก na ๐Ÿš— ๐Ÿš™magari mawili ya kutembelea (tena kwa mikopo!)

๐Ÿ‘‰๐ŸพWapo ๐Ÿ™‡๐Ÿฝ๐Ÿ“šwasomi wengi tu wanaoishi kimasikini, kwa lugha ya kistaarabu tunasema wana maisha ya kuungaunga. Kiukweli idadi ya wasomi walio matajiri ni ndogo sana

๐Ÿ‘‰๐ŸพLakini Umasikini wa wasomi wengi umeanzia huko shuleni na vyuoni wanakopatia usomi wao. Madarasani kuna mambo mawili wanafundishwa wasomi ambayo ndio yanayowaroga

Hii inachangiwa na mambo mawili:-
๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ
I. Wameelimishwa na kuaminishwa kwamba yule anaepata maswali yote kwa usahihi ndio anaonekana amefaulu. Ukikosea unahesabika kuwa u mjinga na wenyewe wanaita umefeli

๐Ÿ‘‰๐ŸพHata hivyo katika maisha ya kawaida hasa kwenye mchakato wa kutafuta hela, kujaribu na kukosea ni sehemu ya mafanikio

๐Ÿ‘‰๐ŸพKadiri unavyojaribu na kukosea mara nyingi ndivyo unavyojifunza na ndivyo nafasi ya kutajirika kwako inakuwa kubwa!

๐Ÿ™‡๐Ÿฝ๐Ÿ“šWasomi wengi kwa sababu ya “mentality” ya kuogopa kukosea huwa hawapendi kujaribu biashara kwa hofu ya kushindwa kuiendesha, na huamua kufa kimasikini wakitegemea mishahara pekee kwa sababu mishahara ndio pato lao la uhakika
๐Ÿ‘‡๐Ÿพ
II. Madarasani kunahimizwa ubinafsi badala ya umoja. Angalia namna mitihani inavyofanyika. Kila mwanafunzi anafanya mtihani peke yake, na ukikutwa unaangalizia ama mnasaidiana na mwenzio ndani ya chumba cha mtihani mtapata adhabu kali ikiwemo kufutiwa mtihani!

๐Ÿ‘‰๐ŸพKatika maisha ya kawaida hasa ya kusaka fedha, unahitajika ushirikiano mkubwa sana, baina yako na wadau, wateja, wafanyakazi wenzio, marafiki n.k. Kwa kifupi unatakiwa kuwa na Networking ya kutosha.

โœ‹๐ŸพHuwezi kufika mbali kiuchumi kama utakuwa na “mentality” ya ubinafsi unaosisitizwa madarasani!

๏ฟฝSimaanishi kusoma hakuna maana, isipokuwa ninakwambia: Kama ukipata nafasi ya kusoma, soma kwa bidii; lakini usibebe kila wanachokulisha madarasani; ukakileta huku mtaani

๐Ÿ›ฃMtaani panahitaji akili ambayo ni tofauti na hiyo iliyopimwa kupitia kukariri ya vitabuni, mwishoni wanakuzawadia makaratasi yaitwayo vyeti

๐Ÿ˜ŽUkitaka kufanikiwa ungana na waliofanikiwa wakuelekeze

๐Ÿ˜€๐Ÿ™๐Ÿฝ Hii habari haitaki hasira, vumilia tu na jiongeze
โ€ฆ.hata mimi sijawa tajiri bado๐Ÿ˜œ๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ‘†๐Ÿฟโ€ฆ But nakaza mwendo Bila kuangalia vipingamizi au ugumu wa safariโ€ฆ

Mbinu 5 za kukunufaisha maishani

Mbinu 5 za kukufanikisha maishani Unaweza ukawa upo kwenye hali ya kulalamika maisha yako ni magumu na unashangaa kwa nini hufanikiwi katika maisha yako kama jinsi unavyotaka wewe. Hali hii inaweza ikawa inakuumiza pengine kila ukiangalia rafiki zako ama maisha ya wengine yanavyozidi kuwa mazuri, wakati wewe upo katika hali ngumu. Na pengine umekuwa ukijiuliza nini siri kubwa ya mafanikio yao ambayo wanaitumia ambayo wewe huna. Kutokana na hali hiyo umekuwa ukijilaumu kujilaumu na kujiuliza kwanini nyingi ambazo hazina majibu. Kitu usichokijua watu hawa huwa wanatumia mbinu fulani kufanikiwa. Kawaida, katika maisha kama ulivyomchezo wa miguu, au michezo mingine mara nyingi huwa zipo mbinu za kufanikisha kile tunachokifanya. Mbinu hizi huweza kutambulika kama sheria, kanuni, au siri lakini zote hulenga kukufanikisha kama unataka mafanikio ya kweli. Mbinu hizi zinapotumiwa kwa bahati mbaya au nzuri huwa hazifanyi ubaguzi zinamwendea yoyote na kuleta matunda unayoyataka. Hata kama ikitokea umezitumia mbinu hizi kwa bahati mbaya bila kujijua ni lazima utafanikiwa katika maisha yako. Mbinu hizi ndizo wanazozitumia wengi wenye mafanikio na kuwafanikisha, ingawa huwa sio kwao kuwa rahisi kukwambia mbinu hizo. Haijalishi unaishi kwa sasa maisha gani au upo kwenye matatizo mengi vipi, ukizitumia mbinu hizi, zitakufanikisha na kukupa maisha ya mafanikio unayoyataka. Acha kulalamika tena na kuishi bila amani. Sasa unaweza ukawa na mafanikio makubwa kama hao unaowaona wamefanikiwa, ikiwa utatumia mbinu hizi kukufanikisha. Unajua mbinu hizi ni mbinu zipi?

Hizo Ndizo Mbinu 5 Za Kukupa Maisha Ya Mafanikio:-
1. Kuwa na nidhamu binafsi.

Ili kupata mafanikio makubwa unayoyahitaji sio suala la kufanya kazi kwa bidii tu, zaidi unachohitaji nikuwa na nidhamu binafsi ambayo itakuongoza kwenye malengo yako. Watu wengi hawana nidhamu binafsi kitu ambacho kinapelekea wengi ndoto zao zinaishia kati. Ni muhimu kuelewa kuwa ni lazima kufanya mambo yale yanayoendana na ndoto zako, hata kama kuna wakati unajihisi umechoka unalazimika kujikaza kufanya jambo hata dogo ambalo litakufikisha kwenye malengo yako. Ukishindwa kuwa na nidhamu binasi katk maisha yako elewa kuwa utashindwa kufikia mipango na malengo iliyo jiwekea.

2. Jifunze kila mara kwa watu waliofanikiwa.

Hii itakusaidia kujua vitu vingi usivovijua kuliko kukaa na kungโ€™angaโ€™nia mbinu zilezile ambazo hazikusaidii. Yapo mambo mengi sana usiyoyajua ambayo yanakufanya ushindwe kufanikiwa. Ikiwa utakuwa na uwezo wa kujifunza kwa wale waliofnikiwa utakuwa upo kwenye nafasi kubwa ya kufanikiwa na kusonga mbele. Maisha yako yanazidi kuwa magumu siku hadi siku, kutokana na kukosa kujifunza kwa wengine kwa kujua hilo badili mwelekeo wako na kuwa mtu wa kujifinza mwisho wa siku mafanikio yatakuwa makubwa kwako.

3. Jifunze kutokana na makosa uliyofanya.

Inawezekana kuna mahali utakuwa umekosea kwa namna moja au nyingine,badala ya kulaumu na kuumia moyo sana jifunze kutokana na hayo makosa liyoafanya ili isije ikawa kwako rahisi kufanya makosa yaleyale kwa mara nyingine. Ikiwa utajifunza kutokana na makosa na kufanyia kazi kile ulichojifunza hapo utakuwa umechukua hatua moja muhimu ya kuweza kukusaidia kusonga mbele kuyafata mafanikio unayoyataka. Unataka mabadiliko makubwa katika maisha jifunze kutokana na makosa yako na acha sana kulaumu.

4. Jenga tabia ya kujisomea kila siku.

Hili ni jambo ambalo nimekuwa nikiliongelea sana kuhusu huu umuhimu wa kujisomea. Unapojisomea unapata vitu vingi sana tena ndani ya muda mfupi. Kupitia huko utaweza kujifunza mambo mazuri yatakayoweza kubadili maisha yako kwa sehemu kubwa na kuwa mtu, tofauti kabisa. Acha uvivu jifunze vitu vipya kila siku. Unaweza ukajifunza kupitia vitabu, ama mitandao mizuri inayoelimisha kama huu wa DIRA YA MAFANIKIO kwa kupata maarifa bora na sahihi kabisa. Unapojifunza inakusaidia kukabiliana na changamoto nyingi, ambapo kwako ingekuwa ngumu kuzikabili.

5. Kuwa na mahusiano sahihi na watu waliofanikiwa.

Katika kutafuta mafanikio ni vizuri ukawa na mahusiano ama mtandao na watu sahihi ambao watakusaidia kukufikisha kwenye lengo ulilojiwekea. Haina haja kuwa na watu ambao hawakusaidii kutimiza malengo yako. Watu hawa watakukwamisha na kukurudisha nyuma katika maisha yako tu siku zote. Jenga tabia ya kuwa na watu sahihi ambao utajifunza kitu kwao, utashirikiana nao na kujifunza mambo mengi huko ya mafanikio na hatimaye utamudu kusonga mbele

Siri za mafanikio na Jinsi ya kufanikiwa

Tafuta fursa kila kona.
Tumia kipaji chako.
Kuwa na nidhamu katika fedha – matumizi mazuri ya pesa, nidhamu kwa watu wanaokuzunguka, usijikweze, usibague jamii, heshimu wote waliokaribu yako nk.

Kuwa na nidhamu katika afya yako: Afya ndio mtaji sahihi katika biashara yoyoteย – kuwa na mazoea ya kuangalia afya yako mara kwa mara nk.

Usipoteze mudaย – jali muda kuliko kitu chochote kwani muda ndio kila kitu, muda ni mali.
Shiriki kwenye makongamano au semina mbalimbali za ujasiriamali.
Kuwa na vyanzo vingi vya kukuletea kipato.

Tafuta maarifa kwa mamilionea mbalimbali dunianiย – soma historia za mamilionea jinsi walivyofanikiwa.

Jenga urafiki na taasisi za kifedhaย – mamilionea wengi hukopa fedha kutoka katika taasisi za kifedha – tembelea taasisi za fedha watakupa ushauri mbalimbali na watakupa mkopo, usisikilize maneno ya watu kuwa taasisi za pesa ni za watu matajiri hiyo sio kweli.

Kuwa na shauku, kuwa na fikra za kuwa milionea na wewe utakuwa.USIWAZIE KUSHINDWA

Kuwa na imani kwamba utakuwa milionea na itakuwa hivyo. KWA KUFANYA. SIO IMAN TU.

Wekeza ktk miradi au biashara mbalimbali. USIOGOPE KUTHUBUTU

Wekeza sehemu yenye mahitaji ya bidhaa inayotakiwa kuzalishwa – angalia fursa hapo ulipo na wekeza. SIO KUFUJA PESA

Kuwa na bajeti katika mapato na matumizi yako. NIDHAMU MUHIMU KATIKA PESA

Kuwa na wazo (Business idea):ย mamilionea wengi hutumia mawazo kutoka kwa watu mbalimbali kutengeneza pesa. Wazo ndio cheti cha kuwa milionea anza sasa fanyia kazi wazo lako ili kukuletea fedha.

Fanya vitu wewe mwenyewe – acha kufanya vitu kama fulani, usiige mtu, buni vya kwako, mamilionea huwa hawaigi, ukiwa mkweli kwako utakuwa mkweli kwa watu

Kuwa na malengo – kumbuka hakuna maendeleo pasipo na malengo, fahamu hilo.,, PLANS AND SELF COMMITMENT

Kuwa na moyo wa ujasiri – usiogope kushindwa jitahidi ktk kupambana na maisha usikubali kubezwa au kuvunjwa moyo. Ukianguka nyanyuka tena, usifikirie kutakuwa na mtu wa kukusaidia zaidi ya kujisaidia mwenyewe.UKIANGUKA USIOGOPE KUINUKA

Kuwa karibu na matajiri -usiogope kwani hao ni binadamu kama wewe, jaribu kuwadadisi ili wakupe mbinu mbali za kuwa tajiri hadi milionea. Ukiwa karibu nao unaweza ukapata nafasi ya kazi au kukuunganishia biashara ukaanza kufanya na kufanikiwa.

Mtangulize Mungu -mwabudu, msifu, mtolee sadaka, saidia masikini, wajane, wagonjwa, jenga nyumba za ibada. Mungu ndio kila kitu mtegemee yeye.

Fanya vitu kitofauti;ย fanya vitu vigeni, muonekano tofauti ingawa biashara ni ile ile, tumia lugha tofauti, panga bei tofauti, nk. Mfano aina tofauti za simenti, chupa za soda na juisi nk.

Acha wogaย – jaribu biashara yoyote, woga wako ndio umasikini wako, usiogope kukosolewa unapokosolewa ndio unajifunza. Usiogope mikopo, mamilionea wengi hufanya mambo ambayo wewe unayaogopa.

Kuwa na mtazamo chanya – usikubali mawazo hasi, marafiki zako wawe na mawazo chanya, usikubali kuvunjika moyo na usikubali mawazo yako yaingiliwe na mtu.
Anza kufanyia kazi wazo lako usisubiri mtu.

Kuwa na mipaka katika mambo yako – usifanye mambo kwa mkumbo, usiige, buni mambo yako. Mamilionea wengi wanabuni mambo yao hawapangiwi na mtu

Kuwa mwaminifu -mamilionea wengi ni waaminifu ktk mali za watu. Wengi walikuwa wakipewa mali wakauze ndio walipe pesa, wanadhaminiwa malighafi za viwandani hadi wanamiliki viwanda vyao. Uaminifu ndio njia ya kukufanya uwe milionea.

Pokea ushauri kwa watu hasa kuhusiana na biashara yako – waulize watu kuhusu huduma yako ya biashara wanaionaje na fanyia kazi ushauri wao.
Kuwa na plani katika kazi zako kila siku.

Kuwa na maono ya jinsi unavyotaka maisha yako yawe

Panua soko la bidhaa zako usitegemee soko la sehemu moja

Ubunifu ni muhimu sana – fanya ubunifu ktk kuuza bidhaa zako ili mauzo yasishuke, kuwa mbunifu ktk wateja wako kwani itakusaidia kugundua wateja wako wanataka nini – kuwa karibu nao, wasikilize, waheshimu nk.

Kuwa milionea kunaanzia kichwani mwako-ukiweka mawazo yako kichwani utakuwa milionea kweli utakuwa sio kusema tu mdomoni. Amini utakuwa milionea na utakuwa kweli
PIGA KAZI

Maneno ya walioshindwa yasikukwamishe safari yako ya kuwa milionea

Ondoa neno haiwezekani wewe kuwa milionea – kila binadamu anaweza kuwa milionea

Mshukuru Mungu kwa hicho alichokupa – kumbuka neema ya Mungu ndio imekufikisha hapo ulipo hivyo toa msaada kwa watu wasiojiweza, yatima, masikini, wajane, wagonjwa, toa sadaka, walemavu nk

HITIMISHO;
Shujaa mwenzangu, kuwa milionea inawezekana kama mimi na wewe tukifuata njia hizi 39 zinazotumiwa na mamilionea wengi duniani..

Ila kuthubutu ndo hatua ya kwanza.

Mizigo tuliyoibeba ambayo haina faida

1.๐Ÿ’ฅUmejipa jukumu la kuwa “mpelelezi” wa maisha ya wengine na umesahau maisha yako.

2.๐Ÿ’ฅUmebeba vinyongo na visasi moyoni vinavyokufanya uwafikirie waliokuumiza zaidi kuliko kufikiria furaha na maendeleo yako.

3.๐Ÿ’ฅ Una marafiki wengi ambao ni kama kupe, wapo kukutumia tu na hawachangii lolote katika maendeleo zaidi ya kujifanya ndio watu wako karibu lakini kumbe wapo kwa maslahi yao!

4.๐Ÿ’ฅUmeweka mbele zaidi “watu watanichukuliaje” kuliko kuangalia maisha yako.Watu ndio wanakuchagulia aina ya maisha unayoishi na unajilazimisha kuishi kama wao hata kama huna uwezo huo.

5.๐Ÿ’ฅUnaongea zaidi ya kasuku lakini vitendo hakuna. Unatamani mafanikio tu moyoni lakini huna mipango ya kuyafikia.
6.๐Ÿ’ฅMaisha yako yote umeyaweka kwenye mitandao ya kijamii. Huna siri hata moja! Hivyo unalazimika kuishi aina ya maisha ambayo yataendelea kufanana na yale uliyoyaweka kwenye mitandao ya jamii kwa sababu ukibadilika tu watasema “umefulia”

7.๐Ÿ’ฅKila aliefanikiwa ni rafiki yako au utasema ni mtu wako wa karibu na unaishia kuwasifia tu na kupiga nao picha lakini hujifunzi kutokana na mafanikio yao na wala hutumii fursa hiyo ya kujuana nao.

8.๐Ÿ’ฅUpo sahihi kila siku(you are always right). Huambiliki, hushauriki na kila wazo atakalotoa mwenzako basi si zuri ila la kwako ndio sahihi na utataka litekelezwe hilo hilo. Mwisho wa siku kila mtu anakukimbia hakuna wa kukuambia “hapa umekosea” kwa sababu ya ujuaji wako.

9.๐Ÿ’ฅHujifunzi maarifa mapya.Mara ya mwisho kusoma kitabu ilikuwa ni “Ngoswe, penzi kitovu cha uzembe” Tena ni kwa sababu ilikuwa ni kwa ajili ya kujibia mtihani. Hujifunzi “life skills” wala ujuzi mwingine.

10.๐Ÿ’ฅUnazurura mno mitandaoni bila faida. Kwako wewe intaneti ni kwa ajili ya kuchati tu na kufuatilia habari za mjini ambazo tangu umeanza kuzifuatilia hujawahi kuingiza hata shilingi moja, zaidi unateketeza tu hela yako ya vocha.

ISHUSHE hiyo mizigo kama kweli inahitaji kusonga mbele!

Umeshawahi kufanya hili jaribio?

Figisu ya Leo. UMESHAWAHI KUFANYA HILI JARIBIO.?

kadri temperature inavyo ongezeka chura nae huwa ana increase temperature ya mwili wake..

pindi inapokaribia kufika boiling point yaani nyuzi 100 chura atashindwa kuongeza temperature ktk mwili wake na hapo ndipo atataka kutoka ktk maji hayo ya moto na yanayo endelea kuchemka..
kutokana na kutumia nguvu nyingi sana ktk kuongeza temperature ktk mwili wake,pindi anapotaka kuruka atashindwa na atakufa humo ndani ya chombo cha maji yanayochemka..
SWALI; NINI KIMEMUUA CHURA.!??
Najua utaniambia ni maji ya motoโ€ฆ
La hashaa.!
kilichomuua chura ni kushindwa kufanya maamuzi mapema ya kutoka katika chombo cha maji yanayochemka hali ya kuwa bado nguvu anazo..
FUNZO
Fanya maamuzi sahihi sasa kabla nguvu za kutaka kufanya changes hazijakuishia kama yaliyomkuta chura..
NOTE; Kuvumilia jambo usiloliweza ni sifa ya punda.
BADILIKA.

Kukataliwa ni mtaji

Hakuna mtu duniani ambaye hajawahi kukutana na hali ya kukataliwa. Yaani kukataliwa katika hali yoyote ile. Waweza kuwa umekataliwa katika kupata ajira, umekataliwa katika mahusiano, umekataliwa kupata nafasi ya kusoma, umekataliwa kupata mtaji wa biashara, umekataliwa tuu..umekataliwa.

โ€”-= Unaweza kuwa umekataliwa katika ajira moja kumbe kuna ajira nyingine tena yenye maslahi zaidi inakusubiri.

โ€”-= Umekataliwa na mteja mmoja na kumbe kuna wateja wengi wanakusubiri.

โ€”-= Umekataliwa katika chuo kimoja mwaka huu kumbe mwakani kuna nafasi yako inakusubiri.

โ€”โ€”= Umekataliwa na mpenzi ulioamini kabisa atakua wako wa maisha kumbe aliye wako haswaa anakusubiri ufike.

Watu wengi kinachowarudisha nyuma, “ni kuacha kuboresha fikra zao ili kuwa watatuzi wa matatizo_(problem solvers)_ ila wameamua kuwa walalamikaji tu kila siku, ili tuendelee ni lazima tujikite katika kutafuta majibu ya matatizo yanayotuzunguka.” Yaani, mara zote jiulize ” *sasa nifanye nini? Na sio kwa nini mimi?”*

Mtaalamu mmoja aliwahi kusema ” _Life is 10% of what happens to you and 90% of how you respond to it_”. Yaani _yale yanayokutokea maishani yanachangia asilimia kumi tu kuboresha au kuharibu maisha yako na asilimia 90 ya maisha yako ni jinsi wewe unavyoyachukulia maisha hayo_. Kwa nini ukate tamaa baada ya kukataliwa. Yape maisha yako maana sana thamani ya juu kabisa ili kukataliwa kwako iwe ni kukupa nguvu ya kufanya vizuri zaidi. Tambua utakacho na unachoweza kukifanya. Jifunze vizuri na ubobee ili kuuhakikishia ulimwengu kwamba wewe sio mzigo ila ni sehemu ya wenye majibu ya matatizo yanayotuzunguka.

Kukataliwa, ni mtaji. Kila jambo lina wakati wake.

Jipe moyo kamwe usikate tamaa

Nilikuwa naangalia mpira wa miguu katika uwanja wa
shule.
Nilipokaa, Nilimuuliza kijana mmoja juu ya Matokeo ya mchezo.

Kwa tabasamu, alijibu “Wako mbele yetu 3-0”!
Nikasema, Kweli!
Mbona huonekani kukata tamaa..?

“Kukata tamaa?
“Yule mvulana aliuliza kwa mshangaoโ€ฆ.”!?

Kwanini nikate tamaa wakati bado refa hajapuliza kipenga cha mwisho?

Nina imani na timu yangu na meneja wa timu; Nina hakika tutashinda!

Na kweli, mchezo uliisha 5-4 timu ya kijana ikiwa mbele!

Alinipungia mkono taratibu, na tabasamu zuri akiondoka uwanjani; nilishangaa, mdomo wazi, ujasiri mkuu kiasi hiki; such beautiful faith;

Nilipofika nyumbani usiku ule, swali lake lilizidi kuja kwangu zaidi:
“Kwanini niogope wakati refa hajapuliza kipenga cha mwisho?”

Maisha ni kama mchezo.
Kwanini ukate tamaa wakati mwenyezi Mungu ndiye meneja wako?

Kwanini ukate tamaa wakati kungalipo uhai ndani yako?

Kwanini ukate tamaa wakati kipenga chako cha mwisho bado hakijapigwa?

Ukweli ni kwamba watu wengi hujipulizia wenyewe vipenga vyao vya mwisho.

Lakini maadamu ungalipo uhai, hakuna kisichowezekana muda haujakuacha.

Nusu kipindi si kipindi kizima na ratiba ya Mungu kwa mwanadamu si ratiba ya mwanadamu kwa Mungu.

Usijipulizie kipenga chako cha mwisho we mwenyewe.

JIPE MOYO USIKATE TAMAA!

KWA MUNGU YOTE YANAWEZEKANA.

KAMWE USIKATE TAMAA.

Ushauri wangu kwa leo: Zingatia hili, hamasika, badilika

Tupo kwenye dunia ambayo tulikuta watu na tutawaacha watu.
Vyote tulivyovikuta vilianzishwa na binadamu wengine wenye mawazo mema na wenye mawazo mabaya pia. Vitu vingi tunavyovifanya tunaendeleza tulivyovikuta ni mara chache kukuta kitu kipya ambacho hakitegemei mazingira na asili ya tulivyovikuta.

Hivyo basi kwa vyovyote vile unahitaji mtu wa kukuongoza au kuku Coach ili ufanikiwe katika pande zote za maisha.

Nitakwenda kuzungumzia sehemu kuu tatu za muhimu sana ambazo unatakiwa uwe na watu wa kukuongoza ili uweze kukua na kupanda viwango kila wakati.

Ni vitu vya kawaida sana lakini leo nitakwenda kuzungumzia uone ilivyo muhimu sana wewe kua na vitu hivi maana bila vitu hivi mafanikio yatakua magumu sana kufikia. Safari yako itakua ngumu zaidi kama utakosea sehemu hizi tatu.

Nitaomba tuelewane kwamba hapa huendi kuiga au kuwa hawa watu utakua wewe na utatimiza lile kusudi la Mungu ndani yako.

Kwanza kabisa uko hivyo ulivyo kwa sababu ya mazingira uliyokulia na watu ulioishi nao tangu ukiwa mtoto hadi hapo ulipo.

Kuna tabia nyingi sana unazo kutokana na mazingira uliyokulia.

(Hapa ndipo nakutana na kitu ambacho nakipenda sana kujifunza kwa wengine napenda kujifunza kwenye mazingira mapya na kwa watu wapya kwa kua wameishi maisha ambayo mimi siyajui na wanafahamu vitu vingi ambavyo mimi sifahamu. Watu wana utajiri mwingi sana ndani yao ukiweza kukaa na mtu ambaye humjui kabisa unaweza kujifunza mambo mengi ya ajabu kwake. )

Hawa ndio watu wa Muhimu sana kwenye safari yako usiwakose ili uweze kusonga mbele.

Sifa zao kabla hujawachagua ni za muhimu sana pia ili wasije wakakupoteza badala ya kukufikisha kule unakotaka kwenda.

(a)Awe na mafanikio (Amefika Mbali) kwenye hiyo sehemu.

(b)Awe na Tabia njema zinazokubalika na jamii yake na dini yake. (mfano hapa ukikutana na mtu ambaye anakuelekeza kuhusu biashara na ni mlevi na mzinzi hizi tabia lazima atakuambukiza kwasababu atakua mtu wako wa karibu sana)

(c)Awe amekuzidi sana kwenye kile unachotaka akulelee (akuongoze).

Hizo ni sifa za muhimu tu za kuangalia zipo nyingine nyingi sana utajifunza mwenyewe.

1. Mlezi wako wa Kiroho

Huyu ni mtu wa muhimu sana na nimemweka wa kwanza.

Bila roho hakuna mwili.

Bila roho mwili wako unakua umekufa.

Unahitaji ukue kiroho na upande viwango kila wakati ili uweze kuvutia mafanikio ya nje.

Ukishindwa hapa hata ukiwa bilionaire inaweza kuwa kazi bure.

Hutaweza kuzifurahia hizo pesa.

Tafuta mtu wa kukulelea kiroho.

Mtu wa kukufundisha kumcha Mungu.

Kama huna katafute mtu wa kukulea kiroho sifa nimezitaja hapo juu.

Mtu huyu anatakiwa akufahamu vizuri na wewe umfahamu vizuri.

Yaani muwe na mahusiano ya karibu sana.

Mtu huyu awe anafuatilia maendeleo yako ya kiroho kwa karibu sana.

Haijalishi uko Dini gani lazima umpate mlezi wa roho yako.

Dini ndio inahusika kulisha roho zetu.
Ndio maana hatufundishwi biashara kule.

2. Mlezi wa Mahusiano/Uchumba/Ndoa

Hapa ni kwa muhimu sana.

Ukiwa vizuri kiroho mahusiano yakawa na tatizo hutafika mbali.

Ukiwa vizuri kiroho ndoa ikasumbua nayo ni tatizo.

Tafuta mtu wa kukulea kwa upande huu pia mtu aliefika mbele zaidi yako.

Aliefanikiwa zaidi yako.

Kama unatafuta mchumba tafuta mtu aliye kwenye ndoa na amefanikiwa.

Ukimtafuta single mwenzako atakupoteza๐Ÿ˜€.

Mtu huyu awe karibu yenu kabisa kulea mahusiano/ uchumba au ndoa yenu.

Hakuna aliyezaliwa anajua kila kitu tunajifunza hapa duniani kwa waliotutangulia na waliopo pia.

3. Mlezi wa Maono yako/Ndoto zako/Malengo yako/Biashara Yako/Pesa. (Coacher).

Mtu huyu ni wa muhimu pia katika maisha yako.

Unataka kumiliki utajiri wa dollar billion moja lazima utafute mtu wa kukulelea na kukuwezesha ufikie huko.

Huwezi kwenda mwenyewe.

Unahitaji mtu wa kukuongoza kwenye kila unachotaka kukifanya.

Wengi wanakata tamaa kwa kua hawana watu hawa wa kuwalelea.

Mtu huyu anatakiwa awe anakufuatilia hatua kwa hatua kwenye kile unachokifanya.

Awe anapata taarifa za maendeleo yako kila wakati ikiwezekana hata kila week.

Ukipata mafanikio yeyote ajue pia ukipata changamoto ajue.

Mtu huyu anatakiwa awe amekupita kwenye kile unachokitaka na hapa huendi kuwa Follower,anakwenda kukutengeneza wewe uwe kiongozi.

Uweze kusimama mwenyewe na hatimae uongoze wengine.

Kwa Tanzania wapo watu wanaofanya kazi hizi kwa malipo pia.

Lakini hapa unaweza kuanza na mtu ambaye una mahusiano nae ya karibu awe anakulelea.

Siku hizi teknolojia imekua rahisi sana unaweza kuwa na mawasiliano na mtu yeyote unayemtaka popote alipo duniani.

Unaweza kujifunza pia vitu vingi sana kupitia mitandao hii kama hapa facebook.

Unaweza kusoma vitabu na vitu vingi sana vile unavyovitaka.

Naomba nimalizie kwa kusema kwamba.
Kwa hiki ulichokipata leo ukikifanyia kazi.

Utakua mshindi uliyezaliwa kuwa.

Utafikia Hatma yako kwa kufuata haya, namaanisha wewe uliyesoma hapa.

I will see you at the top!

Nini kinachokufanya udhani utashindwa sasa?

Kwa mujibu wa Biologia, baada ya tendo la kukutana kimwili takribani mbegu milioni 200 hadi 300 hutolewa na mwanaumeโ€ฆhalafu zote huanza kupiga mbizi kuogelea kwenye njia safarini kukutana na yai la kike.

Ajabu ya kwanza ni kwamba sio zote 200 – 300 ambazo hufanikiwa kulifikia yai( nyingi huchoka na kufia njiani maana si mashindano ya mchezo mchezo).
Ajabu ya pili ni kwamba kati ya hizi 300 zinazofanikiwa kufikia yai, ni moja tu..moja tu itakayoshinda nakufanikiwa kupenya na kurutubisha yai, na kwa mantiki hii ILIYOSHINDA NI WEWE HAPO.

Umewahi kuwaza kuhusu hili vizuri?
Yaani ulishindana mbio hizo ukiwa huna macho na ulishinda, ulishindana bila elimu na ukashinda,ulishindana bila hata cheti chochote wala msaada wa yeyote โ€ฆ.na UKASHINDA.

Nini kinachokufanya udhani utashindwa sasa?
Tena sasa uko na macho yote, miguu, sasa Unamjua Mungu, sasa ukiwa na mipango,ndoto na maono.
Kumbuka ULISHASHINDA toka tumboni huna sababu ya kuwa na hofu yeyote, PAMBANA

AMINI UNA AKILI YENYE UWEZO MKUBWA WA KUBUNI WAZO LA KUWEZA KUKUSAIDIA KUFANIKIWA KIMAISHA

AMINI UNA AKILI YENYE UWEZO MKUBWA WA KUBUNI WAZO LA KUWEZA KUKUSAIDIA KUFANIKIWA KIMAISHA.

Huwa nikikaa na kufikiri ni namna gani binadamu aliweza kubuni ndege, meli kubwa hasa za mizigo, gari na vitu vinginevyo na badae kuja kuwa msaada mkubwa katika dunia yetu ya siku leo hata kurahisisha maisha katika eneo fulani lililokuwa na ugumu kwetu, basi nauona uwezo wa Mungu aliouweka ndani ya binadamu huyu ingawa yeye binafsi kama binadamu wakati mwingine hatulitambui hilo na kama tunalitambua basi ni wachache na wakati mwingine hatujakaa vizuri kuitumia hii fursa ya uwezo huo tuliopewa. Hii inaonyesha ni jinsi gani binadamu alivyo na uwezo mkubwa wa kufanya ubunifu kwa kupitia akili aliyonayo na kuleta mageuzi na mshangao mkubwa katika ulimwengu tunaoishi.

Hebu tazama wengi wa wabunifu waliojitoa kwa kuumiza akili na kubuni vitu vipya katika ulimwengu huu tunaoishi leo hii, ndio tunaowaona matajiri katika dunia hii ya leo kuliko watu wengine waliokataa kutumia uwezo na akili zao walizopewa na Mwenyezi Mungu na zaidi sana kubakia kulalamikia watu wengine wanaofanikiwa. Nataka nikuambie unauwezo mkubwa sana ndani yako unaoweza kuutumia ili kubuni jambo kubwa litakaloleta matokeo chanya na kuwa msaada mkubwa katika jamii yako unayoishi na kwako pia.

Ndio. Una uwezo mkubwa sana tena sana unaoweza kuleta matokeo chanya na makubwa katika ulimwengu wako na ukasahau hata habari ya kuajiriwa na kuanza kujiajiri binafsi kupitia jambo ulilobuni. Tatizo ni kwamba hupendi kutumia akili yako kufikiri kwa upana na kwa kiwango cha juu kwa hofu ya kupoteza muda, kuumiza akili, kutokutaka matatizo (stress), nakadhalika. Kila siku umekuwa ni mtu wa kusema โ€œmimi sitaki kuumiza akili yanguโ€ mara unasema โ€œmimi masuala yanayochosha akili yangu siyatakiโ€ unataka kufanya mambo marahisi marahisi ili utoke kimaisha, ni gumu sana kwa namna hiyo rafiki.

โ€œIf you do what is easy your life will be hard, but if you do what is hard your life will be easy.โ€ โ€“ Les Brown

Nataka nikuambie akili yako inauwezo mkubwa sana, narudia โ€œinauwezo mkubwa sanaโ€ tena sana wa kubuni biashara ya kukutoa kimaisha, kutatua matatizo yaliyo magumu kwa jamii iliyokuzunguka, kuleta mbinu na mikakati mipya kwenye kazi au ofisini ili kusaidia kampuni kusimama, nakadhalika. Tatizo unajitetea na kujenga hofu kubwa ndani yako ya kujitoa na kufikiri ili kuhakikisha unaleta matokeo mapya na makubwa mahali ulipo muda huu. Hebu fikiri kama binadamu huyu huyu unayemjua na aliye kama wewe alibuni balbu za umeme anaitwa Thomas Edison kutoka nchini Marekani; na zaidi sana binadamu huyu huyu kama wewe aliweza kugeuza historia ya muonekano wa magari na kuja na kitu kipya zaidi anaitwa Henry Ford, na binadamu huyu huyu aliweza kubuni biashara ya kuuza kuku walioandaliwa kama chakula na hatimaye kuwa na mgahawa mkubwa wa KFC uliosambaa karibu nchi 123 duniani kote anaitwa Harland Sanders. Na wengine wengi sana ambao sitaweza kuwamaliza kwa kuwataja wote mahali hapa siku ya leo.

Naamini wapo watu wanaoweza kujitetea na kusema kwa kuwa hao ni watu weupe yaani wazungu na sijaona mtu mweusi hata mmoja hapo. Hebu fikiri ni watu wangapi wanabiashara ambayo leo hii inawaingizia mabilioni ya pesa na wakati mwingine biashara wanazozifanya ni za kawaida na zilizokuwa zikidharaulika na watu kwenye jamii zao na wapo hapa afrika. Angalia mtu kama Aliko Dangote kwa sasa zaidi ya kujishughulisha na uzalishaji wa cement na bidhaa nyingine za ujenzi na hata biashara zake kubwa nyingine kwa sasa ameenza kuzalisha nyanya na kuuza kwenye nchi yake huko nchini Nigeria. Ulitegemea mtu kama huyu ambaye ni tajiri wa kwanza afrika kuwaza kufanya biashara kama hiyo ya nyaya kwa sasa? Yawezekana wewe ulipoambiwa kuuza nyanya uliona ni biashara kichaa na haina maana ya kuifanya. Ukweli ni kuwa usipende kuanzia pakubwa bali anza na madogo ili kukupeleka kwenye kilele chako cha mafanikio na kutimiliza ndoto yako uliyonayo.

Hivyo hivyo kwa Bakhresa, Mengi, Dewji, Sheria Ngowi na wengine wengi tunaowaona nchini mwetu Tanzania wamefanikiwa kiuchumi, hii yote ni kutokana na kuamua kubuni kitu kipya kilichoweza kuwa msaada mkubwa kwenye jamii yao na kuweza kuwaletea wao mafanikio makubwa katika maisha yao. Sheria Ngowi pamoja na kusomea masuala ya Sheria nchini India lakini alijua bado ana kitu cha ziada ndani yake kinachoweza kumlipa na kumfanya awe na uhuru wa kifedha na maisha mazuri sawa na anavyotaka. Leo hii ni mbunifu wa mavazi Africa nzima inamjua na kumtazama. Jiulize kama asingetumia akili yake kwa kufikiri zaidi na kufuata ndoto yake aliyokuwanayo leo hii ingekuwaje kwake na kwenye jamii yake iliyohitaji mchango wake?

Nataka nikuambie huwezi kutoka kwa siku moja ni lazima uumize kichwa na akili yako leo hii na kujua ni nini cha kufanya kinachoweza kukupa uhuru unaoutaka kesho. Na suala la kuumiza kichwa chako na akili ni sasa na si kesho, narudia tena suala la kuumiza akili yako kwa ajili ya kubuni wazo la kukutoa kimaisha โ€œni sasa na si keshoโ€ kama unavyofikiri. Usiridhike na maisha yako unayoishi leo, usiridhike na kipato unachokipata huku sema ukweli ndani ya moyo wako na kwa uhalisia hakikutoshelezi kabisa kufikia kwenye kilele cha mafanikio makubwa unayoyataka. Usikubali kuwa mvivu wa kuumiza kichwa na kutumia akili yako kwa ajili ya kuja na kitu kipya kinachoweza kuleta manufaa kwako na kwa jamii yako iliyokuzunguka, anza kuwa mbunifu ili uweze kufikia ndoto yako ya maisha.

Umiza kichwa kuanzia sasa na amini katika wazo (idea) utakayoipata ndani ya moyo na akili yako ili kukusaidia na wewe kuwa miongoni mwa watatuzi wa matatizo katika ulimwengu huu. Unaweza kutumia matatizo yaliyopo kwenye jamii yako kama sehemu ya kukupatia wazo jipya na baada ya hapo kubuni njia na mkakati wa kulitatua tatizo ili kuleta matokeo chanya katikati ya watu waliokuzunguka na kwako pia. Mwombe Mungu akupe mwongozo wa kukusaidia kulitimiza na kulifanya hilo wazo (idea) kuwa wazi katika ulimwengu wa nje ili usibaki na wazo lililo kwenye akili na kichwa tu pasipo kuleta matokeo na mchango wowote makubwa kwa watu wako.

Nakusihi usisubiri kesho. Usione una siku nyingi za kuwaza au kuleta matokeo (ku_implement) ya hilo wazo lako (idea) uliyonayo au ndoto ya siku nyingi unayotembea nayo kila kukicha pasipo kuweka vitendo vya kuifanya izae faida na matunda kwako. Anza leo kuhidhilishia dunia kuwa nawe unauwezo mkubwa aliouweka Mungu ndani yako. Usijikatae wala usiogope kukataliwa na wengine pale utakapofanya uamuzi wa kuja na kitu chako kipya kwenye jamii yako, kumbuka kukataliwa ni sehemu ya kukupeleka katika mafanikio. Kadri unavyoongeza kukataliwa ndio unavyoongeza kufanikiwa.

Kama unahitaji kuwa mbunifu wa mavazi kama sheria ngowi anza kubuni leo hii au ikibidi mtafute na uwe chini yake na afanyike kuwa msaada na mshauri wako (mentor) wa hicho kitu unachotaka kukifanya. Amini inawezekana kwani watu waliofanikiwa si wachoyo unapojishusha na kuonesha uhitaji wa kujifunza kutoka kwao. Kama unataka kuwa mfanyabiashara mkubwa kama Dangote lakini bado huna wazo la biashara. Basi elewa una uwezo mkubwa wa kuumiza kichwa na akili kuanzia sasa na ukapata wazo linaloweza kuishangaza dunia yote hapo badae.

Lakini kumbuka si lazima ukaja na kitu kipya kabisa kwani tambua unauwezo pia wa โ€œkuboresha wazoโ€ au kitu fulani kinachofanyika na watu wengine ila wewe ukaleta ubunifu mpya kwenye hicho kitu na kuleta utofauti mkubwa kwenye eneo (industries) hiyo. Na hii ndio njia inayofanyika kwenye makampuni ya simu, magari, televisheni, nakadhalika. Leo hii samsung akileta simu yenye kamera yenye uwezo wa mega pixel 16 kesho yake utasikia Iphone ametoa simu yake mpya yenye kamera yenye uwezo wa mega pixel 20. Huu ni ubunifu tu ili kuzidi kutawala soko na kuteka wateja wa soko la simu ulimwenguni kote. Nataka nikuambie nawe unauwezo wa kufanya ubunifu mkubwa kwenye jambo lolote lile ili kukuletea mafanikio makubwa na hatimaye ukafanikiwa kufikia katika ndoto yako.

Nataka nikuambie una mawazo milioni na zaidi ndani yako ambayo hadi sasa dunia inayasubiri ili yaweze kuwa msaada kwa watu wengi na kufanyika kuwa faraja kubwa hata kwa watu waliokata tamaa. Ndio. usishangae wala sijakosea kusema ni mawazo โ€œmilioni na zaidiโ€ uliyonayo ndani yako. Ni wewe tu umejidharau, ni wewe unajiona huwezi kuwaza na kutoka na kitu kipya au kilichojaa ubunifu, ni wewe tu unajaa hofu ya kukataliwa kisa unaona utaonekana unaiga, huigi kwani hata waandishi wanaoandika kama mimi wanaandika kutokana na walichokipitia kwenye maisha na kujifunza kwa wengine, ni wewe tu unajiona huna lolote na si chochote katika ulimwengu huu hivyo huwezi kufanya mambo makubwa. Unajikosea heshima kwa kujiwiza mawazo hayo ya chini na kumkosea Mwenyezi Mungu yeye aliyekuumba na kukupa akili zote timamu ili uzitumie kwa ajili ya kuwaza na kubuni mambo mapya yanayoweza kuwa msaada mkubwa kwako na kwa jamii yako iliyokuzunguka. Anza kuwaza na kuumiza akili na kichwa chako leo hii, na amini kesho utafanikiwa.

JIAMINI NA AMINI UNAWEZA. ISHI NDOTO YAKO.

Ni vizuri kujua haya

๐Ÿ‘‰๐ŸฟDegree au vyeti ulivyo navyo haviwezi kukupa mafanikio.
๐Ÿ‘‰๐ŸฟUzuri ulio nao hauwezi kukupeleka kwenye ndoto zako.
๐Ÿ‘‰๐ŸฟUsipobadilisha hao marafiki ulio nao hutofika mahali popote.

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUsipobadilisha vitendo unavyovifanya kila siku hivyo hivyo mafanikio utayasikia kwa wengine.

๐Ÿ‘‰๐ŸฟKazi au ajira unayoifanya usipojiongeza haiwezi kukupeleka kwenye maisha unayoyataka.

๐Ÿ‘‰๐ŸฟHuo mshahara unaolipwa usipoutumia vizuri na kujiwekea akiba au kuwekeza kidogokidogo hutoacha kulalamika kila siku mshahara mdogo au hautoshi.

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUsipoacha kukopa bila malengo mafanikio ni ngumu kuyapata.

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUsipowekeza muda kwa ajili ya kujifunza na kuelewa mambo mengi ya biashara na ujasiriamali kwa ujumla na kufahamu dunia imetoka wapi,iko wapi na inaelekea wapi huytoacha kulalamika.

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUsipolipia gharama za kujifunza na ukajifunza kweli kile unachoelekezwa ikiwa ni pamoja na Pesa na muda haya mambo waachie wengine.

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUsipobadili fikra na mtazamo wako huwezi kubadilisha chochote katika maisha yako.

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUkiacha kusikiliza kila aina ya ushauri unaopewa na ndugu zako,jamaa zako,marafiki zako,familia yako,majirani zako na kujisikiliza wewe mwenyewe utahangaika sana.

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUsipofanya bidii na juhudi na ukakubaliana na changamoto zozote utakazokutana nazo maisha yatakuwa magumu sana kwako.

Kumbuka mtu pekee Wa kuyabadilisha maisha yako na kukusaidia kufikia malengo na ndoto zako wala sio mwingine ni mmoja tu nae ni WEWE.
Badilisha fikra zako,badilisha mtizamo wako,badilisha maisha yako.

Shopping Cart
2
    2
    Your Cart
    ๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About