Sikiliza, hakuna haja ya kuketi chini ili kuelewa ujumbe huu: Ukweli unabaki kwamba wengi wanajihusisha kupita kiasi na yale yasiyo ya msingi katika safari yao ya mafanikio. Kuna msemo wa kiingereza unaosema “mind your own business,” tunapaswa kujiuliza tufanyeje na ushauri huu. Fikiria, unaifuatilia maisha ya Ali Kiba kwa kina kiasi kwamba unajua hata mambo ya faragha kama vile bafuni mwake, unazifahamu ratiba zake za ziara za mwaka mzima, hata zingine unataka kumwekea mipango. Je, ni kweli wewe ni mwanamziki au?
Umeona eee Uko bize kujua simba na yanga mara mbeya city……. Hivi unataka kuwekeza kwenye soka?? Cha ajabu wewe ni mwalimu tena wa Bible knowledge halafu Uko bize na simba mara yanga. Uko kwenye biashara lakini unafatilia Lini bunge litakua live sijui unataka utangaze biashara yako bungeni . Mara Lema ataachiwa Lini, wewe ni mwanasiasa?? See hauko serious kufatilia biashara yako ya vitunguu ina Changamoto zipi, faida, lugha gani utumie kwa wateja au msimu wa soko ni Lini??
Mimi sijawahi kumuona Dewji ana comment kwenye page ya east Africa TV kuchangia Mada zisizohusiana na biashara zake. Unajua matajiri wako bize kufatilia yanayo wafanya kutajirika zaidi wewe Je?? Masikini unafatilia mambo ya kimasikini siyataji unayajua…….
Nimeshindwa kufahamu iwapo utakuwa na mafanikio katika kujua mahali anapoishi Lady Jaydee siku hizi. Wakati huo huo, vitunguu vyako viko nje katika ghalani Iringa, na viko hatarini kuharibiwa na wadudu bila wewe kujua jinsi ya kuchukua hatua ili kupata soko. Muda wako mwingi unaupoteza kwa kutumia vifurushi vya intaneti vya mega mix kutoka Tigo kufuatilia udaku wa Sudy Brown. Inashangaza kuona unajiona kama miongoni mwa waandishi wa umbea wa Shilawadu.
Utaishia kusoma story za mafanikio ya akina Mengi, Dewji, Dangote, shigongo lakini yako itakua tu HISTORIA YA MAREHEMU KWA UFUPI ulisoma darasa la kwanza hadi Saba shule ya msingi mwembengoma……
Historia inafutika hapo hapo….
References:
Google ScholarResearchGate
Semantic Scholar
AckySHINE