SMS Nzuri: Meseji za Vihoja Vya Sikukuu Hii

Alichojibu dalali baada ya kufumwa na mke wa mtu ndani ya nyumba ya kupanga

Dalali aliwatafutia jamaa chumba Buguruni karibu na reli, nyumba nzuri sana. Jamaa na mkewe wakahamia kwa furaha, lakini furaha yao iliisha walipokuja gudundua nyumba ile iko karibu mno na reli treni ikipita mpaka kitanda kinacheza.

Siku hiyo dalali akapita mke akamwita na kumwambia tatizo wakati treni inapita, wakaanza kubishana, yule mama akamwambia dalali kwa kuwa kuna treni itapita sasa hivi… njoo ndani uone mwenyewe.

Bahati mbaya wakiwa wamejilaza kitandani ili dalali aone adhabu wanayopata, Mzee mwenye mali alirudi ghafla, akauliza,

‘Nyie mnafanya nini hapa?’

Masikini dalali kwa woga mkubwa akajibu’ Tunangoja treni’

Huyu mke kwa kupenda hela! Cheki anachomwambia mume wake

Jamaa karudi toka kazini mpole na hana furaha!
MKE; Vipi leo mbona mpole?
MUME; Ofisi yetu imeungua na watu wote waliokuwemo wamekufa.
MKE; Ilikuaje wewe ukapona?
MUME; Nilikua chooni jirani na ofisi najisaidia.
MKE; Loh maskini, familia zao itakuaje?
MUME; Watalipwa million 100 kila mfiwa.
MKE; KWA HASIRA, Ona sasa na wewe kunya kunya kwako umetukosesha mihela.. Ungeenda kunya akhera.

Kisa cha mzaramo na mchaga

MZARAMO V/S MCHAGA.
Mzaramo alitangaza anatibu magonjwa yooooooote
kwa tsh. 100,000/=
Na kama akishindwa kukutibu anakurudishia laki
yako nakukuongeza laki nyingine.
MCHAGA akaona hii fursa yakujipatia hela aiwezi mpita akaenda kutibiwa.
MZARAMO: “unaumwa nini?”
MCHAGA: “Sisikii ladha ya aina yoyote mdomoni kabisaaaa..”
MZARAMO: “sawa, toa laki kabisa..”
Mchaga akatoa.
MZARAMO akamuagiza msaidizi wake; “Naomba kikopo no.27 mpe anywe huyu..”
MCHAGA akanywa akatema faster; “Puh puu puu, Aisee huu si mkojo huu..?”
MZARAMO: “Umepona karibu tena..”
Mchaga aka-mind sana Kesho yake akarudi tena hakuamini ameliwa pesa yake.
MCHAGA: aisee nina tatizo la kumbukumbu nasahau
sanaaaaa..”
MZARAMO akamwambia “hakuna tabu, toa laki tukupe tiba..’
MCHAGA akatoa pesa akijua leo lazima afanikiwe..’
MZARAMO: “nesi naomba kikopo no.27..”
MCHAGA: “ASA CHALII ANGU HICHO SI CHA JANA CHA MKOJO HICHO AISEE..?”
MZARAMO: “UMEPONA KUMBUKUMBU UNAYO.

šŸ˜„šŸ˜„šŸ˜„šŸ˜„šŸ˜šŸ˜šŸ˜šŸ˜šŸ˜šŸ˜

Cheki hawa washikaji wanachokifanya baada ya kuvuta bangi, Bangi si mchezo

Kuna washikaji walikuwa wakivuta bangi… kiberiti kikawaishia… wakamtuma mwenzao akatafute kingine… bangi lilikuwa limemkolea… akazungukazunguka hatimaye akarudi palepale kijiweni…

MSHIKAJI:Ā oyaaa wanangu eeeh… niazimeni kiberiti mwanangu mwenyewe …..

WENZAKE:Ā baharia ee subiria kimtindo kuna mwana tumemtuma akatafute kiberiti.

Cheki huyu mzee alichomfanyia muuzaji wa pharmacy

Mzee kaingia pharmacy,
MZEE: Mambo mwanangu, kuna kitu naomba uonje nitakulipa
MFAMASIA: Kitu gani?….Mzee akatoa kichupa na kijiko akaweka …majimaji yaliyomo kwenye
kichupa kwenye kijiko na kumwambia mfamasia aonje, mfamasia akatia yale maji mdomoni na kuyazungusha zungusha mdomoni akionja;

MZEE: Nipe jibu, ina utamu wa sukari au chumvi au pilipili?
MFAMASIA: Kama chumvichumvi
MZEE: Hakuna sukari
MFAMASIA: Sukari hakuna kabisa
MZEE: Loh asante chukua hii alfu tano nashukuru sana, dokta alinambia nipime mkojo wangu kama nina kisukari, kumbe sina asante bwana mdogo

Haya mapenzi jamani! Umewah kumpenda kwa kihivi??

Sijui Kama ushawai fall in love ile haswaa..

yani unampenda mtoto hadi akikupigia ile sauti ilivo tamu unajiskia kutafuna na kuimeza hiyo simu

Akikuita tu “my love”unajiskia tu kuvua nguo mwenywe
..
hicho kiupendo ukiwa nae unajskia unaweza piga wanaume 8 kwa pamoja

Yani ile love mtashinda pamoja kutwa nzima afu usiku unakopa salio umpigie muongee

Yani yale mapenz kiasi ukiona love story za romeo na Juliet unaona hakuna wanachofanya coz mapenz yao hayafikii yenu..

ile true love akikuangalia machoni akuguse mashavu afu akwambie,”I love u”
Unajishikilia kwenye ukuta usizimie..

yani ukimfikiria unaweza kulala chini ya kitanda Ku dilute hiyo feeling coz ni too much..

Umewahi kufeel hivyo??

Kama ushawai experience hivyo?? Basi HIYO SIYO “LOVE” NI “BANGI” PLZ ACHA KUTUMIA!
#ishakua_biashara_kichaa

Cheki huyu jamaa anavyoungama kwa padri sasa

JAMAA: Baba Padri nimekuja kuungama
PADRI: Haya
JAMAA: Niliiba kamba
PADRI: Kamba?
JAMAA: Ndio, kamba lakini kule mwisho kulikuwa kumefungwa ng’ombe
PADRI: Kwa hiyo uliiba ng’ombe?
JAMAA: Kiukweli nilikuwa nina lengo la kuiba kamba, kwa bahati mbaya mwisho kulikuwa na ng’ombe
PADRI: Mi naona mueleze Mungu direct, mi sikuelewi kabisaaa

šŸ™ˆšŸ˜ƒšŸ˜ƒšŸ˜ƒšŸ˜€šŸ˜€šŸ˜€šŸ˜‚šŸ™Š

Huyu mama mkwe kazidi sasa

Eti kuna mkaka alitembelewa na mama yake mzazi. Wakiwa sebuleni yeye, mama na mke wake, mke wake akaanza kuonekana tofauti kama vile anajiskia vibaya. Akaenda chumbani. Baada ya muda mfupi yule mkaka akamfuata. Wakakaa sana huko kisha mkaka akarudi sebuleni kuendelea kuongea na mama yake. Lakini zipu ya suruali yake ilikuwa wazi. Mama akamuuliza, mkeo anaendeleaje? Akamuambia, anajisikia vzr sasa. Nimempa panadol. Mama akatabasamu na kumwambia mwanaye, sawa. Lakini siku nyingine ukishatoa panadol ukumbuke kufunga pharmacyšŸ˜‚šŸ˜‚

Hii ndio ngoma droo kwa wanaume kati ya wanawake

{ NGOMA DROO}
Sikuizi utawasikia wadada wakisema kuachwa na mwanaume asie na pesa nisawa na kuluhusiwa hospital

{Sasa na sisi} wanaume tunasema
Kuachwa na demu mpenda pesa nisawa na kumaliza mkopo benk šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚
Wanaume atutakagi ujinga!!!! Wanaume heeeeeešŸƒšŸ¾ā€ā™‚šŸƒšŸ¾ā€ā™‚šŸƒšŸ¾ā€ā™‚šŸƒšŸ¾ā€ā™‚

Duh! Tamaa mbaya, cheki kilichompata Huyu

HAHAHAHAHAAAAAA DUH TAMAA MBAYA

Muokota makopo katika uokotaji wake wa makopo akaona chupa ambayo ndani kuna ki2, alipoifungua likatoka jitu la ajabu. Huku akitetemeka lile jitu likamwambia kijana asante sana kwa kuniokoa omba vi2 viwili sasa hivi. Kijana kwa hofu akaomba pesa za kumiliki magari na majumba ya kifahari. Ghafla fuko la hela na pete ya bahati vikadondoka. Akaambiwa ombi la pili,akasema nibadilishe niwe kivutio ili nipendwe sana nakina dada Hapohapo akageuzwa akawa chipsi yai.!!šŸ˜‚šŸ¤£šŸ¤£šŸ¤£

Hii mitoto mingine mijinga, cheki alichokifanya huyu

Nimeamka asubuhi nikiwa na elfu 1 tu mfukoni, nikamtuma mtoto wa jirani akaninunulie maandazi nipate kunywa chai. Baada ya muda namuona anarudi huku analamba askrimu ya AZAM kama Simba vile. Nikamuuliza maandazi yako wapi? Akanijibu eti wakati anafika yanapouzwa maandazi akagundua kuwa kapoteza hela yangu, hivyo akaanza kurudi, ila bahati nzuri wakati anarudi ili kuja kunitaarifu kuhusu kupotea kwa hela yangu, njiani akaokota elfu 1 ambayo kuna mtu alipoteza ndio akaamua kununua askrimu….kwa sasa niko polisi na mtoto yuko dispensari na mamakešŸ˜€šŸ˜€šŸ˜€šŸ˜€šŸ˜€šŸ˜€šŸ˜€

Nilichomfanyia huyu aliyenizingua nilipomuazimisha pasi

šŸ™„šŸ™„šŸ™„šŸ™„šŸ™„šŸ™„
Jana nimeenda kuazima pasi chumba jirani, ili ninyooshe nguo zangu, Jamaa wakaniambia nichukue nguo nikanyooshe room kwao maana hawataki pasi yao itoke.
Sasa leo amekuja mmoja wao kuazima mopper akasafishe room, nimemwambia aje adekie humu humu…

Jamaa ameondoka nadhani atakua ameenda kuchukua maji
šŸ¤’šŸ¤’šŸ¤’

Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    šŸ  Home šŸ“– Reading šŸ–¼ļø Gallery šŸ’¬ AI Chat šŸ“˜ About