SMS Nzuri: Meseji za Vihoja Vya Kukuparaha

Hapo sasa patamu, cheki jamaa alivyowezwa na huyu dogo

Mfugaji mmoja alikwenda kwa mfugaji mwenzake (ambae pia ni bwana mifugo wa eneo lao) asubuhi moja. Alipobisha hodi mtoto wa kiume wa umri upatao miaka 12 akamfungulia mlango. Mazungumzo yafuatayo yakafuatia:

Mkulima: Baba yako yupo?

Mtoto: Hapana Mzee, amekwenda mjini.

Mkulima: Mama yako?

Mtoto: Nae kaenda mjini na baba.

Mkulima: Kaka yako Howard yupo?

Mtoto: Nae hayupo, wote yeye, baba na mama wamekwenda mjini. Kwani una shida gani? Kama kuna kitu unahitaji niambie maana nimeachiwa funguo na najua vifaa vinapowekwa.
Mzee akawaza kidogo halafu akasema: Kwa kweli nilitaka kuongea na baba, mama au kaka yako kwa kuwa kaka yako amempa mimba binti yangu.

Mtoto akafikiria kidogo halafu akasema: Kusema ukweli itabidi umsubirie baba, ila kwa kukusaidia ni kuwa baba hulipisha shilingi laki moja kwa kupandisha dume la ng’ombe na elfu hamsini kwa beberu. Ila sijui baba hutoza shilingi ngapi kwa Howard akifanikiwa kutia mimba.

Hii ndiyo bongo sasa!!

Hii ndio Bongo

Ilikuwa Ijumaa mida ya saa 10 jioni, mzee mmoja aliingia na kibinti kizuri kwenye yard ya magari mapya.

MZEE: Chagua gari unalotaka mpenzi….kabinti akazunguka yard yote mwisho akachagua Verrosa metallic .

BINTI: Mi naitaka hii

MZEE: Hakuna tatizo kabisaaa, mtoto mzuri kama wewe lazima upate gari uloichagua mwenyewe. Mzee akatoa kitabu cha cheki na kuandika palepale na kumpa mwenye yard

MUUZAJI: Sasa Mzee kwa kuwa umetoa cheki, gari utakuja chukua Jumatatu tukishahakikisha kuwa Account yako ina pesa benki. Naomba namba yako ya simu Mzee

MZEE: Hakuna tatizo (akampa namba). Haya twende zetu sweetie Jumatatu tunakuja wote kuchukua gari lako…

Siku ya Jumatatu mwenye yard kampigia simu Mzee.

MUUZAJI: We Mzee kavu sana, akaunti yako haina hata senti tano.

MZEE: Hilo nilijua, lakini wiki endi yangu ilikuwa tamu sana.

💦😆💦

Cheki masifa yalivyomponza huyu, Sifa nyingine ni mbaya jamani

Mbongo, Mganda, na Mkenya walikamatwa na makosa Uchina.

Wakaambiwa adhabu ni ama kifo cha moja kwa moja au adhabu nyingine ambayo atakayeifaulu atakuwa huru, atakayeshindwa atauawa.

Basi wao wakaomba wapewe hiyo adhabu nyingine wajaribu bahati yao.

Wakapelekwa msituni wakaambiwa kila mmoja aende kwa njia yake halafu arudi na matunda kumi ya kufanana.

Wakaingia msituni kila mtu njia yake.

… Mganda akarudi wa kwanza na machungwa kumi. Akaambiwa adhabu yake ni kumeza moja moja likiwa zima bila kufumba macho bila kulia wala kucheka wala kujitikisa mpaka yote kumi yaishe. Akameza la kwanza. Safi. Kumeza la pili, akashindwa kuvumilia akafumba macho. Akapigiwa risasi akafa.

Mkenya akaja. Ana vitunda vidogo vidogo kama pili vilaini. Akasomewa masharti. Akaanza kumeza bila kufumba macho wala kulia, wala nini… alipofika cha tisa akashindwa kuvumilia akaangua kicheko! Akapigwa risasi pia akafa.

Wakiwa kuzimu Mganda akamwuliza Mkenya, “Vipi, mbona ulishindwa kuvumilia wakati kilibaki kitunda kimoja tu?”

Mkenya akamjibu: “Mkuu, nilishindwa kuzuia kicheko maana nilimwona Mbongo anakuja na matikiti maji!”

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About