SMS Nzuri: Meseji za Vihoja Vya Jumatatu

Askari na yeye kumbe muoga, cheki anachomjibu afande

Askari wametumwa nyumba iliyokuwa kuna ugomvi wakafika wakatakiwa kuripoti kwa njia ya simu juu ya walichokikuta
ASKARI: Mkuu tumekuta mama mwenye nyumba kampiga mumewe chuma cha kichwa na kumuumiza vibaya sanaa

AFANDE: Kha! kisa mkasa mpk akafanya hivyo
ASKARI: Mama mwenye nyumba alikua anapiga deki mumewe akaingia ndani viatu kabla sakafu haijakauka
AFANDE: Sasa mmesha mkamata huyo mwanamke
ASKARI: Bado mkuu
AFANDE: Kha! sasa mnangoja nini
ASKARI: Si tunangoja sakafu ikauke

Read and Write Comments

Cheki nilichomfanyia boss wangu

Bosi wangu karudi safari yake kutoka serengeti..! Si akanitumia picha, lakini ilikuwa network yenyewe tabu.. kwahio picha haikufunguka na kwa vile niliona itachelewa kufunguka na ataona sikumjibu basi nami..

Nikampelekea msg nikamuandikia umependeza saana bosi mashaallah…!!
sasa baada tu ya kumfika msg.. na huku picha ikafunguka kumbe picha ya Sokwe..!!
Basi Kaniambia kesho niende ofsini kwake kuna barua yangu..
Nahisi hyo barua ina pesa, hapa cjalala, nmekosa usingizi kabisa,nawaza ninunulie nn hyo pesa.Na kesho asubuhi sa 12 asubuhi atanikuta ofisini kwake naisubiri barua, sipendagi ujinga mimi.

Read and Write Comments

Kilichompata sista duu bishoo wakati akijidai kununua pete

Mwanamke mmoja aliingia duka la vito vya thamani, akaona pete moja ya dhahabu nzuri sana amabayo ilikuwa kwenye shelf ya chini, wakati anainama apate kuitazama vizuri kwa bahati mbaya (au nzuri!), shuzi likamtoka- druuuuuu, soni ikamuingia huku akigeuka haraka kuangalia kama kuna yeyote dukani pale ameliskia shuzi lake, macho yakagongana na mwenye duka ambaye alikuwa karibu huku uso ukiwa umejaa tabasamu zito, mwana mama hakuwa na uhakika kama amesikika au hakusikika, akaona atumie nafasi ile kuyeyusha…Akauliza “Hii pete bei gani?” . Jamaa mwenye duka, huku akiangua kicheko, akajibu “Umeiona tu umejamba, je nikikuambia bei yake si utakunya kabisa?”Read and Write Comments

Shopping Cart