SMS Nzuri: Meseji za Vichekesho Vya Msimu

Jinsi ya Kubana matumizi X-mass

Badala yakupika PILAU tutapika TAMBI kwenye Xmas maana tutakua tumeokoa sh.15,000/= Vitunguu swaumu 2000, Vitunguu maji 1000, hiliki 1000, Magome 1000, Michele wa 2000, Soda 3000, Nyama 5000 . Fedha hizi zitatumika kununua mfuko wa cement ili tuanze kujaza kibubu cha ujenzi wa nyumba badala ya kupanga. Karibuni saana maji ya kunywa tumechemsha ndoo nzima.

🎀✨Marry Xmas & Happy new year.✨🎀

Cheki huyu mzee alichomfanyia muuzaji wa pharmacy

Mzee kaingia pharmacy,
MZEE: Mambo mwanangu, kuna kitu naomba uonje nitakulipa
MFAMASIA: Kitu gani?….Mzee akatoa kichupa na kijiko akaweka …majimaji yaliyomo kwenye
kichupa kwenye kijiko na kumwambia mfamasia aonje, mfamasia akatia yale maji mdomoni na kuyazungusha zungusha mdomoni akionja;

MZEE: Nipe jibu, ina utamu wa sukari au chumvi au pilipili?
MFAMASIA: Kama chumvichumvi
MZEE: Hakuna sukari
MFAMASIA: Sukari hakuna kabisa
MZEE: Loh asante chukua hii alfu tano nashukuru sana, dokta alinambia nipime mkojo wangu kama nina kisukari, kumbe sina asante bwana mdogo

Ndege ya Tanzania

Kuna maprofesa 40 walipanda AIR TANZANIA ili wasafari. Kabla ndege haijaanza kuondoka, Lilipita tangazo kama ifuatavyo:

Ndugu wasafiri wote, ndege unayotarajia kusafiri nayo imetengenezwa na wanafunzi wa Kitanzania.
Baada ya tangazo maprofesa wote waliteremka isipokuwa mmoja alibaki kwenye kiti chake
Walipomuuliza ni kwanini hakuondoka akajibu kwa haraka na furaha kuwa:
Kama ndege hii imetengenezwa na watanzania, hata kuwaka haitawaka!

Tofauti ya ukopaji wa mzungu na mswahili

MZUNGU: Hi, I need $100, will pay back on Monday

MSWAHILI: Kaka vipi, shwari? Dah.. hatuonani mzee, mishe vipi, mnatunyima nini? Juzi nimekuona kwa mbaaali… mzee shavu dodo, full kipupwe! Sie tupo bwana, shida tu, afu misiba mingi tu, wife nae kajifungua ghafla. Sasa, kuna cheque naisubiri haijatoka hadi leo, wanasema itatoka next week, hapa nimekwama kweli. Naweza pata ‘Laki Moja’ ya karibu hapo nitarudisha mwisho wa mwezi…?😂😂😂😂😂

Askari na yeye kumbe muoga, cheki anachomjibu afande

Askari wametumwa nyumba iliyokuwa kuna ugomvi wakafika wakatakiwa kuripoti kwa njia ya simu juu ya walichokikuta
ASKARI: Mkuu tumekuta mama mwenye nyumba kampiga mumewe chuma cha kichwa na kumuumiza vibaya sanaa

AFANDE: Kha! kisa mkasa mpk akafanya hivyo
ASKARI: Mama mwenye nyumba alikua anapiga deki mumewe akaingia ndani viatu kabla sakafu haijakauka
AFANDE: Sasa mmesha mkamata huyo mwanamke
ASKARI: Bado mkuu
AFANDE: Kha! sasa mnangoja nini
ASKARI: Si tunangoja sakafu ikauke

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About