SMS Nzuri: Meseji za Vichekesho Vya Msimu
Namna wazazi wanavyoongea na mabinti katika umri tofauti
Miaka 13: Usipende wavulana ni wabaya.
Miaka 18: Sitaki nikuone na yule mvulana tena!
Miaka 23: Lini utatuletea mchumba wako?
Miaka 26: Wenzio wanaolewa.
Miaka 30: Tumekuambia kwamba acha
kuchagua sana wanaume, hutaki kusikia!
Miaka 33: Kuna mtu wa Mungu yupo kule
anaombea unaweza kupata mchumba
Miaka 36: At least pata mtoto mmoja.
Miaka 39: We will take care of all the wedding
billsโฆyeyote ni sawa sisi tutagharamia kila kitu mwanetu wee mlete tu .
Miaka 45: hivi kweli nani alikuroga.?
๐๐๐ changamkia fulsa umri ukifika
Kali ya mwaka iliyotokea Benki Baada ya wezi kuiba
Kuishi kijijini kunahitaji moyo sana
..unaenda kuoga, unakumbuka kuwa umesahau sabuniโฆunaenda kuchukua sabuni kurudi bafuni, unakuta ng’ombe amekunywa maji yote..unaamua kufuata mengne,unarudi unakuta mbuzi kala sabuniโฆ๐๐๐๐
Angalia huyu jamaa alivyomuweza huyu binti wa chuo
๐๐๐๐ .. TABU KUDATE NA MADEMU WA CHUO
Demu ;ย Baby Safari Hii Nataka Pale Hostel Niwafunike Mashoga Zangu Wote.
Jamaa ;ย Poa Sweetie Ondoa Shaka Nitakununulia #Turubai Utawafunika Woteโฆ!!!
Demu:ย Mxiuuuuuuuu Lione Sura Kama Goti La mbuzi Na Namba yangu futa Nakublock Mpaka Sanduku la postaโฆ!!!
๐๐๐๐nmecheka adi nmelazwa
Angalia huyu polisi kitu alichonijibu
Nimefika hapa Polisi Station nimefarijika sana na Kustuka baada ya kumkuta Askari hapa Kaunta anasoma Biblia nikajisikia fahari kuona anasoma neno kituo cha Polisi. Nikamuukiza Afande ni Nani alimuua Goliathi? Akasema Muulize Afande Mwita mlango namba 2 ndo anausika na Kesi za Mauaji.๐๐
Faida 3 za uvutaji wa sigara
Ni hizi
1. Mvuta sigara hazeeki
2. Mvuta sigara haumwi na mbwa
3. Mvuta sigara nyumbani kwake haingii mwizi
UFAFANUZI
1. Hazeeki kwa sababu hufa mapema kwa kifua kikuu
2. Haumwi na mbwa kwa vile kifua na mapafu yanapooza na hulazimika kutembea na bakora
3. Nyumbani kwake haingii mwizi kwa kuwa inafika wakati ambapo halali:
atakohoa usiku kucha hivyo mwizi anajua yupo macho
kumbe kikohozi tu!
Kilichowakuta boss, mke wake na mfanyakazi wao
Bakari ni house boy mara nyingi huiba wine ya boss wake na kisha kuongeza maji kwenye chupa ili boss asigundue.
Mara kadhaa boss alihisi ladha tofauti anapokunywa wine hivyo kuhisi kuna mchezo mchafu alihisi tu Bakari anahusika.
Ilikua ni bahati tu alimvizia na
kumbamba Bakari akichakachua wine, kwa kuwa mkewe alikua
anamtetea Bakari, ili kumthibitishia mkewe kuwa Bakari ndo culprit, boss alianza kwa kumuuliza Bakari maswali.
Siku hiyo Bakari alikua jikoni, boss na mkewe walikua sebuleni.
Boss: Bakariiii!
Bakari: Naam baba!
Boss: nani anakunywa wine yangu?
Bakari kimyaaaa hajibu kitu!
Boss: Bakariiiii !
Bakari: naam baba!
Boss: nauliza nani anakunywa wine yangu halafu anajazia majiii!
Bakari kimyaaaaa!
Boss akaamua amfuate hukohuko jikoni.
Boss: Kwanini nikikuita unaitikia, nikikuuliza unanyamaza?
Bakari: baba huku jikoni ndo kulivyo, unasikia jina tu likiitwa lakini maneno menginehusikii, na kama huamini baki jikoni mi niende sebuleni.
Bakari akaenda sebuleni akaanza kuita.
Bakari:Babaa!
Boss: naam Bakari!
Bakari: Saa sita usiku huwa unaenda kufanya nini chumba cha house girl?
Boss kimyaaaa!
Bakari: Baba babaa!
Boss:ndio Bakari!
Bakari: Nauliza hivii, chumbani kwa house girl saa sita za usiku huwa wafuata nini?
Boss kimyaaaaaaa!
Boss akatoka nje: Bakari huku jikoni ni kweli husikii kitu zaidi ya jina!
Mke wa Boss akaingilia kati
Mama: nyie msinitanie kabisa mnasemaje?
Bakari: kweli mama ukiwa jikoni husikii kitu nenda uone
Mama akaenda na Bakari akaanza
Bakari: mamaaaa!
Mama: abeee!
Bakari: hebu niambie hiyo mimba ni ya baba au yangu?
Mama kimya
Bakari: mamaaaa!
Mama: abeeee!
Bakari: hebu niambie ukweli hiyo mimba ni ya baba au yangu??
Mama kimya
Mama akatoka nje: kweli humu jikoni kuna tatizo nilikuwa nasikia jina tu
Huyu mwanafunzi kweli kiboko
Ticha: Wa kwanza kujibu swali langu ataenda Home mapema..
John kusikia hivyo….Karusha begi la daftari nje…..`ย
`Ticha akauliza: Nani karusha begi nje!?!`*
`John: Mimi….. Kwa herii Mwalimu……` ๐๐,๐๐
Hapo sasa akili itakuja
Pale unapo gundua kuwa yule ulie mtukana kwenye bajaji ndio boss anaeenda kukufanyia interview๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ญ
My freand apo ndo utagundua kwaanini wimbo wa Taifa tokea 1961 ni audio aujatolewa video
๐๐๐๐๐๐๐๐



I’m so happy you’re here! ๐ฅณ









































































Recent Comments