SMS Nzuri: Meseji za Vichekesho Vya Msimu
Kapresha kakiamua kuja kanakujaga tuu, cheki kilichompata huyu mme wa mtu mpenda michepuko
Kimchepuko chako kinakuandikia meseji kama hii…
…Samahani baby kama unavyojua nimeokoka ,nimetubu kanisani lakini nabii kaniambia niwaombe msamaha wote niliowakosea.
Nimemkosea sana mkeo kwa kumwibia mumewe na nimepanga kuja kumwomba msamaha kesho ntakuja na nabii na Mchumba wangu mpya nilie mpata kanisani.
Samahani kwa usumbufu uliojitokeza lakini hilo ni kwa ajili ya utukufu wa bwana!!!
Wako Manka wa Magorofani😅😅
Angalia huyu Jamaa alivyomuweza huyu mrembo
Nipo kwenye daladala siti ya nyuma kabisa nimekaa na mrembo mzurii.sasa nikawa namtongoza kwa sauti ya chini sana watu wengine wasiskie,akawa hanijibu kitu,mala gafra akapayuka kwanguvu na kwa sauti ya juu iliyomshtua kila mtu.
”Nimesema stakii,stakii tena unikome”😳😳
Nami nikamjibu kwa sauti ya juu vile vile
”Kama umejamba nisikwambie bhanaa,kwani ww nani?”☹
😂😂😂😂😂😂😂😂😂
MIMI SIO MTU WA MCHEZO MCHEZO
Sipendag ujuinga mim
Eti kwa nini Watu hawapostigi hii? Hata selfie sijaonaga
Vijana mkiwa mnaendesha magari mna post mukiwa mpo beach mna post mkiwa kwenye masherehe mna post Lakin mkiwa mmeenda kwa mganga siwaoni kupost mitunguli na vibuyu vya mganga unakuwa je wa zee tena. 😀😀😀😀
Dunia ina mambo! Angalia kilichotokea baada ya mgonjwa kuwekewa macho ya paka
Kuna jamaa alipata ajali akapofuka macho👀, akaenda hospital akawekewa macho ya paka🐈🐱,
dokta akamuuliza: vipi saizi unaona?
jamaa: naona ila naona panya tu
👀🐀🐁🐀👀
BREAKING NEWS: WAZIRI ANASWA KOFI
Mkazi wa Mbagala Kibondemaji, Waziri Salum (23) amejikuta akinaswa makofi baada ya kupishana kauli na jirani yake.
Omba omba sio barabarani tuu
Boy:- baby ivi nikifa utakuja msibani?
Girl:-ntakuja ukinitumia nauli.
Hapo ndo unagundua kuwa sio kila omba omba yuko barabarani.
🤒🤒🤒🤒🤒🤔
Hii kazi kweli kweli, Ungekua wewe ungefanyaje?
UNATOKA SEBULENI UNAENDA ZAKO CHOONI UNAINGIA TU HIVI GHAFLA UNAKUTANA NA MZIGO MKUBWA WA MAVI JUU YA CHOO ALAFU UNAAMUA KURUDI ZAKO ILE UNATOKA TU UNAMUONA DEMU MZURI ULIYEMTONGOZA JANA ANAKUJA KUINGIA CHOO ULICHOTOKA WW NA KINA MZIGO WA MAVI JUU NA AMEKUONA WW NDIO UMETOKA MLE NDANI ..unaamua kurudi ili uka flash bahat mby maji hakuna.!!!
😁😁😁HAPO NDIO UTAJUA KWANINI SIKU HIZI HATUPENDI UJINGA😆😆😆😆
Soma hii, kama wewe ndio mzazi wa huyu msichana ungefanyaje?
Wewe ni mzazi mwanao anasoma kidato cha tatu mkoani umemsafirisha leo kwenda shule baada ya masaa matano ukasikia gari alilo panda mwanao limepata ajali wamekufa watu wote upo ktk harakati za kuandaa msiba,
mwanao anakupigia simu baba/mama mimi mzima sijafa mpenzi wangu ABDUL aliniambia nishuke Chalinze ili niwe nae kwa siku mbili alafu niende shule je, wewe mzazi unge mfanyaje mwanao?
Nani Mkali Hapa kati ya DEMU na MSHIKAJI?
“MAENEO FLANI ya KISHUA”
-Mshikaji kamwona demu mkali
anakatiza kitaa akamkubali akaamua
amfuate amtemee cheche
MSHIKAJI- mambo dada?
DEMU- pouwa
MSHIKAJI-
umependezaa!!!
DEMU- asante.
MSHIKAJI- unaweza ukanisaidia
namba
yako ya simu……..
maana duh
nmekukubali
kinyama.
Demu baada ya kuambiwa vile
akazama kwenye pochi lake akatoa
noti ya
sh.10000 akaandika namba yake
kwenye
noti akampa mshikaji.
Mshikaji kapokea ile noti kachana
sehem
iliyoandikwa namba halafu
kamrudishia
Demu noti yake..!!!
NANI ANA DHARAU
NA NANI JEURI..
DEMU AU MSHIKAJI??!
Recent Comments