SMS, Vichekesho, Mahusiano, Biashara na Ujasiriamali, Afya, Chemsha Bongo, Dini pamoja na Vitabu kwenye PDF

Karibu AckySHINE

🤣😃😂

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Madhara ya kunywa soda

Tafiti zinasema kwamba mtu mmoja anayekunywa soda moja kwa siku, anakunywa zaidi ya galoni au dumu 56 za soda kwa
mwaka.
Japokua kuna watu wamekiri kunywa hata zaidi ya soda moja kwa siku ambayo huenda wanakunywa zaidi ya hicho kipimo.

Biashara ya soda inalipa sana duniani kwani ni kinywaji cha pili
kinachoongoza kunywewa duniani baada ya maji.
Sasa ukiangalia mahusiano ya unywaji mdogo wa soda kila siku kiafya una madhara makubwa kuliko unywaji mdogo wa pombe kila
siku.

Yaani ni bora unywe chupa moja ya bia kila siku kuliko chupa moja ya soda kila siku.

Yafuatayo ni madhara ya soda ambayo yatakufanya ufikirie mara mbili kunywa soda tena.

1.Ugonjwa wa kisukari;

Kunywa soda moja ni sawa na kunywa vijiko 10 vya sukari, baada ya kunywa sukari hupanda sana mwilini na kongosho hutoa homoni ya insulini nyingi ili kushusha sukari.
Muda unavyozidi kwenda insulini huendelea kuishiwa nguvu[insulin resisitance] na hali hii husababisha kisukari.

2. Unene na kitambi;

Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Havard umegundua kwamba watu wanaokunywa soda hunenepa mara mbili zaidi ya wale ambao hawanywi hivyo kama uko busy unapunguza uzito na pia mnywaji wa soda basi unapoteza muda.

3. Upungufu wa madini muhimu mwilini;

Soda ina kemikali inayoitwa phosporic acid ambayo huzuia mwili kuchukua madini ya calcium kwenye chakula ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya mifupa na misuli yenye afya kweye mwili wa binadamu.

4. Ugonjwa wa kansa;

Soda ina kemikali inayoitwa caffeine ambayo imehusishwa na cancer mbalimbali za mwili mfano kansa ya kongosho, kansa ya utumbo na magonjwa mengine kama presha ya damu na kansa ya matiti.

5. Huongeza sumu mwilini;

Soda haina lishe wala faida yeyote ile kwenye mwili wa binadamu hivyo huongeza kiasi kikubwa cha sumu mwilini ambacho ni hatari sana kwa afya mtumiaji.
Sumu hizo huongeza hatari ya kupata ugonjwa wa presha, na kuua figo.

6. Hubadilisha rangi ya meno;

Kila mtu anataka kuwa na meno masafi na meupe lakini baadhi ya soda zina kiasi kikubwa cha tindikali ambacho hushambulia na kuharibu meno kwa muda mfupi hivyo kama unasumbuliwa na meno basi huu ni muda mzuri wa kuachana nayo.

7. Addiction;

Soda nyingi zina tabia ya kumfanya mtu apate ulevi wa soda husika yaani kuna watu unakuta anapenda sana soda fulani na asipoinywa kwa siku atahisi kama amepungukiwa kabisa na kitu fulani mwilini.
Hii itakufanya uwe mtumwa wa mwili wako mwenyewe.

8. Huongeza kasi ya uzee;

Sumu ambazo unazipokea kwenye soda zinazeesha mtu mapema sana yani kijana mdogo wa miaka 20 hujikuta anaonekana kama miaka 35.

9. Hupunguza sana maji mwilini ;

Soda ina kiwango kikubwa cha madini ya sodium ambayo humfanya mtu abaki na maji kidogo na kwa muda mrefu atapata matatizo mengine ya kiafya kama mawe ya kwenye figo[kidney stone] na mawe kwenye nyongo ya binadamu.

10.Mwisho;

Ni vizuri kubadili mfumo wako wa maisha na kuanza kunywa vitu ambavyo haviharibu mwili yaani badala ya kunywa soda basi tumia juice (unayoitengeneza mwenyewe) ambayo ni mbadala mkubwa wa soda, lakini pia unaweza kunywa maziwa na kadhalika.

Dunia haijali mazuri yako ila ubaya wako, jiamini songa mbele

Siku moja mwalimu wa shule aliandika ubaoni kama ifuatavyo:
9×1=7
9×2=18
9×3=27
9×4=36
9×5=45
9×6=54
9×7=63
9×8=72
9×9=81
9×10=90
Alipo maliza kuandika tu, akaona wanafunzi wote walikua wanamcheka, kwasababu alikua amekosea swali la kwanza.

Mwalimu aliwatazama wanafunzi, kisha akawaambia yafuatayo:
`”Nimejikosesha lile swali la kwanza makusudi, kwasababu nilihitaji mjifunze kitu kimoja muhimu sana. Mnapaswa kujua namna ambavyo dunia inaweza kuwachukulia. Unaona hapo, nimeandika kwa usahihi mswali tisa (9), lakini hakuna kati yenu aliyenipongeza kwa hilo; wote mmecheka na kunilaumu kwasababu ya kosa moja tu nililofanya.”`
Hivyo, hili ni somo kwenu:
`”Dunia haijali mazuri unayofanya hata ukiyafanya mara milioni, lakini fanya baya moja uone jinsi watakavyo kulaumu…”`
“`Hata hivyo usikatetamaa, MARA ZOTE SIMAMA IMARA NA USHINDE VIKWAZO VYOTE.” `
JIAMINI

Utajuaje kama una upungufu wa maji mwilini? Dalili ni hizi

Upungufu wa maji ni pale mwili unapopoteza kiasi kingi cha maji kwa njia mbalimbali, ikiwemo jasho na mkojo, mwili hupungukiwa maji na hivyo mtu huyo huambiwa ana upungufu wa maji. Tunaelezwa kuwa karibu theluthi mbili ya miili yetu imejaa maji.

Ili mwili uweze kufanya kazi yake vizuri, kiwango cha maji mwilini hakipaswi kupungua hata kidogo, hivyo kila mtu ana wajibu wa kunywa maji ya kutosha kila siku ili kulinda kiwago chake cha maji kisipungue na kinapopungua ndipo hapo mwili huanza kuonesha dalili za kukaukiwa maji (dehydration).

Zifutazo ndizo dalili za upungufu wa maji mwilini;

Dalili za upungufu wa maji kwa mtoto.

Kwa kawaida, dalili za upungufu wa maji mwilini hujitokeza zaidi kwa watoto wadogo kuliko watu wazima au wazee. Dalili za upungufu wa maji mwilini kwa watoto huweza kusabababishwa ama na kuharisha, kutapika, kutokunywa maji au vimiminika vingine vya kutosha.

Mtoto mwenye dalili za upungufu wa maji huweza kuonesha dalili zifutazo:

  1. Kukojoa mara chache sana
  2. Mdomo na ulimi kukauka
  3. Mtoto kulia mara kwa mara na anapolia machozi hayatoki.
  4. Mtoto kutokuwa mchangamfu
  5. Macho, tumbo au mashavu kubonyea

Dalili za upungufu wa maji kwa wazee.

Dalili za upungufu wa maji kwa wazee ni tofauti na watu wazima. Wazee wa umri zaidi ya miaka 60 huwa na ngozi iliyosinyaa na hata ukiiminya, hubaki katika hali hiyo kwa muda na unapoikwaruza alama hubaki.
Halikadhalika, wazee hukosa haja ndogo kwa muda mrefu, hupungukiwa uzito kwa kiasi kikubwa na hupatwa na homa.

Dalili za upungufu wa maji kwa wajazito.

Upungufu wa maji mwilini kwa waja wazito ni hatari kwa mama pamoja na mtoto. Dalili zinazoweza kujitokeza kwa waja wazito ni pamoja na:

  1. Kukojoa mkojo wa njano nyeusi
  2. Kuumwa na kichwa.
  3. Mwili kukosa nguvu.
  4. Kichefuchefu na kutapika.
  5. Kukaukwa na mdomo.

Ili kujiepusha na matatizo ya upungufu wa maji na hatimaye kujikuta unakumbwa na dalili kadhaa zilizoelezewa hapo, ambazo ziko pia kwa watu wazima wengine, ni kuwa na mazoea ya kunywa maji ya kutosha kila siku. Hata utakapozidiwa na kukimbizwa hospitali, hakuna dawa nyingine utakayopewa zaidi ya maji (re-hydrating solution) . Kwa nini usubiri hali hiyo ikutokee wakati unaweza kuizuia kwa kunywa maji tu?

Hivyo wito wetu kwako kuendelea kunywa maji mengi ya kutosha kadri uwezavyo hii itakusaidia sana kwa namna moja ama nyingine kuwa na afya bora

Jinsi ya Kulima Mgagani: Kilimo bora cha Mgagani

Utangulizi

Migagani, migange, mikabili au miangani ni mimea ya jenasi Cleome katika familia na oda Brassicales (kabichi). Mgagani (Cleome gynandra) au Spider plant kwa kingereza, ni mmea wa asili ya Afrika unaostawi vizuri kwa kumwagiliwa hapa afrika ya mashariki wakati wa joto. Pia huchumwa mashambani ikiwa imeota yenyewe zao hili hushambiliwa na magonjwa na wadudu mara chache. Majani na Matawi machanga yana virutubisho kuliko Sukuma wiki na kabichi. Mahitaji yake yanaongezeka kwenye miji midogo na mikubwa kila siku.

Mgagani wa kawaida, huliwa takriban kila mahali pa Afrika na katika mabara mengine pia. Wanawake wengi wenye mimba au waliozaa hula mmea huu, kwa sababu una chuma nyingi kiasi na husaidia kuongeza damu. Mboga ya mgagani huitwa magagani.

Aina Za Mgagani

Kwa Afrika kuna aina 50 za mgagani , lakini ni aina nne tu zinazoliwa. Aina bora zinazalishwa na kituo cha AVRDC-THE WORLD VEGETABLE CENTER zina majani mapana, uchungu kidogo na ina majani mengi Zaidi na huvunwa kwa muda mrefu. Aina hizi ni pamoja na PS ambayo ina shina na matawi ya zambarau na GS I yenye shina na matawi ya kijani, mbegu za aina bora zina weza kupatikana toka kwenye kituo cha the world Vegetable Center, Arusha Tanzania. Ikumbukwe kuwa wakilima wengi wa nchi za Tanzania na kenya wanalima na kuuza mbegu za aina hizi na pia baadhi ya makampuni ya mbegu yameanza kuuza.

Mazingira Mgagani Unapoota

Kwa asili mgagani unastawi vizuri sehemu zenye joto na udongo wa aina mbalimbali kama tifutifu. Zao hili halikui vizuri katika udongo unaotuamisha maji, au katika maeneo ya baridi au kivuli. Katika eneo la mita za mraba 1-2, familia inaweza kupata mgagani wa kula kwa muda wa miezi minne.

 


Kutayarisha Shamba La Kuotesha Mgagani

Anza kwa kutifua ardhi vizuri na changanya na mbolea ya samadi kwa kiwango cha kilo moja hadi mbili kwa mita mraba. Mgagani waweza kuoteshwa peke yake au kwa kuchanganywa na mazao mengine kama mnavu au mchicha.

Uoteshaji Wa Mgagani

Baada ya kuandaa shamba lako sia mbegu kwa kutawanya au katika mstari ya umbali wa sm 30-50, majira ya mvua au kwa kumwagilia, kina cha mstari kisizidi sm1, funika kwa udongo kidogo na mwagilia kama hakuna mvua. Punguza miche iliyosongamana inapokuwa na majani manne hadi matano na iwe katika nafasi ya sm 15-20 toka mche hadi mche kwa upandaji wa kutawanya.

Palizi Ya Mgagani

Hakikisha shamba ni Safi hasa mwezi wa kwanza baadae magugu yanaweza kuzuliwa Na kivuli cha mgagani umeota vizuri.

Umwagiliaji Wa Mgagani

Unyevu wa kutosha ni muhimu kwa zao hili na inashauriwa kumwagilia ni majira ya kiangazi angalau mara mbili kwa wiki. Mgagani hustahimili ukame kuliko nyanya au mchicha lakini mimea isiachwe ikanyauka.

Uvunaji Wa Mgagani

Kwa uvunaji wa moja kwa moja mimea inaweza kung’olewa baada ya wiki nne hadi sita, kwa kuvuna majani, uchumaji unaweza kufanyika kila mara hadi miezi minne, Mimea iliyo na umri wa Zaidi ya miezi minne, inaweza kukatwa shina na kuchipua na kuendelea kuvunwa baada ya wiki nne hadi miezi minne kulingana na hali ya hewa na matunzo.

 

Uzalishaji Wa Mbegu Za Mgagani

Kwa kawaida mgagani hutoa mbegu kwenye shina au matawi vifuko vya mbegu vikikauka huwa mbegu imekomaa. Mimea ikatwe usawa wa ardhi na kutungiwa kwenye sakafu. Safi na ngumu, kuondoa mbegu toka kwenye maganda. Ondoa maganda, mashina na majani yaliyochanganyika na mbegu. Uchafu mwingine mbegu zihifadhiwe katika mifuko ya plastiki au ya karatasi au makopo na kuweka sehemu iliyo kavu. Kwa kuwa mbegu zina mafuta ya asili ya dawa za kuua wadudu ni vigumu sana kushambuliwa na wadudu waharibifu.

Mauzo Ya Mbegu Za Mgagani

Makundi ya wakulima yaliyopata mafunzo ya uzalishaji wa mbegu sasa yanazalisha kwa ajili ya wakulima wengine. Katika nchi ya kenya ambapo mgagani unaliwa sana, uzalishaji wa mbegu hupatia wakulima mapato Zaidi kuliko kuzalisha mboga mbegu za mgagani zinaptikana madukani.

Mauzo Ya Mgagani

Matawi malaini na machanga yenye majani yanaweza kuvunwa na kuwekwa kwenye mafungu ya uzito wa gramu 100-200. Majani yaliyo kaushwa kwa jua na kuwekwa kwenye vyombo mbalimbali huuzwa.

Jinsi ya kuchagua rangi sahihi wakati wa Kujipodoa

YAPO mambo mabalimbali katika tasnia ya urembo hasa katika vipodozi yanayopaswa kuzingatiwa katika kuboresha muonekano wa mtu.
Moja ya mambo hayo ni ujuzi na uelewa wa kutumia rangi katika kujipodoa kwani ni wanawake wachache wenye ujuzi huu.
Katika makala hii, nitakuelezea namna ya kuchanganya na kutofautisha rangi za vipodozi, lengo likiwa ni kuboresha muonekano wako.

Uchanganyaji wa rangi za vipodozi ni muhimu sana kwani katika kujipodoa, rangi zote za vipodozi unavyopaka zinatakiwa zioane ili kuleta muonekano ulio sawa na wa kueleweka.

Kwanza kabisa unatakiwa uwe makini katika kuoanisha rangi za vipodozi pamoja na rangi ya ngozi yako, hivyo katika hili unatakiwa kuwa na ujuzi maalumu ili usije ukafanya makosa na kuharibu muonekano wako.

Pia inabidi ufahamu hatua za upakaji vipodozi ili usije ukafanya vipodozi vingine visionekane katika uso wako.

Namna ya kuoanisha na kutofautisha rangi

Siku zote vipodozi vyako lazima viendane na mavazi yako ili kuleta maana zaidi kwa mfano, mara nyingi rangi ya mdomo ‘lipstick’ huendana na vazi lako wakati shedo ‘eye shadow’ zinatofautiana.

Kwa nguo za pinki

Katika mavazi haya, unatakiwa kupaka rangi ya mdomo yenye rangi ya pinki ambayo itaendana sawasawa na mavazi yako huku ukichanganya na shedo ‘eyeshadow’, inaweza kuwa ya rangi ya bluu ili kuitofautisha na mavazi yako, hapo utakuwa sawa katika kanuni za urembo.

Vazi la kijani

katika vazi hili unatakiwa kupaka rangi ya mdomo yenye rangi ya kahawia huku ukichanganya na shedo ya rangi ya kijani au kahawia iliyoingiliana na pinki au rangi ya machungwa.

Kwa vazi la njano au kahawia

Katika vazi hili unatakiwa kupaka ‘lipstick’ ya rangi ya kahawia iliyokolea, kwa upande wa shedo waweza kupaka ya rangi ya dhahabu.

Kwa vazi la bluu

Katika vazi hili unatakiwa kupaka ‘lipstick’ yenye rangi ya pinki huku ukipaka shedo ya rangi ya bluu kwa mtindo huu utakuwa mwenye kuvutia siku zote.

Alichojibu dalali baada ya kufumwa na mke wa mtu ndani ya nyumba ya kupanga

Dalali aliwatafutia jamaa chumba Buguruni karibu na reli, nyumba nzuri sana. Jamaa na mkewe wakahamia kwa furaha, lakini furaha yao iliisha walipokuja gudundua nyumba ile iko karibu mno na reli treni ikipita mpaka kitanda kinacheza.

Siku hiyo dalali akapita mke akamwita na kumwambia tatizo wakati treni inapita, wakaanza kubishana, yule mama akamwambia dalali kwa kuwa kuna treni itapita sasa hivi… njoo ndani uone mwenyewe.

Bahati mbaya wakiwa wamejilaza kitandani ili dalali aone adhabu wanayopata, Mzee mwenye mali alirudi ghafla, akauliza,

‘Nyie mnafanya nini hapa?’

Masikini dalali kwa woga mkubwa akajibu’ Tunangoja treni’

Umuhimu wa kuvaa soksi

Miguu ni sehemu mojawapo inayotoa jasho sana hivvo ni vema kuiweka mikavu kuzuia ukuaji wa bacteria au fungus.Wakaka tunajua umuhimu wa soksi au tunavaa bila kujua na wengine hatuvai? Hii ni kwa wadada pia wanaovaa viatu kama raba au hata nyumbani. Ni vema sana kufahamu kwanini tunavaa soksi na mda mwingine soksi gani tuvae.

1. KUZUIA MAGONJWA YA NGOZI MIGUUNI.

Tumia sekunde tatu tu kuvaa soksi na ujikinge na maradhi haya ya fungus na bacteria, kama sio mpenzi was soksi nashauri ufikirie tena maamuzi yako ya kutovaa soksi.

2. EPUKA HARUFU MBAYA YA MIGUU

Image result for atletes foot
Kwa kweli hii ni kero kwako na wanaokuzunguka.Usipovaa soksi jasho lote la miguu litaenda kwenye viatu na ivo viatu kutoa harufu.Soksi hunyonya lile jasho na huzuia harufu iyo. Aya basi tushtuke aibu hii ya nini katika karne ya watanashati sisi.Tuvae soksi na kubadili kila siku.

3. LAINISHA NGOZI YA MIGUU YA YAKO

Nani hapendi miguu soft?? wadada kutwa kusugua miguu saloon.Simple ukirud nyumban kama sakafu ni ngumu vaa soksi zako nyepesi safi miguu iwe laini.Baadhi ya viatu pia vina surface ngumu kwa chini (wakaka) ukiweka soksi zako safi hamna maneno.

4. KUPUNGUZA MAUMIVU MIGUUNI

Hii hasa kwa watoto wadogo ..tuwazoeze mapema kuvaa soksi.Mtoto anatembea ndani Mara akanyage maji mara vitu vya ncha Kali….Pia kuna viatu ukivaa bila soksi lazima upate maumivu na kupata zile sugu nyeusi.

5. KUPATA JOTO NYAKATI ZA BARIDI

Wale was mikoa iliyo na baridi kwa sasa naamini tuna soksi za kutosha za miguuni na mikono.Kama kuna sehemu inayongoza kutoa joto ni miguuni na mikononi.Basi vaa soksi ili kuzuia joto lisipotee.

6. MVUTO

Ili sio geni, mi mtu akivaa viatu bila soksi kwa kweli napunguza maksi za utanashati…wengine wanasema kuna viatu vya kutovaa soksi. .hakuna kitu kama icho kuna soksi ndogo ambazo hazionekani kwa juu zimejaa tele madukani tutafte.Ebu mtu kavaa kiatu chake safi akiweka na soksi safi inaonekana mvuto lazima uwepo….Nani hapendi kuvutia??basi sote tunapenda tuvae soksi

Siandiki mengi sana, soksi sio jambo geni, tubadilike tujijali,.Ok unavaa soksi Je?unavaa soksi pea moja mara ngapi, unafua na kukausha vizuri maana soksi mbichi ni janga jingine la uchafu na maradhi.Kitu kingine ujue aina ya soksi nyakati za joto usivae soksi ambazo ni nzito sana vaa nyepesi, ambazo ni nzito vaa nyakati za baridi. Na soksi za watoto tununue ambazo hazibani sana.

Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About