SMS, Vichekesho, Mahusiano, Biashara na Ujasiriamali, Afya, Chemsha Bongo, Dini pamoja na Vitabu kwenye PDF

Karibu AckySHINE

πŸ€£πŸ˜ƒπŸ˜‚

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Jinsi ya kuongeza kiasi cha utokaji wa maziwa kwa kina mama wanaonyonyesha na kwa afya ya mtoto

Maziwa ni chakula kikuu cha mtoto punde anapozaliwa. Mama anahitaji kuwa na Maziwa ya kutosha ili mtoto aweze kuwa na afya. Zipo sababu mbalimbali zinazopelekea wakina mama wengi kushindwa kuzalisha maziwa mengi kwa ajili ya kuwanyonyesha watoto zao. Hata hivyo kama wewe ni mama na una tatizo hilo basi unatakiwa kufanya yafuatayio ili utengeneze maziwa kwa wingi;

1. Nyonyesha mara kwa mara.

Nyonyesha angalau mara nane kwa siku. Kadri unavyonyonyesha, ndivyo utatengeneza maziwa zaidi.

2.Tumia vinywaji vya kutosha na kula zaidi.

Epuka kukosa mlo wowote wa siku.

3. Pumzika mara kwa mara.

Iwapo baba na wanafamilia wengine watasaidia na kazi zingine za nyumbani, mama atamhudumia mtoto vizuri zaidi.

4. Hakikisha maziwa yametoka yote wakati wa kunyonyesha au unapokamua.

Usiache maziwa yako kujaa kwa muda mrefu. Hata kama uko mbali na mtoto hakikisha unakamua maziwa.

5. Hakikisha mtoto amenyonya maziwa yote mara mbili kila unaponyonyesha
6. Kwa kina mama ambao hawana maziwa ya kutosha wanaweza kuongea na daktari akawaandikia dawa za kusaidia kuzalisha maziwa.

Dondoo kuhusu tezi dume

Tezi dume kila mwanaume anazaliwa nayo ambayo inasaidia kutoa maji maji ambayo yanaweza kusaidia kutengeneza mbegu za kiume.

Maji maji hayo yana alkaline ambayo husaidia Wakati Wa tendo la ndoa asidi (acid) iliyopo Kwa mwanamke isiue mbegu za kiume.

Kwahiyo alkaline ikichanganyika na asidi tunapata neutral na hivyo kusaidia mbegu za kiume zisife zinapoingia Kwa mwanamke.

Kwenye uke kuna asidi ambayo inaua kila bacteria wanaoingia.

Acid+base=salt+water

Tezi dume endapo itakuwa zaidi ndo huweza kuleta madhara ambayo ni kufunga mkojo usitoke kwani hubana mrija unaotoka kwenye kibofu kwenda nje.

Tatizo hilo huwakumba zaidi wanaume zaidi ya miaka 50,60,80 japo sio wote.

Kinga yake.
1. Kunywa maji ya kutosha.
2. Kupunguza kula nyama nyekundu.
3. Kupunguza ulaji wa mafuta.
4. Kula matunda na mbogamboga.
5. Kushiriki tendo la ndoa angalau Mara moja au mbili Kwa wiki ili kupunguza maji maji kwenye tezi dume.
6. Kufanya mazoezi ya viungo.

Kwahiyo tezi dume ni kiungo ambacho wanaume huzaliwa nacho isipokuwa kinaleta madhara endapo kitakuwa kupita kiasi na hutibiwa na kupona.

Matibabu yake ni kufanya upasuaji na kupunguza ukubwa pamoja na kudhibiti homoni za ukuaji wake.

Tiba nzuri ya tezi dume ni kufuata ushauri hapo juu na si vidole

Jinsi ya Kuondoa Makovu Mwilini

Makovu sio kidonda naomba hili uelewe, ila makovu ni alama ya majeraha ambayo yamebaki kwenye ngozi baada ya kupona majeraha.
Kuna baadhi ya watu husumbuliwa na shida ya kuwa na makovu sehemu mbalimbali ya mwili.
Hivyo kama wewe ni miongoni mwao maandishi haya yanakuhusu sana.

Zifuatazo ndizo mbinu za kuondoa makovu mwilini.

1. Tango

Unachotakiwa kufanya ni; Pondaponda tango na kisha kutumia mchanganyiko wake kwa kupaka juu ya kovu. Hii husaidia sana kulainisha makovu na ikiwa utatumia kwa muda mrefu huondoa makovu pia.

2. Aloe vera.

Unachotakiwa kufanya ni; kata majani hayo na utumie utomvu wake kupaka katika makovu kisha mara baada ya muda Fulani utaona mabadiliko na itapunguza na kuondoa makovu.

3. Asali

Unachotakiwa kufanya; Paka asali juu ya kovu na kuiacha usiku kucha. Rudia mara kwa mara kupaka asali hadi pale kovu litakapotoweka.

Hii ndio sababu kwa nini huwezi kufanikiwa kibiashara

HUWEZI KUFANIKIWA KIBIASHARA KAMA UNAPENDA KUJIHURUMIA HURUMIA!
πŸ’₯Mama mmoja Mzungu alitembelea mlima Kilimanjaro miaka iliyopita. Alikuwa amepanga kupanda mlima Kilimanjaro mpaka kileleni, yaani Kibo na Mawenzi, ili hatimaye apewe cheti cha kupanda mlima mrefu Afrika.

πŸ’₯Lakini kwa bahati mbaya akiwa amefika katikati ya mlima alizidiwa kiafya na hatimaye akashushwa mlimani akiwa amezirai hadi hospitalini.

πŸ’₯Siku ya tatu alipozinduka hospitalini huku marafiki zake wakimpa pole, aliwajibu kuwa β€œMlima Kilimanjaro hauwezi kuongezeka urefu, lakini mimi mwanadamu nina uwezo wa kuongeza maarifa, nguvu na mbinu za kupanda milima wowote duniani. Kwa hiyo nitarudi tena wakati mwingine mpaka nipande mlima Kilimanjaro hadi kileleni, ingawa nimepata changamoto wakati huu.”.

πŸ’₯Alivyorudi kwao Marekani, alianza kufanya mazoezi tena ya kukimbia na kupanda vichuguu na vilima kwa muda wa mwaka mzima, na kisha mwaka uliofuata alirudi tena Tanzania, akapanda mlima Kilimanjaro mpaka kilele cha Kibo na mawenzi, na hatimaye akapewa cheti cha kupanda mlima Kilimanjaro!.

πŸ’₯Je huyo mzungu angeamua kusubiri mlima Kilimanjaro upungue urefu ndipo aje Tanzania kuupanda, jambo hilo lingewezekana?

πŸ’₯Je unataka maisha yawe rahisi ndipo uyamudu? Je unataka viwanja vishuke bei ndiyo ujenge nyumba yako? Je unataka ada za shule ziwe chini ndipo usome? Je unataka gharama za hospitali ziwe chini ndipo utibiwe? Je unataka mahari iwe chini ndipo uoe? Je unataka vitabu vya mafunzo ya biashara viwe bei chee ndiyo ununue? Unataka mshahara wako uwe mkubwa ndipo ufanikiwe? Je unataka shetani auwawe ndiyo umche Mungu? Je unataka dunia irudi nyuma, ndipo uweze kuyamudu maisha? Je, unataka urudi tumboni mwa mama yako ili uwe unakula na kulala bure? Ebo!πŸ™Š

πŸ’₯Kama nia yako ni kufanikiwa hutakiwi kujionea huruma, nenda kwa wakati na ujitoe hadi kieleweke.

Kila la kheri na pia nakutakia MAFANIKIO makubwa sana wewe na kizazi chako! Siri ya utajiri ni ubahil asikudang’anye mtu tumia hela ikuzoee hakuna aliyezaliw kuwa maskin!

Mambo ya kufanya ili kupona majeraha mapema

Hakuna mtu anayependa kupata majeraha au kuchelewa kupona majeraha. Kwa kuwa uhai na uzima wetu haupo mikononi mwetu, ni vyema tukafahamu kuwa kuna wakati tunaweza kuumia.

Kwa kutambua hili karibu nikufahamishe mambo matano unayoweza kuyafanya ili kuharakisha kupona majeraha.

1. Kula vizuri

Lishe bora ni muhimu wakati wote, lakini ni muhimu zaidi mara unapokuwa na majeraha. Ili uweze kupona majeraha mapema unahitaji ule matunda na vyakula vyenye protini, vitamini C, B12 pamoja na madini ya chuma kwa wingi.

Vyakula na matunda hayo ni kama vile machungwa, mapapai, mayai, maziwa, samaki, maharage, n.k. Kwa kula vyakula hivi mwili utaweza kutibu majeraha kwa haraka zaidi.

2. Pumzika vya kutosha

Kupumzika ni njia ya kuupa mwili nafasi ya kujijenga na kujitibu wakati wa majeraha. Kutokana na mtindo wa maisha au changamoto za kiuchumi, baadhi ya watu hawapati muda wa kupumzika wapatapo majeraha.

Hivi leo utamkuta mtu akiendelea na shughuli zake huku akiwa na plasta, au bandeji bila hata kujali. Ili uweze kupona mapema unahitaji kuupumzisha mwili kwa kiasi cha kutosha ili upone vyema.

3. Fuata maelekezo

Kutokana na majeraha uliyoyapata daktari anaweza kukataza usile au sifanye kitu fulani lakini wewe hutaki; je unafikiri utaweza kupona mapema?

Watu wengi hukatazwa vitu kama vile pombe au kazi ngumu mara wapatapo majeraha, lakini ni wachache ndiyo wanaoheshimu hili.

Ni lazima ufuate ushauri wa daktari ikiwa unataka kupona mapema.

4. Kunywa maji mengi

Maji huchukua takriban asilimia 70 ya mwili wa binadamu. Kunywa maji mengi uwapo na majeraha kutakuwezesha kupona majeraha yako mapema.

Maji huboresha kinga mwili, huboresha misuli pamoja na viungio (joints) mbalimbali hivyo kukuwezesha kupona majeraha mapema.

5. Ogea maji ya baridi

Tafiti mbalimbali zilizofanywa zimeonyesha kuwa kuna manufaa makubwa ya kuogea maji ya baridi. Manufaa haya pia yapo kwa mtu aliyepata majeraha.

Kuogea maji ya baridi kutasababisha mzunguko mzuri wa damu, hivyo viini lishe na tiba vitasafirishwa vyema kwenda kuponya majeraha; pia maji baridi hupunguza maumivu ya vidonda au majeraha.

Kwa hakika lishe bora ni tiba ya maradhi takriban yote. Katika makala hii umeona jinsi lishe bora pamoja na kuzingatia kanuni chache za msingi za afya kunaweza kukusaidia kupona majeraha mapema.

Askari na yeye kumbe muoga, cheki anachomjibu afande

Askari wametumwa nyumba iliyokuwa kuna ugomvi wakafika wakatakiwa kuripoti kwa njia ya simu juu ya walichokikuta
ASKARI: Mkuu tumekuta mama mwenye nyumba kampiga mumewe chuma cha kichwa na kumuumiza vibaya sanaa

AFANDE: Kha! kisa mkasa mpk akafanya hivyo
ASKARI: Mama mwenye nyumba alikua anapiga deki mumewe akaingia ndani viatu kabla sakafu haijakauka
AFANDE: Sasa mmesha mkamata huyo mwanamke
ASKARI: Bado mkuu
AFANDE: Kha! sasa mnangoja nini
ASKARI: Si tunangoja sakafu ikauke

Mavazi Mazuri kwa wanawake wanene

Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakiangaika kupata aina ya nguo za kuvaa tena hasa wanawake wanene, kutokana na maumbo yao wanaona ni kazi sana kutafuta nguo, wengine hukosa hata uhuru wa kutoka out na watu wao wa karibu kwa sababu tu wanakosa nguo.Wengi ujikuta wakichagua nguo pana pana ili kuficha maumbo yao, lakini kumbe unaweza kuwa huru sana na mwili wako.

Zifuatazo ni badhi ya tips zinazoweza kukusaidi kuchagua nguo za kuvaa kwa mwanamke mnene.Inawezekana nguo hizi unazo ndani lakini unashindwa kuzipangilia;

1. Kabla ya kuchagua nguo ni lazima kujua mwili wako una unene wa aina gani,ikiwa wewe ni mnene na unatumbo kubwa basi ni bora kuvaa gauni maana gauni uweza kukuweka vizuri na pia ni mazuri hasa kwa watu wanene.

2. Lakini pia kama wewe ni mnene na umebahatika kuwa na maziwa makubwa, ni vizuri kupendelea kuvaa nguo zenye v-shape, siri ya nguo hizi ni kwamba huwa na tabia ya kuficha ukubwa wa maziwa na kufanya uwe maridadi zaidi ila zingatia kuchagua brazia nzuri kuikaa blauzi yako sawia.

3. Kwa mwanamke mwenye hipsi anashauriwa kuvaa nguo zinakazo mfanya hasionyeshe sana hipsi zake tofauti ya yule hasiekuwa na hipsi , maana yeye anatakiwa kuvaa nguo itakavyo onyesha hipsi zake , hata hivyo kwa wanawake wanene wenye hipsi hawana haja ya kujibana sana kwa sababu hipsi huweza kujitokeza zenyewe tu.

4. Lakini pia kuchagua rangi ya nguo nzuri pia husaidia kupunguza au kuongeza umbile la mtu, kuna rangi huweza kukufanya ukawa mnene sana au mwembamba sana,kwa mfano nguo zenye mistari ya kulala sio nzuri kwa watu wanene maana hutanua miili yao.Lakini pia rangi za giza hupunguza muonekano wa unene ilihali rangi za mwanga huangaza na kufanya mtu aonekane sana.

Zingaia:

-Ni bora zaidi katika kuchagua rangi nguo za rangi nyeusi na nyeupe iliyochanganywa ni nzuri zaidi inafanya muonekano wa mtu uonekane maridadi zaidi.

-Lakini pia jitahidi kuvaa viatu vinavyoendana na mwili wako ,sio lazima kuvaa kiatu kirefu wakati mwili wako hauimili mikikimikiki ya kiatu kirefu, flatshoes pia hupendeza zaidi kwa mtu mnene .

Mambao ya saluni ni shida, cheki kilichotokea kwa huyu

DADA alienda Salon wakati anasukwa akaingia
MKAKA mtanashati,
DADA akaamua kujaribu bahati yake.
DADA:Mambo? KAKA:Poa.
DADA:Mimi na wewe tunaweza kuongea baade?
KAKA:Kuhusu nini?
DADA:Nimekupenda nataka nikutoe out.
KAKA:Sawa ila nitamwambia nini
MKE wangu?
DADA:Aah ilo sio tatizo mdanganye tu,mwambie unakwenda kumtembelea rafiki yako hospitalini.
KAKA:Mwambie mwenyewe huyo hapo anayekusuka.

Β 

Unajua nn kiliendelea?

Soma hii Kabla hujafikiria kula nyama ya nguruwe tena

JEE NYAMA YA NGURUWE (KITI MOTO) NI SALAMA KWA BINADAMU???

Hapa huwa kuna mvutano wa kidini sana juu ya nguruwe, Ila Leo napenda kuliweka sawa, kitaalamu kwa mujibu waΒ MEDICINE (Science)!!

Nguruwe ni mnyama anaeliwa na 38% ya watu wote duniani Na walaji wake ni nchi Magharibi na Kusini mwa Asia, Europe, Sub-Saharan Africa, America ya kaskazini , kusini mwa America, na Oceania.

Nguruwe ni mnyama ambae, Ana umbo la pekee sana, tukiangalia kuhusu madhara yake au faida yake , tunangalia vitu vinavyopatikana ktk mwili wake, tukilinganisha Na Faida.

FAIDA ZA NYAMA YA NGURUWE KITAALAMU

πŸ‘‰πŸΎKunapatikna vitamini muhimu ktk mwili Wa binadamu; ambavyo ni B1, B6 and B12
πŸ‘‰πŸΎUnapata madini ya Chuma, ambayo husaidia kuimarisha mifupa.
πŸ‘‰πŸΎNyama ya nguruwe inaimarisha ngozi yako Na kuifanya iwe laini.
πŸ‘‰πŸΎNyama ya nguruwe ina magnesium kwa wingi ambayo ina faida ktk mwili Wa binadamu
πŸ‘‰πŸΎNyama ya nguruwe ina protein ya kutosha, ambayo husaidia ulinzi wa mwili
πŸ‘‰πŸΎNyama ya nguruwe ina mafuta ambayo hutupa nguvu mwilini

HASARA YA NYAMA YA NGURUWE

Licha ya faida tajwa hapo juu, vile vile kuna hasara ya kutumia nyama hii.
πŸ‘‰πŸΎNyama ya nguruwe ; ina sumu yaΒ carcinogenΒ ambayo inasababisha kansa; kwa mujibu wa utafiti uliofanyika Na shirika la afya duniani (Β WHO), NaΒ The International Agency for Research on Cancer!!Β Utafiti huo ukaonesha kuwa ukila kila siku 50gms basi uwezekano Wa wewe kupata kansa unaongezeka kwa 18%
πŸ‘‰πŸΎAnasababisha Swine Flu kwa binadamu; hivi ni virusi vinavyosababisha mafua kwa binaadamu. Kwa mujibu wa utafiti uliofanyika naΒ Centers for Disease Control and PreventionΒ inaonesha influenza virus H1N1 na H3N2 ambaye anatokana Na Nguruwe(kiti moto) imeripotiwa kusababisha maradhi ya mripuko kwa nchi zaΒ MAREKANI
πŸ‘‰πŸΎNyama ya nguruwe ina minyoo wajulilanao kwa jina la trichinella worm , ambao wadudu hawa ni vigumu sana kuweza kufa kwa joto Hata la 100C , utafiti uliofanyika 1998 Na WHO ukaonesha nyama ya Nguruwe iliopikwa kwa Joto la 104C , Huwa asilimia 52.37% ya trichinella worm wanabaki kuwa hai!! Wadudu hao wakiingia ktk mwili Wa binadamu husababisha ugonjwa ujulikanao kwa jina la trichinosis;Β ambao huwa Na dalili kama ifuatavyo:
βœ…Homa kali sana
βœ…Kichwa kuuma
βœ…Kukosa nguvu
βœ…Maumivu ya nyama za mwili
βœ…Macho kuwa rangi ya pink(conjunctivitis)
βœ…Kuvimba uso Na kope
βœ…Kudhuriwa Na mwanga
πŸ‘‰πŸΎNyama ya nguruwe ina virus aina ya Hepatitis E virus (HEV); ambaye husababisha homa ya ini aina E
πŸ‘‰πŸΎWadudu wengine ni kama;
πŸ₯„Nipah virus
πŸ₯„Menangle virus
πŸ₯„Viruses Ktk kundi Paramyxoviridae
Ambao wote hao; huwa wanaleta madhara kwa mwili Wa binadamu!!
πŸ‘‰πŸΎNyama ya nguruwe husababisha Maradhi ambayo Yana resistance(ukinzani) NaΒ ANTIBIOTICS
πŸ‘‰πŸΎNyama ya nguruwe ina minyoo aina ya Taenia solium. Kwa mujibu ya shirika la Afya duniani(WHO) – Reference….open_http://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/taeniasis-cysticercosis
Wanasema; minyoo hii huwa;
πŸ‘‰Unaweza kuipata ikiwa hautapika nyama vizuri au Ukila nyama ya kuruwe ilioathirika(infected): Kwa hyo sio kila nyama ya Nguruwe iliopikwa vizuri, huwezi kupata minyoo hii.
πŸ‘‰Minyoo hii ikiingia ktk mwili Wa binadamu husababisha matatizo ya mfumo Wa fahamu (central nervous system) iitwayo neurocysticercosis
Mfano wake ni kifafa
πŸ‘‰30% ya wagonjwa wenye kifafa huwa ni wale ambao hushambuliwa Na minyoo hii ipatikanayo kwenye nguruwe
πŸ‘‰πŸΎWatu milioni 50 duniani wanaopata kifafa , huwa ni walaji wazuuri Wa Nguruwe.

JEE NG’OMBE, MBUZI, KONDOO NA WANYAMA WENGINE WALIWAO NA WENGI HAWANA MINYOO??

Ukweli ni kwamba Hata wanyama wengine nyama zao huwa zina minyoo aina ya Taenia saginata.
Ila minyoo ya Taenia saginata ni tofauti Na Taenia solium kwa sababu; Saginata wanakufa kwa joto Dogo sana, lakini solium wanahitaji 71C bila Hata kupungua!!
Swali langu kwako wewe msomaji Wa nakala hii;
πŸ‘‰πŸΎNani anaepika huku akipima joto limefika au laa???

HITIMISHO

Tahadhari, sana Na nyama ya nguruwe , kwa sababu madhara yake ni makubwa kuliko faida yake!!!

Shared from;
Dr Isack

Kilimo bora cha matikiti maji

Ili kulima tikiti maji, inakubidi uwe na sehemu ya kutosha, yenye jua la kutosha, maji mengi na ardhi yenye rutuba ya kutosha, matikiti maji hukua haraka kama mimea mingine ya jamii yake itambaayo mfano matango, maboga na makwash.

Hali ya Hewa

Matikiti yanahitaji hali ya hewa yenye joto na mwangaza wa jua wa kutosha.Yanahitaji kiwango kidogo cha unyevu kwa sababu unyevu mwingi unasababisha maradhi. Unyevunyevu mwingi unaadhiri ubora na utamu wa tunda.Pia kiwango cha joto kiwe baina ya sentigredi 18 hadi 38

Udongo unao hitajika

Matikiti yanastawi vizuri katika aina mbalimbali za udongo. Matikiti yanahitaji ardhi yenye rotuba ya kutosha na wenye kupitisha maji vizuri. Uzalishaji wa matikiti unaweza kuathiriwa na maradhi ya vimelea ya
Fusari (Fusarium). Wakulima wanahitajika kupanda mbegu zinazohimili
magonjwa ama kuwa na mfumo wa mzunguko wa mimea kwa zamu katika
kipindi cha miaka saba. Kiwango cha uchachu (pH) kiwe baina ya of 5.0-6.8 ilikuiwezesha mimea kufyonza madini.

Utumizi wa mbolea

Nitrojeni ina nyunyizwa mara mbili; wakati mmea una matawi kati ya 2 na 4 na pia sehemu inayobeba matunda inapoanza kutambaa.

Nafasi katikati ya mimea

Ukubwa wa tunda unaohitajika ndio utakao eleza nafasi inayopaswa kuachwa katitati ya mimea. Nafasi kati ya sentimita 100 kwa 150 ndio bora zaidi. Ekari moja inahitaji mbegu 5,000. Mimea zaidi inaweza kupandwa ikiwa unyunyizia maji ni kwa mifereji na dripu (drip irrigation).

Maua na uchavushaji

Uchavushaji ni muhimu. Weka mzinga wa nyuki ili kuhakikisha kuwa uchavushaji unafanyika. Njia zinazotumika kuzuia wadudu zitekelezwe kwa njia itakayo wahifadhi nyuki Inastahili kuwe na unyevu kiasi wakati wa maua na matunda

Jinsi ya kuzuia wadudu na magonjwa

Wadudu wanao vamia matikiti, melon fly na aphids ndio tishio kubwa katika kuvuna matikiti.Unatakiwa kutumia madawa yaliyo sajiliwa kupigana na wadudu hawa.
Maradhi ya fangasi kama Alternaria, Fusarium, Antrachnose na ubwiri poda (Powdery Mildews) ni makali lakini yanaweza kukabiliwa kwa kutumia madawa ya Fungicide na kupanda mbegu yenye kuhimili maradhi.
Magugu yaendelee kungo’lewa, angalia usiharibu mizizi ya
mimea.

Uvunaji

Matikiti maji huvunwa yakiwa karibu sana na kuiva. Huu ni wakati ambapo sehemu ya juu ya tunda inayo gusa mchanga ina rangi ya samli/njano au sehemu inayo beba tunda inapoanza kusinyaa.
Sehemu inayobeba ua inakatwa kuizuia kukwaruza ngozi ya tunda ambayo inaweza kusababi sha maradhi mengine. Matikiti yana hatari ya kupasuka wakati au baada ya kuvuna ikiwa mkulima atakosa kuzimudu vizuri Matikiti hayafai kurushwa wakati wa kuvunwa, wala kukanyagwa au kurundikwa zaidi.

Yafahamu Mambo Mbalimbali ya muhimu kuhusu kilimo cha Mazao ya Mboga Mboga kwa Ku-Download Kitabu cha MBINU ZA KILIMO BORA CHA MBOGA

Ni kitabu kinachotoa elimu ya Kilimo Cha Mboga. Kipo katika Mfumo wa PDF (Soft copy).

Kina kurasa 100 na utaalamu wa mazao zaidi ya 10, ambayo ni nyanya, kabichi, bamia, vitunguu maji, vitunguu twaumu, hoho, matikiti, karoti, uyoga na matango. Bila kusahau kilimo cha mboga kama chainizi na mchicha.

Pia utaweza kufahamu mbinu mbalimbali za kilimo cha mboga kama vile kuandaa shamba na kitalu, udhibiti wa wadudu na magonjwa katika mboga, kuvuna na kuhifadhi mboga, vilevile utajifunza kuhusu kilimo cha matone.

Kitabu hiki ni Soft copy [pdf] kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.

Shopping Cart
2
    2
    Your Cart
    🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About