SMS, Vichekesho, Mahusiano, Biashara na Ujasiriamali, Afya, Chemsha Bongo, Dini pamoja na Vitabu kwenye PDF

Karibu AckySHINE

๐Ÿคฃ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜‚

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Askari na yeye kumbe muoga, cheki anachomjibu afande

Askari wametumwa nyumba iliyokuwa kuna ugomvi wakafika wakatakiwa kuripoti kwa njia ya simu juu ya walichokikuta
ASKARI: Mkuu tumekuta mama mwenye nyumba kampiga mumewe chuma cha kichwa na kumuumiza vibaya sanaa

AFANDE: Kha! kisa mkasa mpk akafanya hivyo
ASKARI: Mama mwenye nyumba alikua anapiga deki mumewe akaingia ndani viatu kabla sakafu haijakauka
AFANDE: Sasa mmesha mkamata huyo mwanamke
ASKARI: Bado mkuu
AFANDE: Kha! sasa mnangoja nini
ASKARI: Si tunangoja sakafu ikauke

Madhara ya kumlaza mtoto kifudifudi, kumlaza kwa tumbo

Unafahamu nini kuhusu suala la kumlaza mwanao? Maana Mapokeo tuliyo yapokea enzi na enzi ni kuwa ukitaka mtoto wako alale bila kushtuka basi alalie tumbo. Bado watu wengi wanaendelea kufanya hivyo hata sasa hivi unaposoma makala haya.

Je madaktari wanasemaje kuhusu suala hili?

Sayansi inashauri kuwa ni hatari kumlaza mtoto kwa tumbo. Visa kadhaa vya watoto kupoteza maisha vimehusishwa na watoto kulalia tumbo.

Kuanzia mwaka 1992 Madaktari wa watoto nchini Marekani walipendekeza kuwa watoto wachanga walale chali ( walalie Mgongo) ili kuepuka vifo vya ghafla vya watoto. Kifo cha ghafla hutokea pale ambapo mtoto mchanga anakutwa amefariki akiwa usingizini.

Tangu pendekezo hilo la madaktari idadi ya vifo vya ghafla vya watoto imepungua zaidi ya nusu ya vifo vyote vya watoto vinavyotokea wakiwa usingizini.

Ni vizuri kuhakikisha kuwa kila mtu anayekusaidia kulea mtoto anajua jinsi ya kumlaza mtoto chali.

Muhimu

Hata hivyo kuna baadhi ya watoto unaweza kushauriwa na daktari iwapo mwanao usimlaze chali na alalie tumbo.

Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya Dengu (Dengue fever)

Ugonjwa wa dengue ni tishio la ugonjwa hatari linaongezeka siku hadi siku. Dengue ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyoenezwa na mbu aitwae aedes.

Ugonjwa huu huenea zaidi msimu wa nvua. Huchukua siku 3-14 kwa mgonjwa kuonyesha dalili za dengue. Dalili kuu za dengue huwa ni maumivu makali ya kichwa, mgongo pia kutokwa na damu maeneo ya wazi kama puani maskioni (Hasa watoto) .

Siku zote kinga ni bora kuliko tiba hivyo huna budi kufanya yafuatayo kujikinga na ugonjwa hatari wa dengue:

1. Epuka Kuvaa nguo fupi kama kaptura, shati au tisheti kata mikono. Vaa suruali na shati/sweta la mikono mirefu
2. Usiweke Makopo chini ya Viyoyozi kwani hudondosha maji yanayoweza kuwavutia mbu.
3. Maji ya kwenye makopo ya maua yabadilishwe mara kwa mara.
4. Epuka Kuanika nguo Mbichi ndani ya nyumba. Hii huwavuta mbu kuzaliana
5. Osha vyombo visivyotumika angalau mara moja kwa wiki.
6. ondoa madimbwi yoyote yanayotuwamisha maji.
7. Tumia chandarua unapolala nyakati za mchana.
8. Funika makopo ya taka ili kutowavutia mbu.
9. Kunywa maji mengi na jenga mazoea ya kunywa juice za matunda.
10. Usiache milango wala madirisha wazi bila sababu ya msingi.

Ifahamu Saratani ya Tezi Dume, chanzo, Dalili, Uchunguzi na Tiba

Tezi Dume ni nini?

Tezi dume (prostate), ni tezi iliyo kwenye kizazi cha mwanaume inayozalisha maji maji yanayobeba manii/shahawa. Inaizungukaย urethra, mrija unaotoa mkojo kwenye kibofu kwenda nje. Tezi dume ya kila mwanaume huongezeka ukubwa kadri umri unavyoongezeka. Kadri tezi inapokua na kuongezeka ukubwa,inaweza kukandamizaย urethraย na kusababisha matatizo ya kibofu na matatizo ya kukojoa. Tezi dume inapoongezeka ukubwa huitwa โ€benign prostatic hyperplasiaโ€ kwa kifupi โ€BPHโ€. Hii sio saratani, na haiongezi hatari ya kupata saratani ya tezi dume.

Saratani ya tezi dume inashika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo vinavyotokana na kansa kwa wanaume duniani. Pia ni chanzo kikuu cha vifo vinavyosababishwa na saratani kwa wanaume wenye umri wa miaka 70 na kuendelea. Hata hivyo, satarani ya tezi dume kwa sasa inawapata sana wanaume kuanzia miaka 25. Lakini kabla ya kuendelea mbele hebu kwanza tujue tezi dume ni zipi.

Kama tulivyosema neno saratani ni jina la gonjwa ambalo hutokea wakati chembe chembe za uhai au seli katika sehemu fulani ya mwili zinapoanza kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili na kutengeneza vijiuvimbe vidogo vidogo. Kwa kawaida seli huwa zinajigawa, kupevuka na baadaye kufa kwa kufuata taratibu za mfumo wa mwili. Lakini seli za saratani hazifuati mfumo huo. Badala ya kufa, zenyewe huishi muda mrefu kuliko chembe chembe za kawaida na wakati huo huo huendelea kutengeneza seli nyingine na kuwa uvimbe wa saratani au tumour.
Tezi dume linapatikana katika mwili wa mamalia dume tu na pale seli katika kiungo hicho zinapoanza kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili hapo ndipo mtu hupata saratani ya tezi dume. Ugonjwa huu pia hujulikana kama saratani ya kibofu cha mkojo. Saratani ya tezi dume huwapata wanaume tu na hasa wenye umri wa takribani miaka 50 na kuendelea. Kutokana na tafiti mbali mbali, saratani hii imethibitika kushika nafasi ya pili, ukiachia mbali saratani ya mapafu kwa kusababisha vifo vya wanaume wenye umri wa takribani miaka 50 na kuendelea.
Tafiti za Chama cha Saratani cha Marekani (ACS) na cha Afrika Kusini (CANSA) zimebaini kuwa, mwanaume mmoja kati ya sita hupata saratani ya tezi dume katika uhai wake. Kutokana na takwimu za mwaka 2010 za dunia nzima, malaria iliua watu laki tano, kifua kikuu watu milioni 2.1, Ukimwi watu milioni 1.8 na saratani watu milioni 9.9. Kwa mujibu wa takwimu hizo, idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na ugonjwa wa saratani ni kubwa ikilinganishwa na ya magonjwa mengine. Dk Emmanuel Kandusi ambaye ni miongoni mwa waathirika wa saratani hiyo, na mwanzilishi wa kampeni ya kuangamiza saratani ya tezi dume nchini Tanzania ya ’50 Plus Campaign’ anasema kuwa, ugonjwa huu ukitambuliwa mapema huweza kutibika kwa urahisi. Ameongeza kuwa, kutokana na ugonjwa huo kuwa hatari nchini, ifikapo mwaka 2020 unatarajiwa kuua watu milioni 20.

VIHATARISHI VYA TEZI DUME

Kuna vihatarishi vingi vinavyochangia mwanamume kupata saratani ya tezi dume. Vifuatavyo ni baadhi yake:-

๐Ÿ‘‰๐ŸฟKwanza kabisa ni umri. Nafasi ya kupata saratani ya tezi dume huongezeka sana hasa ukifikia umri wa karibu miaka 50 na kuendelea.

๐Ÿ‘‰๐ŸฟNasaba ni kihatarishi kingine ambapo wanaume wenye historia ya tatizo hili kwenye familia zao, yaani wale ambao mmoja wa ndugu zao wamewahi kuugua ugonjwa huu huwa katika hatarini ya kupata kansa hiyo kutokana na kurithi jeni za ugonjwa huo.

๐Ÿ‘‰๐ŸฟSuala jingine ni lishe ambapo wanaume wanaopenda kula nyama au (red meat) na walaji wa chakula chenye kiasi kikubwa cha mafuta hasa ya wanyama huwa katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume.

Vilevile wataalamu wanatumbia kuwa, wanaume wasiopenda kufanya mazoezi, wanene na wenye upungufu wa virutubisho vya Vitamin E pia wako kwenye hatari zaidi ya kupata saratani ya kibofu cha mkojo.
Wanaume wengine walio katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume ni pamoja na wale wenye asili ya Afrika (Weusi) ikilinganishwa na wazungu, wakulima wanaotumia aina fulani ya mbolea za kemikali, wanaofanya kazi katika viwanda vya kutengeneza matairi na wachimbaji madini, hususan aina ya cadmium.

DALILI ZA TEZI DUME

Hayo yote yakiwa ni tisa, kumi ni je, dalili za saratani ya tezi dume ni zipi?Katika hatua zake za awali, dalili za saratani ya tezi dume hazitofautiani na zile za kuvimba kwa tezi dume au BPH.
Dalili hizo ni pamoja na,

1) Kupata shida wakati wa kuanza kukojoa.

2) Kutiririka kwa mkojo baada ya kumaliza kukojoa.

3) Kukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu.

4) Kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku.

5) Kujikakamua wakati wa kukojoa na kushindwa kumaliza mkojo wote

6) kutoa mkojo uliochanganyika na damu.
Pamoja na kueleza dalili hizo watu wanapashwa kutambua kuwa, mwanaume anapoanza kuona na kuhisi baadhi ya dalili hizo, anapaswa kujua kuwa, seli za saratani katika tezi dume lake huwa zina umri wa takribani miaka saba na kuendelea.
Iwapo saratani imesambaa mwilini kiasi cha kuhusisha sehemu nyigine za mwili, mgonjwa anaweza kuwa na maumivu makali ya mifupa katika maeneo ya nyonga, mapajani na kiunoni.
Aidha mgonjwa huwa na dalili nyingine zinazoweza kumpata mgonjwa mwingine yeyote wa saratani kama vile kupungua uzito, kuhisi kichefuchefu, uchovu, kizunguzungu na kadhalika.

UCHUNGUZI WA TEZI DUME

Wanaume wanashauriwa kufanyiwa uchunguzi wa saratani ya kibofu cha mkojo au prostate cancer kwa kuwa imegundulika kuwa wanaume wengi wakiziona na kuzihisi dalili hizo huona soni kwenda kumwona daktari na kufanyiwa uchunguzi.
Baadhi ya watu huzihusisha na magonjwa ya zinaa au na dhana potofu za kishirikina. Wapo wanaokwenda mbali zaidi hata kuuita ugonjwa huo kuwa ni wa walawiti huku wengine wakiurahisisha kwa kuuita kuwa ni ugonjwa wa utu uzima kana kwamba saratani ya tezi dume ni jambo la kawaida kwa watu wazee.
Mambo kama hayo hupelekea wanaume wengi kujinyanyapaa wenyewe na hata wengine kujitibu kwa uficho au kwa kutumia waganga wababaishaji mpaka pale mambo yanapokuwa yamewazidi ndipo hupelekwa mahospitalini na mara nyingine huwa wamechelewa na kupoteza maisha yao bure kwa ugonjwa ambao ungeweza kutibiwa mapema.
Kwa ajili hiyo tunatoa wito kwa wanaume kutoona soni na kuwa na tabia ya kufanyiwa uchunguzi wa afya kwa ujumla, na hasa tezi dume angalau mara moja kwa mwaka.
Kuna vipimo viwili ambavyo daktari anaweza kumpima mwanaume ikiwa ni hatua ya kwanza ya kugundua ugonjwa huo. Vipimo hivyo vya kwanza ni “Digital Rectal Exam (DRE)” na cha pili ni “Prostate Specific Antigen (PSA)”. DRE pamoja na PSA huonesha uwepo wa tatizo kwenye tezi dume, lakini vipimo hivi havina uwezo wa kutofautisha iwapo tatizo hilo linamaanisha saratani au uvimbe katika tezi dume. Hivyo basi, ili kuweza kutofautisha kati ya magonjwa hayo mawili, kipimo kiitwacho Prostate biopsy hufanywa. Baada ya vipimo hivyo kama vitaashiria saratani ya tezi dume basi daktari anaweza kuamuru vipimo vingine ili kuthibitisha uwepo wa ugonjwa huo kama vile transrectal ultrasound au prostate needle biopsy.

MATIBABU YA TEZI DUME

Kuna njia kadhaa za matibabu ya saratani ya tezi dume. Hata hivyo uamuzi wa njia gani itumike unategemea ushauri na maoni ya daktari kulingana na hatua ya ugonjwa ulipofikia na umri wa mgonjwa husika. Katika hatua za awali za ugonjwa, daktari anaweza kushauri mgonjwa atibiwe kwa kufanyiwa upasuaji na tiba ya mionzi.
Hii ni katika hali ambayo kwa wagonjwa wazee, daktari anaweza kushauri mgonjwa kuwa chini ya uangalizi tu bila kufanyiwa upasuaji au bila kupatiwa tiba ya mionzi.

Matumizi ya dawa

Alpha 1-blockersย kama vileย doxazosin, prazosin, tamsulosin, terazosin, na alfuzosinย ni dawa zilizo kwenye kundi la dawa zinazotumika kutibuย shinikizo la juu la damu. Dawa hizi hulegeza misuli ya shingo ya kibofu na tezi dume. Hii huruhusu mkojo kutoka kwa urahisi. Watu wengi wanatumia dawa yaย Alpha 1-blockers,ย na husaidia sana kupunguza dalili zao.

Finasterideย naย dutasterideย ย ni dawa zinazopunguza kiwango cha homoni zinazotengenezwa na tezi dume,hupunguza ukubwa wa ย tezi dume, huongeza kiwango cha mtiririko wa mkojo, na kupunguza dalili zinazotokana na ukubwa wa tezi dume kuongezeka. Inaweza kuchukua miezi 3 hadi 6 kabla ya kuona mabadiliko makubwa katika dalili zako. Kutumiaย finasterideย naย dutasterideย kunaweza kuwa na athari kama vile, kupungua kwa nguvu za kiume na hata kuwa hanithi.

Daktari anaweza kuagiza upewe dawa za antibiotikiย ili kutibu kuvimba kwa tezi dume (prostatitis), mara nyingiย prostatitisย huambatana na kuongezeka kwa ukubwa wa tezi dume.

Upasuaji

Upasuaji wa tezi dume unaweza kupendekezwa ย iwapo :

  • Unajikojolea/ unashindwa kuzuia mkojo
  • Unakojoa mkojo wenye damu mara kwa mara
  • Unashindwa kukojoa mkojo wote,(Mkojo unabaki kwenye kibofu hata baada ya kukojoa)
  • Maambukizi ya mara kwa mara kwenye njia ya mkojo
  • Kushindwa kwa figo kufanya kazi
  • Mawe kwenye kibofu

Uchaguzi wa aina maalum ya upasuaji, mara nyingi hutegemea ukali wa dalili ,ukubwa na umbo la tezi dume.

  • Transurethral resection of the prostate (TURP): Hii ni aina ya upasuaji inayopendelewa zaidi kutibu ugonjwa wa tezi dume.ย TURPย hufanyika kwa kuingiza kifaa chenye kamera kupitia kwenye uume na kisha kukata na kuondoa tezi dume kipande baada ya kipande.
  • Transurethral incision of the prostate (TUIP): Upasuaji huu unafanana kidogo naย TURP, na hufanyika kwa wanaume walio na tezi dume isiyo kubwa sana. Kwa kawaida upasuaji hufanyika na kisha mgonjwa huruhusiwa kwenda nyumbani (hakuna kulazwa). Kama ilivyo kwaย TURP, kifaa chenye kamera huungizwa kupitia kwenye uume mpaka kuifikia tezi dume. Kisha, badala ya ย kukatakata na kuiondoa, daktari hufanya mkato mdogo kupanuaย urethraย ili kuruhusu mkojo kupita.
  • Simpleย Prostatectomyย : Mgonjwa hupewa dawa ya nusu kaputi na kisha daktari hupasua tumbo (chini ya kitovu) ili kuifikia tezi dume. Sehemu ya ndani ya tezi dume huondolewa . sehemu ya nje huachwa . Huu ni utaratibu unaochukua muda mrefu, mgonjwa huhitajika kulazwa hospitalini kwa siku 5 hadi 10.


Iwapo saratani imesambaa na kuathiri sehemu nyingine za mwili, matibabu yake yanaweza kujumuisha upasuaji wa kuondoa korodani, matumizi ya dawa za kupunguza kiwango cha homoni ya testosterone katika damu au hormonal therapy, au matumizi ya kemikali za kuua seli za saratani (chemotherapy).

Tukumbuke kuwa, saratani ya tezi dume ni ugonjwa wa kawaida kama yalivyo magonjwa mengine na uchunguzi na matibabu ya mapema huweza kuokoa maisha ya waathirika wengi wa ugonjwa huo.

Mambo 10 ambayo wanawake wamewazidi wanaume

1. Wana Nguo Nyingi KulikoWanaume.
2. Wanafahamu Nani Ni Baba HalisiWa Watoto Wao.

3. Ni Wepesi Kupenda NaWakipenda Hupenda Kweli.

4.Wanaoga Mara Nyingi Zaidi KwaSiku.

5. Wana Huruma Sana Ingawa MaraNyingi Huwa Inawaponza.

6. Wana Uwezo Wa KubadilishaTabia Ya Mwanaume Muda Wowote.

7.Wana Uwezo Wa Kuishi NaKupendeza Bila Kuwa Na Kazi WalaBiashara Yoyote.

8. Kwao Nywele Na Kucha Ndo Vitu Vya Kwanza Kufikiria WakitakaKutoka.

9. Wana Uwezo Wa Ku-Pretend Kwa Muda Mrefu Zaidi Hasa Kwenye Mapenzi.
10. Hawapendi pesa

Samahanini Jamani. hiyo ya 10 imeniponyoka ๐Ÿคฃ๐Ÿ˜Ž

Yafahamu Mambo Mbalimbali kuhusiana na Wanawake kwa Ku-Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

Kitabu hiki kina topiki Zifuatazo;
1. Mambo anayohitaji mwanamke kutoka kwa Mwanaume
2. Mambo yanayowavutia wanawake kutoka kwa wanaume
3. Mambo wanayoyapenda wanawake wakati wa kufanya mapenzi
4. Dalili za mwanamke kicheche
5. Maswali ya kujiuliza kama mwanamke anakupenda kwa dhati au anakudanganya
6. Tabia za mwanamke anayekupenda lakini hawezi kusema
7. Ishara za mwanamke aliyevutiwa na wewe
8. Dalili za mwanamke anayeelekea kukukubali
9. Mambo ambayo mwanamke hawezi kukwambia
10. Njia za kudumisha na kuamsha mapenzi na mwanamke

Kitabu hiki ni Soft copy [pdf] kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.

Tabia za kuepuka ili uweze kuwa tajiri

UKIWA NA HIZI TABIA 9, JIANDAE KUFA MASKINIโ€ฆโ€ฆโ€ฆโ€ฆ
By Kashindi Edson

“Umasikini hauji kwa bahati mbaya kama ubaguzi wa rangi au ukoloni, umaskini hutokana na matendo ya kila siku ya mwanadamu” (Nelson Mandela, R.I.P)

“Kila mtu anataka kufanikiwa, lakini si kila mtu yuko tayari kushika majukumu na wajibu wa kumpeleka kwenye mafanikio”(Mwl Nyerere, R.I.P).

“Kile unahokifanya muda huu ndicho kinachoashiria na kutoa picha kamili ya baadae yako”(Mahatma Gandhi, R.I.P)

“Ukizaliwa maskini sio kosa lako, ila ukifa maskini hilo ni kosa”(Bill Gate, The richest man in the world).

Mwalimu wangu wa chuo aliwahi kuniambia kuwa, “mstari unaomtenganisha maskini na tajiri ni mwembamba sana, kwa hiyo ni rahisi sana kuwa tajiri pia ni rahisi sana kuwa maskini”. Mpaka leo sijaelewa alimaanisha nini.

Watu wote waliofanikiwa katika nyanja mbalimbali za maisha, kwenye uongozi, biashara, kilimo, elimu, siasa, michezo, uandishi, muziki, afya, imani, utangazaji, nk huwa hawana hizi tabia 9 nilizokuandalia leo, kwa hiyo kama una kiu ya mafanikio kwa hicho unachopambania, achana na haya mambo 9 yafuatayo;

1. KUTOKUJARIBU.

Katika kutafuta mafanikio huwa kuna vitu viwili tu vya kuchagua. Tambua kuwa maisha ni vita. “Chagua kufa, au kupambana”. “Siogopi kufa, naogopa kutokujaribu'(Jay Z). Hakuna alie zaliwa anajua, jiamini, jaribu utafanikiwa.

2. KUTOKUJIFUNZA.

Che Guava mpaka anafariki library yake ilikuwa na vitabu zaidi ya 2000, mwenzangu na Mimi sijui hata kama una Biblia au Quran ghetoni kwako. Nkwameh Nkrumah library yake ilikuwa na vitabu zaidia ya 3000, Obama anakuambia kila akiamka asbuhi lazima asome kitu kipya. “JOSEPH=Jifunze, Ona, Soma, Elimika, Pitia, Hamasika.(Prof Jay)

3. WOGA & WASIWASI.

“Tunaweza tukamsamehe mtoto anayeogopa gizani, lakini sio mtu mzima anaeogopa mchana”(Plato, R.I.P). Kitu cha kuogopa katika maisha ni woga wenyewe. Kama hujiamini hutakuja kuwa mshindi katika jambo lolote. Fanya hicho unachofikiria kukifanya kwa moyo wa dhati, kama unaamini ni cha harali na kia manufaa kwako na familia yako, na jamii nzima. Acha tabia ya kuogopa kitu ambacho hakijatokea.

4. KUJILINGANISHA.

Kuna baadhi ya watu, huwa wangetamani kuwa kama watu Fulani. Kuwa wewe pia jiamini. Usitamani kuwa Magufuli, Kassim Majaliwa au Paul Makonda. Kila mtu ni wa pekee na maalumu. Jikubali kwanza afu wengine ndo watakukubali wewe. Weka nguvu kwenye ubora wako na sio kwenye madhaifu yako. Ukijilinganisha sana utakosa furaha ya nafsi maisha yako yote.

*5. KUWEKA VINYONGO.**

“Kuweka chuki na konyongo moyoni ni sawa na kunywa sumu ukidhani atakufa mtu mwingine”. Onesha upendo, sambaza upendo, hayo ndo mafanikio ya kweli.

6. UONGO

“Uongo utakupa ushindi wa siku moja, ukweli utaishi milele”(WEUSI), “Muongo hata akiongoea ukweli usimuamini”(FID Q). Ukiwa muongo huwezi kufanikiwa hata siku moja. “Unaweza ukawadanganya watu, lakini huwezi kuwadanganya watu wote, wakati wote”(Bob Marley). Ukweli kama jua, katika safari ya mafanikio huwezi kuvificha.

7. UVIVU & UZEMBE

“Nyumba yenye njaa ukisizi unapata zero”(Fid Q). Mafanikio huja kwa kupenda unachokifanya. Neno “kazi” katika biblia limeandikwa mara 600. Dangote analala masaa 3 tu kila siku, Mohammed Dewj anaamka saa 11 asbuhi kila siku. We kwepa majukumu tu, kesho utakula magodoro. “Uvivu unalipa muda huu, bidii & juhudi vinalipa baadae”.

8. STAREHE & ANASA KUPINDUKIA

Pombe, sigara, ngono, unga, bange, shisha, cocaine, nk vitu vibaya sana. Ni ngumu sana kufikia mafanikio makubwa kama una tabia kama hizi. “Sisi ni kile tunacho kula”. Mafanikio ya kwanza huanzia kwenye afya yako”. Afya ni utajiri. Pia starehe hupoteza muda sana. “Mavuno ya uzee, ni swaga za ujana, kwa ukila ujana kumbuka kula kiungwana”(Nikki Mbishi,).

9. LAWAMA & UMBEA

“Watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiria hujadili kuhusu mawazo, uwezo wa kati hujadili kuhusu matukio na wale wenye uwezo wa chini, hujadili kuhusu watu” We upo kwenye kundi gani? Bora ukawa kundi la kati kuliko hilo la chini kabisa, hilo ni la “wachawi”. Tusilamike, tupambane,lawama hazisaidii chochote.Ukiweka malengo yako, vizuri na ukaacha hizo tabia hapo juu, muda si mrefu itazifikia ndoto zako

Angalia huyu bibi alichotufanyia kwenye gari

โ€‹tulikua kwenye gari kibao ad wengne mlangon likasmimama kituo kimoja kulikua kuna bibi anataka kupandaโ€‹

Konda- bibi twende sit kibao ata utalala

Bibi – oooh sawa mjukuu

Konda – simama tu apo wanashuka mbele

Bibi – akacheka sana tu

Konda- mbona unacheka bibi

Bibi – mjukuu hawa wote hawashuki wanakufa apo mbele

Watu- simamisha gar

Saiv bibi kabaki mwenyewe amelala sit ya nyuma๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜…๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Jielewe, kipato chako kinakusaidia nini?

ASSET AND LIABILITY
Asset ni kitu chochote kinacho kuingizia pesa mfukoni uwepo au usiwepo.

Liability ni kitu kinachotoa pesa mfukoni kwako.
Ukitaka kuwa tajiri,hiki ndio kitu pekee unacho hitaji kukijua na kukifanyia kazi.
Matajiri wote wananunua Assets,lakini Masikini na wenye wenye maisha ya saizi ya kati wananunua Liabilities wanazodhani kua ni Assets.

Watu wengi ukiwauliza una Asset gan unayomiliki atakutajia vitu kama,nyumba,gari,simu,laptop, duka.
Ni sawa kama tu hivyo vitu vinakuingizia pesa,lakini kama havikuingizii chochote hivyo sio Assets bali ni Liabilities.

Hebu tuangalie nyumba,kama una nyumba yako ya kuishi mwenyewe hiyo ni Liability kubwa sana,maana haikuingizii hata mia,badala yake inakutolea pesa,utalipa umeme,maji,ukarabati na malekebisho ya vitasa,taa,furniture n.k,hayo yoote yanatoa pesa mfukoni.

Lakini kama nyumba umepangisha,hiyo ni Asset. Gari,kama unaitumia kwa matumizi yako binafsi ya kila siku hiyo ni Liability kubwa,itahitaji mafuta,service,na kama umenunua kwa mkopo wa Bank ndio balaa zaidi,ila kama ni la biashara hiyo ni Asset.
Simu ambayo haikuingizii pesa yoyote zaidi ya kukumalizia vocha na kuishia kuchart,hiyo ni Liability, Tv na radio hata duka pia,maana siku umelifunga huingizi chochote,matumizi yoote unategemea dukani,badala ya duka kukupa faida,unachukua mshahara unaongeza mtaji.

Wasomi wengi walioajiliwa wanakufa masikini kwasababu mishahara yao na mikopo wanayochukua inaishia kununua liabilities kama furniture, TV,radio,simu kubw,gari,fridge,nguo,viatu, badala ya Asset ambazo zingewaingizia pesa zingine,mwisho wanaishia kuuza liabilities zao na kubaki masikini kabisa.

Watu wengi wanadhani wakiongezewa mshahara wata tatua matatizo yao,badala yake matatizo yanaongezeka maana mshahara(Income) ukiongezeka,matumizi(Expenses) pia yanaongezeka hivyo kuongeza column ya Liabilities. Na hii yote ni kwasababu hatufundishwi elimu ya pesa dalasani.

Matajiri woote wana kuza upande wa kipato(Income) na kupunguza upande wa matumizi(Expenses) kwa kununua Assets nyingi na kupunguza Liabilities,wananunua Luxuries kama gari,tv ,sm kubwa pale tu Assets au vitu walivyowekeza vinapowapatia faida,hivyo faida ndio inanunua magari,nyumba,TV nnk, ndio maana wanasema siri ya utajiri ni ubahili,lakini watu wengine kadri kipato kinapoongezeka na matumizi yanaongezeka.
Kama unataka kua tajiri lazima ujue pia maana halisi ya neno utajiri(Wealth).

Wealth is a person’s ability to survive so many numbers of days toward, or if you stopped working today,how long could you survive?
Maana yake,kama leo utaacha kufanya kazi ambazo zinakuingizia kipato,una uwezo wa kuendelea kuishi kwa muda gani??
Ukiona ukiacha kufanya kazi huna uwezo wa kumudu mahitaji ya kila siku kwa muda hata wa mwaka mmoja ujue wewe bado huna Mali(wealth) maana huna Assets zinazoweza kukuingizia kipato cha kuweza kukufanya uendelee kuishi pindi uachapo kazi.

Jiulize msharaha wako unanunua Assets au Liabilities, na pia ujiulize are you Wealth or not?

Mambo ya Muhimu kufahamu kuhusu tatizo la mgongo wazi

Uti wa mgongo ulio wazi( Spinal bifida) ni hali ambayo mtoto anazaliwa nayo huku uti wa mgongo (mishipa ya fahamu mkubwa unaotoka kwenye ubongo) ukiwa wazi kutokana na mifupa (vipingili vya uti wa mgongo) kutokufunga vizuri.

Mgongo wazi(spinal bifida) inaweza pata watoto 3 kati ya watoto 10000 wanaozaliwa.

Uti wa mgongo hutengenezwa mara tu baada ya mimba kutungwa, ikiwa kuna kasoro katika utengenezaji wa uti huu basi sehemu fulani ya uti wa mgongo itabaki bila kuzibwa.

Visababishi

Kuna sababu mbalimbali zinapelekea uti wa mgongo kutoziba, ambazo zinaweza zuhilika, nazo ni Upungufu wa folic acid(vit B9) na vitamin B12 katika kipindi cha ujauzito, katika kipindi cha miezi ya awali.

Mama mjamzito kupiga X-ray, mattumizi ya dawa za kifafa katika kipindi cha ujauzito .

Pamoja na maambukizi ya baadhi ya virusi kwa mama mjamzito.

Aina

Zipo aina mbiliza tatizo la tundu katika mgongo ama mgongo wazi

Aina ya kwanza ni occultaย ambapo huwa na aina mbili pia, aina ya kwanza ni ile ambapo panakuwa na vinyweleo tu vinavyoonekana nyuma chini ya mgongo bila kuwa na dalili zozote zile, ama kunaweza kujitokeza kwa kuta zinazofunika mishipa ya fahamu tu.

Aina ya pili ni ni cysticaย ambapo panakuwa na vifuko vinavyofunika mishipa ya fahamu pamoja na mishipa ya kuchomoza katika tundu la mgongoni.

Aina hii ni mbaya zaidi kwani linaweza kusababisha mtoto asitembee ama asiweze kuzuia haja kubwa na ndogo.

Dalili

Dalili huwa kama zifuatazo
Kuwa na uvimbe nyuma chini ya mgongo.

Kuwa na vinyweleo sehemu za chini za mgongo bila kuwa na tatizo la mishipa ya fahamu
Kushindwa kutembea ama kukosa hisia katika miguu

Mtoto anaweza kushindwa kuzuia haja kubwa ama ndogo endapo mishipa yote ya fahamu imepita katika tundu hilo.

Na dalili zingine zinazoambatana kuharibika kwa mishipa.

Matibabu

Upasuaji
Upasuaji ni tiba pekee ya uti wa mgongo ulio wazi(spinal bifida) inayofanywa na madaktari bingwa wa upasuaji wa mishipa ya fahamu(neurosurgeons) wanachofanya ni kuziba lile tundu lililowazi.

Dawa na viinirishe

Wanawake wengi walio katika kipindi cha kuzaa na wajawazito hawatumii vyakula vyenye vitamin B na folic acid inavyopaswa, vyakula hivyo ni matunda,mboga za majani, mbaazi na choroko.

Mwanamke mjamzito akipata lishe yenye virutubisho hivyo pamoja na kunywa vidonge vya folic acid, kwa asilimia 30% inaweza kupunguza hatarishi ya kupata watoto wenye uti wa mgongo ulio wazi.

Pia kwa wanawake wajawazito katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo, wanashauriwa kutokupiga X-ray.Inawezekana mwanamke akawa hatambui kama ni mjamzito,kipimo cha mkojo cha ujauzito(UPT-urinary pregnancy test) kifanyike kwa haraka kama mwanamke haelewi vizuri mzunguko wake wa hedhi kabla hajapiga X-ray ikiwa ana tatizo lingine la kiafya,

Mwanamke mwenye kifafa akiwa mjamzoto pia yupo kwenye matibabu, awahi haraka kwa daktari kushauriana ni nini zaidi cha kufanya ili kumsaidia.

Wanawake wajawazito wanashauriwa kuhudhulia kliniki mapema zaidi ili wapate elimu ya lishe na kuweza kuanza mapema kutumia folic acid kama kinga ya Mgongo wazi.

Kumbuka kwamba

Jamii inapaswa kujua kuwa Mgongo wazi(Spinal bifida) haitokani na mambo ya kishirikina bali ni hali ambayo inaweza kuzuilika. Mzazi yeyote mwenye mtoto mwenye Mgongo wazi anashauriwa ampeleke mtoto wake hospitali ili apate maelekezo ni wapi mtoto anaweza kupata matibabu ya upasuaji.)

Mambo ya Msingi kujua kuhusu uvaaji wa Tai

Kuna mambo mengi ya kufanya ili tuwe watu wa kuvutia kila wakati.Mpangilio wa mavazi hufanya mtu kuonekana maridadi.

Kama wewe ni mvaaji wa tai unapovaa unazingatia mambo yapi? Na je unafunga tai yako kwa namna inayokubalika?

Wengine huwa hawafahamu jinsi ya kufunga tai na hivyo kuleta mushkeri wakati wa kuvaa tai na kusababisha tai kukaa upande. Unapoamua kuvaa tai na shati ambalo halijanyooshwa ambalo linakuwa kwenye mikunjo au kuvaa tai na ndala unakuwa umeua maananzima na kulivunjia heshima vazi hili.

Tai ni vazi lawatu walio maridadi kama huwezi kuwa maridadi basi vazi hili halikufai kabisa.
Unapovaa taa unatakiwa kuzingatia aina ya umbo lako kama wewe ni mnene vaa tai inayoendana na mtu mnene na kama wewe ni mwembamba basi vaa tai inayoendana na mtu mwembamba.

Kuna wengine huvaa tai zinazofika magotini na kuwa kichekesho anapopita mtaani
Tai ni vazi ambalo huongeza heshima na hadhi ya mvaaji cha muhimu ni jinsi gani unavaa tai yako na ikiwezekana jaribu kumechisha tai na suruali kwa vile ili tai upendeze ni laima iendane na nguo unayovaa.

Ni vyema ukahakikisha kuwa unakuwa na tai zenye rangi tofauti ambazo zitaendana na nguo unazovaa.

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About