SMS, Vichekesho, Mahusiano, Biashara na Ujasiriamali, Afya, Chemsha Bongo, Dini pamoja na Vitabu kwenye PDF

Karibu AckySHINE

๐Ÿคฃ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜‚

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Angalia huyu jamaa alivyoachika na msichana wake kwa kujidai kuongea kingereza na mwishowe kuchanganya maneno

MSICHANA: Mbona jana nimekupigia simu hujapokea?
JAMAA: please beby forget me.
MSichAnA: eeeh unaniambia hivo mimi?
JAMAA: nakuomba sana forget me.
MSICHANA: aya bwana poa maisha mema.

Msichana anakata simu jamaa ndo ananiuliza.”sasa
sijui amekasirikia lipi?” Mi nikamwambia we zuzu
umemwambia AKUSAHAU, dah, kumbe
ningemwambiaje? hahaha, ungemwambia
ForgivE me! au Ungesema Tu NaombA nSameHe.

Tabia 10 zinazoweza kuharibu figo

1.Kubana mkojo kwa muda mrefu
2.Kutokunywa maji ya kutosha kila siku
3.Kutumia chumvi nyingi kuliko kawaida
4.Kula nyama mara kwa mara au mara nyingi
5.Kutokula chakula cha kutosha

6.Kuchelewa kujitibu maambukizi madogo
madogo haraka na kwa usahihi
7.Kutumia visivyo dawa za kutuliza maumivu
8.Kutumia dawa kwa ajili ya insulin kwa muda
mrefu
9.Kunywa pombe.
.
10.Kutopata muda wa kutosha wa kupumzika
USHAURI!!Kunywa glasi 2 za juisi ya parachichi
(avocado). Na angalau bilauli nne za maji asubuh
badala ya supu ya kongoro.. kila siku kutaziweka
figo zako katikahali ya usafi na afya.

Angalia huyu secretary anavyomjibu bosi wake

Boss mmoja aliingia kazini kwake kasahau kufunga zipu ya suruali yake sasa secretary wake akamfuata na mazungumzo yakawa hivi:

SECRETARY: Boss leo umesahau kufunga geti nyumbani kwakoโ€ฆ

Boss akabaki anashangaaโ€ฆ Baadae wakati anakwenda chooni kujisaidia ile anataka kufungua zipu akaikuta iko wazi ndio akajua alichokuwa ameambiwa na Secretary wake.

Akarudi mpaka kwa secretary na mazungumzo yakaendelea:

BOSS: Bibie ulivyoona geti wazi je uliona benz langu lime paki auโ€ฆ?

SECRETARY: Hapana Boss niliona kitoroli kidogo kimepaki kina matairi mawili

Namna ya kutibu chunusi kwa kutumia Binzari, maziwa na asali

Unahitaji vitu vifuatavyo:

a)Binzari ya unga
b)Maziwa fresh
c)Asali
d)Bakuli
e)Kijiko cha chai

Hatua kwa hatua namna ya kutumia:

a)Weka kijiko kidogo kimoja cha binzari ya unga ndani ya bakuli
b)Ongeza kijiko kidogo kimoja cha asali ndani yake
c)Ongeza tena kijiko kidogo kimoja au viwili vya maziwa fresh
d)Changanya vizuri mchanganyiko huu upate uji mzito
e)Pakaa pole pole sehemu yenye chunusi mchanganyiko huu
f)Baada ya dakika 5 au 7 hivi jisafishe uso wako
g)Fanya zoezi hili mara 2 au 3 tu kwa wiki

Jinsi ya kulima vitunguu (vitunguu maji) kwa mbinu za kilimo bora na kwa faida

Vitunguu ni zao la mbogamboga na hulimwa kwa ajili ya balbu zake ambazo hutumika kama kiungo cha chakula. Vitunguu vina matumizi mengi sana na vina madini joto, chuma, vitamin A, vitamin B, vitamin C na vitamin E.
Vitunguu hulimwa na hukubali zaidi nyanda za baridi. Nyanda zenye joto vitunguu hulimwa pia. Vitunguu vinaweza kulimwa mwaka mzima endapo maji yanapatikana.

Aina za vitunguu vinavyolimwa Tanzania

  • Red Creole
  • Bombay Red
  • Hybrid F1

Hali ya hewa

Joto linatakiwa sana kwa ajili ya ukuaji wa balbu ila joto likizidi vitunguu hukomaa mapema kabla balbu hazijafikia ukubwa unaostahili, hivyo mkulima anaweza kupata mazao kidogo.

Udongo

Vitunguu huweza kupandwa kwenye udongo wowote wenye rutuba, usiotuamisha maji na usionata sana. Hufanya vizuri kwenye udongo wenye asidi kidogo japo udongo wenye alkali kidogo sio mbaya sana. Kwenye udongo wenye mchanga mchanga umwagiliaji ni lazima. Udongo mzuri sana kwa ustawi wa vitunguu ni tifutifu-kichanga.

Mbolea

Epuka matumizi ya mbolea mbichi isioiva vizuri kwani husababisha vitunguu kuwa na shingo pana sana majani hukua sana badala ya balbu.

Umwagiliaji

Umwagiliaji ni muhimu sana hasa wakati wa kuanza kutengeneza balbu. Unyevu uliozidi ni hatari sana kipindi cha ukuaji.

Kitalu cha vitunguu

Ni muhimu kumwagilia maji ya kutosha siku kumi za mwanzo tangu kusia mbegu kitaluni. Vitunguu hukaa kitaluni kwa wiki 6-8 na miche ifikiapo upana wa penseli na urefu wa sm 15 ni tayari kwa kuhamishia shambani/bustanini.

Upandaji

Kabla ya kupanda udongo ni lazima utifuliwe vizuri na reki kuondoa mabaki ya mimea na mawe ama Vipande vikubwa vya udongo. Matuta yawe na upana wa mita moja. Vitunguu hupandwa kwa mstari mojakwamoja ama kutokea kitaluni. Pia huweza kupandwa kwa mstari pacha. Vitunguu hupandwa sm 10-15 kutoka mmea hadi mmea na sm 10-15 kutoka mstari hadi mstari, kama inavyoonekana kwenye mchoro hapa chini. Pia epuka kupanda vitunguu mahali palipopandwa mboga jamii ya vitunguu siku za nyuma. Mfano Vitunguu saumu na vitunguu majani.

Utunzaji wa shamba

Kutandazia shamba na majani yaliyooza vizuri ama mabua inashauriwa ili kuongeza ruba ya ardhi, zuia magonjwa yatokanayo na udongo na magugu. Kupanda vitunguu kwenye matuta yaliyoinuka ni muhimu sana kuzuiya utuamishaji wa maji na mlipuko wa magojwa ya miche. Kungoa magugu na uvunaji ufanywe kwa mkono.
Vitunguu hufanya vizuri kama shamba litawekewa mbolea ya samadi ama mboji ilioiva vizuri. Kiasi cha tani 25-40 kwa heka kinashauriwa. Hii ni sawa na kilo 7.5 -12 kwa tuta lenye urefu wa mita 3 na upana wa mita 1.

Uvunaji

Vitunguu huvunwa kuanzia siku 90-150 tangu kusia mbegu. Dalili za kukomaa ni kuanguka kwa majani. Vitunguu huvunwa kwa kuvuta kwa mkono na kuhifadhiwa siku kadhaa shambani vikiwa vimefunikwa na majani. Baada ya hapo majani hukatwa na balbu hupakiwa kwa ajili ya kuhifadhi kusubiria bei nzuri. Vitunguu huweza kuhifadhiwa hadi miezi 9 tangu vivunwe bila kuharibika. Vitunguu vihifadhiwe kwenye nyuzijoto chini ya 4.4 ยฐC ama juu ya nyuzijoto 25ยฐC ili visiharibike.

Yafahamu Mambo Mbalimbali ya muhimu kuhusu kilimo cha Mazao ya Mboga Mboga kwa Ku-Download Kitabu cha MBINU ZA KILIMO BORA CHA MBOGA

Ni kitabu kinachotoa elimu ya Kilimo Cha Mboga. Kipo katika Mfumo wa PDF (Soft copy).

Kina kurasa 100 na utaalamu wa mazao zaidi ya 10, ambayo ni nyanya, kabichi, bamia, vitunguu maji, vitunguu twaumu, hoho, matikiti, karoti, uyoga na matango. Bila kusahau kilimo cha mboga kama chainizi na mchicha.

Pia utaweza kufahamu mbinu mbalimbali za kilimo cha mboga kama vile kuandaa shamba na kitalu, udhibiti wa wadudu na magonjwa katika mboga, kuvuna na kuhifadhi mboga, vilevile utajifunza kuhusu kilimo cha matone.

Kitabu hiki ni Soft copy [pdf] kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.

Cheki kilichotokea stesheni ya treni, mambo mengine ukipaniki inakula kwako kama huyu jamaa

Jamaa Wawili Walifika Stesheni, wakakuta Treni ndo kwanza inaondoka. Wakaanza Kuikimbiza. Mmoja akafanikiwa kupanda akaondokaโ€ฆ

Yule aliyebaki akaanza kucheka sanaa mpaka machozi yakamtoka. Watu wakamuullza, unacheka nini sasa wakati umeachwa? Akawajibu: “kinachonichekesha, yule aliyepanda alikuwa ananisindikiza.

Angalia jinsi maamuzi yako ya jana na ya leo yanavyoweza kukuathiri

By Malisa GJ,
Nimeitoa kwa Comrade Markus Mpangala na kuitafsiri kwa Kiswahili (kisicho rasmi sana).
Mwaka 1998 “Google” walitaka kuiuza kampuni yao kwa “Yahoo” kwa dola Milioni 1 (sawa na Shilingi Bilioni 2) lakini Yahoo wakakataa. Yani Yahoo wakakataa kuinunua Google.

Mwaka 2002 Yahoo wakagundua kwamba walifanya makosa kuikataa Google kwahiyo wakarudi na kutaka kuinunua kwa dola Bilioni 3 (sawa na Trilioni 6). Lakini Google wakataka wapewe Dola Bilioni 5 (sawa na Trilioni 10). Yahoo wakagoma.

Mwaka 2008 kampuni ya Microsoft ikataka kuinunua Yahoo kwa Dola Bilioni 40 (sawa na Trilioni 80) lakini Yahoo wakakataa offer hiyo. Wakaona ni “ndogo”

Lakini Yahoo ikazidi kuporomoka kwenye soko na ilipofika mwaka 2016 hatimaye ikauzwa kwa dola Bilioni 4.6 (sawa na Trilioni 9) kwa kampuni ya Verizon.

#MyTake:

Unajifunza nini kupitia kisa hiki cha Yahoo? Binafsi nimejifunza mambo kadhaa:

#Mosi ni kuhusu fursa. Ukipata fursa leo itumie huwezi kujua kesho itakuaje. Yahoo wamechezea fursa nyingi sana. Kama wangekua makini huenda wao ndio wangekua wamiliki wa Google leo. Au wangeuzwa kwa bei kubwa (Trilioni 80) kwa Microsoft mwaka 2008. Lakini maringo yao yamewafanya kuja kuiishia kuuzwa bei ya “mbwa” (trilioni 9). Usifanye makosa ya Yahoo.!

#Pili ni kuhusu Thamani. Ukiwa kwenye nafasi leo usijione una thamani kuliko asiye na nafasi hiyo. Huwezi kujua kesho itakuaje. Maisha ni kupanda na kushuka. Unaweza kumnyanyasa mtu leo kwa sababu una nafasi fulani, kesho ukaenda kuomba kazi ukakuta ndio “boss” anayeajiri. Unayemuona leo yupo chini kesho aweza kuwa juu, na aliye juu akawa chini. Yahoo ilikua juu sana miaka ya 1990’s lakini kwa sasa imebaki “skrepa”. Hata sijui kama kuna watu wanaitumia siku hizi zaidi ya wale wabibi waliofungua email kipindi kile cha zama za kale za mawe.

Yahoo ilijiona juu kuliko wengine kwahiyo ikadharau kampuni zingine. Hata Google ilipotaka kuuzwa kwa Yahoo mwaka 1998, Yahoo iliona kama vile kuinunua Google ni kupoteza fedha. Leo inatamani kuwa hata “department” ya Google lakini haiwezekani. Usifanye makosa ya Yahoo.!

#Tatu nimejifunza majuto ni mjukuu. Wamiliki wa Yahoo huenda wanajuta sana kwa kupoteza fursa zote zilizokuja mbele yao. Vivyo hivyo katika maisha kuna maamuzi unaweza kufanya leo kesho ukayajutia. Mwanadada anaweza kukataa kuchumbiwa na kijana kwa sababu hana kazi, hana nyumba wala gari. Lakini baada ya miaka kadhaa anamuona yule kijana amefanikiwa kuliko alivyofikiri. Anatamani awe hata mchepuko wake lakini haiwezekani.
Usifanye makosa ya Yahoo.!

#Nne nimejifunza kuwa ukichagua sana nazi utapata koroma. Yahoo walijifanya kuchagua sana. Kila aliyekuja na “Offer” walikataa. Matokeo yake wakaja kuuzwa bei ya kuku za kienyeji kutoka Singida. Mwaka 2008 Microsoft walitaka kuinunua Yahoo kwa Dola bilioni 40 wakagoma. Lakini miaka 8 baadae (2016) wamekuja kuuzwa Dola bilioni 4.6 (yani 10% ya kile walichokua wapewe mwaka 2008).

Vivyo hivyo na binadamu ndivyo tulivyo. Ngoja nitumie mfano wa akina dada ili unielewe vzr. Kuna kina dada kuringa kwao ni fahari. Sisemi kina dada wasiringe. Ni vizuri kuringa lakini isiwe “too much”. Sasa wewe unaringa wanaume zaidi ya 10 waliokuja kukuposa, wote unawakataa unataka uolewe na nani?

Mwenye elimu umemkataa, mwenye gari umemkataa, mwenye nyumba umekataa, mwenye biashara umekataa. Umewakataa wote. Ukija kuhamaki umekuwa kama “Yahoo”โ€ฆ una miaka 35 na huna hata mchumba wa kusingiziwa. Unaanza kwenda kwenye mikesha ya maombi ili upate muujiza. Miaka mitatu inaisha hakuna muujiza wala mazingaombwe.

Unaamua kuweka tangazo gazetini “natafuta mchumba mwenye miaka 40 na kuendelea. Hata kama hana kazi mimi nina kazi tutasaidiana”. Miaka miwili inapita hupati. Unagundua ulikosea kama Yahoo. Hakuna mwanaumwe wa miaka 40 ambaye yupo single. Unarekebisha na kusema kuanzia miaka 25, wakati wewe una 40.

Unaamua kujilipua kama Jackline Wolper na Harmonizer. Au Zari na Diamond. Au Wema na Idris. Hujui wakati Wema anachukua taji la Miss Tanzania Idriss alikua form one?? Lakini leo wanamitana mababy?? Kwahiyo unaona miaka 25 kwa 40 sio issue. Na wewe unaamua kuingia kwenye kundi la “akina bibi wanaolea wajukuu zao”

Lakini hupati “husband material”. Unawapata “maplay boy” wa mjini. Wanakuja wanakuta ni bibi wa miaka 40 wanakuuliza “umemaliza eddah” wakidhani ni mjane umefiwa na mume unataka kuolewa tena. Kumbe hujawahi kutolewa mahari hata mara moja. Wanakuambia ngoja tufikirie, halafu haoooo wanapotea kama Microsoft ilivyopotea mbele ya uso wa Yahoo. Hawarudi ng’o.

Baadae baba yako anaamua kuondoa tangazo la “Jihadhari mbwa mkali” lililokuwa getini anaweka tangazo jipya “tunauza barafu” Na hapo ndipo utakapogundua kuwa vifusi vya mchanga wa mgodini vinaweza kutumika kupiga “plasta” nyumba yenu.

My dear Life is too short to be complicated. Live your life. Enjoy every moment of your life. Tumia fursa zote muhimu unazozipata. Usiringe. Usimdharau mtu. Heshimu kila mtu. Mche Mungu. Usifanye makosa ya “Yahoo”.!

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia Uwatu (Fenugreek)

Uwatu ni dawa nyingine ya asili inayotumika kutibu chunusi. Uwatu unaondoa sumu na maambukizi mbalimbali.

Hizi ni hatua chache za kutibu chunusi kwa kutumia uwatu

a)Chukua kijiko kidogo cha unga wa mbegu za uwatu
b)Ongeza maji kidogo kupata uji mzito (paste)
c)Pakaa mchanganyiko huu sehemu yenye chunusi
d)Acha kwa dakika 20 au kwa usiku mzima
e)Kisha jisafishe a maji safi
f)Fanya zoezi hili mara 2 au 3 kwa wiki

Jinsi ya kumshawishi mwanamke kufanya mapenzi

Zifuatazo ni njia za kuamsha hamu ya kufanya mpenzi ya mwanamke. Njia hizi zimegawanyika katika hatua mbili kuu, kwanza ni kumfanya akukubali na kisha kuamsha hisia zake.

 

Mfanye akukubali

Njia za kumfanya akukubali ni kama ifuatavyo

Uwe na muonekano mzuri

Wanawake wanapenda wanaume wasafi na watanashati kwa hiyo ukiwa msafi na mtanashati utakua na mvuto kwake. Hivyo utakapoamua kumshawishi kufanya mapenzi itakua rahisi yeye kuwa rahisi kukubali.

Mfanye ajisikie huru

Ni rahisi mwanamke kufanya mapenzi na mtu anayejisikia huru mbaele zake na ambaye yupo huru kuongea na kufanya nae mambo mengine ya kawaida katika maisha. Kwa hiyo ili uweze kumshawishi mwanamke kufanya mapenzi na wewe njia nzuri ni kumfanya ajisikie yupo huru mbele yako na kasha atakua huru kufanya mapenzi na wewe.

 

Mfurahishe

Mfanye ajisikie mwenye furaha kila anapokuwa na wewe na atamani kuwa na wewe. Akishajiskia mwenye furaha kila anapokuwa na wewe ni rahisi kushawishika kuwa na wewe kimapenzi.

Mfanye ajione kuwa yeye ni mzuri

Mwanamke anapenda sana na anavutiwa na mwanamme anayeona ubora wake au anayemsifia kuwa ni mzuri.

Mfanye akuamini

Mfanye aamini kwamba hata baada ya kufanya mapenzi bado mtakua pamoja na sio mwisho wa mahusiano yenu au urafiki wenu.

 

Usiwe na haraka, Mpe muda

Usiwe na haraka ya kumwambia kuwa unataka kufanya mapenzi na yeye bali subiri mpaka utakapoona yupo tayari au anaelekea kukuhitaji.

Mfanye akuone mwaminifu

Mfanye akuone mwaminifu kwa kutomchanganya na wanawake wengine. Usimuonyeshe kuwa una mahusiano na wanawake wengine. Mfanye aamini kuwa unamuhitaji yeye tuu.

 

Mjali kama mwanamke

Mfanye ajiskie kuwa mwanamke. Jaribu kuonyesha kuwa mwelewa, onyesha kuwa unajali, mkarimu na muonyeshe kuwa wewe ni msaada kwake. Mfungulie mlango, mbebee begi au pochi yake n.k.

Onyesha kuwa unapenda kila kitu kutoka kwake

Muonyeshe kuwa unampenda yeye na vyote vyake. Onyesha kuwa umevutiwa na yeye na mambo yake yote na sio mwili wake tuu.

 

Amsha Hisia zake

Baada ya kumvutia, sasa amsha hisia zake. Njia za kuamsha hamu ya kufanya mpenzi ya mwanamke au Hatua za kufuata kuamsha hisia za mwanamke ni kama ifuatavyo

Andaa mazingira

Andaa mazingira ya kuamsha hisia zake, fanya kitu kitakachowasogeza karibu na kuamsha hisia zake Kwenye akili yake kabla ya kugusa mwili. Mfano, weka mziki au muvi nzuri n.k. Kisha tengeneza mazingira ya kuwa karibu kimwili na kugusana.

 

Kaa kwa kubanana naye

Unapokuwa na mwanamke ambaye umemzimia, tafuta kisababu cha kukaa na yeye karibu. Toa simu muangalie pamoja videos kama vile za kuchekesha, ama unaweza kuchukua kitabu/gazeti umuonyeshe habari ambazo anapenda ilimradi tuu muwe karibu.

Usimwonyeshe/usiongee wazi kile unachotaka

Usijaribu kutumia lugha ya kutongoza ama utamfanya aanze kukushuku. Tayari anajua kuwa miguso ya mikono yako ya mara kwa mara inaashiria kitu fulani. Kile unachotakiwa kufanya ni kuivuruga akili yake kwa kuleta mada ambayo itamvutia huku ukiendelea gusa mwili wake

 

Anza kutumia lugha ya kumsuka

Wakati mtakuwa mnaendelea unaweza kutumia maneno ya kumsuka lakini yawe ya kichini chini. Mfano unaweza kumwambia “Unanukia utamu”, “nimependa kitambaa cha nguo yako”,”nishawahi kukuambia kuwa macho yako yanapendeza? Nimependa vile yanang’aa nikiwa karibu yako.” Maneno kama haya unaweza kumrushia mwanamke huyu bila hata yeye kusongea mbali na wewe. Mwanzo atakuwa anapenda kuyaskia.

Isome miondoko yake

Ukianza kumuona anazungumza polepole na kukusongelea karibu yako, ishara kuu ni kuwa yupo tayari. Kwa hiyo kufikia hapa unaweza kurudia hatua za kumsuka, kumgusa na kujaribu kufikia viungo vyake vingine vya mwili ilimradi nyote wawili mnafurahia.

 

Mbusu

Baada ya kuandaa mudi au mazingira na kuamsha hisia zake sasa tafuta namna ya kumbusu. Mbusu taratibu kwa namna ambayo haitamshtua na kumfanya aogope au akatae.

Mhikeshike

Wakati wa kumbusu mshike mwili wake ili kuamsha hisia zake. Anza na mikono kasha rudi kichwani Kwenye nywele zake na kisha maliza sehemu nyingine za kuamsha hisia zake

Usimlazimishe bali mbembeleze

Kama hataki usimlazimishe bali mbembeleze au muache mpaka wakati mwingine atakapokuwa tayari.

 

NB: Ni makosa makubwa na ni dhambi kufanya mapenzi kabla ya ndoa. Mbinu hizi zitumie kwa mwenzi wako wa ndoa

Yafahamu Mambo Mbalimbali kuhusiana na Wanawake kwa Ku-Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

Kitabu hiki kina topiki Zifuatazo;
1. Mambo anayohitaji mwanamke kutoka kwa Mwanaume
2. Mambo yanayowavutia wanawake kutoka kwa wanaume
3. Mambo wanayoyapenda wanawake wakati wa kufanya mapenzi
4. Dalili za mwanamke kicheche
5. Maswali ya kujiuliza kama mwanamke anakupenda kwa dhati au anakudanganya
6. Tabia za mwanamke anayekupenda lakini hawezi kusema
7. Ishara za mwanamke aliyevutiwa na wewe
8. Dalili za mwanamke anayeelekea kukukubali
9. Mambo ambayo mwanamke hawezi kukwambia
10. Njia za kudumisha na kuamsha mapenzi na mwanamke

Kitabu hiki ni Soft copy [pdf] kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.

Mambo 8 ya kuzingatia kabla ya kuleta mifugo (kuku, ng’ombe,mbuzi n.k) wapya bandani

Mambo hayo ni haya yafuatayo;
1. Hakikisha unaondoa matandazo yote ndani ya nyumba,
2. Ondoa vyombo vya kulishia na kunyweshea.

3. Ondoa uchafu wote unaoonekana bandani.
4. Safisha banda lote kwa kutumia maji na dawa.
5. Suuza na uache likauke.
6. Puliza dawa ya kuua wadudu.
7. Weka matandazo mapya,
8. Weka viombo vya kulishia na kunyweshea.

Kushindwa au vikwazo sio sababu ya kutofanikiwa

“Nilibakwa nikiwa na miaka 9 lakini leo mimi ni mmoja wa wanawake wenye ushawishi mkubwa duniani”- OPRAH WINFREY!

“Sikumaliza elimu yangu ya Chuo Kikuu lakini mimi ndiye binadamu tajiri kuliko wote duniani” – BILL GATES!

“Nilikuwa napata matokeo mabaya sana darasani wakati nilipokuwa shule ya msingi lakini bado mimi ni Daktari Bingwa wa Upasuaji duniani” – DR. BEN CARSON!

“Nilimwambia baba yangu tutakuwa na mali na utajiri mkubwa lakini hakuamini, leo hiyo ndiyo hali halisi”
– CHRISTIANO RONALDO!

“Nilikuwa mhudumu kwenye mgawahawa wa chai ili kulipia ada za mafunzo yangu ya mpira lakini leo mimi ni mchezaji bora wa dunia” – LIONEL MESSI!

“Nilikuwa nalala chini kwenye vyumba vya marafiki zangu, natafuta chupa tupu za soda nipate chakula, pesa na mlo wa bure wa kila wiki lakini bado mimi ndiye mwanzilishi wa APPLE” – STEVE JOBS!

“Walimu wangu waliniita mwanafunzi mjinga na asiyejiweza lakini bado nimekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza” – TONY BLAIR!

“Niliendesha TAKSI ili kulipia ada yangu Chuo Kikuu lakini leo mimi ni Bilionea” – MIKE ADENUGA!

#NOTE: Kushindwa au Vikwazo vya nyuma ni mambo yasiyo na nafasi kwa UWEZO mkubwa uliomo ndani yako. Kwa mtu anayeamini, kila kitu kinawezekana. Ni tunu ulizonazo na talent ulizopewa ndizo ufunguo wa maisha yako. Usiende kukopa shaba kwa jirani wakati umeacha dhahabu nyumbani kwako, tumia dhahabu zako

Cheki huyu jamaa anavyoungama kwa padri sasa

JAMAA: Baba Padri nimekuja kuungama
PADRI: Haya
JAMAA: Niliiba kamba
PADRI: Kamba?
JAMAA: Ndio, kamba lakini kule mwisho kulikuwa kumefungwa ng’ombe
PADRI: Kwa hiyo uliiba ng’ombe?
JAMAA: Kiukweli nilikuwa nina lengo la kuiba kamba, kwa bahati mbaya mwisho kulikuwa na ng’ombe
PADRI: Mi naona mueleze Mungu direct, mi sikuelewi kabisaaa

๐Ÿ™ˆ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜‚๐Ÿ™Š

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About