SMS, Vichekesho, Mahusiano, Biashara na Ujasiriamali, Afya, Chemsha Bongo, Dini pamoja na Vitabu kwenye PDF

Karibu AckySHINE

🤣😃😂

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Mambo ya kuzingatia kuhusu ugonjwa wa Kaswende

Kaswende husababishwa na bakteria aitwaye Treponema pallidum , ambaye pia huitwa spirochetes kutokana na umbo lake la mzunguko. Viumbe hawa hujipenyeza kwenye ngozi laini inayotanda midomo au sehemu nyeti. Yafuatayo ni mambo Muhimu ambayo unapaswa kuyafahamu kuhusu Ugonjwa wa Kaswende.

Jinsi ugonjwa wa Kaswende unavyoonea

Ugonjwa huu huenezwa kwa kugusa moja kwa moja mchubuko wa kaswende (syphilitic sore) uliopo kwenye ngozi. Kaswende haiambukizi kwa kuchangia vyoo, vitasa vya milango, mabwawa ya kuogelea, kuchangia nguo au vyombo vya chakula.

Kwa njia ya Kujamiiana

Kaswende ni ugonjwa unaoambukiza haraka sana, mara nyingi huambikizwa kupitia ngono. Kwa sababu ugonjwa huu huenezwa kwa kugusa moja kwa moja mchubuko wa kaswende (syphilitic sore) uliopo kwenye ngozi, njia kuu ya kuenea ni kupitia ngono ya kawaida, ya kutumia midomo na ile ya kinyume na maumbile.

Kwa njia ya kugusana Miili

Mara chache ugonjwa huu huweza kuambukiza kwa kubusiana au kugusana miili. Pamoja na kuwa ugonjwa huambukiza kupitia michubuko, mara nyingi michubuko hatarishi haitambulikani. Mtu aliyeambukizwa huwa hajielewi na hivyo kumwambukiza mpenzi wake.

Kwa mtoto kipindi cha ujauzito

Mwanamke mwenye mimba na ugonjwa huu anaweza kumwambukiza mtoto aliye tumboni kupitia placenta au wakati wa kuzaliwa.

Aina hii ya kaswende huitwa congenital syphilis, na inaweza kusababisha kujifungua mtoto mfu au mtoto akafa muda mfupi baada ya kuzaliwa. Watoto wengi hawaonyeshi dalili wanapozaliwa. Baadaye watoto huota vijipele, hupata matatizo ya meno, na kubonyea kwa mfupa wa pua – hali inayoitwa saddle nose, kuwa viziwi, kuwa na watoto wa jicho na kifafa.

Hatua za Kaswende

Ugonjwa wa kaswende hugawanywa katika hatua na kila hatua ikiwa na dalili tofauti, lakini wakati mwingine hakuna dalili zitakazojitokeza kwa miaka mingi.

Uambukizaji unatokea kwenye hatua ya kwanza, ya pili na mara chache mwanzoni mwa hatua ya latent phase.

Hatua Ya kwanza Ya Kaswende – Primary Syphilis

Kaswende huanza kama mchubuko mmoja (au zaidi ya mmoja) mgumu usio na maumivu unaojulikana kama chancre kwenye sehemu za siri, kwenye mdomo, au kwenye ngoz,i siku 10-90 (wastani wa miezi 3) baada ya maambukizi.

Mchubuko huu unaweza kubaki hapo bila kuleta usumbufu kwa kipindi kirefu na hata maiaka mingi. Mchubuko huu wa mviringo hutokea kwenye eneo la maambuikizi. Hata bila ya tiba yo yote, mchubuko huu unaweza ukapona wenyewe bila kuacha kovu katika wiki sita.

Hatua Ya Pili Ya Kaswende – Secondary Syphilis

Hatua ya pili inaweza ikadumu kwa mwezi mmoja hadi miezi sita ikianza kama wiki sita hadi miezi sita baada ya maambukizi.
Dalili
Katika hatua ya pili, vijipele huota mara nyingi vikianzia mgongoni na kuenea mwili mzima, pamoja na kwenye viganja vya mikono na kwenye nyayo. Vijipele hivi huwa vya mviringo vyenye rangi nyekundu au vyenye wekundu wa kahawia.
Michubuko inayofanana na chunjua hutokea kwenye sehemu za midomo na mkundu. Vile kutatokea maumivu ya misuli, homa, kukauka koo, kuvimba tezi, kupunyuka nywele, kukonda na uchovu wa mwili.

Latent Syphilis
Kama tiba ya kaswende ya hatua ya pili haitatolewa, ugonjwa utaendelea kwenye hatua iitwayo latent stage. Katika hatua hii inayoweza kudumu kwa miaka kadhaa, mwili utautunza ugonjwa bila kuonyesha dalili zo zote. Pamoja na kuwa hakuna dalili zo zote zitakazoonekana, ugonjwa huu unaweza kuendelea kwenye hatua ya mwisho.

Hatua Ya Tatu Ya Kaswende – Tertiary syphilis

Asilimia 15 ya watu ambao hawakupata tiba kwenye hatua ya pili ya kaswende watapata kaswende ya hatua ya tatu – tertiary syphilis. Hatua hii inatokea miaka 10 hadi 30 baada ya dalili za mwanzo za kaswende.
Dalili
Dalili za kaswende za hatua hii ni pamoja na kushindwa kumudu matumizi ya viungo vya mwili, ganzi, upofu, ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu, madhara kwenye moyo na mishipa ya damu, madhara kwenye ini, mifupa na maungio ya mifupa. Kifo huweza kutokea kutokana na uharibifu wa viungo vya mwili.

Matibabu ya ugonjwa wa Kaswende

Ugonjwa wa kaswende unatibika. Kuwahi kumpa tiba mgonjwa wa kaswende ni muhimu kwani kuchelewa kunaweza kumletea madhara makubwa ya mwili au kifo. Kama ugonjwa haujazidi mwaka mmoja, mara nyingi dozi moja ya ya penicillin hutosha.

Kaswende iliyoendelea kwenye hatua nyingine, dozi nyingine zitahitajika.

Faida na namna ya kutumia mafuta ya Zaituni Olive Oil kwenye nywele

Faida ya Mafuta Ya Zaituni Olive Oil kwenye nywele.

1. Yanasaidia kufanya mzunguko wa damu kufanya kazi vizuri kwenye ngozi ya kichwa na kupenyeza hadi kwenye shina ya nywele kisha kuifanya nywele inayoota kuwa imara

2. Yanasaidia kupambana na mba kwenye ngozi ya kichwa

3. Yanasaidia uzalishwaji wa mzizi au shina ya nywele

4. Yanasaidia uzalishwaji wa melanin ambayo inafanya kazi ya kutoa rangi ya nywele inayotakiwa.

5. Yanasaidia kuifanya nywele isiwe kavu sana.

NAMNA YA KUZIHUDUMIA NYWELE:

Unaweza kuchanganya na Mdalasini pamoja na Asali.

1. Olive oil vijiko 2 vya chakula

2. Asali kijiko 1 cha chakula

3. Mdalasini kijiko 1 cha chai

Pasha moto olive oil kisha changanya vyote kwa pamoja pakaa kwenye nywele acha kwa muda wa dakika 20 kisha osha nywele zako na upakae mafuta zikishakauka.

Ninashauri utumie mafuta haya kwenye nywele na ngozi ni mazuri sana. Ukiwa na mba pakaa kwenye ngozi mba itaisha na muwasho utaondoka.

Hii ndiyo Ladha ya bia zote usiyoijua

Ladha ya bia ya 1 hadi ya 6..

Kwa wanywaji wazuri wa bia,

chupa ya kwanza 🍺 huwa haileti hisia yoyote. Mnywaji humaliza chupa hiyo bila kuona matokeo yoyote zaidi ya kupoza koo… Na mara nyingi huwa mkimya, pengine huwa anasoma gazeti lake au kwa siku hizi anawasiliana na ndugu na jamaa kupitia simu yake.

chupa ya pili 🍺🍺 kimsingi ndipo mazungumzo ya awali na wanywaji jirani huanza na haya huwa mazungumzo ya busara, yakihusu muelekeo wa ligi mbalimbali, siasa, idadi za ajali na kadhalika na wakati huu hata takwimu hutolewa zilizo sahihi….

Mtu anaweza kukutajia wachezaji wote wa ligi daraja la tatu la huko Ujerumani bila kukosea, hata idadi ya wachezaji wa Yanga bila kukosea.. Ila wakati huu kama unaanzisha mashindano ya kucheua ni wakati mzuri kwani bia ya pili huongeza hisia za kucheua.

Bia ya tatu 🍺🍺🍺 huanza kumfanya mnywaji aanze kusikia furaha na pia huu huwa wakati ambapo karanga na korosho huliwa sana…. Pamoja na mazungumzo kuhusu mpira na siasa, ghafla mazungumzo kuhusu michepuko huanza kujitokeza…..

Bia ya nne 🍺🍺🍺🍺 huanza kusababisha masikio yaanze kupoteza nguvu za kusikia kwani utaona mnywaji ghafla amepandisha sauti, na ukijumlisha na kuwa baa zetu huwa na muziki una kelele utadhani waliopo wote wana matatizo ya kusikia….. bia hii humsaidia kuongea kwa nguvu kushindana na kelele za muziki.

Bia ya tano 🍺🍺🍺🍺🍺 ni hatari kidogo kwani ukiinuka kwenda chooni mara nyingi unarudi hujafunga zipu……na kipindi hiki ni kibaya kwa wanywaji wa kike maana unaweza kumkuta akienda chooni akijiangalia kwenye kioo anaanza kulia peke yake na kulalamika; ‘Mi sipendwi mpaka leo sijaolewa’ au ‘ Mume wangu sijui yukoje hanijali’

Japokuwa lazima isemwe ukweli ukifikisha bia hii, maisha ni raha sana unaweza ukaanzisha shoo ya kukata mauno katikati ya baa na kudai wewe ni mkali kuliko Shilole.

Kuanzia bia ya sita 🍺🍺🍺🍺🍺🍺 na kuendelea, chochote utakachosema au kufanya ni wazi kesho yake asubuhi utajilaumu sana. ……. …Kuna watu husema ukilewa ndipo unakuwa mkweli, hivyo basi wakati huu hata bosi wako akitokeza unamueleza ukweli jinsi alivyo fala na hajui kuendesha kampuni.

Au unasema ukweli jinsi unavyompenda mke wa jirani yako ambaye mmekaa mnakunywa naye. Kimsingi uwezekano wa kutapika pia upo karibu na kama umekaa na mchumba wako huu ni muda ambao pia uchumba unaweza kuvunjika…….

Cheki huyu jamaa anavyoungama kwa padri sasa

JAMAA: Baba Padri nimekuja kuungama
PADRI: Haya
JAMAA: Niliiba kamba
PADRI: Kamba?
JAMAA: Ndio, kamba lakini kule mwisho kulikuwa kumefungwa ng’ombe
PADRI: Kwa hiyo uliiba ng’ombe?
JAMAA: Kiukweli nilikuwa nina lengo la kuiba kamba, kwa bahati mbaya mwisho kulikuwa na ng’ombe
PADRI: Mi naona mueleze Mungu direct, mi sikuelewi kabisaaa

🙈😃😃😃😀😀😀😂🙊

Mlevi kazua tafrani, angalia alichokifanya hapa

MLEVI mmoja aliingia baa akavuta kiti na kukaa mhudumu akatokea kumsikiliza.
MHUDUMU: Nikusaidie nini?
MLEVI: Eeh! nipe bia ya baridi kisaha wasikilize wote waliokaa hapa, wape bia na wao maana sipendi kunywa pombe wengine wananiangalia
Akaja mhudumu wa jikoni “nikusaidie nini?”

MLEVI: Niletee supu kisha wasikilize wote waliokaa hapa na wao wape supu sipendi kunywa supu watu wananiangalia
Safari hii watu wakapiga makofi
Baadae akamuita mhudumu
MLEVI: Niandikie bili zangu kisha waandikie wote bili zao sipendi kulipa huku watu wananiangalia

Wale wateja wakamvaa na kumshushia kichapo… teh teh teh teh teh hii kali hakuna cha bure mjini hahahaha na jasho la mtu haliliwi wandugu

Namna ya kuondokana na tatizo la kunuka Kikwapa

Harafu ya jasho inakera, kibaya zaidi ni kuwa wewe mwenyewe husikii harufu hiyo ila wale walio karibu yako. Kwa upande mwingine kujaribu kuzuia kutoka jasho ni hatari kwa afya yako na kujaribu kuondoa harufu kwa kutumia pafyumu husababisha madhara mengine ya kiafya na kwa bahati mbaya perfume zina jaribu poteza harufu kwa mda mfupi tu na sio kutokomeza tatizo hilo.

Dawa rahisi ya kuondoa harufu kwenye kwapa o ni kutunza mwili wako ikiwa ni pamoja kuoga mara kwa mara hata ikibidi mara tatu kwa siku kwa kuanzia, kwani harufu mbaya ya kwapa inatokana na kuwepo kwa bakteria katika kwapa hasa kukiwa na unyevu au maji maji kwapani.

Ili kukomesha tatizo hili ni lazima kuoga mara nyingi pia wakati unaoga mkazo utiliwe kwenye kwapa tumia dodoki na sabauni unaposafisha kwapa lako, pili ni lazima ukaushe kwapa barabara ili kuondoa unyevu ambao unakaribisha bakteria ambao wanajaribu kuvunja vunja jasho lako na ndiyo maana linatoa harufu kali.

Vile unashauriwa mara baada ya kuoga tumia potassium alum au sulphur.

Vile vile jitahidi kuepuka nguo za polista (polyster) vaa nguo za pamba 100%

Punguza kula vyakula vyenye viungo vikali kama vitunguu swaumu nk.

Sababu za kumuacha mke kama umemchoka

Ukimchoka mkeo, waweza kumtaftia sababu za kumuacha kama hizi

_
1. Missed calls 16? Umeua betri la simu yangu. Kwa hiyo hata mimi unaweza kuniua… It’s Over!!!
_
2. Hata hunieshimu. Mi naongea na wewe lakini we upo bize unavuta pumzi? It’s over!
_
3. Nimekupigia umepokea simu hapohapo. Huna subira. It’s over!!
_

4. Nilikwambia huwa napenda chakula cha moto lakini hujanipashia ice cream. Hunijali. It’s over!
_
5. Nimekupa mayai mawili, moja uchemshe jingine ukaange. We umekaanga ambalo ulitakiwa kuchemsha na umechemsha ulilotakiwa kukaanga. Huniheshimu, It’s over!
_
6. Nimekuita DARLING na wewe ukaniita HONEY. Yani kwa maana nyingine unamuita mama yangu NYUKI. Huheshimu wazazi wangu, fungasha kilicho chako. its over.

😄😂😄😂😄😂😄😂😄

Jinsi ya kuandaa mbangimwitu kama Dawa ya magonjwa na ya kuulia wadudu shambani

Mbangi mwitu au kwa kisayansi ni African marigold / (Tagetes erecta) Unazuia Bakteria, fungusi na wadudu kama vile Siafu, bungo pamoja na aina nyingine za wadudu.

Hatua za Maandalizi ya dawa na kutumia

  1. Ponda gramu 100-200 za matawi, mizizi na maua;
  2. Weka lita moja ya maji yaliyochemka;
  3. Loweka kwa masaa ishirini na nne;
  4. Ongeza lita moja ya maji baridi,
  5. Nyunyiza kwenye mimea au mchanga.
Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About