SMS, Vichekesho, Mahusiano, Biashara na Ujasiriamali, Afya, Chemsha Bongo, Dini pamoja na Vitabu kwenye PDF

Karibu AckySHINE

🤣😃😂

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Jinsi wigo wa mimea kwenye shamba unavyoweza kukinga mazao yako na wadudu waharibifu

Jinsi wigo wa mimea kwenye shamba unavyoweza kukinga mazao yako na wadudu waharibifu

Wigo wa mimea ni kinga nzuri ya mazao shambani. Mimea ya wigo inaweza kutumika kama kizuizi cha wadudu kuhama hama.

Wigo hutatiza vidukari kuhama na kuingia bustanini. Kwa mfano, mimea kama tithonia ni kizuizi kwa aina nyingi sana za wadudu.

Safu za mbaazi zimekuwa zikitumika kulinda nyanya, viazi, kabichi dhidi ya buibui wekundu.

Maharage yanaweza kupandwa kati ya mistari ya kabichi yakiwa kama mitego kwani yanasaidia kulinda kabichi dhidi ya buibui wekundu.

Maharagwe yanapandwa kama mtego kwenye kabichi lakini yanafanya kazi ya kudhibiti wadudu (mtego), kuboresha udongo, chakula cha mifugo, matandazo au kutengenezea mbolea.

Vile vile wigo wa mimea ni makazi ya wanyama/wadudu wanaowinda.

Faida za kula Karoti kiafya

Asilimia kubwa tunapenda kutumia karoti katika kuunga katika mboga ya nyama na si kuila karoti kama karoti. wataalamu wanashauri ili uwe na afya bora unatakiwa ule karoti sita kwa wiki au moja kwa siku. Unaweza kula karoti ya kuchemshaa,juisi au mbichi.

Zifuatazo ndizo faida za kutumia karoti;

·Karoti ina element ijulikanayo kama beta-carotene ambayo husaidia kupambana na kansa.

·Pia ni chanzo kizuri cha vitamin na husaidia kuongeza kinga ya mwili,

·Karoti ina vitamin A ambayo ina patikana kwa wingi husaidia kuongeza uwezo wa kuona na mawasiliano ya seli.

· Pia ina madini kama sodiam,sulphur,chlorine na iodine.

·Juisi ya caroti husaidia sana katika kutibu ngozi iliyo kauka na ulaji wa mara kwa mara hupunguza uwezo wa kupata vidonda vya tumbo pamoja na madhara mengine kwenye mfumo wa chakula.

Dalili za mwanamke anayeelekea kukukubali baada ya kurusha voko a.k.a kutongoza

Dalili ni hizi;

Anaongeza ukaribu

Ukiona anapenda kuwa karbu na wewe na kuandamana na wewe na anajisikia ufahari kuwa na wewe jua anaelekea kukukubali. Ukiona anajishauri ujue labda anaona hamlingani kuwa pamoja.

Anaanza kukuchunguza

Ukiona haachi kukuuliza maswali binafsi na kutaka kufahamu unaishije ikiwa na pamoja na kufahamu mambo unayoyapenda mfano unapenda vyakula vipi ujue anapenda kukujua zaidi ili akupendeze.

 

Anaulizia ndugu zako

Ukiona anapenda kukuulizia habari za ndugu zako na kutaka kuwafahamu basi ujue tayari amekukubali na anaanza maandalizi ya kujenga mahusiano nao.

Anakwambia mambo yake

Ukiona hupenda kukupasha habari zake binafsi na za ndugu zake wakiwemo marafiki zake basi ujue amekukubali na anakuaandaa kuwa kama mwenzake.

 

Anaonyesha kwa matendo

Kwa mfano anajishikashika maeneo ambayo yanautangaza uzuri wake kama usoni, nywele zake au hata kurekebisha nguo zake jua anajaribu kuwa mtanashati mbele yako ili akuvutie. Katika mazingira hayo dalili zote zipo kuwa kuna uwezekano mkubwa tayari anakukubali.

Yafahamu Mambo Mbalimbali kuhusiana na Wanawake kwa Ku-Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

Kitabu hiki ni Soft copy [pdf] kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.

Mambo ya msingi kujua kuhusu ugonjwa wa ngiri

Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikilia au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiliwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Tatizo la ngiri huweza kumpata mtu yeyote. Miongoni mwa vitu vinavyoweza kumsababisha mtu apate ugonjwa wa ngiri ni: Kuwa na uzito mkubwa wa mwili au kuongezeka uzito kwa ghafla, kazi ya kubeba au kunyanyua vitu vizito, tatizo la kukohoa au kupiga chafya kwa muda mrefu, ujauzito au matatizo yanayojitokeza kwa mwanamke wakati wa kujifungua pia kuharisha au kuvimbiwa (Constipation). Vitu hivyo pamoja na mtu kuwa na misuli au tishu zilizopoteza uimara au uwazi (opening or hole) humfanya mtu apate ngiri (hernia).

Ngiri hutambuliwa kwa kutokea kitu kama uvimbe au kujaa katika eneo husika (baadhi ya maeneo yametajwa hapo juu) na pia kwa kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara na daktari huwezesha kugundua tatizo hili.

Njia inayoweza kutatua tatizo hili ni kwa mtu mwenye ngiri kufanyiwa upasuaji ili kurekebisha misuli au tishu zilizolegea. Pia kutegemeana na kihatarishi cha tatizo hili, mtu unaweza kuwa unafanya mazoezi ili kupunguza uzito wako na kuweka utaratibu mzuri wa kula chakula kinachojumuisha mboga mboga au matunda yenye nyuzi nyuzi (fibers), hii itasaidia pia mmeng’enyo (digestion) wa chakula tumboni na kuepusha kuvimbiwa. Matunda (Vitamin C) husaidia kuunganisha tishu zilizolegea na pia husaidia kupona haraka kwa sehemu iliyofanyiwa upasuaji (operesheni). Na kama tatizo lako ni la kukohoa kwa muda mrefu kunakosababishwa na uvutaji wa sigara, ni vyema ukasitisha uvutaji ili kupunguza madhara au makali ya ngiri lakini pia kusitisha sigara kwa ajili ya usalama wa afya yako.

Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About