SMS, Vichekesho, Mahusiano, Biashara na Ujasiriamali, Afya, Chemsha Bongo, Dini pamoja na Vitabu kwenye PDF

Karibu AckySHINE

๐Ÿคฃ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜‚

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Jinsi msongo wa mawazo unavyoweza kukusababishia ugonjwa wa moyo

Kila mmoja wetu anaweza kuwa na sababu tofauti inayoweza kumsababishia msongo (stress). Sababu kubwa ambazo husababisha msongo ni masuala ya kazi hata pia masuala ya kijamii. Masuala ya kikazi ni kama kutokuwa na furaha kazini, kazi nyingi, kufanya kazi kwa masaa mengi, kutokuwa na mipangilio bora, kutokujiwekea malengo na mengine mengi.

Masuala ya kijamii ambayo hupelekea msongo ni kama kupoteza mtu umpendaye, ndoa kuvunjika, kupoteza kazi, kuongezeka majukumu ya kifedha, magonjwa sugu, matatizo ya familia na mengineyo mengi.

Wakati mwingine msongo waweza kutokana na nafsi ya mtu mwenyewe na siyo sababu za nje ya mtu. Mfano mtu kujitengenezea mazingira ya kufikirika yanayoogofya yamleteayo wasiwasi na msongo.

Jinsi msongo wa mawazo unavyosababisha Magonjwa ya moyo

Watu walio na msongo (Stress) wanakuwa katika hatari zaidi ya kupata magonjwa ya moyo kuliko wale wenye utulivu, hii ni kwa mujibu wa wataalam na watafiti mbalimbali wanaohusiana na magonjwa ya moyo. Magonjwa haya ya moyo ni kama shinikizo la juu la damu, moyo kwenda mbio na mengineyo.

Matabibu wanafahamu kuwa, msongo wa ghafla waweza kusababisha magonjwa hatari ya moyo kama shambulizi la moyo. Watu wenye matatizo ya moyo hawana budi kuepuka hali ya msongo na kujifunza jinsi ya kukabiliana na maisha katika hali ya utulivu kwa kadiri iwezekanavyo.

Hivyo ili uweze kuepuka ugonjwa huu unachoptakiwa kufanya ni kuhakisha unaepuka visababishi vyote vya ugonjwa huu vya msongo, ambavyo nimekwisha vielezea hapo awali.

Matumizi ya juisi ya limao kutibu shinikizo la chini la damu

Juisi hii ni nzuri sana katika kutibu shinikizo la juu la damu.

Lakini inaweza pia kutumika kutibu shinikizo la chini la damu hasa ikiwa hili shinikizo la chini la damu limesababishwa na upungufu wa maji mwilini (dehydration).

Kutibu shinikizo la chini la damu unaweza kuchanganya juisi ya limau na chumvi kidogo na sukari au unaweza kutumia maji maji ya miwa.

Misemo 10 bora ya kuchekesha itakayokuacha mdomo wazi

1. Mwanaume hata awe bahili vipi, hawezi kumpa mwanamke mimba nusu.

2. Hata uwe na magari mangapi chooni utaenda kwa miguu.

3. Kama ubinadamu kazi mbona hatupewi mishahara?

4. Ukichanganya wali na choroko unapata mseto, lakini hautibu malaria.

5. Hata njiwa nae ana makinda, lakini hawezi kuwa spika wa Bunge.

6. Hata uwe na haraka vipi kwenda Zenj, huwezi kupanda Jahazi ya Yusuph Mzee.

7. Umeme hauna kiuno lakini unaongoza kwa kukatika.

8. Hata uwe kauzu vipi, huwezi kujamba wakati unatongoza.

9. Hata uwe na imani kali vipi, huwezi kusali wakati unafanya mapenzi.

10. Hata kizibo ni mfuniko lakini hauwezi
kufunika sufuria.

Vyakula 7 vya kuepuka kula ili uwe na afya nzuri

Inasemwa kuwa โ€œwewe ni kile unachokulaโ€ kwa kumaanisha kuwa mwonekano wetu na afya ya mwili na akili unajengwa na chakula tunachokula. Madhara ya chakula chetu tunachotumia yako pia katika ngozi. Kuna vyakula vinavyozeesha ngozi kwa haraka na ni budi kuvijua na kuviepuka.

Vyakula hivi japo tunavipenda sana lakini vina athari mbaya kwa miili yetu na muhimu kujenga tabia ya kuviacha katika milo yetu. Kama si rahisi kuacha kabisa basi angalau kupunguza matumizi yake.

Vifuatavyo ni vyakula 7 vinavyozeesha ngozi na unashauriwa kuvitoa katika mlo wako:

1. Nyama Nyekundu
Mojawapo ya vyakula vinavyozeesha ngozi ni nyama hasa nyama nyekundu. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa nyama nyekundu inayotokana na wanyama kama ngโ€™ombe,mbuzi,kondoo,nguruwe n.k ni mbaya kwa afya njema ya binadamu na hivyo kwa ngozi pia. Nyama nyekundu ina kemikali aina ya carnitine ambayo inafanya mishipa ya damu kukakamaa na kusababisha kuzeeka kwa ngozi.

Hivyo nyama nyekundu ni mojawapo ya vyakula vibaya kwa afya ya binadamu na vya kuvizuia.

2. Chumvi

Chumvi hasa yenye madini ya iodine ni mbaya sana kwa afya ya ngozi. Inasababisha chembechembe za nyama katika ngozi kuvimba.

3. Sukari

Sukari japo tunaipenda sana ni adui mkubwa wa afya ya binadamu. Inadhoofisha mfumo wa kinga za mwili. Kiasi kingi cha sukari mwilini kinafanya ngozi kuwa kavu na kufanya mwili utengeneze makunyazi kwa sababu inaharibu kemikali ya collagen na elastin ambazo zinafanya kazi ya matengenezo ya ngozi kuifanya isiharibike na kuwa chakavu.

Sukari nyingi inasababisha mwili kukosa nguvu ya kupambana na bacteria wabaya. Ongezeko la bacteria hawa kunafanya utengenezwaji wa kemikali mbaya ambazo husababisha uchakavu wa ngozi.

Watu wanashauriwa kutumia sukari asilia kama ya matunda na asali kuliko zile zinazopatikana katika vinywaji kama soda na pipi , jojo,biskuti au vitafunwa vingine vyenye sukari ya kuongeza.

4. Vyakula vya Kukaangwa

Vyakula vya kukaangwa kama chipsi,nyama za kukaanga vinasababisha uingizaji wa mafuta mengi mwilini. Mafuta haya yenye vitu vinavyoitwa โ€œFree Radicalsโ€ yanasababisha uzibaji wa vijitundu katika ngozi. Ukiachia ngozi mafuta mengi mwilini yanasababisha madhara mengi mengine yakiwemo magonjwa ya moyo na kisukari.

5. Mkate Mweupe,Tambi na Keki

Vyakula hivi vina kemikali ya glucemic kwa kiwango kikubwa ambayo inaleta madhara ya magonjwa ya ngozi (Ugonjwa wa madoa katika ngozi)

6. Pombe

Unywaji wa pombe unasababhisha kupoteza maji mengi mwilini kwa njia ya mkojo na huleta madhara mabaya kwa ngozi kwa kuifanya iwe kavu.

7. Kahawa (Caffeine)

Kemikali ya caffeine iliyomo katika kahawa na vinywaji vingine inasababisha ukosefu wa maji ya kutosha katika ngozi na kuifanya iwe kavu. Lakini pia caffeine inasababisha utengenezwaji wa kemikali ya cortisol ambayo inachangia uzeekaji wa ngozi.

Badilisha Tabia Yako ya Ulaji

Vyakula hivi ni baadhi ya vingi ambayo vimo katika ulaji wetu wa kila siku na una madhara makubwa kwenye ngozi zetu. Wanawake wanaathirika sana na ngozi ukilinganisha na wanaume. Au niseme wanajali sana ngozi zao kuwa zenye afya na kuvutia kuliko wanaume hivyo wanaweza kufaidika sana kwa kupunguza au kutotumia kabisa hivi vyakula vinavyozeesha ngozi.

Fahamu kuwa afya yako ni mtaji mkubwa hivyo ni kitu muhimu kuipa afya ya mwili wako kipaumbele na hivyo zingatia ulaji wako.

Mbinu za kuzuia magonjwa kwa kuku

Mbinu hizo ni hizi zifuatazo;

Namna ya kufanya Ukaguzi wa mara kwa mara wa banda la kuku kuzuia magonjwa

Ukaguzi wa Kila siku
โ€ข Hakikisha unasafisha vyombo vya kulishia na kunyweshea pamoja na viota.
โ€ข Ondoa kinyesi kwa kuku.
โ€ข Waangalie kuku wako kwa makini ili kujua afya na maendeleo yao. Yaani ili kutambua kama kuna mwenye ugonjwa

Ukaguzi Kwa wiki
โ€ข Ondoa matandazo machafu na kuweka mapya ili kuzuia kuzaliana kwa vijidudu vya magonjwa.

Ukaguzi kwaKwa mwezi
โ€ข Angalia uwepo wa wadudu na chawa, kisha utibu kama kuna ulazima.

Mambo 8 ya kuzingatia kabla ya kuleta mifugo (kuku, ng’ombe,mbuzi n.k) wapya bandani

Mambo hayo ni haya yafuatayo;
1. Hakikisha unaondoa matandazo yote ndani ya nyumba,
2. Ondoa vyombo vya kulishia na kunyweshea.

3. Ondoa uchafu wote unaoonekana bandani.
4. Safisha banda lote kwa kutumia maji na dawa.
5. Suuza na uache likauke.
6. Puliza dawa ya kuua wadudu.
7. Weka matandazo mapya,
8. Weka viombo vya kulishia na kunyweshea.

Jinsi ya kutunza nyumba ya kuku ili kuzuia magonjwa

1. Nyumba ya kuku iwe safi na kavu muda wote kuzuia ueneaji na kuzaliana kwa vijidudu vya magonjwa

2. Nyumba ya kuku iwe na nafasi za kupitisha hewa ya kutosha ili kuepuka joto na unyevunyevu ambao unachangia uwepo wa magonjwa kwa kuku

3. Hakikisha unaondoa matandazo na takataka zote kwenye banda wakati wote hasa yenye unyevu.

4. Fagia banda na kuhakikisha ni safi wakati wote. Weka matandazo mapya mara kwa mara.
5. Weka sehemu za kutosha kuku kupumzikia.
6. Weka viota vya kutosha.
7. Weka maji sehemu ambayo ni rahisi kusafisha.
8. Hakikisha unaondoa wanyama kama panya na wadudu nyemelezi kwenye sehemu ya malisho ya kuku kwani wao hubeba vimelea vya magonjwa.

Namna ya kutunza kuku na kuwakinga na magonjwa

1. Zingatia chanjo muhimu kwa kuku ili kuzuia magonjwa kama utakavyoshauriwa na mtaalamu wa mifugo.
Chanjo huanza katika wiki ya kwanza (mfano chanjo ya kuzuia sotoka) na inaweza kurudiwa baadaye.

2. Epuka kuweka kuku wengi mahali pamoja.
Ni rahisi magonjwa kuenea kwa haraka kuku wanaporundikana.

3. Kumbuka kutenganisha vifaranga na kuku wakubwa (isipokuwa kutoka kwa mama) kwa sababu vifaranga ni rahisi na wepesi sana kushambuliwa na magonjwa.

4. Hakikisha unaweka mipaka na madaraja ya sehemu za kuku kuzunguka/kucheza.

Namna ya kulisha kuku ili wasipatwe na magonjwa

Safisha vyombo vya kulishia na kunyweshea kila siku. Osha, sugua vizuri, kisha suuza kuondoa utando unaobeba bakteria.

Kuku wanahitaji wapewe chakula cha kutosha na chenye virutubisho vyote. Unaweza kuwaongezea majani, makombo, nafaka, mchanga laini, au maganda ya mayai.

Wapatie kuku maji safi muda wote. Wafugaji wengi wameripoti kuwa na matokeo mazuri baada ya kuchanganya dawa ya kuua vimelea kwenye maji ya kunywa.

Nunua chakula kwa wauzaji wazuri na wanaoaminika ili kuepuka minyoo na sumu hatarishi. Usiwape kuku chakula chochote kinachoonekana kuoza au kunuka uvundo.

Hifadhi chakula cha kuku katika sehemu kavu isiyo na joto na isiwe kwa zaidi ya miezi mitatu ili kuepuka kuharibiwa na fangasi.

Namna ya kukabiliana na Magonjwa ya kuku

Hakikisha unamuona mtaalamu wa mifugo mara uonapo dalili zozote za kuumwa kwa mifugo wako.

Tenga na wapatie tiba au kuwaua na kuteketeza kabisa kuku wagonjwa kuepuka kuenea kwa magonjwa.

Ondoa ndege waliokufa mara moja, uwafukie au kuchoma moto. Usile kuku aliekufa. Baadhi ya magonjwa ya ndege yanaweza kuambukizwa kwa binadamu.

Endapo kuna mlipuko wa ugonjwa katika eneo lako, usiruhusu watu kutembelea banda lako. Watu wanaweza kuleta maambukizi kwa miguu yao katika mabuti, nguo na mikono.

Pia magari yanaweza kuleta madhara kwa mabanda yako kupitia matairi na upakuaji wa mizigo.

Jinsi wigo wa mimea kwenye shamba unavyoweza kukinga mazao yako na wadudu waharibifu

Jinsi wigo wa mimea kwenye shamba unavyoweza kukinga mazao yako na wadudu waharibifu

Wigo wa mimea ni kinga nzuri ya mazao shambani. Mimea ya wigo inaweza kutumika kama kizuizi cha wadudu kuhama hama.

Wigo hutatiza vidukari kuhama na kuingia bustanini. Kwa mfano, mimea kama tithonia ni kizuizi kwa aina nyingi sana za wadudu.

Safu za mbaazi zimekuwa zikitumika kulinda nyanya, viazi, kabichi dhidi ya buibui wekundu.

Maharage yanaweza kupandwa kati ya mistari ya kabichi yakiwa kama mitego kwani yanasaidia kulinda kabichi dhidi ya buibui wekundu.

Maharagwe yanapandwa kama mtego kwenye kabichi lakini yanafanya kazi ya kudhibiti wadudu (mtego), kuboresha udongo, chakula cha mifugo, matandazo au kutengenezea mbolea.

Vile vile wigo wa mimea ni makazi ya wanyama/wadudu wanaowinda.

Faida za kula karanga mbichi

Karanga ni muhimu sana katika afya ya mwili wa binadamu. Kiukweli karanga siyo chakula cha kupuuziwa iwapo utajua faida zake kama nitakavyokujuza leo katika makala haya.

1. Kwanza kabisa karanga husaidia katika kutibu magonjwa ya moyo.

Kama ilivyokuwa kwa korosho, karanga nazo ni chanzo kizuri cha mafuta mazuri aina ya monounsaturated fatsโ€™ ambayo yanatiliwa mkazo kutumiwa kwa afya ya moyo. Kwa mujibu wa utafiti, watu wanaokula karanga mara kwa mara hupunguza hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo (cardiovascular heart disease).

Aidha, katika taarifa iliyochapishwa kwenye jarida moja la Uingereza la โ€˜Journal of Nutritionโ€™ ambako kuna matokeo ya taarifa nne za utafiti, imeonesha pia watu wanaotumia karanga mara kwa mara, angalau mara nne kwa wiki, hujipa kinga nyingine dhidi ya ugonjwa wa moyo (coronary heart disease) kwa zaidi ya asilimia 37.

Mbali ya kuwa na mafuta mazuri yanayotoa kinga kwenye moyo, karanga pia, zinaelezwa kuwa na kiwango kikubwa cha virutubisho vinavyotoa kinga ya mwili (antioxidants) kuliko hata kile kinachopatikana kwenye tunda la epo na karoti!

Ili kupata kinga hiyo dhidi ya aina hizo mbili za ugonjwa wa moyo, ambao unatesa watu wengi duniani na kugharimu pesa nyingi kwa matibabu, unashauriwa kula karanga pamoja na bidhaa zake kama vile peanut butte, angalau kijiko kimoja cha chakula, mara nne kwa wiki.

2. Kinga dhidi ya kiharusi.

Ugonjwa mwingine hatari unaosumbua watu wengi hivi sasa ni kiharusi au strokeโ€™, lakini unaweza kujikinga nao kwa kuwa na mazoea ya kula karanga tu.

Utafiti umeonesha kuwa karanga ina kirutubisho aina ya Resveratrol ambacho hupatikana pia kwenye zabibu na mvinyo mwekundu (red wine). Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa maabara na kuchapishwa kwenye jarida la Kilimo na Kemia ya Chakula (Journal of Agricultural Food Chemistry),

umeonesha kuwa kirutubisho hicho huimarisha utembeaji wa damu kwenye mishipa inayokwenda kwenye ubongo kwa kiasi cha asilimia 30.

3. Kinga dhidi ya magonjwa ya moyo.

Faida nyingine inayoweza kupatikana kwenye mwili kutokana na ulaji wa karanga, ni kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani ya tumbo. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa, unaonesha kuwa virutubisho vya folic acid, phytosterols, phytic acidโ€™ (inositol hexaphosphate) na resveratrolโ€™ vinavyopatikana kwenye karanga, huweza kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani ya tumbo.

Zaidi utafiti huo umeonesha kuwa ulaji wa karanga hata mara mbili tu kwa wiki, una uwezo wa kupunguza uwezekano wa kupatwa na saratani ya tumbo kwa asilimia 58 kwa wanawake na asilimia 27 kwa wanaume. Kwa maelezo hayo kuhusu faida za karanga mwilini bila shaka chakula hiki kinapaswa kupewa kipaumbele katika orodha ya vyakula tunavyokula.

kila siku na hakika Mungu ametupenda sana kwakutupa kinga dhidi ya maradhi yote yanayotukabilikwa njia ya vyakula.

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About