Ujumbe mzuri wa mapenzi kwa mpenzi uliye mmiss
Nina huzuni moyoni sijui kwa kuwa siku hizi sikuoni,
naishia kukuota ndotoni,
hivi kweli nipo kwako moyoni? Nakupenda
Nina huzuni moyoni sijui kwa kuwa siku hizi sikuoni,
naishia kukuota ndotoni,
hivi kweli nipo kwako moyoni? Nakupenda
Joto ndio kitu nachotarajia kutoka kwao mke wangu
mtarajiwa, usisikilize maneno yakuambiwa, ni wewe tu
mwenye thamani kwangu katika hii dunia.
Ngozi kavu inaweza kukufanya ukose raha kutokana na kuwasha mara kwa mara, lakini pia kupauka hii inaweza kusababisha mikunjo ya ngozi na hata kupatwa na vidonda katika ngozi. Ngozi kavu husababishwa na baridi lakini pia unaweza ukawa umezaliwa nayo tu upo hivyo. kama una ngozi ya aina hii basi haya ni mambo matatu ya kuyaepuka kufanya.
Epuka kuoga maji ya moto mara kwa mara kunaweza kufanya yale mafuta natural yanayo moisturize mwili kukauka, ili kuepuka tatizo hili ni vyema ukatumia maji ya uvuguvugu au baridi katika kuoga au kunawa mwili wako.
Alcohol nyingi husababisha ngozi kuzidi kuwa kavu, wakati wa kwenda kununua vipodozi vyako hakikisha unasoma maelezo na kujua kiasi cha alcohol kilichopo kama ni nyingi usichukue chukua yenye kiasi kidogo.
Kuosha ngozi mara nyingi sana na sabuni ni njia ya mojawapo ya kupata ngozi kavu. Ngozi kavu iliyokasirika huathirika zaidi na maambukizi ya bakteria kwa sababu kuosha mara nyingi huondosha safu za kinga ya ngozi yako.
Mzee mmoja alipanda Gari Stend;
Wakati wa kugombania Siti,
Akaibiwa Nauli.
Akasimama katikati ya Gari-Akasema; “Jamani Naomba Aliyeniibia Pesa yangu Arudishe Haraka,
Tena Fasta kabla Sijafanya Tukio kama Nililofanya 1977″
Abiria kuskia hivyo wakaogopa.
Ikabidi Mwizi Ajitokeze,
Akarudisha Pesa na Kuomba Msamaha! Mtu Mmoja akauliza,
Mzee,
Kwani 1977 Ulifanya nn?
Si nilienda kwa Miguu mpaka Nyumbani!
Uscheke Peke Yako, wa2mie na wengine ili nao wacheke!
Maneno huanza na ABC. Namba 123. Muziki na do re mi na
mapenzi huanza na mimi na wewe.
๐๐ ๐๐๐๐๐๐ Jamaa kagombana na mkewe, akasusa kula๐ฝ๐จ kurudi kazini kamkuta mkewe amevaa kanga imeandikwaย ukisusa wenzio walaย ilipofika asubuhi mke akavaa kanga imeandikwaย ukitoka ๐ถ๐ถmwenzio anaingia๐๐
jamaa akagoma kwenda kazini ๐ฌ๐ฌ mke akabadili kanga na kuvaa iloandikwaย nimemdhibiti ndo mana hatoki๐ท jamaa akaenda kuomba ushauri kwa rafiki yake akaambiwa twende nyumbsni kwako, walipofika walimkuta mke kavaa kanga imeandikwaย ulidhani rafiki yako kumbe adui yako๐ค๐ค jamaa akaamua kusafiri siku tano ili kupunguza hasira. Aliporudi akamkuta mke amevaa kanga imeandikwaย ni bora nimpe jirani kuliko kiozee ndani
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
hata kama hupendagi ujinga kwa maneno ya kwenye kanga utasanda tu
Udongo ni kiungo muhimu sana katika uzalishaji wa mazao. Ni mfumo wa uhai kwa mimea. Kwa hiyo, mkulima ni lazima alenge katika kutunza uhai wa udongo na kuepuka usumbufu kwa uhai wa udongo.
Sababu muhimu za kulima/kutifua udongo ni:
โข Hulainisha udongo ili kuruhusu mizizi ya mimea kupenya kwa urahisi.
โข Kutifua kunaboresha uwezekano wa kupenya kwa nitrogen na oxygen kutoka kwenye hewa.
โข Kunawawezesha viumbe hai waliopo kwenye udongo kufanya kazi zao ipasavyo.
โข Kunasaidia Kuandaa sehemu ya kuwekea mbegu.
โข Kutifua kunauongeza uwezekano wa maji kupenya kwenye udongo na kupunguza uyeyukaji wa maji.
โข Kuchanganya mabaki ya mimea na samadi kwenye udongo
Kama ilivyo kwa binadamu, viumbe hai wanahitajika kwa udongo wenye rutuba, pia mimea inahitajika kwa ajili ya binadamu kupata hewa safi ya oxygen. Kuchanganya matandazo,na mboji kwenye udongo ni muhimu sana ili kuboresha mzunguko wa hewa. Viumbe hai wadogo wadogo, wadudu, minyoo, na wanyama wengineo wanapenyeza hewa kwenye udongo.
Huu ni utaratibu wa kufunika udongo kwa kutumia mabaki ya mimea, kwa mfano, matawi madogo madogo ya miti, majani, mabaki ya mimea ya mazao, magugu na kadhalika. Hata hivyo inahitajika nguvu kazi kwa ajili ya kutawanya matandazo.
Matandazo yanazuia mmomonyoko wa ardhi unaotokana na maji na upepo, yanasaidia ardhi kunyonya maji ya mvua, kutunza unyevu unyevu kwenye udongo kwa kuzuia myeyuko wa maji ardhini.
Matandazo yanapo oza hutoa virutubisho vinavyoboresha na kuongeza rutuba kwenye udongo, mbali na hilo pia hubadilika kuwa udongo mweusi wenye rutuba zaidi. Kama kuna uhitaji wa kuharakisha kuoza kwa matandazo ili kuongeza rutuba kwenye ardhi kwa haraka, kinyesi cha ngโombe kinaweza kuwekwa na kutandazwa juu ya matandazo, hii husaidia kuongeza virutubisho vya nitrogen.
Matandazo yana faida nyingi sana kwenye ardhi, lakini pia yanaweza kusababisha madhara. Mabaki ya mboga za majani yasitumike kama matandazo kwani yanaweza kusababisha wadudu na magonjwa kwa mimea. Viumbe hatari kama bangu (stem borers) wa shina wanaweza kuishi kwenye mabaki ya mimea.
Mabaki ya mimea iliyokuwa imeathiriwa na magonjwa ya virusi au fangasi yasitumike kama matandazo kuepuka uwezekano wa magonjwa hayo kuambukizwa kwa mazao yatakayopandwa msimu utakaofuata. Kilimo cha mzunguko ni njia bora kuepuka athari hiyo.
Kupanda mazao kwa mzunguko ina maana ya kuwa na aina mbalimbali ya mazao katika eneo moja kwa msimu.
Kwa mfano, kama shamba lako umepanda mahindi na maharagwe kwa kipindi cha mwaka mmoja, mkulima anaweza kubadili mzunguko kwa kupanda aina nyingine ya mazao katika eneo hilo kwa mwaka unaofuata.
Mimea iliyo mizuri zaidi katika kilimo cha mzunguko ni pamoja na jamii ya kunde, au malisho kama sesbania ambayo husaidia kuongeza rutuba kwenye udongo.
Udongo unatakiwa ulishwe ili uwe na virutubisho. Hii ni kazi muhimu sana kwa kila mkulima. Mkulima anaweza Kuulisha udongo kwa kutumia samadi na mboji. Kumbuka udongo uliotumika sana bila virutubisho, umekufa, hauwezi kuzalisha.
Maji ni mazuri shambani, lakini maji yakizidi ni hatari. Maji yakizidi shambani yanaweza kusababisha mmomonyoko wa udongo. Mmomonyoko wa udongo ni tishio na baa hatarishi kwa rutuba kwenye udongo. Mmomonyoko unaondoa tabaka la juu la udongo, sehemu ambayo ndiyo yenye rutuba zaidi.
Kupanda mimea kwa matuta (kontua) hupunguza kasi ya maji. Baada ya miaka kadhaa, nyasi zinazopandwa zinazopandwa kwenye matuta ya kontua husaidia kuunganisha na kusawazisha sehemu iliyotengwa, kwa kuwa udongo unaomomonyolewa hukusanyika katika sehemu iliyozuiwa na kuunganishwa kwa matuta.
Kwenye mwinuko mkali, kuta au mashimo, ndiyo njia pekee inayoweza kuzuia mmomonyoko wa udongo. Changanya na mimea kama matete, inasaidia kuzuia mmomonyoko na pia kutoa malisho kwa mifugo.
Mbali na matandazo (tazama hatua ya 3) mimea inayotambaa ni mbinu nyingine nzuri zaidi inayoweza kuzuia mmomonyoko wa ardhi. Matone ya maji hufikia ardhi yakiwa na nguvu kidogo sana hivyo kuepuka kumomonyoa ardhi, kwa kuwa yanakuwa tayari hayana nguvu ya kutiririka kwa kasi. Pia mimea inayotambaa hutumika kama kivuli kwa udongo. Mmea wowote unaofunika udongo na kuongeza rutuba unaweza kutumika.
Mfano maharage na mimea mingine ya jamii ya kunde, ambayo ina virutubisho vya nitrogen kwa wingi. Mimea inayopendekezwa ni ile ya jamii ya kunde. Inastahimili ukame, inatoa virutubisho vya naitrojeni, inatoa chakula, na pia inaweza kutumika kama chakula cha mifugo kilicho na protini nyingi. Kwa kuongezea inaweza pia kukabiliana na wadudu waharibifu.
Jamaa alimpa ujauzito mwanafunzi akashtakiwa kumbe yule jamaa ana bibi yake mtaalam wamambo yetu ya Jadiโฆ
Jamaa akaongea na bibi yake amuwekee jinsia ya kike ili akashinde Mahakamani na akitoka arudishiwe mambo yake kama kawaida.
Bibi akampachika jamaa jinsia ya kike alipofika mahakamani kuhojiwa akasema mi sijampa ujauzito kwasababu minina jinsia ya kike piaโฆ!
Kwa kuthibitisha akajifunua nguo, basi jamaa akashinda kesi.
Jamaa akawa anarudi Home, lakini wakati anakaribia kufika akaona watu wengi wamejaa home wanalia akauliza kulikoni akaambiwa “Bibi amefariki”!
Vuta picha hapoโฆ!!!
Darasa lolote lile (hasa vyuoni) lazima liwe na wanafunzi wafuatao:
1. Mrembo wa darasa.
2. Playboy/playgirl. Hawezi kutembea na msichana/mvulana mmoja mara mbili.
3. Group ya marafiki watatu. Kila mara wako pamoja.
4. Mtu mwenye maswali ya kuudhi/kukera.
5. Msongolist kimeo. Huyu huwa anasoma sana bt hana bahati ya kufanya vizuri. Yani msuli tembo, bt matokeo sisimizi.
6. Mlafi. Huyu huwa hakatai offer.
7. Mtoro wa kudumu. Haji darasani hata km hana sababu.
8. Mchelewaji wa kudumu. Anakuja kipindi kiko katikati au kinakaribia kuisha.
9. Miss/Mr.Misifa. kila mara ataeleza the way nyumbani kwao walivyo matajiri.
10. Less talkative bt kiwembe. Jamaa mkimya bt unakuta ametembea na karibu wasichana 15 hapo class.
11. Handsome boy ambaye hana mpango na wanawake.
12.Chips addicted. Hawa wanaweza kula chips asubuhi mchana na jioni. Jumatatu hadi jumatatu.
13. Back benchers. Hawa huwa watundu sana na ni watu wa jokes. Huwa hawajibu swali, but wanasubiri wakati wa kushangilia waongeze bezi.
14. Wambea. Hawapitwi na kitu darasani na washazoea kufeli.
15. Mchungaji/Mtumishi wa Mungu,
16. Waimbaji/Wasanii,
17.Walevi
18.Mabishoo.
19. Team popo. Hawa wewe na hela wasiwe na hela wanakesha club,
20.Mwenye aibu kusimama mbele za watu. Wakati wa Presentation anakimbilia kusimama nyuma ya wenzie,
21. Viherehere. Hawa mara nyingi hutokea kupendwa sana na waalimu.
22. Wanaosoma ili kushindana kwny GPA.
23. Kupe. Huyu boom likitoka atawaganda wenzie hadi ziishe, halafu yeye anaanza kula zake alone.
24. Wise man/woman. Huyu huwa ni mtu anayeaminika na kila mtu darasani. Hutumika sn kushauri pale mambo yanapoenda mrama. Mara nyingi huwa ni mtu mzima.
25.mpenda supu” yeye hata ya nyani atakunywa tu.
26.Fix man. Huyu atakuomba jero, akafuatilie dili la milioni kumi town, kumbe hana hela ya chai.
27. Photocopy machine. Huyu ukimuonesha majibu kwny mtihani anaweza kucopy hadi jina lako.
๐ฅUsposema wewe uko namba ngapi mwngine atakusema๐๐๐
๐
๐
๐
๐
โโpiga chini kitambiโโ
๐นTikiti๐ 1
๐นTangawizi kidogo
๐นLimao nusu ama apple cider vinegar
โNjiaโ
๐ฒSafisha matunda yako Kwa maji Safi,menya tikiti๐,katakata weka kwenye Brenda ,
๐ฅMenya tangawizi katakata Ila usiweke nyingi,weka kwa Brenda,
๐Kamulia limao kwenye matunda yako saga,baada ya hapo itakua tayar.Mimina kwenye grasi yako๐ธ,ukiweza kunywa kabla hujala kitu,asubuh na endelea kunywa siku nzima,juic hii ni nzuri,na huondoa sumu mwilin ,husaidia kupata choo,huyeyusha mafuta,hung’arisha ngoz
Tukiwa kanisani mdada alikuwa amelala , akaamka akasikia Pastor anasema
” SIMAMA”
Yule dada akasimama akashangaaa kanisa zima linamtizima kwa mshangao akiwemo mumewe, akaangalia kanisa zima akashtuka kujiona yeye peke yake ndiye aliesimama
Pastor akaendelea vizur endelea kusimama, tumepata mmoja hadi sasa aliyesimama narudia kwa mara ya mwisho kama hujasikia vizuri
” kama wew umewahi kumsaliti au bado unasaliti ndoa yako SIMAMA”
Binti akazimia
๐๐๐๐๐๐
Jana nimeenda kuazima pasi chumba jirani, ili ninyooshe nguo zangu, Jamaa wakaniambia nichukue nguo nikanyooshe room kwao maana hawataki pasi yao itoke.
Sasa leo amekuja mmoja wao kuazima mopper akasafishe room, nimemwambia aje adekie humu humuโฆ
Jamaa ameondoka nadhani atakua ameenda kuchukua maji
๐ค๐ค๐ค
Nakupรฉndรค mpรจnzi wรจwรจ รนnรฅumuhimu mkubwa kwenye maisha
yangu kwani ukiniacha mpenzi utanisababishia kovu ambalo
halitapona .nakupenda sana
Tafuta fursa kila kona.
Tumia kipaji chako.
Kuwa na nidhamu katika fedha – matumizi mazuri ya pesa, nidhamu kwa watu wanaokuzunguka, usijikweze, usibague jamii, heshimu wote waliokaribu yako nk.
Kuwa na nidhamu katika afya yako: Afya ndio mtaji sahihi katika biashara yoyoteย – kuwa na mazoea ya kuangalia afya yako mara kwa mara nk.
Usipoteze mudaย – jali muda kuliko kitu chochote kwani muda ndio kila kitu, muda ni mali.
Shiriki kwenye makongamano au semina mbalimbali za ujasiriamali.
Kuwa na vyanzo vingi vya kukuletea kipato.
Tafuta maarifa kwa mamilionea mbalimbali dunianiย – soma historia za mamilionea jinsi walivyofanikiwa.
Jenga urafiki na taasisi za kifedhaย – mamilionea wengi hukopa fedha kutoka katika taasisi za kifedha – tembelea taasisi za fedha watakupa ushauri mbalimbali na watakupa mkopo, usisikilize maneno ya watu kuwa taasisi za pesa ni za watu matajiri hiyo sio kweli.
Kuwa na shauku, kuwa na fikra za kuwa milionea na wewe utakuwa.USIWAZIE KUSHINDWA
Kuwa na imani kwamba utakuwa milionea na itakuwa hivyo. KWA KUFANYA. SIO IMAN TU.
Wekeza ktk miradi au biashara mbalimbali. USIOGOPE KUTHUBUTU
Wekeza sehemu yenye mahitaji ya bidhaa inayotakiwa kuzalishwa – angalia fursa hapo ulipo na wekeza. SIO KUFUJA PESA
Kuwa na bajeti katika mapato na matumizi yako. NIDHAMU MUHIMU KATIKA PESA
Kuwa na wazo (Business idea):ย mamilionea wengi hutumia mawazo kutoka kwa watu mbalimbali kutengeneza pesa. Wazo ndio cheti cha kuwa milionea anza sasa fanyia kazi wazo lako ili kukuletea fedha.
Fanya vitu wewe mwenyewe – acha kufanya vitu kama fulani, usiige mtu, buni vya kwako, mamilionea huwa hawaigi, ukiwa mkweli kwako utakuwa mkweli kwa watu
Kuwa na malengo – kumbuka hakuna maendeleo pasipo na malengo, fahamu hilo.,, PLANS AND SELF COMMITMENT
Kuwa na moyo wa ujasiri – usiogope kushindwa jitahidi ktk kupambana na maisha usikubali kubezwa au kuvunjwa moyo. Ukianguka nyanyuka tena, usifikirie kutakuwa na mtu wa kukusaidia zaidi ya kujisaidia mwenyewe.UKIANGUKA USIOGOPE KUINUKA
Kuwa karibu na matajiri -usiogope kwani hao ni binadamu kama wewe, jaribu kuwadadisi ili wakupe mbinu mbali za kuwa tajiri hadi milionea. Ukiwa karibu nao unaweza ukapata nafasi ya kazi au kukuunganishia biashara ukaanza kufanya na kufanikiwa.
Mtangulize Mungu -mwabudu, msifu, mtolee sadaka, saidia masikini, wajane, wagonjwa, jenga nyumba za ibada. Mungu ndio kila kitu mtegemee yeye.
Fanya vitu kitofauti;ย fanya vitu vigeni, muonekano tofauti ingawa biashara ni ile ile, tumia lugha tofauti, panga bei tofauti, nk. Mfano aina tofauti za simenti, chupa za soda na juisi nk.
Acha wogaย – jaribu biashara yoyote, woga wako ndio umasikini wako, usiogope kukosolewa unapokosolewa ndio unajifunza. Usiogope mikopo, mamilionea wengi hufanya mambo ambayo wewe unayaogopa.
Kuwa na mtazamo chanya – usikubali mawazo hasi, marafiki zako wawe na mawazo chanya, usikubali kuvunjika moyo na usikubali mawazo yako yaingiliwe na mtu.
Anza kufanyia kazi wazo lako usisubiri mtu.
Kuwa na mipaka katika mambo yako – usifanye mambo kwa mkumbo, usiige, buni mambo yako. Mamilionea wengi wanabuni mambo yao hawapangiwi na mtu
Kuwa mwaminifu -mamilionea wengi ni waaminifu ktk mali za watu. Wengi walikuwa wakipewa mali wakauze ndio walipe pesa, wanadhaminiwa malighafi za viwandani hadi wanamiliki viwanda vyao. Uaminifu ndio njia ya kukufanya uwe milionea.
Pokea ushauri kwa watu hasa kuhusiana na biashara yako – waulize watu kuhusu huduma yako ya biashara wanaionaje na fanyia kazi ushauri wao.
Kuwa na plani katika kazi zako kila siku.
Kuwa na maono ya jinsi unavyotaka maisha yako yawe
Panua soko la bidhaa zako usitegemee soko la sehemu moja
Ubunifu ni muhimu sana – fanya ubunifu ktk kuuza bidhaa zako ili mauzo yasishuke, kuwa mbunifu ktk wateja wako kwani itakusaidia kugundua wateja wako wanataka nini – kuwa karibu nao, wasikilize, waheshimu nk.
Kuwa milionea kunaanzia kichwani mwako-ukiweka mawazo yako kichwani utakuwa milionea kweli utakuwa sio kusema tu mdomoni. Amini utakuwa milionea na utakuwa kweli
PIGA KAZI
Maneno ya walioshindwa yasikukwamishe safari yako ya kuwa milionea
Ondoa neno haiwezekani wewe kuwa milionea – kila binadamu anaweza kuwa milionea
Mshukuru Mungu kwa hicho alichokupa – kumbuka neema ya Mungu ndio imekufikisha hapo ulipo hivyo toa msaada kwa watu wasiojiweza, yatima, masikini, wajane, wagonjwa, toa sadaka, walemavu nk
HITIMISHO;
Shujaa mwenzangu, kuwa milionea inawezekana kama mimi na wewe tukifuata njia hizi 39 zinazotumiwa na mamilionea wengi duniani..
Ila kuthubutu ndo hatua ya kwanza.
Mchanganyiko wa chumvi na mafuta ya zeituni (olive oil) ni dawa nyingine inayotibu chunusi. Mafuta ya zeituni yandhibiti bakteria na huondoa sumu vitu ambavyo vinafanya kuwa dawa nzuri kutibu chunusi na matokeo ya chunusi.
Mapenzi ni upepo,mimi sivumi na kupotea,mapenzi ni mahaba
sili nikamaliza,nikimaliza nitakula nini kesho?nakuahidi
kukupenda leo hata kesho ukiwepo na hata usipokuwepo.
Upungufu wa damu ni tatizo linalosababishwa na kupoteza damu nyingi, kupungua kwa uzalishaji wa chembe hai za da damu na uharibifu wa chembe za damu kutokana na matatizo na magonjwa mbali mbali seli mundu, ujauzito, hedhi nzito, kurithi, magonjwa sugu na Lishe duni yenye ukosefu wa madini ya folic, chuma na vitamini B12.
Dalili zifuatazo zinakuwezesha kutambua kama una tatizo la upungufu wa damu hivyo kukusaidia kuwahi hospitali au kubadili mfumo wa chakula ili kuepuka madhara makubwa ya baadae.
ยท Kushindwa kupumua vizuri
ยท Vidonda kwenye ulimi au mdomoni
ยท Sehemu nyeupe ya jicho kuwa bluu
ยท Ngozi kuwa na rangi ya kijivu
ยท Kucha kuwa dhaifu
ยท Kusikia hasira na kuhamasika haraka
ยท Kuchoka sana kuliko kawaida
ยท Maumivu makali ya kichwa
ยท Kupungua kwa uwezo wa kufikiria
ยท Kusikia kichwa chepesi pale unaposimama
ยท Miguu na mikono kuwa ya baridi sana
ยท Uchovu wa mara kwa mara
Upungufu wa damu hutibiwa mapema kwa kubadili lishe pamoja na kuongeza lishe yenye vitamini C na B12 pamoja na madini ya Chuma kutokana na visababishi vya tatizo. Mara nyingine vidonge na sindano zenye lishe hizi huweza kutumika hosipitali na matibabu ya tatizo linalosababisha na iwapo mgonjwa yuko katika hali mahututi huweza kuongezewa damu.
Jifunze kujikagua, jifunze kujiuliza je hapa ndipo napotakiwa kuwa? Usifurahie tu kwamba upo hapo kwa muda mrefu yamkini unaona panakufaa and you are settled lakini ukweli ni kwamba sio pako na haukutengenezwa kuwa hapo. Hata kama tai ataonekana kwenye banda la kuku lakini ukweli ni kwamba tai kaumbiwa kuwa angani tofauti na kuku aishie bandani. Jiulize hapo ulipo ni pako??
Na ndio maana kwenye maisha, mafanikio ya leo ni matokeo ya tulichojifunza kutoka kwa waliopita, baada ya wao kukosea mahali nasi tukaboresha, na kwa hakika vizazi vijavyo navyo vitaendelea kurekebisha pale tunapokosea sisi na hii yote ndiyo huleta ladha ya maisha. Ukipitia Changamoto mwenyewe na ukapambana kujikwamua mwenyewe, utapata somo litakalokufunza zaidi kuliko kusimuliwa changamoto walizopiti wengine.
Maisha ni Maamuzi, aliyekula Sahani mbili za wali mchana ili usiku asile tena, anaweza kuwa sawa na aliyeamua kutokula Mchana ili usiku ale sahani mbili za wali, japo hawa hawawezi kuwa sawa sawia na aliyeamua kula sahani moja ya wali mchana na moja ya wali usiku, Ijapokua mwisho wa siku wote wamekula sahani Mbili za wali kwa siku. Jumapili Njema kwenu nyote.
JIKUNG’UTEโฆ.JIPANGEโฆ..ANZAโฆโฆ
“Mimi sitaki kuwa kila kitu kwa kila mtu, lakini napenda
kuwa kitu kwa mtu.na mtu mwenyewe ni wewe”
nakupenda laazizi
“Kama mimi nilikuwa na maua kila wakati
mawazo yangu
yangekuwa juu yako,nisingefikiri wa kumpa mwingine kabla
yako je wewe ungekuwepo nayo
ungempa nani kwanza? “
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikilia au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiliwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.
Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).
Tatizo la ngiri huweza kumpata mtu yeyote. Miongoni mwa vitu vinavyoweza kumsababisha mtu apate ugonjwa wa ngiri ni: Kuwa na uzito mkubwa wa mwili au kuongezeka uzito kwa ghafla, kazi ya kubeba au kunyanyua vitu vizito, tatizo la kukohoa au kupiga chafya kwa muda mrefu, ujauzito au matatizo yanayojitokeza kwa mwanamke wakati wa kujifungua pia kuharisha au kuvimbiwa (Constipation). Vitu hivyo pamoja na mtu kuwa na misuli au tishu zilizopoteza uimara au uwazi (opening or hole) humfanya mtu apate ngiri (hernia).
Ngiri hutambuliwa kwa kutokea kitu kama uvimbe au kujaa katika eneo husika (baadhi ya maeneo yametajwa hapo juu) na pia kwa kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara na daktari huwezesha kugundua tatizo hili.
Njia inayoweza kutatua tatizo hili ni kwa mtu mwenye ngiri kufanyiwa upasuaji ili kurekebisha misuli au tishu zilizolegea. Pia kutegemeana na kihatarishi cha tatizo hili, mtu unaweza kuwa unafanya mazoezi ili kupunguza uzito wako na kuweka utaratibu mzuri wa kula chakula kinachojumuisha mboga mboga au matunda yenye nyuzi nyuzi (fibers), hii itasaidia pia mmengโenyo (digestion) wa chakula tumboni na kuepusha kuvimbiwa. Matunda (Vitamin C) husaidia kuunganisha tishu zilizolegea na pia husaidia kupona haraka kwa sehemu iliyofanyiwa upasuaji (operesheni). Na kama tatizo lako ni la kukohoa kwa muda mrefu kunakosababishwa na uvutaji wa sigara, ni vyema ukasitisha uvutaji ili kupunguza madhara au makali ya ngiri lakini pia kusitisha sigara kwa ajili ya usalama wa afya yako.
Recent Comments