Huyu Jamaa ubahili umezidi kwa hiki anachomwambia huyu dada
Kama ni ubahili hapa umezidi
mdadaย Bby naomba hela nimpeleke mdogo wangu hospital kang’atwa na nyoka
JAmaaย embu mpe huyo nyoka cm niongee nae.. maisha yanakaba..๐๐
Kama ni ubahili hapa umezidi
mdadaย Bby naomba hela nimpeleke mdogo wangu hospital kang’atwa na nyoka
JAmaaย embu mpe huyo nyoka cm niongee nae.. maisha yanakaba..๐๐
Ni matumaini nyote mnaendelea vyema, nami alhamdulillah ala kul Hali naendelea vyema
Leo naona ni bora tukazungumzia tatizo la kutokwa na harufu mbaya ukeni maana watu wengi hudhani kuwa na harufu mbaya itokayo ukeni ni matokeo ya uchafu tu.
Ndio maana wanaume huwachamba wake zao kuwa hawajuhi kujisafisha na kufanya wanawake kuongeza jitihada katika kujisafisha ukeni, leo napenda kuzungumzia tatizo hili linalowasumbua wanawake wengi na kuwaumiza kichwa kutokana na kwamba lina athari kubwa sana kwani hufanya ndoa zao kudumaa NK,
~ Kitaalamu Hali ya mwanamke kutokwa na maji yenye rangi nyeupe au njano ni Hali ya kawaida na sio tatizo Lakini endapo maji yanatoka yapo katika Hali ya ute mzito wenye rangi nyeupe au kahawia na yanatoa harufu kali au kuwasha hapo una tatizo
~ Majimaji au ute unaoteleza kutoka sehemu za siri ni njia inayowezesha viungo vya uzazi vya mwanamke kujisafisha au kutoa uchafu wa seli zilizokufa na mabaki ya damu ya hedhi nnje ya mwili pia huvikinga viungo vya uzazi dhidi ya maaambukizi ya bacteria
~ Kwa kawaida huwa hayatoi harufu na huwa hayawashi na huwa na rangi nyeupe au njano pia huwa na asidi ya LACTIN ambayo huzuia bacteria kuzaliana
~ Mwanamke hutoa kiasi cha grams 2 za seli zilizokufa kutoka kwenye mji wa kizazi na grams 3 za ute mwepesi kila siku, kiwango hicho kinaweza kuongezeka au kupungua kutegemeana na mzunguko wa hedhi pia Kuna wakati ute huwa mwepesi na unaovutika na Kuna wakati pia huwa mzito wa rangi ya njano hautoi harufu
Sababu za kutokwa na uchafu ukeni una vyanzo vingi sana vifuatavyo ni vyanzo vya tatizo hili
Chanzo halisi cha ugonjwa huu hakijafanikiwa kuwa wazi,kinachotokea ni kuongezeka kwa ghafla kwa idadi ya ya bacteria hawa na kubadilisha uwiano wa kawaida katika mazingira ya uke, wanawake wenye wapenzi wengi na wanaofanya mapenzi kwa njia ya mdomo Wana hatari ya kupata tatizo hili
Maambukizi haya hutokana na Aina ya protozoa wa seli moja, trichomonas mara nyingi huambukizwa kwa njia ya ngono, protozoa huyo huweza kukaa kwenye unyevu unyevu kwa Muda wa saa 24 Bila kufa hivyo kufanya taulo na chupi zisizokauka kuwa chanzo kingine cha tatizo hili
Kwa kawaida Kuna kiwango kidogo cha yeast (candida albicans) katika uke, huwa tunasema Kuna maambukizi pale kiwango kinapozidi Hali ambayo inatokana na kubadilika kwa Hali ya hewa ukeni (Change in the PH balance of vagina)
Maambukizi ya yeast hayatokani na tendo la ndoa.
Mtu anapokua na kansa ya uke, hutokwa na maji ya harufu mbaya, hivyo ni heri uwe unafanya check up ili kujua Afya yako na kwakuwa cancer ya kizazi inapona hivyo ni vema ukatambua mapema uanze tiba
Kuna baadhi ya magonjwa kama vile KASWENDE NA KISONONO yanasababishwa na ngono na kuwa chanzo cha tatizo hili.
Tatizo la kutokwa na maji wakati mwingine husababishwa na muhusika kua mchafu yan mtu unaoga kwa siku mara moja, chupi moja ndio hiyo hiyo mwaka mzima, pads unakaa nayo saa 24, ukienda kukojoa ujitawadhi na maji masafi hivyo unategemea utakua salama kweli??? Zingatia usafi mrembo
Kutokwa na uchafu ukeni unaoambatana na kuwashwa au kutokewa na vipele, hii hutokana na kuharibika kwa uwiano wa bacteria hivyo kuwa na madhara na uchafu hutoka wa aina tofauti hapa chini nitaelezea kila Aina ya uchafu na dalili zake.
Huu uchafu huonyesha dalili ya kuwa mzunguko wako wa hedhi umevulugika na wakati mwingine ni dalili ya kansa ya kizazi, mwanamke anayepata tatizo hili hutoa damu nyingi kuumwa sana nyonga
Endapo uchafu huo utatoka kama povu na wenye rangi ya kijani au njano na ukiambatana na harufu mbaya huwa ni dalili ya ugonjwa wa trichomonas, maambukizi ya parasite yanatokana na ngono zembe, dalili Yake nyingine ni maumivu na kuwashwa wakati wa kutoa haja ndogo.
Mara nyingi hii huwa ni dalili ya maambukizi ya fangasi(YEAST INFECTION) na dalili nyingine huwa ni kuvimba sehemu ya nje ya siri, kuwashwa na kupata maumivu makali wakati wa tendo la ndoa.
Uchafu wa Aina hii ni dalili ya maambukizi ya bacteria vaginosis, mara nyingi mwenye tatizo hili husikia muwasho na maumivu sehem ya nnje ya uke.
Matibabu ya tatizo hili hufanyika baada ya kugundua chanzo cha tatizo na mara nyingi tiba Yake ni tiba ya dawa za antibiotics kitu ambacho si tiba nzuri zaidi kwasababu tatizo huweza kujirudia kila wakati na kusababisha matatizo zaidi hivyo tiba nzuri ni kuepuka hili tatizo kwa kufanya yafuatayo
๐EPUKA KUJIINGIZA VIDOLE MARA KWA MARA UKENI
๐EPUKA MATUMIZI YA DAWA ZA ANTIBIOTICS MARA KWA MARA
๐PUNGUZA KULA VYAKULA VYENYE SUKARI NYINGI
๐TUMIA PADS ZENYE ANIONS NI SALAMA KWA AFYA YAKO
๐SAFISHA VIZURI NGUO ZAKO ZA NDANI NA UZIANIKE JUANI NA HATA KUZIPIGA PASI
๐KUNYWA JUICE YA APPLE,STRAWBERRY, NANASI KWA WINGI
๐EPUKA KUFANYA NGONO ZEMBE
๐HAKIKISHA UNAJISAFISHA KILA UNAPOMALIZA KUJISAIDIA
๐EPUKA KUTUMIA DAWA ZA KUZUIA MIMBA
๐EPUKA KUTUMIA SABUNI AU VITU VYA MANUKATO UKENI,
Wanawake wengi mnapenda kutumia baadhi ya dawa kwa lengo la kuongeza vionjo kwenye mapenzi pia kufanya uke kunukia vizuri, au kukaza uke rafiki uke una harufu nzuri sana ambayo haipatkan kokote hivyo haihitaji kuwekwa pafyumu Wala kusafishwa kwa sabuni za kemikali kwani huwa panajisafisha hivyo ni heri ukaacha kutumia kwani madhara Yake hayaonekani sasa ila baada ya Muda huonekana.
Tattoo ni nini?
Hii ni uwekaji wa wino kwenye ngozi ya ndani kitaalamu kama dermis kubadilisha rangi kabisa maisha yako yote au kwa muda tu, inateemea na uwekaji..
Kwa dunia ya sasa kujichora tatoo ni kama fasheni fulani kwenye jamii, ukienda kuchora tattoo kuna uwezekano mkubwa sana isitoke maisha yako yote hivyo kwa usalama wako ni vizuri ukamuona mtaalamu wa tattoo ambaye ni maarufu na ana sifa kubwa katika shughuli hizo, anaweza kua ana gharama kubwa lakini binafsi itakusaidia.kwa sasa nchi ya marekani inaongoza kwa kua na watu wengi wenye tattoo duniani.
Hivyo kabla hujaamua kujichora tattoo basi madhara yake haya hapa..
Kansa ya ngozi;ย hapo mwanzoni wataalamu walikua wanasema hakuna mahusiano kati ya kansa ya ngozi na na tabia ya kujichora tattoo lakini hivi karibuni tafiti kutoka uingereza zinaonyesha kuna aina fulani za wino ambazo zinaweza kusababisha kansa zikitumika kuchora tattoo.
Allergy ya ngozi;ย haijalishi unaweka tattoo kwa muda au ya moja kwa moja kumetokea kesi nyingi za watu wanaopata allergy baada ya kupakwa tattoo, utafiti unaonyesha rangi nyekundu ndio inaongoza kwa kusababisha allergy hizo huku rangi zingine kama nyeusi, purple na zingine hazisababishi. mara nyingi allergy hizi huonekana mtu akikaa juani.
makovu;ย mwili unataambua tattoo kama adui wake hivyo hujaribu kuiondoa kwa njia mbalimbali na kwa kufanya hivyo husababisha makovu ya muda mrefu ambayo yanaweza kuleta magonjwa mengine ya ngozi.
Maambukizi ya ukimwi na ugonjwa wa hepatitis;ย tabia ya kurudia sindano zilezile wakati wa kuchora tattoo kunaweza kusababisha maambukizi ya virusi vya ukimwi na maambukizi ya virusi vinavyoshambulia ini kitaalamu kama hepatitis b. ugonjwa huu wa hepatitis b husababisha kansa ya ini ambayo haitibiki. ni vizuri kua makini ili uone kama sindano inayotumika kwako ni mpya.
Matatizo kipindi cha kufanya kipimo cha MRI;ย hichi kipimo ni cha mionzi na kirefu chake ni magnetic resonance imaging, hutumika kupima viungo vya mwili ambavyo havionekani kwa macho ndani ya mwili wa binadamu kama x ray inavyofanya. tatizo ni kwamba kipimo hiki kina sumaku kali kiasi kwamba mtu hatakiwi kuingia kwenye mtambo huo akiwa amevaa chuma chochote na hata kama kiko ndani ya mwili kitavutwa nje, sasa mara nyingi tattoo nyeusi hua imetengenezwa na compound kitaalamu kama iron oxide ambayo ina chembechembe za chuma. hii inaweza ikaleta changamoto kubwa kwenye vipimo.
Kubadilika kwa ngozi ya rangi;ย sehemu inayochorwa tattoo hubadilika moja kwa moja na kua na rangi tofauti, hakuna jinsi unaweza ukaitoa hiyo rangi tena, hata baada ya muda mrefu tattoo ikipungua nguvu lakini ngozi haiwezi kua kama zamani.
Hutaruhusiwa kuchangia damu;ย mara nyingi watu wenye tattoo hawaruhusiwi kuchangia damu kwani wana hatari ya kusambaza ugonjwa kwenda kwa mtu mwingine, kimsingi mtu aliyechora ndani ya muda mfupi ndio haruhusiwi lakini kwasababu wakati mwingine sio rahisi kutofautisha tattoo mpya na ya zamani basi hawa watu huwa hawaruhusiwi kabisa.mchezaji wa kimataifa christian ronaldo hachori tattoo kwa sababu ya hili.
Unaweza kukosa fursa mbalimbali;ย kuna kampuni mbalimbali duniani haziwapi watu kazi kwasababu wamechora tattoo kulingana na imani za kampuni husika lakini pia kazi yeyote ya jeshi duniani hairuhusu tattoo hivyo kama wewe unayesoma hapa umeshachora tattoo ujue kazi ya jeshi huna tena.
Tattoo huingiliana na matumizi ya dawa fulani;ย kama wewe unatumia dawa za kuzuia damu isingane mwilini ukichora tattoo inaweza kufanya utoke damu nyingi sana kwani dawa hizo huzuia uwezo wa mwili kukausha damu na kuponyesha vidonda.
Magonjwa ya ngozi;ย wakati mwingine bacteria huweza kuvamia sehemu zenye vidonda vya tattoo na kusababisha kutopona haraka, dalili huweza kua homa kali, maunivu makali na sehemu ya tattoo kuvimba.
Damu kuganda juu ya ngozi[haematoma];ย hii husababishwa na kuvuja kwa damu nyingi chini ya ngozi, huonekana sana pembeni pembeni ya sehemu ambapo rangi ya tatoo imepita na huchelewesha kupona kwa kidonda.
Siku hizi kuna tattoo zinachorwa juu ya ngozi kama hina na kuondoka baada ya muda fulani, hizi hazina madhara kabisa, huchorwa kwa bei ndogo na hukupa nafasi ya wewe kubadilisha tatoo za aina mbalimbali kwenye sehemu moja ya mwili.
Ni ngumu sana kuifuta tattoo na hii ni changamoto kwa watu ambao wamechora tattoo za majina au sura za wapenzi wao wa zamani. kuna kikaa kinaitwa laser ambacho kinaweza kutumika kufuta tattoo yote au sehemu ndogo tu ya tattoo. mara nyingi rangi nyeusi zinaweza kutoka ukilinganisha na rangi zingine. maumivu yanayotumiaka kuiondoa tattoo ni makali kuliko maumivu ya kuiweka na hapa kwetu tanzania siana uhakika kama huduma hii ya kuondoa tattoo ipo.
Ulisha wahi kukaa ukajiuliza mbona kuna baadhi ya watu wana ngozi nzuri laini na soft? lakini kwako ni tofauti?
Ukawaza labda wanatumia vitu vya bei ghali ambavyo wewe huwezi ku โ afford, au umesha hangaika na ma โ cosmetics lakini bado ngozi yako haikubali kukaa vizuri?
Jaribu hii Home made Yogurt Cleansing, Tumia mtindi ambao hauna mafuta mengi au hauna kabisa (low fat),
Paka mtindi wako usoni fanya kama una sugua kwa muda mchache halafu uache kwa dakika 15, fanya hivi mara mbili kila siku na utapata matokeo kwa muda mchache.
Hii husaidia kuondoa cell za ngozi zilizo kufa (dead skin cells) na protein tighten the pore.
Mbolea ya kunyunyiza ni nzuri kwani inasaidia kuupa mmea virutubisho moja kwa moja kupitia kwenye majani au shina ambapo ndipo chakula kinahitajika.
Faida za mbolea ya maji ni pamoja na kuongezeka kwa kiwango cha mavuno, uwezo wa mimea kukabiliana na wadudu pamoja na magonjwa, kuvumilia ukame, na kuongeza ubora wa mazao.
Mbolea ya maji hutengenezwa kwa kuchukua kiroba kilichojazwa samadi, aina mbalimbali ya mimea yenye virutubisho na inayoaminika kuwa dawa ya mimea. Kiroba hicho kinafungwa kwenye kijiti, na kutumbukiza kwa kuningโinia kwenye pipa lililojazwa maji.
Kiroba hicho ni lazima kichukue kati ya kilo 30-50 za samadi pamoja na aina nyingine za mimea kwa maji lita 200 (tazama mchoro). Unaweza kushika upande mmoja wa mti na kunyanyua na kushusha kila baada ya siku tano ili kuchanganya na kuharakisha kutolewa kwa virutubisho zaidi.
Kwa kawaida mchanganyiko huo unakuwa na harufu kali sana maana Nitrojeni nyingi inayopatikana hugeuka kuwa Amonia. Ni vizuri kufunika pipa ili kuzuia kuyeyuka kwa nitrojeni. Harufu ikishaisha, ujue mbolea yako ipo tayari kwa matumizi.
Ongeza maji na utingishe vizuri kabla ya kutumia. Nyunyizia mimea yako kila wiki mpaka utakapoona mabadiliko.
Mbolea hii hutengezwa kwa kuchukua majani mabichi na kuyakatakata na kisha kuyachanganya na maji kidogo.
Baada ya kuchanganya na maji unaacha kwa siku tatu au nne ambapo utatikisa mchanganyiko wako kila siku.
Baadae utatikisa na kuchanganya na maji na kunyunyiza shambani.
Vilevile Unaweza kutumia mbolea ya majani ambayo itakuwa kama dawa ya kuulia wadudu, kwa kutumia aina ya mimea kama vile mivule, mibangi mwitu, majani ya minyanya, mwarobaini, mashona nguo, pamoja na vitunguu saumu. Aina hii ya mimea inasaidia sana katika kuzuia magonjwa, wadudu na kutoa virutubisho muhimu kwa mimea vinavyosaidia mkulima kupata mazao bora bila gharama ya ziada ya kununua virutubisho.
Ili upate matokeo mazuri wakati wa kunyunyiza mbolea ya maji unatakiwa kufuata vigezo vifuatavyo:
โข Inashauriwa kutumia mbolea iliyochanganywa vizuri ili kuepukana na kuunguza mimea.
โข Acha maji utakayotumia kuchanganyia mbolea yako nje katika pipa lililowazi usiku kucha, hii inasaidia kutoa madini hatarishi, na kufanya mchanganyiko wenye faida kwa mimea.
โข Unatakiwa kutingisha vizuri mbolea yako ya maji kabla ya kunyunyiza. Chembechembe ndogo ambazo hazikuyeyuka zinaweza kuziba mdomo wa bomba la kunyunyizia.
โข Matokeo mazuri yanaweza kupatikana endapo mbolea imechanganywa vizuri na kunyunyiziwa wakati hakuna upepo.
โข Unatakiwa kunyunyizia mbolea wakati wa asubuhi au jioni wakati hakuna joto na upepo ukiwa umepungua.
Angalizo
Kabla ya kunyunyiza dawa au mbolea uliyoitengeneza mwenyewe shambani nyunyiza kwenye eneo dogo au mimea michache kwanza ili uone kama inaunguza au haiunguzi. Kumbuka kuwa mchanganyiko mwingine ukiwa cream au ukikolea sana unaweza kuchoma. Kwa hiyo kuepuka hili nyunyiza mahali padogo kwanza.
Njia za kuamsha hamu ya kufanya mpenzi ya mwanamke au Hatua za kufuata kuamsha hisia za mwanamke ni kama ifuatavyo
Andaa mazingira ya kuamsha hisia zake, fanya kitu kitakachowasogeza karibu na kuamsha hisia zake Kwenye akili yake kabla ya kugusa mwili. Mfano, weka mziki au muvi nzuri n.k. Kisha tengeneza mazingira ya kuwa karibu kimwili na kugusana.
Unapokuwa na mwanamke ambaye umemzimia, tafuta kisababu cha kukaa na yeye karibu. Toa simu muangalie pamoja videos kama vile za kuchekesha, ama unaweza kuchukua kitabu/gazeti umuonyeshe habari ambazo anapenda ilimradi tuu muwe karibu.
Usijaribu kutumia lugha ya kutongoza ama utamfanya aanze kukushuku. Tayari anajua kuwa miguso ya mikono yako ya mara kwa mara inaashiria kitu fulani. Kile unachotakiwa kufanya ni kuivuruga akili yake kwa kuleta mada ambayo itamvutia huku ukiendelea gusa mwili wake
Wakati mtakuwa mnaendelea unaweza kutumia maneno ya kumsuka lakini yawe ya kichini chini. Mfano unaweza kumwambia “Unanukia utamu”, “nimependa kitambaa cha nguo yako”,”nishawahi kukuambia kuwa macho yako yanapendeza? Nimependa vile yanang’aa nikiwa karibu yako.” Maneno kama haya unaweza kumrushia mwanamke huyu bila hata yeye kusongea mbali na wewe. Mwanzo atakuwa anapenda kuyaskia.
Ukianza kumuona anazungumza polepole na kukusongelea karibu yako, ishara kuu ni kuwa yupo tayari. Kwa hiyo kufikia hapa unaweza kurudia hatua za kumsuka, kumgusa na kujaribu kufikia viungo vyake vingine vya mwili ilimradi nyote wawili mnafurahia.
Baada ya kuandaa mudi au mazingira na kuamsha hisia zake sasa tafuta namna ya kumbusu. Mbusu taratibu kwa namna ambayo haitamshtua na kumfanya aogope au akatae.
Wakati wa kumbusu mshike mwili wake ili kuamsha hisia zake. Anza na mikono kasha rudi kichwani Kwenye nywele zake na kisha maliza sehemu nyingine za kuamsha hisia zake
Kama hataki usimlazimishe bali mbembeleze au muache mpaka wakati mwingine atakapokuwa tayari.
Kitabu hiki kina topiki Zifuatazo;
1. Mambo anayohitaji mwanamke kutoka kwa Mwanaume
2. Mambo yanayowavutia wanawake kutoka kwa wanaume
3. Mambo wanayoyapenda wanawake wakati wa kufanya mapenzi
4. Dalili za mwanamke kicheche
5. Maswali ya kujiuliza kama mwanamke anakupenda kwa dhati au anakudanganya
6. Tabia za mwanamke anayekupenda lakini hawezi kusema
7. Ishara za mwanamke aliyevutiwa na wewe
8. Dalili za mwanamke anayeelekea kukukubali
9. Mambo ambayo mwanamke hawezi kukwambia
10. Njia za kudumisha na kuamsha mapenzi na mwanamke
Kitabu hiki ni Soft copy [pdf] kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.
Wakati wa ujauzito ni kipindi cha kubadili mambo mengi katika mfumo wa maisha wa mjamzito. Mjamzito anapaswa kubadili mambo mbalimbali ili kuhakikisha anakua na afya nzuri katika kipindi chote cha ujauzito na ili kuhakikisha kwamba atajifungua mtoto mwenye afya nzuri. Moja ya mambo makubwa ni pamoja na tabia ya kuvaa viatu vyenye visigino virefu. Mjamzito hashauriwi kuvaa viatu vyenye visigino virefu kutokana na athari zinazoweza kutokana na aina hizi za viatu.
Mjamzito akivaa viatu vyenye visigino virefu anakua katika hatari kubwa ya kuanguka. Hii huweza kusababisha majeraha makubwa kwa mtoto aliyeko tumboni hali inayoweza kusababisha mimba kutoka.
Wadada hupenda kuvaa โhigh heelsโ husababisha misuli ya mapaja kukaza na kuwa na muonekano mzuri. Katika ujauzito, mabadiliko ya homoni huweza kupelekea misuli hii kuwa na maumivu tofauti na ilivyokua kabla ya ujauzito.
Ni wazi kuwa uzito huongezeka wakati wa ujauzito na mabadiliko ya vichocheo vya mwili huweza kupelekea kizunguzungu cha hapa na pale. Hii huongeza hatari ya kuanguka iwapo utavaa โhigh heelsโ na kupelekea majeraha kwako na kwa mtoto aliyeko tumboni.
Uvimbe miguuni.
Ni jambo la kawaida miguu kuvimba wakati wa ujauzito. Kuvaa viatu vyenye visigino virefu na vyenye kubana huweza kuongeza tatizo hilo na kupelekea maumivu.
Wakati wa ujauzito, uzito mkubwa huhamia mbele na misuli ya nyonga hulegea. Mabadiliko haya ya kimsawazo huweza kusababisha maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo na kiuno.
Iwapo kuna ulazima sana wa kuvaa viatu hivyo, unapaswa kuzingatia yafuatayo:
Jamaa alichukua paka wake na kwenda kumtupa
mbal,aliporudi nyumban alimkuta paka
amekwisharudi,jamaa alikasirika sana.
Siku ya 2
akamchukua na kwenda naye zaid ya kilometa 50
akapiga chochoro za kutosha kisha
akamtupa,akaanza safar ya kurud nyumban
baada ya muda akampigia cm mkewe.Vp mke
wangu huyo paka yupo? MKE:Ndio mume wangu
tena ametulia hapa kwan imekuaje? JAMAA:hebu
mpe cm anielekeze njia ya kurud nimepotea๐ณ
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Kifua kikuu ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vya bacteria na kuenezwa kwa njia ya hewa. Mtu mwenye maambukizi ya kifua kifua kikuu akikohoa, kupiga chafya au kutema mate ovyo husambaza vijidudu hewa, huweza kumwabukiza mtu mwingine kama atakuwa hajaanza kutumia dozi ya kifua kikuu.
Ugonjwa huu unakingwa kwa chanjo ya kifua kikuu kwa kitaalamu (BCG) ambayo hutolewa mara tu mtoto anapozaliwa.
Chanjo ya kifua kikuu hutolewa baada ya mtoto kuzaliwa au anapofika kliniki kwa mara ya kwanza
Iwapo kovu kwa mtoto halijajitokeza chanjo irudiwe katika kipindi cha miezi 3.
Ugonjwa wa kifua kikuu unatibika. Matibabu yake huchukua muda mrefu wa miezi 6 hadi 8 na ni ya gharama kubwa.
Inashauriwa mgonjwa awahi matibabu mapema kwenye vituo vya kutolewa huduma za kinga.
Ugonjwa wa kifua kikuu ni hatari, hata hivyo unakingwa kwa chanjo.
Mzazi au mlezi hakikisha kila mtoto anapozaliwa anapata chanjo ya kuzuia kifua kuu
โKumbuka chanjo ya kifua kikuu (BCG) Itamkinga mtoto dhidi ya ugonjwa wa kifua kikuuโ.
pendo ni silaha kali zaidi duniani hu uwa wasio na hatia
na hujeruhi bila kutarajia,wengine hujitolea muhanga nayo
,silaha hiyo itumikapo vizuri huleta marafiki na kuongeza
furaha,je we unaitumiaje silaha hiyo?
Mapenzi ni magumu na yatabaki kuwa hivyo, lakini kumbuka
kuna akupendaye naye ni MIMI!.
Ni ngumu kwa watu wawili kupendana wanapoishi Dunia
tofauti, lakini Dunia hizo zikutanapo na kuwa kitu kimoja,
hiyo ndiyo maana ya kuitwa wewe na mimi.
Ningependa nikuambie neno ambalo halina gharama na likutumiwa vibaya halina maana wala thamani.
Neno hilo haliandikiki kwenye karatasi wala hata halitamkiki ila tu Linatokea Bila kujua na halina sababu.
Neno hilo mi mwenyewe silijui ila ndo linatufanya tuwe pamoja Japo tupo Kasi Na Kusi.
Nakupenda sana Dear
MASSAWE alienda na marafiki zake bar kunywa, baada ya kumaliza kutumia akaletewa bili kama ifuatavyo:
Manka 35,000
Marieta 20,000
Kekuu 30,000
Kitime 15,000
Kinabo 10,000
TOTAL 110,000/=
MASSAWE akaicheki akasema “Wote nitawalipia lakini huyo “TOTAL” Yesuu simlipii.
Kwansa anamiliki sheli kibao sa mafuta hapa bongo. Shensi taip ! Na amekunywa nyingi kuliko wote alipe mwenyeweโฆ
Lazima utakuwa mwizi sababu umeiba moyo wangu, umechoka
sababu unakimbia mara zote akilini mwangu, na labda mimi
sina shabaha sababu mara zote nikikulenga nakukosa.
Wachambuzi wa mambo ya saikolojia wanasema kwamba kwa kuchukua tai na kulivaa ile rangi ndiyo itakayoweza kupeleka ujumbe wa wewe unataka nini au unataka watu wakutambue kwa namna gani.
Wakati Joshua Blue, Makamu mkuu wa shule ya Kennedy mjini Hong Kong, anapoendesha baraza la wanafunzi anavaa tai lenye rangi ya light violet ili kumpa mamlaka.
Tai la rangi ya bluish-purple anasema ni โcolourful yet mutedโ, anaamini kwamba rangi ya bluu inawafanya wanafunzi wasiboreke wakatiw anasikiliza, anajizuia kutumia brighter purples na pinks wakati akiwa mbele ya wanafunzi.
โHuhitaji kuwa na rangi nyingi zinazongโaa kwani watoto watajivuruga,โ anasema Blue mwenye umri wa miaka 35.
Hakika inaweza kuwa kama kichekesho lakini wataalamu wanasema kwamba uchaguzi wa rangi ya tai inasaidia sana kupeleka ujumbe unaotakiwa kwa wahusika. Na hii haijalishi ni mteja, mdau wafanyakazi au watoto.
โRangi hutoa aina Fulani ya ishara,โ anasema David Zyla, Mwandishi mwenye makao makuu yake New York anayeandika Color Your Style.
โSuti ile ile inaweza kubadilishwa kimtindo yaani salamu zake kwa kubadili rangi ya tai, na kila mvao ukawa na ishara na salamu tofauti.โ
Baada ya kusoma maelezo yote hayo, nikuulize je sasa unaweza kufikiria unataka kuvaa tai gani katika mkutano wako ujao.Labda nikusaidie kwa namna hii.:
Si bahati mbaya au kitendo cha kubahatisha kwa wanasiasa wengi kuvaa tai lenye rangi nyekundi ndani ya suti zilizo dark na mashati mepesi.
โTai nyekundu inaonesha mamlaka,โ anasema Mark Woodman, mchambuzi wa mambo ambaye amejifunza masuala ya huko Laurel, Maryland, Marekani. โKuna kitu Fulani kipo ndani ya rangi nyekundu ambacho mara zote kinajitokeza kumuimarisha mtu na kumpa mvuto wa pekee.โ
Ofisa Mtendaji wa JPMorgan, Jamie Dimon huvaa tai nyekundu anapozungumza na wananchi
Hata hivyo wataalamu wanasema kwamba kuna rangi nyekundu na rangi nyekundu.Nyekundu iliyokoza kwa miondoko ambayo wazungu wanasema ni burgundy, husaidia kuleta imani na matumaini wakati ile nyekundu nyepesi na pink inakuwa zaidi onesho la ubunifu na namna ulivyo kistaili.Katika miaka michache iliyopita rangi ya pink inaweza kuonesha mshikamano na wamama anasema Woodman.
Wakati unaendesha mradi au unataka kupeleka ujumbe Fulani kwa kruu yako fikiria kuvaa tai la rangi nyekundu iliyokoza ambayo inashaini.Tai la rangi nyekundi unaweza kuwa njia bora ya kuonesha mamlaka.
Ross Znavor, Mtendaji katika moja ya taasisi za kifedha mjini New York yeye huvaa tai la rangi ya purple na si nyekundu katika mikutano ya kibiashara,Rangi hii huonesha kujiamini na humsaidia watu kuendelea kumkumbuka.
Anasema kuvaa tai hilo kunampatia mtu mwingine kukubali kwamba wewe unaweza kushirikiana naye na kujenga uhusiano wa kudumu.
Lindsay anasema purple, kiasili ni rangi ya utiifu na utajiri na kwa sasa inaaanza kukubalika maeneo ya kazi.
Arnold Schwarzenegger huonesha kujiamini kwa kuvaa tai rangi ya purple.
โWanaume wanaovaa mashati ya lighter purple na tai za darker purple, hutaka kutambulika haraka katika kundi bila kuleta ushawishi mwingine wa kipuuzi unaovurugaโ.
Inawezekana huvai kila siku au kila mahali lakini ukivaa tai nyeusi katika mikutano ya watendaji, kwenye dhifa unakupa wewe hali ya muondoko mweroro wenye utanashati mkubwa , anasema Zyla.
Muigizaji sinema Leonardo DiCaprio huvaa tai nyeusi katika mikutano au maeneo ambayo ni ya kikazi zaidi.
Lakini ni kweli kuwa rangi nyeusi inakufanya kuwa na ujeuri wa aina Fulani na wengine wanasema kusema kwamba inakuwa overdressed katika mazingira mengi. โRangi hii inafaa kutotumika kama wewe unataka kuendelea kupanda ngazi, wapandisha ngazi wanaweza kufikiria kwamba wewe ni jeuri wa aina Fulani hivi,โ anasema Zyla.
Ni vyema sana kama mtu atakuwa amejipatia grey shades, anaongeza Woodman. Tai la rangi ya grey linaweza kukupa mwonekano wenye mvuto mweroro usio na jeuri na usiojinata anasema Woodman.
โGrey iko poa, iliyotulia na ya kisasa zaidi,โ anasema.Ili kuifanya iwe imetulia zaidi piga tai hili na shati ambalo ni lighter, pastel-coluored. Tafadhali angalia lighter grey shades na malizia na shaini ili kukupa muonekano ambao ni polished.
Rangi ya kijani ina maana nyingi kuanzia kuzaliwa upya hadi rangi ya fedha kwa mataifa Fulani.Lakini cha ajabu ni rangi yenye โkeleleโ nyingi katika maeneo ya kazi.
Wakati mwingine kijani inakuwa too much.
โJe unataka kukumbukwa akwa ajili ya tai au kama wewe binafsi?,โ anauliza Woodman .Anasema kuchagua rangi ya kijani inayostahili ni kazi kubwa.Kijani inayowaka inavuruga kutokana na mwako wake na pia inakuwa na taabu sana kupata suti inayoambatana nayo au hata shati. Hata hivyo tai la light green likiwa na subtle print linaweza kuwa jema katika shati ambalo rangi yake ni neutral.
Tai ya rangi ya njano, ni tai la kiasili kwa nchi nyingi hata waingereza wanaliheshimu kwa sababu linakupa uhakika, kukuweka mngโavu na mwenye siha hasa ya kufaa.
Ni rangi inayoonesha jua, hivyo watu wengi wanaweza kuwa na kishawishi cha kuzungumza nawe kwa sababu ya ukweli kuwa ni rangi yenye mvuto wa kipekee. Kwa wengi kuvaa tai la rangi ya njano kunaonesha kwamba maisha yeye anayaangalia katika dunia chanya zaidi, anasema Eve Roth Lindsay, mshauri wa masuala ya muonekano wa Hong Kong.
Lakini kiukweli kuwa unapaswa kuwa mwangalifu usije ukafanya kosa la uasili na utamaduni wa eneo lenu inapokuja suala la rangi.
Mathalani rangi ya njano nchini india ina maananisha kwamba wewe ni mfanyabiashara wakati rangi nyeupe nchini China inamaana upo katika kipindi cha maombolezo.
Unahofu ya kupeleka ujumbe ambao uhuhitaji kwa kutumia tai uliyovaa yaani rangi yake?basi ni vyema ukafikiria kutumia tai ya rangi ya bluu.
Rangi hii hutumika katika matukio yote.
Rangi ya bluu ni rangi bomba kwa kuwa inawakumbusha watu anga na bahari, vitu vyenye kutuliza maisha ya binadamu anasema Lindsay.
โRangi ya bluu hakika ni salama zaidi kuivaa,โ anasema.
Tai ya Patterned blue hutoa hali ya kutulia na kitaalamu zaidi na inaweza kutumiwa katika mikutano ya kimataifa ya kibiashara na mazingira bila kupeleka ujumbe usiotakiwa.
Tai ya subtle blue inaweza kuwa na mvuto na kujionesha undani wakati cobalt au royal blue hukufanya ujiachie ndani ya kundi kwa namna Fulani. โBluu iliyokoza ni rangi ya marubani watukuka. Bluu bahari ni rangi inayoaminika, inayokupa imani na kiburi cha uwezo,โ anasema Lindsay .
โKabati lako likiwa na rangi rafiki za asili kama tan, kahawia, earthy colours, salmon na njano hufaa sana kwa watu wanaojishughulisha na wengine kama wafanyabiashara (mauzo), walimu na watu wa huduma mbalimbali,โ anasema Lindsay.
Hakikisha kwamba tai la rangi ya kahawia haiku pekee kwani inaweza kuonesha ugoigoi katika wajihi. Hata hivyo tai la beige linaweza kukuonesha kwamba huna matatizo, yuko huru.
Epuka kuvaa tai la rangi ya udongo na shati linalofanana nalo. Na kama unataka kujishebedua na kuonekana kweli katika eneo la kazi rangi hizi za asili achana nazo kabisa.
Msanii mmoja anaitwa ”KINYA” alikuwa ana perfom jukwaan..!!!
Kawaida kila msanii lazima ajitambulishe, mfano:-
”YEAH NI TEMBA hapa au
YEAH NI CHEGE hapaโฆ!!!
Yeye akasema: “YEAH NIKINYA HAPAโฆ!!!”
Watu wakapiga kelele ”UTAZOAAA” mwenyewe bwenge wee
JE, WEWE UNGEJITAMBULISHAJE NAITAJI JIBU LAKO TUONEโฅ
Matumizi ya maji ya kunywa ni moja ya dawa rahisi kabisa ya shinikizo la chini la damu.
Hii ni kwa sababu Maji ni mhimu kwa kila ogani ndani ya mwili iweze kufanya kazi zake sawa.
Kwa hiyo sababu kuu ya mtu kuwa na shinikizo la chini au hata la juu ni matokeo ya mishipa ya damu kutokuwa na vimiminika vya kutosha.
Mishipa ya damu imeundwa kwa maji maji ya damu (serum) na seli za damu.
Maji yanapopungua kwenye mwili hata vipenyo vya mishipa yako navyo hupungua ukubwa wake jambo linaloleta kushuka kwa shinikizo la damu.
Matatizo yote haya ni matokeo ya kutokunywa maji ya kutosha kila siku.
Kwa sababu hii, ili kupandisha juu shinikizo la damu unahitaji kunywa zaidi maji sambamba na juisi nyingine za matunda au za mboga mboga kila siku.
Hii inasaidia kuongeza vimiminika katika mishipa ya damu.
Mzee kaingia pharmacy,
MZEE: Mambo mwanangu, kuna kitu naomba uonje nitakulipa
MFAMASIA: Kitu gani?โฆ.Mzee akatoa kichupa na kijiko akaweka โฆmajimaji yaliyomo kwenye
kichupa kwenye kijiko na kumwambia mfamasia aonje, mfamasia akatia yale maji mdomoni na kuyazungusha zungusha mdomoni akionja;
MZEE: Nipe jibu, ina utamu wa sukari au chumvi au pilipili?
MFAMASIA: Kama chumvichumvi
MZEE: Hakuna sukari
MFAMASIA: Sukari hakuna kabisa
MZEE: Loh asante chukua hii alfu tano nashukuru sana, dokta alinambia nipime mkojo wangu kama nina kisukari, kumbe sina asante bwana mdogo
Recent Comments