SMS, Vichekesho, Mahusiano, Biashara na Ujasiriamali, Afya, Chemsha Bongo, Dini pamoja na Vitabu kwenye PDF

Karibu AckySHINE

πŸ€£πŸ˜ƒπŸ˜‚

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Angalia kilichotokea baada ya dogo kupewa ada na kuitumia kubeti

Dogo kampigia simu baba yake;
DOGO: Baba katika zile shilingi laki mbili ulizonipa
nikalipe ada nimetumia shilingi alfu 30 kubeti
BABA : Unasema nini we mpumbavu mshenzi
mkubwa? Nimekukanya mara ngapi kuhusu kubeti?
DOGO : Lakini baba
BABA : Lakini baba nini ngoja urudi utaona
ntakachofanya.
DOGO : Nilitaka kukwambia kuwa nimeshinda
shilingi milioni 3
BABA : Ndio hayo ninayosema wewe mpumbavu
sana kwanini hukutumia laki nzima kubeti? Si
ungepata pesa nyingi zaidi? Ngoja urudi niwataarifu
ndugu zako kuhusu uulivyo na akili za kuamua
haraka mwanangu mpenzi…

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Namna wazazi wanavyoongea na mabinti katika umri tofauti

Miaka 13: Usipende wavulana ni wabaya.
Miaka 18: Sitaki nikuone na yule mvulana tena!
Miaka 23: Lini utatuletea mchumba wako?
Miaka 26: Wenzio wanaolewa.
Miaka 30: Tumekuambia kwamba acha
kuchagua sana wanaume, hutaki kusikia!
Miaka 33: Kuna mtu wa Mungu yupo kule
anaombea unaweza kupata mchumba
Miaka 36: At least pata mtoto mmoja.
Miaka 39: We will take care of all the wedding
bills…yeyote ni sawa sisi tutagharamia kila kitu mwanetu wee mlete tu .
Miaka 45: hivi kweli nani alikuroga.?

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ changamkia fulsa umri ukifika

Mambo ya Kuzingatia ili uwe mrembo siku zote

Katika Jamii nyingi duniani, dhana ya urembo imekuwa na mitazamo tofauti kwa watu wengi. Kila mmoja anautafakari urembo kwa namna yake kulingana na malezi na tamaduni za mahali husika. Wako wanaoamini kuwa mrembo ni lazima awe na ngozi nyeupe, wengine hudhani kuwa ili kuonekana mrembo, lazima uwe na nywele ndefu, lakini pia wapo wanaodhani kwamba ili uwe mrembo ni lazima uwe na umbo namba nane na wapo wanaojua urembo ni kuwa mwembamba (kimbaumbau au Miss) au kuwa mrefu na wapo wanaoamini urembo ni kuwa mnene.

Hiyo yote ni mitazamo tu, lakini tafsiri halisi kutoka kwa wataalamu wa urembo ni kwamba; urembo ni hali ya kuwa na afya bora.

Je, Mpenzi msomaji ulikuwa unajua hili? Nakuomba Kabla hujafanya chochote kuhusu afya yako, unatakiwa kuamini kwamba wewe ni mrembo. Ikiwa utasimama katika hilo ni kweli utakuwa mrembo siku zote. Basi ili kubaki kuwa mrembo tujifunze haya machache leo ya kufanya:

1. SAFISHA NGOZI YAKO:

Hakikisha ngozi yako inakuwa safi muda wote. Unaweza kutumia njia mbalimbali kama vile kuondoa ngozi zilizokufa mara kwa mara. Kuondoa mafuta yaliyogandamana katika ngozi kwa kufanyia masaji ngozi yako ili kurahisisha mzunguko wa damu yako.
Ikiwa hili litafanyika kwa umakini ni wazi kuwa matatizo ya kuwa na chunusi au weusi katika ngozi yako havitakuwepo kwako.

2. SAFISHA NYWELE ZAKO:

Tumia bidhaa za nywele, ambazo zinaendana na nywele zako na hakikisha unazingatia mambo muhimu katika uboreshaji wa nywele zako.
Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na kutokutumia vifaa vinavyounguza vywele.

Epuka kuosha nywele kwa maji ya moto, pia kuchana nywele zikiwa na maji, kwani unaweza kusababisha kukatika kwa nywele zako.

3. USIPAKE VIPODOZI MARA KWA MARA:

Tumia vipodozi pale inapobidi, usipendelee kutumia vipodozi mara kwa mara kwani wakati mwingine matumizi ya mara kwa mara ya vipodozi, husababisha madhara katika ngozi yako, hasa unapotumia bila kufuata maelekezo ya wataalamu.

4. PATA USINGIZI WA KUTOSHA:

Hakikisha unapata usingizi wa kutosha kila siku. Kwa mujibu wa wataalamu, unatakiwa kulala si chini ya saa nane kila siku. Ikiwa utapata usingizi wa kutosha ni wazi kuwa macho yako yataonekana yenye nuru siku zote. Pia utazidi kuonekana kuwa mrembo zaidi.

5. FANYA MAZOEZI YA VIUNGO:

Hakikisha mazoezi yanakuwa sehemu ya maisha yako, hii itasaidia kukufanya uonekane siyo tu mrembo, bali pia mwenye kujiamini.

6. SAFISHA MENO YAKO:

Usafi wa meno pia ni miongoni mwa mambo ya kuzingatia unapoamua kuboresha urembo wako. Hakikisha unapiga mswaki walau mara mbili kwa siku kila siku au kila baada ya kula.

Haya yameorodheshwa na wataalamu mbalimbali kuwa ni mambo yanayochangia urembo wa asili na mvuto wa ngozi na mwili.

Huu ndio uchawi unaweza kufanyika siku mpenzi wako akikutambulisha kwao

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
*UCHAWI* ni nini?

`Uchawi ni pale mpenzi wako anapokupeleka kwao kufika tyu ghafla unakutana na dada yake getini ambaye alikuwa ni mpenzi wako wa zamani, ile kuingia ndani unamuona kaka yake ambaye mlipigana baada ya kukufumania na mke wake, hujakaa vizuri unamuona mama yake ambaye ndiye jimama shangingi lako anayekuweka mjini akupaye jeuri ya kutamba ambapo hata gari unalolitumia alikupa yeye na hataki upajue anapoishi, wakati unataka kuondoka unakutana uso kwa uso na baba yake ambaye alikuwaga wakili wako kwenye kesi ya ubakaji`

πŸ€£πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ€£

Hii ndio inaitwa mbinu ya biashara

Anakuja Mchina anasema anahitaji Paka🐈,
ananunua mmoja kwa bei ya 20,000/=, basi
wanakijiji wanahaha kusaka Paka🐈,
wanawaleta mchina ananunua wote anasepa
nao. Anarudi tena anasema vipi, naona
wameadimika, sasa ntanunua kwa bei ya
35,000 Paka🐈 mmoja, wanakijiji wanaenda
deep zaidi msituni, kamata Paka🐈, leta kwa
mchina, mchina anasepa nao.

Afu wiki
mnayofuatia Mchina anasema bado anataka
Paka🐈, saivi atanunua kwa Laki. Wanakijiji
macho yamewatoka, hawana tena paka🐈.
Mchina anasema basi ntaftieni kwa Laki na
Nusu. Keshoake inasikika kuwa kuna Mchagga
anauza Paka kijiji cha pili, anauza kwa
100,000/=, wanakijiji wanawahi fasta
wanaenda nunua Paka🐈🐈🐈🐈 wote wa kijiji cha
pili. Wanarudi kijijini hawana pesa ila wana
Mapaka 🐈🐈🐈 wakijua watamuuzia mchina fasta kwa
laki na nusu, Mchina hatokei Ng’oooo!!!!
Infact, yule mchina alikuwa anawakusanya tu
na kuwahifadhi kule kijiji cha pili akijua ataja
wauza kwa 100,000/= kwa hawa hawa wa kijiji
hiki.
This is what called business strategy.πŸ˜ƒ

Ushauri wangu kwa leo

Kuna watu wengi sana huwa wanani-challenge ninaposema kwamba ni muhimu sana mtu kuishi katika kusudi la maisha yake. Na moja kati ya hoja zao ni kwamba haya maisha ya sasa mtu akisema aanze kutafuta kusudi la maisha yake atakufa maskini. Hivyo wanaonelea ni bora kufanya chochote kitakachotokea mbele yake ilimradi mwisho wa siku anapata pesa. Yaani anachagua kuwa mtumwa wa Pesa

Kusudi la maisha ya mtu huwa halina ukomo na halibadiliki, kinachobadilika au kufikia ukomo ni malengo ya kuli-ishi kusudi hilo. Kwa hiyo unapopanga malengo yako au unapokuwa na ndoto zako ni lazima uweze kupambanua mwisho wa siku hizo ndoto au hayo malengo yanakwenda kukidhi kiu ya aina gani inayofukuta ndani yako.

Ukifanikiwa kulitambua kusudi la maisha yako na ukafanikiwa kuli-ishi kwa vitendo, ni dhahiri utakuwa maarufu kwenye mazingira yanayohusiana na maisha yako. Mazingira yanayohusiana na maisha yako yapo ndani ya kusudi la maisha yako.

Ni wakati gani mtu anaweza kusema amefanikiwa katika maisha yake? Ni pale ambapo tu mtu anapoweza kutatua tatizo fulani katika jamii; Kugundua uhitaji wa kutimizwa au kukamilishwa kwa jambo fulani katika jamii. Ukiweza kuziba pengo fulani. Ukiweza kupata ufumbuzi wa kukamilishwa kwa hilo jambo kwa faida ya jamii fulani au niseme ukiweza kutatua tatizo hilo hapo unaweza kusema umefanikiwa. Huwezi kutatua tatizo lolote katika jamii kama hujawekeza ndani yako.

Haijalishi ni jambo gani unafanya katika jamii na liko kwenye kiwango kipi ilimradi liko ndani ya mstari wa maisha yako. Kwa mfano, una kamtaji kadogo na unaamua kuanzisha genge la kuuza mahitaji madogo madogo ya nyumbani (hasa jikoni) naamini unakuwa umeanzisha kwa sababu umeona eneo hilo kuna uhitaji wa aina hiyo ya huduma. Wewe unaweza kuwa unafanya tu labda kwa sababu ya shida fulani za maisha lakini wakati huo huo moyo wako unafurahia kile unachokifanya na unajikuta kila siku unabuni mbinu mpya na mikakati wa kuboresha genge lako. Kidogo kidogo unafungua genge lingine sehemu nyingine, na lingine na lingine, nk. Mwishowe unajikuta unatamani kuwa na duka kubwa la vyakula na mahitaji mengine ya kila siku au supermarket. Ukijiona unang’ang’ana kwenye β€œline” moja ya shughuli (Biashara) basi tambua hilo ndio kusudi lako na ndani yako una zawadi kubwa sana ya kutoka kwa Mungu ya kuhudumia jamii kupitia uuzaji wa mahitaji ya nyumbani.

Lakini ukijiona unatanga tanga leo umefanya shughuli hii kesho umefanya shughuli ile ambazo mwisho wa siku hakuna mahali zinakutana kwa namna yoyote ile japo unapata pesa, basi wewe hujatambua kusudi la maisha yako na usipokuwa makini utakuwa mhangaikaji hadi mwisho.

Ukifanya jambo nje ya kusudi ya maisha yako hutakaa ulifurahie kamwe, litageuka kuwa mateso hata kama linakuingizia pesa nyingi. Unaweza ukawa unafanya kitu nje ya mstari wako wa maisha hata kama kinakulipa mabilioni yaani bado utakuwa kama SAMAKI ALIYETUPWA NJE YA MAJI. Samaki akiwa nje ya maji, zile dakika chache kabla hajafa huwa anahangaika sana na ukimmiminia tone moja la maji kwenye mkia utaona anavyojaribu kutaka kuogelea. Kale katone ka maji kwenye mkia wa samaki akiwa nchi kavu ni sawa na wewe unapokuwa unafanya shughuli nje ya kusudi la maisha yako inyokupa hela nyingi lakini ikatokea katika kuhangaika ukafanya ka-kitu kadogo ambako kako ndani ya kusudi la maisha yako – moyo waku unakuwa na amani sana na unafurahi sana. Lakini unajikuta huendelei kufanya hilo jambo kwa sababu halikuingizii hela nyingi kwa wakati huo ukilinganisha na lile lingine hivyo unaamua kuendelea kuishi nje ya kusudi la maisha yako ili upate mali za nje na kuunyanyasa moyo wako. Maana yake ni kwamba, kama unafanya shughuli inayokuingizia kipato iliyo nje ya kusudi la maisha yako, hutokaa uache kuhangaika kujaribisha vitu vya aina mbalimbali. Kwa sababu moyo wako hautotosheka wa kuridhika – HUWEZI KUKATA KIU YA MAJI KWA KUNYWA SODA AU JUISI JAPOKUWA VYOTE NI VIMIMINIKA. . Ndio sababu huwa napenda kusisitiza sana kupata muda kwa ajili ya maisha yako binafsi, hii inakusaidia kujitambua.

Tatizo wengi hatutaki kuanzia chini, tunapadharau huku chini lakini matajiri wakubwa duniani kama unafuatilia historia za maisha yao na jinsi walivyoanza utagundua kwamba walianza wengine wakiwa hawana kitu kabisa. Ukiwa na nidhamu ya maisha hasa kwa kufuata kanuni za maisha, kanuni za biashara/shughuli unayofanya na kanuni za maisha yako binafsi huwezi kuacha kufanikiwa. Mafanikio ni safari. Umaarufu hauji bila kuwa umefanikiwa kwenye jambo fulani hata kama ni ujinga utapata umaarufu kwa wajinga wenzako.

Mafanikio yanaanza kwa wewe kuweza kujitofautisha na maisha yako ya nyuma. Usiruhusu maisha yako ya nyuma kukuwinda na hivyo kuwa kikwazo cha maisha yako unayoyaendea. Usiishi kwa mazoea ya nyuma. Mafanikio ni pale unapoweza kujitambua na kusimama imara katika kanuni za maisha ulizojiwekea na kujitofautisha na watu wengine wote kwa sababu wewe ni wa tofauti, kila binadamu ni wa tofauti ndio mana kila mtu ana nafsi yake mwenyewe hata mkiwa mapacha mmeunganika viungo vya mwili.

MAFANIKIO YANAANZA NAWEWE

SMS nzuri sana ya kutakia usiku mwema

Dah! Safari yetu ilikuwa ngumu kweli ila hatimaye tumefika japo ni usiku sana hebu tupige hodi tusije kabwa na vibaka hapa nje. Hodiiiiii, Hodiiiii, Tunaomba tufungulie Mlango,, sisi tunaitwa FURAHA, AMANI na UPENDO. Tumebeba HEKIMA, BUSARA na MAFANIKIO. Tulikuwa wengi HURUMA na UPOLE wanakuja nyuma. CHUKI na WIVU hawana nauli. TABU ni mahututi. SHIDA yuko jela. MATATIZO amepigwa shoti ya umeme. MIKOSI amefariki njiani. LAANA ameliwa na mamba. UVIVU ameungua na maji ya moto hajiwezi. Tutakuwa nawe daima maana tumefika kwa NEEMA . Mungu akulinde na mabaya yote katika dunia hii. ucku mwema.

Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa

Angalia huyu jamaa alivyomuweza huyu binti wa chuo

😁😁😁😁 .. TABU KUDATE NA MADEMU WA CHUO
Demu ;Β Baby Safari Hii Nataka Pale Hostel Niwafunike Mashoga Zangu Wote.
Jamaa ;Β Poa Sweetie Ondoa Shaka Nitakununulia #Turubai Utawafunika Wote…!!!
Demu:Β Mxiuuuuuuuu Lione Sura Kama Goti La mbuzi Na Namba yangu futa Nakublock Mpaka Sanduku la posta…!!!

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚nmecheka adi nmelazwa

Dalili za homa ya dengu (Dengue fever)

Dengue ni moja kati ya homa kali inayodhoofisha na kuambatana na maumivu makali. Kwa sasa hakuna kinga ya homa ya dengue, njia pekee ya kuepuka ugonjwa huu ni kuzuia kuumwa na mbu anayesambaza homa ya dengue.

Dalili za ugonjwa huu ni;

β€’Homa kali ya ghafla

β€’Maumivu makali ya kichwa

β€’Macho kuuma

β€’Maumivu ya viungo

β€’Kichefuchefu

β€’Kutapika

β€’Vipele ambavyo hutokea siku nne baada ya homa kuanza

β€’Kutoka damu puani, kwenye fizi na kuchubuka kirahisi

Mara nyingi dalili huwa sio kali na wengi hudhania ni homa ya mafua au maambikizi mengine ya virusi. Dalili hizi huanza kutokea baada ya wiki mbili, lakini kwa wengi huchukua wiki moja ya kwanza na tayari utaanza kuona dalili za dengue.

Suluhisho rahisi la nguvu za kiume hili hapa

NI muujiza! Pengine hivyo ndivyo yeyote anaweza kusema pindi akisikia kwa mara ya kwanza juu ya namna mihogo mibichi na nazi kavu maarufu kama mbata vinavyoweza kuwasaidia watu kiafya, na hasa wanaume.

Uchunguzi uliofanywa kwa siku kadhaa ukihusisha mahojiano na baadhi ya madaktari na pia maandiko yatokanayo na tafiti mbalimbali, umebaini kuwa mihogo na nazi mbata ambavyo huuzwa kwa wingi na kina mama jijini Dar es Salaam, vina uwezo mkubwa wa kurejesha heshima kwa kina baba mbele ya wenzi wao kwa kuimarisha uwezo wa kushiriki tendo la ndoa.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, imebainika kuwa uwezo wa mihogo na nazi mbata katika kuwasaidia wanaume kwenye ushiriki wa tendo la ndoa hutokana na wingi wa virutubisho vilivyomo, hasa madini ya Zinc na Potassium (kwenye mihogo mibichi) na kiambata cha selenium kinachopatikana kwenye nazi mbata.

β€œVyakula hivi vina maajabu makubwa kwa afya ya kina baba… vinapoliwa kila mara na tena kwa kuzingatia usafi, huwasaidia wengi katika kuimarisha nguvu zao za tendo la ndoa na hivyo kuwapa heshima kwa wenzi wao,” mtaalamu mmoja wa masuala ya lishe jijini Dar es Salam aliiambia Nipashe.

Ofisa Utafiti wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Walbert Mgeni, alisema mihogo mibichi na nazi kavu (mbata) ni vyakula ambavyo vimethibitika kitaalamu kuwa husaidia kuiamrisha nguvu za tendo la ndoa kutokana na madini mbalimbali yanayopatikana, na hasa Zinc.

Alisema ni kwa sababu hiyo, anaamini ndiyo maana kuna kina baba wengi hutumia bidhaa hizo jijini Dar es Salaam na kwingineko nchini huku wauzaji wake wakubwa wakiwa ni kina mama.

β€œKuna uvumi mwingi kuhusu faida za mihogo mibichi na nazi kavu kwa wanaume. Wengi huhusisha na masuala ya tendo la ndoa…ukweli ni kwamba wanaozungumzia suala hilo wako sahihi ingawa wanaweza kuwa siyo wataalamu.

Vitu hivyo vina madini mengi yakiwamo ya Zinki ambayo husaidia kurutubisha mbegu za kiume na kuongeza nguvu za kiume kwa mtu anayekula kwa usahihi na kwa muda mrefu,” alisema Mgeni.

Alisema zaidi ya kuimarisha mfumo wa uzazi kwa wanaume, mihogo mibichi na mbata vina faida nyingine nyingi mwilini mwa walaji ikiwa ni pamoja na kuimarisha milango ya fahamu, kusaidia uponaji wa vidonda vya ndani na nje ya mwili, kutunza ngozi na kuilinda, nywele na pia kusaidia uponaji wa matatizo mengi ya macho.

MUUJIZA ZAIDI
Dokta John Kimai wa Kituo cha Afya cha Arafa kilichopo Kimara jijini Dar es Salaam alisema ni kweli mihogo mibichi na nazi mbata husaidia kuiamrisha afya za walaji katika maeneo mengi ikiwamo via vya uzazi.

Aidha, alisema faida nyingine kiafya, hasa kwenye nazi mbata ni kuepusha matatizo ya moyo yatokanayo na wingi wa lehemu kwa kuwa nazi aina hiyo huwa na kiwango kikubwa cha kiambata kiitwacho β€˜lauric acid’.

Alisema faida nyingine ya nazi mbata ni kusaidia mlaji kuepukana na athari za kuvimbiwa, kuongeza nguvu za mwili kutokana na mafuta yake kuelea kwa kiasi kidogo kwenye damu (medium chain triglycerides – MCT) na hivyo huyafanya kusafirishwa moja kwa moja hadi kwenye ini ambako hutumika kama chanzo cha haraka cha nguvu.

Aidha, kwa mujibu wa Dk. Kimai, mbata husaidia pia kuimarisha kinga dhidi ya maradhi mbalimbali kutokana na uthibitisho wa tafiti mbalimbali kuthibitisha kuwa β€˜lauric acid’ hubadilishwa kuwa acid inayojulikana kama β€˜monolaurin’. Aidha, nazi kavu husaidia pia kuzisisimua seli na shughuli za ubongo na kwa kufanya hivyo husaidia kuzuia matatizo ya akili (dementia) na upotezaji wa kumbukumbu (Alzheimer).

Akielezea kuhusu faida za mihogo mibichi, daktari mwingine alisema kuwa ina madini mengi pia yakiwamo ya calcium, phosphorus, chuma na potassium ambayo kwa pamoja husaidia ukuaji wa tishu za mwili wa binadamu.

β€œKwa mfano, calcium ni muhimu kwa ajili ya kuimarisha mifupa na meno kwa mwanadamu na hivyo mtu anayekula kwa wingi mihogo mibichi huimarisha meno yake na kuyafanya kuwa na nguvu,”alisema.

Katika mbata, baadhi ya virutubisho vingine vilivyomo ni Folates, Niacin, Pantothenic acid,
Pyridoxine, Riboflavin, Thiamin, Sodium na Copper

Faida za kutumia mafuta ya Nazi

Mafuta ya nazi hung’arisha ngozi:

Siyo sehemu za ndani tu ya mwili zinazofaidika na mafuta haya ya nazi kama yanavyofanya mafuta mengine ya asili, kama unataka kuwa na ngozi nzuri yenye mng’aro na yenye afya na yenye muonekano wa asili basi paka mafuta ya nazi kila siku kwenye ngozi yako, mafuta ya nazi yana uwezo mkubwa katika kuua bakteria, virusi, na vijidudu vya aina yeyote vinavyoweza kuidhuru ngozi, haya ni mafuta kwa mwili mzima yaani pakaa kwenye ngozi yote usoni, mwilini, kwenye nywele na kwenye kucha. Pia unaruhusiwa kuyatumia mafuta haya wakati wa masaji.

Huongeza nguvu mwilini:

Mafuta ya nazi ni chanzo kizuri cha nguvu ya mwili kwani yana sifa ya kuelea kwa kiasi kidogo kwenye damu β€˜medium chain triglycerides – MCT’ ambapo sifa hii huyafanya kusafirishwa moja kwa moja hadi kwenye ini ambako hutumika kama chanzo cha haraka cha nguvu au hubadililishwa kuwa β€˜ketones’ ambacho ni chakula cha ubongo. Kwahiyo ikiwa unatafuta lift ya kuinua nguvu yako basi chukua kijiko kimoja cha chai cha mafuta ya nazi weka kwenye kikombe chako cha juisi au uji na utaona maajabu.

Hutumika kulainisha uke mkavu:

Mafuta ya nazi yana matumizi mengi sana mwilini zaidi ya 100, kuna wanawake wana tatizo la kuwa na uke mkavu muda wote hata wakisisimuliwa vipi bado huwa wakavu, kuondokana na tatizo hilo pakaa mafuta ya nazi katika uke wako na utaona faida yake tena bila madhara yeyote hasi.

Husaidia katika ugonjwa wa mzio/aleji:

Tukisema tuelezee faida zote za mafuta ya nazi kwa hakika hatutaweza, moja ya faida zake zinazoshangaza wengi ni uwezo wa kudhibiti dalili za ugonjwa wa aleji, kila siku pakaa mafuta ya nazi ndani ya pua zako na uone kama utapiga chafya unapokuwa karibu na kile kinachokuletea aleji/mzio.

Ni mafuta mubadala ya kupikia yenye afya:

Tofauti na mafuta ya alizeti au hata mafuta ya zeituni, kupika chakula kwa mafuta ya nazi ni zaidi ya afya. Mafuta haya yana uwezo mkubwa wa kuungua na bado yakabaki na viinilishe vyake kama kawaida hata baada ya kuunguzwa au kuchomwa katika moto, hii ni kwamba mafuta kama ya zeituni ambayo huweza kuliwa hata yakiwa mabichi lakini yanapochomwa katika moto basi ubora wake hupungua au kwa maneno mengine huzalisha taka sumu kama ilivyo kwa vitu vingi vinapounguzwa lakini hili halitokei kwa mafuta ya nazi!

Ni mafuta mazuri kwa wasiopenda kutumia mafuta yatokanayo na wanyama:

Siyo kupika tu na mafuta ya nazi ndiko huleta afya, bali pia ni mafuta mazuri kwa wasiopenda kutumia mafuta yatokanayo na wanyama kama mubadala kwa siagi au vitu vingine mnavyopaka juu ya mikate mnapokula. Hii nikwa sababu mafuta ya nazi hubaki kuwa magumu hata katika joto la kawaida la chumba tofauti na mafuta mengine.

Huzuia maradhi mengi hatari mwilini:

Kama ilivyo katika kuipunguza kolesteroli, mafuta ya nazi yanao uwezo mkubwa katika kuzuia na kutibu magonjwa mengine sababu ya kuwa na kiasi kingi cha asidi iitwayo lauric acid. Utafiti mwingi umeendelea kuthibitisha kuwa hii lauric asidi hubadilishwa kuwa asidi mafuta nyingine ijulikanayo kwa kitaalamu kama β€˜monolaurin’ ambayo inayo sifa ya kudhibit na kuvizuia baadhi ya virusi ikiwemo vile vya ukimwi kuziingia na kuzidhuru seli za mwili na kusababisha maradhi mwilini. Ili kutibu virusi vya ukimwi inashauriwa kunywa glasi 4 za tui la nazi kila siku kwa muda wa miezi mitatu mine na utaona maajabu.

Hutibu tatizo la kupoteza kumbukumbu:

Hii inaweza ikakushangaza kidogo unapoisikia kwa mara ya kwanza lakini tafiti nyingi zimeonyesha kuwa mafuta ya nazi yanao uwezo kuziamusha seli na shughuli za ubongo na katika kufanya hivyo kutasaidia kuzuia matatizo ya uwendawazimu au ukichaa (dementia) na kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).

Mafuta ya nazi kwa afya ya Moyo:

Mafuta ya nazi yana asidi mhimu sana kwa afya ya moyo iitwayo β€˜lauric acid’ ambayo ina uwezo mkubwa kuuweka moyo wako katika hali ya afya na furaha kwa kuidhibiti kolesteroli/lehemu mbaya katika moyo na mwili kwa ujumla. Lauric acid huongeza uwepo wa kolesteroli nzuri mwilini ijulikanayo kwa kitaalamu kama High Density Lipoprotein (HDL) huku ikiishusha ile kolesteroli mbaya ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama Low Density Lipoprotein (LDL) jambo ambalo ni mhimu kwa afya ya moyo kama anavyosema Lovisa Nilsson, mtaalamu wa lishe wa Lifesum.

Mafuta ya nazi huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula:

Hii ndiyo moja ya faida ya mafuta ya nazi niipendayo zaidi. Ndiyo mafuta ya nazi yanayo uwezo kusaidia kudhibiti uzito uliozidi kwa sababu mafuta haya ni mepesi kumeng’enywa na hayagandi kama yalivyo mafuta mengine mazito (fatty acids) jambo linalosaidia kuuondoa uzito uliozidi mwilini. Kutokana na kitendo hiki cha kuongeza uwezo wa mwili kukimeng’enya chakula, watu wanaoyatumia mafuta haya kupikia vyakula vyao kila siku kwa kawaida huwa na uzito wa kawaida. Anasema Geeta Sidhu Robb, mtaalamu wa lishe na mwanzilishi wa Nosh Detox.

MHIMU: Hakikisha unapata mafuta ya nazi ambayo ni ya asili kwa asilimia 100, ikiwa utanunua dukani kuna uwezekano mkubwa yakawa yamechanganywa na kemikali zingine au haidrogeni kitu kinachoyapunguzia thamani ile ya asili. Kama unapikia kwenye chakula najuwa wengi mnapenda wali wa nazi au hata tui lake likiwekwa kwenye samaki au hata mboga yoyote lazima utajing’ata ulimi, basi nakushauri usichanganye na mafuta mengine kwenye hicho chakula.

Mambo ya kufanya ili kupona majeraha mapema

Hakuna mtu anayependa kupata majeraha au kuchelewa kupona majeraha. Kwa kuwa uhai na uzima wetu haupo mikononi mwetu, ni vyema tukafahamu kuwa kuna wakati tunaweza kuumia.

Kwa kutambua hili karibu nikufahamishe mambo matano unayoweza kuyafanya ili kuharakisha kupona majeraha.

1. Kula vizuri

Lishe bora ni muhimu wakati wote, lakini ni muhimu zaidi mara unapokuwa na majeraha. Ili uweze kupona majeraha mapema unahitaji ule matunda na vyakula vyenye protini, vitamini C, B12 pamoja na madini ya chuma kwa wingi.

Vyakula na matunda hayo ni kama vile machungwa, mapapai, mayai, maziwa, samaki, maharage, n.k. Kwa kula vyakula hivi mwili utaweza kutibu majeraha kwa haraka zaidi.

2. Pumzika vya kutosha

Kupumzika ni njia ya kuupa mwili nafasi ya kujijenga na kujitibu wakati wa majeraha. Kutokana na mtindo wa maisha au changamoto za kiuchumi, baadhi ya watu hawapati muda wa kupumzika wapatapo majeraha.

Hivi leo utamkuta mtu akiendelea na shughuli zake huku akiwa na plasta, au bandeji bila hata kujali. Ili uweze kupona mapema unahitaji kuupumzisha mwili kwa kiasi cha kutosha ili upone vyema.

3. Fuata maelekezo

Kutokana na majeraha uliyoyapata daktari anaweza kukataza usile au sifanye kitu fulani lakini wewe hutaki; je unafikiri utaweza kupona mapema?

Watu wengi hukatazwa vitu kama vile pombe au kazi ngumu mara wapatapo majeraha, lakini ni wachache ndiyo wanaoheshimu hili.

Ni lazima ufuate ushauri wa daktari ikiwa unataka kupona mapema.

4. Kunywa maji mengi

Maji huchukua takriban asilimia 70 ya mwili wa binadamu. Kunywa maji mengi uwapo na majeraha kutakuwezesha kupona majeraha yako mapema.

Maji huboresha kinga mwili, huboresha misuli pamoja na viungio (joints) mbalimbali hivyo kukuwezesha kupona majeraha mapema.

5. Ogea maji ya baridi

Tafiti mbalimbali zilizofanywa zimeonyesha kuwa kuna manufaa makubwa ya kuogea maji ya baridi. Manufaa haya pia yapo kwa mtu aliyepata majeraha.

Kuogea maji ya baridi kutasababisha mzunguko mzuri wa damu, hivyo viini lishe na tiba vitasafirishwa vyema kwenda kuponya majeraha; pia maji baridi hupunguza maumivu ya vidonda au majeraha.

Kwa hakika lishe bora ni tiba ya maradhi takriban yote. Katika makala hii umeona jinsi lishe bora pamoja na kuzingatia kanuni chache za msingi za afya kunaweza kukusaidia kupona majeraha mapema.

Shopping Cart
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About