Karibu AckySHINE
Karibu AckySHINE
Chagua Unachotaka Kusoma Hapa
Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.
Upendo na Matamanio ya Mungu kwa Wanadamu
Kama vile Baba anavyotamani mwanae akue katika maadili na aelekee katika njia nyoofu. Ndivyo na Mungu anavyotamani uachane na dhambi na kumfuata yeye.
Usiruhusu tabia hii itawale akili yako
Tabia ya kijidharau na kujiona hufai ama huwezi kufanya lolote ukafanikiwa maishani, hakuna mwanadamu aliyeumbwa ili ashindwe,, sote tu washindi zaidi, tunatofautiana njia za kufikia huo ushindi.
Rafiki yawezekana umeshajidharau⦠na kujitamkia maneno kadha wa kadha ambayo kimsingi yamekukatisha tamaa kabisa ya kufikia lengo fulani maishani⦠na ukabaki kushuhudia mafanikio ya wengine kila siku maishani.
Embu ondoa dhana ya kushindwa na kujidharau katika kila hatua upitiayo maishani haijalishi umeshindwa mara ngapi, jifunze kuwa na moyo mgumu na wa subila kwa kila hatua upitiayo maishani,, haijalishi upo katika hali gani? Maishani.
Kama ni maskini sana, usijidharau na umaskini wako ukaona wewe ni wa hali hiyo hiyo maisha yako yote,, no.. hapana, haukuumbwa ili uje kuwa maskini. Ila ni juhudi zako mwenyewe ndizo zitakazokutoa katika umaskini ulionao, haijalishi wewe una ulemavu wa aina yeyote ukajidharau na kujiona huwezi fanya lolote mbele ya jamii likakubalika.
Rafiki kuna walemavu kama wewe, wamejitambua na wameamua⦠hakika wamefikia mafanikio makubwa maishani. Ondoa dharau katika nafsi yako amini unaweza. Kuna walioshindwa kama wewe wakadharauliwa na kutemewa mpaka mate⦠ila walitambua kusudi la maisha yao na leo hii wamefikia mafanikio makubwa sana maishani, kwa nini?? Wewe ukate tamaa na kujidharau katika hali uliyopo ukajiona hauna maana? Hakika unaweza ukiamua,
Mapishi ya Mandazi ya nazi
Mahitaji
Unga wa ngano (self risen flour) vikombe 2 na1/2
Sukari (sugar) 1/2 kikombe
Hamira (yeast) 1/2 kijiko cha chai
Hiliki (cardamon powder) 1/4 kijiko cha chai
Tui la nazi (coconut milk) kiasi
Baking powder 1/4 kijiko cha chai
Siagi (butter)1 kijiko cha chakula
Mafuta ya kukaagia
Matayarisho
Changanya unga na vitu vyote kasoro tui la nazi na mafuta ya kukaangia. Ukisha changanyika vizuri tia tui la nazi na uanze kuukanda mpaka uwe mlaini. Baada ya hapo usukume na ukate mandazi katika shape uipendayo, Kisha uyawe katika sehemu yenye joto (warm place) ili yapate kuumuka.
Yakisha uumuka yakaange katika mafuta mpaka yaive kisha ipua na uyaache yapoe tayari kwa kuliwa. (Mafuta ya kukaangia yasiwe yamoto sana kwani yatayababua mandazi na hivyo ndani hayataiva vizuri.
Faida za kutumia mafuta ya Nazi
Mafuta ya nazi hungβarisha ngozi:
Siyo sehemu za ndani tu ya mwili zinazofaidika na mafuta haya ya nazi kama yanavyofanya mafuta mengine ya asili, kama unataka kuwa na ngozi nzuri yenye mngβaro na yenye afya na yenye muonekano wa asili basi paka mafuta ya nazi kila siku kwenye ngozi yako, mafuta ya nazi yana uwezo mkubwa katika kuua bakteria, virusi, na vijidudu vya aina yeyote vinavyoweza kuidhuru ngozi, haya ni mafuta kwa mwili mzima yaani pakaa kwenye ngozi yote usoni, mwilini, kwenye nywele na kwenye kucha. Pia unaruhusiwa kuyatumia mafuta haya wakati wa masaji.
Huongeza nguvu mwilini:
Mafuta ya nazi ni chanzo kizuri cha nguvu ya mwili kwani yana sifa ya kuelea kwa kiasi kidogo kwenye damu βmedium chain triglycerides β MCTβ ambapo sifa hii huyafanya kusafirishwa moja kwa moja hadi kwenye ini ambako hutumika kama chanzo cha haraka cha nguvu au hubadililishwa kuwa βketonesβ ambacho ni chakula cha ubongo. Kwahiyo ikiwa unatafuta lift ya kuinua nguvu yako basi chukua kijiko kimoja cha chai cha mafuta ya nazi weka kwenye kikombe chako cha juisi au uji na utaona maajabu.
Hutumika kulainisha uke mkavu:
Mafuta ya nazi yana matumizi mengi sana mwilini zaidi ya 100, kuna wanawake wana tatizo la kuwa na uke mkavu muda wote hata wakisisimuliwa vipi bado huwa wakavu, kuondokana na tatizo hilo pakaa mafuta ya nazi katika uke wako na utaona faida yake tena bila madhara yeyote hasi.
Husaidia katika ugonjwa wa mzio/aleji:
Tukisema tuelezee faida zote za mafuta ya nazi kwa hakika hatutaweza, moja ya faida zake zinazoshangaza wengi ni uwezo wa kudhibiti dalili za ugonjwa wa aleji, kila siku pakaa mafuta ya nazi ndani ya pua zako na uone kama utapiga chafya unapokuwa karibu na kile kinachokuletea aleji/mzio.
Ni mafuta mubadala ya kupikia yenye afya:
Tofauti na mafuta ya alizeti au hata mafuta ya zeituni, kupika chakula kwa mafuta ya nazi ni zaidi ya afya. Mafuta haya yana uwezo mkubwa wa kuungua na bado yakabaki na viinilishe vyake kama kawaida hata baada ya kuunguzwa au kuchomwa katika moto, hii ni kwamba mafuta kama ya zeituni ambayo huweza kuliwa hata yakiwa mabichi lakini yanapochomwa katika moto basi ubora wake hupungua au kwa maneno mengine huzalisha taka sumu kama ilivyo kwa vitu vingi vinapounguzwa lakini hili halitokei kwa mafuta ya nazi!
Ni mafuta mazuri kwa wasiopenda kutumia mafuta yatokanayo na wanyama:
Siyo kupika tu na mafuta ya nazi ndiko huleta afya, bali pia ni mafuta mazuri kwa wasiopenda kutumia mafuta yatokanayo na wanyama kama mubadala kwa siagi au vitu vingine mnavyopaka juu ya mikate mnapokula. Hii nikwa sababu mafuta ya nazi hubaki kuwa magumu hata katika joto la kawaida la chumba tofauti na mafuta mengine.
Huzuia maradhi mengi hatari mwilini:
Kama ilivyo katika kuipunguza kolesteroli, mafuta ya nazi yanao uwezo mkubwa katika kuzuia na kutibu magonjwa mengine sababu ya kuwa na kiasi kingi cha asidi iitwayo lauric acid. Utafiti mwingi umeendelea kuthibitisha kuwa hii lauric asidi hubadilishwa kuwa asidi mafuta nyingine ijulikanayo kwa kitaalamu kama βmonolaurinβ ambayo inayo sifa ya kudhibit na kuvizuia baadhi ya virusi ikiwemo vile vya ukimwi kuziingia na kuzidhuru seli za mwili na kusababisha maradhi mwilini. Ili kutibu virusi vya ukimwi inashauriwa kunywa glasi 4 za tui la nazi kila siku kwa muda wa miezi mitatu mine na utaona maajabu.
Hutibu tatizo la kupoteza kumbukumbu:
Hii inaweza ikakushangaza kidogo unapoisikia kwa mara ya kwanza lakini tafiti nyingi zimeonyesha kuwa mafuta ya nazi yanao uwezo kuziamusha seli na shughuli za ubongo na katika kufanya hivyo kutasaidia kuzuia matatizo ya uwendawazimu au ukichaa (dementia) na kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).
Mafuta ya nazi kwa afya ya Moyo:
Mafuta ya nazi yana asidi mhimu sana kwa afya ya moyo iitwayo βlauric acidβ ambayo ina uwezo mkubwa kuuweka moyo wako katika hali ya afya na furaha kwa kuidhibiti kolesteroli/lehemu mbaya katika moyo na mwili kwa ujumla. Lauric acid huongeza uwepo wa kolesteroli nzuri mwilini ijulikanayo kwa kitaalamu kama High Density Lipoprotein (HDL) huku ikiishusha ile kolesteroli mbaya ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama Low Density Lipoprotein (LDL) jambo ambalo ni mhimu kwa afya ya moyo kama anavyosema Lovisa Nilsson, mtaalamu wa lishe wa Lifesum.
Mafuta ya nazi huuongezea nguvu mfumo wa mmengβenyo wa chakula:
Hii ndiyo moja ya faida ya mafuta ya nazi niipendayo zaidi. Ndiyo mafuta ya nazi yanayo uwezo kusaidia kudhibiti uzito uliozidi kwa sababu mafuta haya ni mepesi kumengβenywa na hayagandi kama yalivyo mafuta mengine mazito (fatty acids) jambo linalosaidia kuuondoa uzito uliozidi mwilini. Kutokana na kitendo hiki cha kuongeza uwezo wa mwili kukimengβenya chakula, watu wanaoyatumia mafuta haya kupikia vyakula vyao kila siku kwa kawaida huwa na uzito wa kawaida. Anasema Geeta Sidhu Robb, mtaalamu wa lishe na mwanzilishi wa Nosh Detox.
MHIMU: Hakikisha unapata mafuta ya nazi ambayo ni ya asili kwa asilimia 100, ikiwa utanunua dukani kuna uwezekano mkubwa yakawa yamechanganywa na kemikali zingine au haidrogeni kitu kinachoyapunguzia thamani ile ya asili. Kama unapikia kwenye chakula najuwa wengi mnapenda wali wa nazi au hata tui lake likiwekwa kwenye samaki au hata mboga yoyote lazima utajingβata ulimi, basi nakushauri usichanganye na mafuta mengine kwenye hicho chakula.
Kwa nini tarehe ya Pasaka hubadilika
KALENDA za mwanzo ziliutumia mwezi wa
angani kama kipimo cha muda. Ziliitwa
βLunar calenderβ au Kalenda-Mwezi. Tarehe 1
ya Mwezi ilikuwa ni siku ulipoandama yaani
Mwezi-Mdogo (Crescent Moon).
Mwezi unapofika siku ya 15 unakuwa
umefikia ukubwa wa juu na huitwa Mwezi-
Mkubwa (Full Moon). Hivyo kwa kalenda ile
tarehe 15 ilikuwa ni siku ya Mwezi-Mkubwa.
Mwaka 45KK, Julius Caesar alitangaza
kalenda mpya ikaitwa βJulian Calenderβ iwe
na siku 365. Wakati huo ikijulikana kwamba
jua huzunguka kwa siku 365.25. Hivyo pengo
la kalenda na mzunguko likabaki robo siku.
Robo hiyo ifidiwe kila baada ya miaka minne
mwishoni mwa mwezi Februari ambayo sasa
ulifanywa kuwa wa pili baada ya January.
Inapofanyika hivyo, huo ukaitwa mwaka-
mrefu (Leap year).
Mwaka mrefu ukachaguliwa kuwa ni ule tu
unaogawanywa kwa nne mfano miaka
ifuatayo 1700, 1800, 1900, 2100, 2200, 2300.
Baadaye iligundulika kuwa jua huzunguka
kwa siku 365.24218967 ziitwazo βTropical
yearβ. Hizi ni chache kuliko siku 365.25
zilizokadiriwa mwanzoni. Uchache huu
husababisha kuwe na pengo la dakika 11 na
sekunde 14.812512 kwa mwaka.
Pengo hili ni dogo, lakini hupanuka hadi kuwa
siku nzima kila baada ya miaka 128.0355.
Mwaka 1545 lilivuka siku 9.25.
Kuondoa tatizo hili, Papa Gregory XIII
aliamuru iundwe kalenda mpya na akachagua
Oktoba 04, 1582 iwe siku ya mwisho
kutumika βJulian Calenderβ. Kesho yake,
kalenda mpya ikaanza kutumika.
Ungetegemea hiyo kesho iwe ni Oktoba 05,
1582. Lakini ili uzibe pengo lile lililofikia siku
kumi, ilibidi kalenda mpya kuziruka siku hizo
siku kumi. Hivyo hii mpya iliyoitwa
βGregorean Calenderβ ikaanza kama Oktoba
15 badala ya Oktoba 05.
Ndiyo sababu katika historia ya nchi nyingi
Ulaya, hakuna tarehe za Oktoba 05, 1582
hadi Oktoba 14, 1582. Watu walilala Oktoba
04, 1582 kesho yake wakaamka ikiwa ni
Oktoba 15, 1582.
Teresa Alonso huandikwa kwamba alifariki
Oktoba 1582, kwenye usiku wa tarehe NNE
kuamkia tarehe KUMI NA TANO!
Alipotangazwa kuwa Mtakatifu, Kanisa
Katoliki likaifanya Oktoba 15 kuwa siku ya
kumkumbuka, yaani siku ya Mtakatifu Teresa
wa Avila.
Usipofahamu kwamba Mtakatifu Teresa
alifariki siku kalenda zinabadilishwa, utadhani
aliyeandika vile tarehe za kifo chake
amekosea!
Waandishi, William Shakespeare wa
Uingereza na Miguel de Cervantes wa Spain
huandikwa kwamba wote walifariki Aprili 23,
1616. Lakini ukweli ni kwamba hawakufa siku
moja bali walipishana siku kumi kwani
England ilichelewa kwa karibu miaka 200
kuikubali βGregorean Calenderβ!
βGregorean Calenderβ haikuundwa ili kuishia
kuliziba lile pengo. Bali pia, kuhakikisha
halitokei tena. Tumeshaona kuwa lile pengo
ni dakika 11 na sekunde 14.812512. Hivyo,
linapanuka na kuwa siku tatu ndani ya miaka
400.
Hivyo kuliziba inatakiwa kupunguza siku tatu
kila baada ya miaka 400.
Je, zipunguzweje?
Kipande cha miaka 400 kina miaka mitatu ya
karne inayogawanyika kwa 4 lakini
haigawanyiki kwa 400.
Ikakubalika kwamba unaogawanyika kwa 4,
lakini haugawanyaiki kwa 400, usiendelee
kuwa mrefu. Humo siku moja ichomolewe na
uwe mfupi.
Ndipo miaka 1700, 1800, 1900 haikuwa tena
mirefu. Ndivyo pia miaka 2100, 2200, 2300
nayo haitakuwa mirefu. Kwa sababu ni miaka
ambayo βGregorean Calenderβ inachomoa
siku moja ili kutosababisha pengo tena.
Kipande hiki cha miaka 400 kikaleta wastani
mpya wa siku 365.2425 kwa mwaka. Sasa
lile pengo lile la siku moja si rahisi kufikiwa.
Kwenye βJulian Calenderβ tumeona lilikuwa
miaka 128.0355 lakini sasa limekuwa miaka
3,222.
Sasa tuijadili tarehe ya siku ya Pasaka
tukiwa na ufahamu wa kalenda zile. +++ Je, tarehe ya Pasaka imetajwa ndani ya Biblia?
Kuna kifungu kinasema hivi:
β..Mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya
mwezi, wakati wa jioni, ni Pasaka ya BWANA.
Na siku ya kumi na tano ya mwezi huohuo ni
sikukuu ya BWANA, ndiyo siku ya mikate
isiyotiwa chachu. (Walawi 23:5)..β. Hivyo
Pasaka ni tarehe 15 ya mwezi wa Kwanza.
Lakini Biblia pia inautaja mwezi wa kwanza
kwa jina la Nisan (Esta 3:7, Nehemia 2:1).
Yesu alisulubiwa mwaka ambao Ijumaa
iliitangulia sikukuu ya Pasaka kwa siku moja
(Yohana 18: 28, Marko 15:42-43). Hivyo
tarehe ya Yesu kusulubiwa ni Ijumaa, Nisan
14. Siku moja kabla ya Nisan 15. Siku moja
kabla ya Mwezi-Mkubwa.
Baada ya Yesu, Wakristo wengi Pasaka
waliiadhimisha Jumapili, lakini utata
ulijitokeza kuhusu tarehe ya kuiweka hiyo
Jumapili ya Pasaka. Ilifika wakati jimbo moja
la Wakristo linaadhimisha siku tofauti na
jingine na kwa njia wanayoijua wao.
Utata huu uliondolewa kule Nicaea mwaka
325 ambapo Kanisa Katoliki lilipoamua kuwa,
tarehe ya Pasaka iwe moja tu duniani kote,
yaani iwe ni Jumapili inayokuja baada ya
Mwezi-Mkubwa (Full Moon) unaotokea baada
ya siku ya Ikweta, yaani baada ya Machi 21
(Equinox).
Baada ya uamuzi huu, wataalamu walipania
kuunda chati maalum zenye tarehe za Mwezi-
Mkubwa zitazokasaidia kuitambua tarehe ya
Pasaka kwa mwaka wowote.
Mwezi huizunguka dunia kwa siku
29.5305891203704 (Synodic Month), wakati
dunia hulizunguka jua kwa siku
365.24218967 (Tropical year).
Mizunguko hii miwili ikianza safari siku moja,
itapishana kila mwaka, lakini itakutana tena
mwezi unapokamilisha mizunguko 235. Dunia
nayo inakuwa imekamilisha mizunguko 19,
yaani miaka 19.
Wataalamu wakaitumia hii miaka 19
kutengeneza chati yenye tarehe za Mwezi-
Mkubwa unaotokea March 22 hadi April 18.
Tarehe zile zikaitwa tarehe za Mwezi-
Mkubwa Wa Pasaka au Ecclesiastical Full
Moon (EFM).
Ndani ya ile miaka 19, kila mwaka ukapewa
tarakimu iitwayo Golden Number
inayosimama badala ya mwaka ikiwa na
tarehe zile ziliorekodiwa za Mwezi Mkubwa
wa Pasaka. Chati yenyewe ya Golden
Number na tarehe zake (siku/Mwezi) ni hii
ifuatayo: {1=5/4, 2=25/3, 3=13/4, 4=2/4,
5=22/3, 6=10/4, 7=30/3, 8=18/4, 9=7/4,
10=27/3, 11=15/4, 12=4/4, 13=24/3, 14=12/4,
15=1/4, 16=21/3, 17=9/4, 18=29/3, 19=17/4}
Golden Number ya mwaka inapatikana
kuanza kuugawa mwaka kwa 19.
Tulifundishwa mashuleni kuwa namba
inayosalia baada ya kugawa huitwa βBakiβ .
Hii βBakiβ ukiijumlisha na 1 unapata Golden
Number (GN).
Mfano unatafuta GN ya 27. Hatua ya kwanza
ni kutafuta βBakiβ baada ya kugawa 27 kwa
19. Hizi ni hesabu za βmoduloβ , yaani
zinahitaji tu namba inayobaki baada ya
kugawa.
Ikiandikwa hivi: (27 mod 19) inatakiwa
namba inayobaki baada ya kuigawa 27 kwa
19. Jibu ni 8. Hivyo tulipaswa tuandike hivi:
(27 mod 19=8). βBakiβ 8 tuliyoipata, ndiyo
tunaihitaji ili tuijumlishe na 1 ili tupate GN
ambayo hapa ni 9 kwani (8+1=9).
Tungeweza pia kuandika hivi : 27 mod 19 +
1=9. Hivyo kanuni ya kupata GN kwa mwaka
wowote ni hii:
(MWAKA mod 19 + 1). Yaani, ugawe huo
mwaka kwa 19, kisha namba itakayobaki
ijumlishe na moja.
Ukishaipata GN, itafute kwenye ile chati
ambapo utaiona ikiwa na mwezi na tarehe.
Jumapili inayofuata baada ya tarehe hii ndiyo
tarehe ya Pasaka ya mwaka huo.
Tutumie chati ile na kanuni hii kujua tarehe
ya Pasaka ya mwaka 1474. GN ni (1474 mod
19 + 1=12). Hivyo GN ni 12.
Kwenye chati, 12 inaonyesha ni tarehe 4/4.
Hivyo, mwaka 1474 Mwezi-Mkubwa wa
Pasaka ulikuwa tarehe 4/4/1474. Hiyo ilikuwa
ni Jumatatu. Hivyo Pasaka ilikuwa ni
Jumapili iliyofuata yaani tarehe 10/4/1474.
Lakini, Kanisa Katoliki liliikubali kanuni hii
karne ya sita. Hii ndiyo sababu, tarehe za
Pasaka zinazojulikana ni zile tu zinazoanza
mwaka 533.
Ndivyo Pasaka ilivyotafutwa miaka ile. Sasa
tuone Pasaka ya kizazi chetu. Kizazi cha
βGregorean Calenderβ iliyoanza mwaka 1582.
Tumelijadili lile pengo la siku lililofikia ambalo
mwaka 1582 lilishafika siku 10. Ukweli ni
kwamba kabla halijazibwa, Pasaka ilikuwa
inawadia lakini uhalisi ni kwamba inakuwa
tayari imepitwa siku 10. Kinyume kabisa na
maamuzi ya Kanisa kule Nicaea!
Ili kulizuia lisitokee tena, tumeona uchomoaji
wa siku moja toka kwenye miaka inayofunga
karne, isiyogawanyika kwa 400. Uchomoaji
huu umewekwa kwenye kanuni (formula)
iitwayo βSolar Equationβ.
Kama mwendo wa kuzunguka jua
umezingatiwa na βGregorean Calenderβ, vipi
kuhusu mwendo wa mwezi?
Tumeuona kwamba mizunguko ya mwezi na
dunia hukutana kila baada ya miaka 19.
Kadirio la dunia kuzunguka kwa siku 365.25
linafanya ikizunguka kwa miaka 19 zinakuwa
siku 6,939.75. Mwezi utakuwa nao
umezunguka mara 235, huku kila mzunguko
ukitumia siku 29.5305891203704.
Hivyo, kukutana kule ndani ya kila miaka 19,
huleta pengo dogo la saa 1, dakika 28,
sekunde 38.5.
Mapengo madogo haya tunayoyapuuza
mwanzoni, yameshatugharimu vya kutosha.
Pengo hili kwa mwaka ni dogo lakini kwa
miaka 2500 linakuwa hadi kufika siku nane.
Kwenye hesabu za kutafuta Pasaka
urekebishaji wa hili pengo hutokea kwenye
kanuni iitwayo βLunar Equationβ. Lakini kwa
sababu ya tofauti ya uelekeo wa mzunguko
wa mwezi na dunia, βLunar Equationβ
hujumlisha mara nane kila baada ya miaka
2500.
Hivyo, mahesabu yoyote ya kuitafuta tarehe
ya Pasaka hayakosi kanuni hizi mbili βSolar
Equationβ na βLunar Equationβ .
Tumeona kwamba kalenda ilianza mwaka
1582. βSolar Equationβ inaondoa siku moja
toka kwenye miaka 1700, 1800, 1900. Hivyo,
ni kujidanganya kusema kwamba miaka yote
inayogawanyika kwa nne ni mirefu, jambo
ambalo hata mimi nilifundishwa shuleni.
Hapa tumeona kwamba βSolar Equationβ
imeondoa siku moja kwenye mwaka 1900 na
hivyo haukuwa mwaka mrefu ingawa
unagawanyika kwa nne.
βLunar Equationβ huongeza siku moja kwenye
miaka 1800, 2100, 2400. Mwaka 1800
unaguswa na vyote βSolar Equationβ na
βLunar Equationβ. Hivyo hauathiriki.
Kanuni zote za kuitafuta Pasaka huzingatia
zaidi ya niliyoyaeleza, lakini cha muhimu
zaidi ni hizi mbili yaani βSolar Equationβ na
βLunar Equationβ ambazo sijawahi kuzisikia
kwa kiswahili.
Ni vigumu kuepuka hesabu za βmoduloβ au
βmodβ unapotafuta tarehe ya Pasaka. Lakini
ukiwauliza wanafunzi wa darasa la nne
kwamba machungwa 2011 yakipangwa
kwenye mafungu 19, ni mangapi yatakosa
fungu?
Wapo watakaopata jibu sahihi kwamba ni
machungwa 16. Kimahesabu swali hilo
linaandikwa hivi: (2011 mod 19) na jibu lake
ni 16, yaani (2011 mod 19=16).
Ifuatayo ni moja ya kanuni zinazotumika
kuipata tarehe za Pasaka ya mwaka wowote
kuanzia 1700 hadi 2099:
(1) : a=MWAKA mod 19;
(2) : b=MWAKA \ 100;
(3) : c=MWAKA mod 100;
(4) : d=b \ 4;
(5) : e=b mod 4;
(6) : f=c \ 4;
(7) : g=c mod 4;
(8) : h=(b + 8)\25;
(9) : i=(b β h + 1)\3;
(10) : j=(19xa + b β d β i + 15) mod 30;
(11) : k=(32 + 2xe + 2xf β j β g) mod 7;
(12) : m=(a + 11xj + 22xk) \ 451;
(13) : n=j + k β 7xm + 114;
(14) : Tarehe=(n mod 31) + 1
(15) : Mwezi =n\31;
Penye neno MWAKA, andika mwaka
unaotafuta kujua tarehe yake ya Pasaka.
Panapotokea alama (\) ni kugawanya
ambako hata kama jibu litaleta desimali, basi
hiyo desimali unatakiwa kuachana nayo ili
jibu libaki namba nzima. Penye alama (x)
hiyo ni ya kuzidisha.
Yafuatayo ni majibu niliyopata kwa hatua
zote baada ya kuuingiza mwaka 2015 ili
kujua siku ya Pasaka ya mwaka huu: (1): 1,
(2): 20, (3): 15, (4): 5, (5): 0, (6): 3, (7): 3,
(8): 1, (9): 6, (10): 13, (11): 1, (12): 0, (13):
128, (14): 5, (15): 4.
Tarehe imepatikana kwenye hatua ya 14
ambako jibu ni β5β. Mwezi umepatikana
kwenye hatua ya 15 ambako jibu ni β4β. Hivyo
Pasaka ya mwaka (2015) huu ni Tarehe 5,
mwezi wa 4.
Hivyo, kwa njia hii, unaweza kujua tarehe za
Pasaka kwa miaka ijayo kama unavyoijua
tarehe ya Krismas. Kama kuna tukio
lilifanyika siku ya Pasaka miaka iliyopita na
hukumbuki tarehe, basi tumia kanuni hii.
Zifuatazo ni siku zinazoitangulia Pasaka kwa
idadi ya siku zilizoandikwa kwenye mabano:
Jumatano Ya Majivu (46), Jumapili ya
Matawi (7), Ijumaa Kuu (2).
Zinazotanguliwa na Pasaka ni hizi zifuatazo:
Kupaa (42), Pentekoste (49), Utatu Mtakatifu
(56), Ekaristi (63).
Mwanzo tuliona kwamba Mwezi-Mkubwa wa
Pasaka au βEcclesiastical full Moonβ ni ule wa
March 22 hadi April 18. Ukitokea March 22
basi kuna uwezekano siku hiyohiyo ikawa
Pasaka na ikawa imevunja rekodi ya kuwahi
mapema.
Ukitokea April 18, kuna uwezekano wa
Pasaka kuwa siku saba zaidi ya hapa yaani
April 25, na hiyo ikawa ni tarehe ya juu mno
ya Pasaka. Hivyo, Pasaka yoyote haiwezi
kuwa chini ya Machi 22, wala haiwezi
kuwazaidi ya April 25.
Pasaka tuliyoiona mwaka 2008 ndiyo ya
mwisho kwa kizazi chetu kuiona ikiwahi
mapema kiasi kile, kwani ilitokea Machi 23 na
itairudia tena tarehe hiyo mwaka 2160!
by JOSEPH MAGATA
Tamaa ni asili
Tamaa ni tabia ya kiasili ya kila mtu, tofauti ya mtu na mtu ni namna ya kukabili tamaa.
Mapishi ya tambi za mayai
Tambi za mayai ni moja kati ya vyakula ambavyo napenda kuandaa pale ninapokua ninaharaka au sina muda mrefu wakukaa jikoni.pishi hili huchukuca muda mfupi sana na nimlo uliokamilika.
Mahitaji
- Tambi Β½ paketi
- Vitunguu maji 2 vikubwa
- Karoti 1
- Hoho 1
- Vitunguu swaumu(kata vipande vidogo) kijiko 1 cha chakula
- Carry powder kijiko 1 cha chai
- Njegere zilizochemshwa Β½ kikombe
- Mafuta kwa kiasi upendacho
- Mayai 2
- Chumvi kwa ladha upendayo
Njia
1.Chemsha maji yamoto yanayotokota,ongeza chumvi na mafuta kidogo,weka tambi kwenye maji hayo chemsha adi ziive.Chuja maji yote ili kupata tambi kavu
2.Katika bakuli piga mayai kisha weka pembeni
3.Katika kikaango,weka mafuta,vitunguu maji ,vitunguu swaumu,hoho, karoti na carry powder,kaanga kwa pamoja katika moto mdogo kwa muda mfupi kwani mboga hazitakiwi kuiva.
4.Ongeza tambi na njegere katika kikaango,geuza kila mara ili kuchanganya .
5.Ongeza mayai kwenye tambi kisha geuza kwa haraka bila kupumzika adi mayai yaive na tambi ziwe kavu.Tayari kwa kula
Katika hatua hii ongeza moto uwe wa wastani,moto ukiwa mdogo mayai yatafanya tambi zishikane na kufanya mabonge.
Ungekua wewe ndio boss wa huyu jamaa ungempa kazi? Ungemjibu nini?
*Boss*:-kijana unataka nini ndani ya ofisi zangu?
*Jamaa*:-Samahani naomba kazi ya ulinzi ndugu.
*Boss*:-umesoma mpaka wapi?
*Jamaa*:-mpaka form four.
*Boss*:-unajua kingereza?
*Jamaa*:-kwani hao wezi wanakuja na wazungu???.
π
π
π
π
π
π
Jinsi ya kulima mahindi kitaalamu kama inavyotakiwa
Mahindi ni miongon mwa mazao makuu ya chakula hapa nchin Tanzania na ulimwa karibu kila mkoa. Ulimwa zaidi nyanda za juu kusini katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Ruvuma, Njimbe na Katavi. Pia mikoa ya Morogoro Mwanza Dodoma Shinyanga Arusha Tanga na mikoa mingine. Kwakua ni zao la biashara hivyo karibu kila mkoa unalima zao hili.
Matumizi.
Zao hili ulimwa na utumika kwa matumizi mbalimbali yakiwemo yafuatayo
β
Chakula (stample food)
β
Chakula kwa mifugo
β
Nishati (biofuel)
βDawa za asiri(mbelewele zake)
βkutengenezea mapambo.
βmabaki utumika kama mbolea n.k.
Pia wapo wakulima waliojikita katika kulima zao hili kibiashara ambao uuza katika soko la ndani ya mkoa nje ya mkoa na nje ya nchi. Hapa itategemea uwekezaji wa mkulima husika.
MAZINGIRA NA HALI YA HEWA NZURI KWA MAHINDI
Mahindi uota vizuri katika jotoridi lenye wastani wa 20-30 nyuzi joto za centigradi. Pia linaitaji mvua hasa wakati wa uotaji na uotaji wa mbelewele.
MBEGU ZA MAHINDI
Kuna aina nyingi za mbegu. Zipo za Asili na pia zipo mbegu chotara (Hybrid F1 & F2) kutoka makampuni mbalimbali, za mda mfupi na za mda mrefu kulingana na kipindi/vipindi vya mvua kwa mwaka kwa mkoa usika.
Kwakua Tanzania ina kanda tofauti za hali ta hewa ikiwemo nyanda za juu kusini, nyanda za juu kaskazini, nyanda za kati na maeneo mengine ya pwani na pia ndani ya mkoa mmoja panaweza pakawa na matabaka tofauti yakijografia (geographical/ecological zone).
Hivyo mbegu za mahindi zinazofanya vizuri mikoa ya Pwani Morogoro Arusha Mwanza haziwezi kufanya viruzi katika mikoa ya Njombe Iringa n.k kwakua utofautiana katika ukanda.
Mbegu zinazofanya vizuri Njombe mjini ama wanging’ombe zinaweza zisifanye vizuri Ludewa ama Makete wilaya tofauti lakini mkoa mmoja.
Hivyo ni vema kujua kua mbegu upandao inafaa kwa ukanda upi?? Wa mvua za mda mrefu! Mda mfupi! Ama sehemu zenye ukame!!.
NAFASI
Hii itategemea aina ya mbegu na pia namna ya utunzaji ambao utegemea sana kusudi la ulimaji (chakula ama biashara).
UPANDAJI WA MAHINDI
Mche hadi mche ni sm 30-40. Mstar hadi mstari ni sm 70-75.
Yaani sm 75X30, pia waweza tumia sm 80X25 punje moja moja za mbegu chotara ya mahindi.
Ni vema ukapanda siku moja ambayo utaweka na mbolea. Anza na mbolea 5g kwa shimo fukia kidogo kisha weka mbegu ( mbegu moja kama ni Hybrid).
Mbolea nzuri zaidi yenye maboresho na lishe linganifu kwa mmea (balanced nutrition) ni YaraMila Cereal, Yara Vera Amidas na YaraBela Sulfan kutoka kampuni ya Yara Tanzania ltd. Mfuko mmoja mmoja, utapandia, utakuzia mkuzio wa kwanza na utamalizia mkuzio wa pili kama zilivyo orodheshwa hapo.
PALIZI YA MAHINDI
Kuna aina tatu za kupambana na magugu.
1. Palizi la mkono/jembe.
Hili lina gharama zaidi na linachukua mda mwingi na pia SIO SAHIHI kwakua halireti majibu mazuri katika kuzuia magugu.
2. Mbinu za Asiri.
Hapa utumika matandazo kama majana makavu, majani ya mgomba, pumba za mpunga n.k ( Mulching). Huitaji kujipanga zaidi na piaupatikanaji wa matandizo wakati wakilimo unaweza ukawa ni shida.
3. Palizi la Dawa.
Hapa ndio upatikana suluhisho sahihi kwa mkulima ingawa changamoto zipo katika ubora wa dawa wingi wa madawa uwepo wa dawa feki na gharama.
Ni vema ukatumia dawa zinazotumika kuzuia magugu mara baada yakupanda kabla ya magugu kuota (somo la magugu litafuata sio mda).
Tumia PRIMAGRAM GOLD kutoka Syngenta Tanzania Ltd epuka palizi la mkono okoa mda pata faida pata mda wakupumzika na kujishughurisha na mambo mengine na uongeze kipato.
WADUDU NA MAGONJWA KWENYE MAHINDI
WADUDU WA MAHINDI
Maize aphids, African armyworms, Bollworm, Stalk borer, leaf hoppers.
Dawa nzuri kuzuai hili ni Match 050EC na Karate 5EC/Karate 5CS(Originali kutoka Syngenta epuka dawa feki ilikopiwa nembo/lebo)
MAGONJWA YA MAHINDI
Magonjwa ya ardhini (soil born disease), kutu ya majani n.k.
Magonjwa ya kuvu sio tatizo sana ktk kilimo hiki ingawa maeneo ya nyanda za juu kaskazini yameoneka.
Tumia Artea na Amistar Kutoka kampuni ya Syngenta.
UVUNAJI WA MAHINDI
Mda ambao mahindi uchukua kukaa shamban hadi kuvunwa inategemea na ukanda na pia na mbegu, mahindi ukaa wastan wa miezi mitano toka kupandwa shambani. Lakini ni tamaduni za wakulima wengi kuacha mahindi shambani kwa mda mrefu zaidi ili yakauke kwa matumizi ya biashara. Mahindi kwa ajiri ya gobo ukaa mda mfupi (sio kila mbegu ni ya gobo/mahind yakuchoma) zaidi uvunwa kabla yakukomaa.
Idadi ya gunia utazopata kwa ekari moja utegemea
β utaratibu uliofuatwa wakitaalum (Agronomic practices)
β aina ya mbegu
βmazingira (ukanda)-mvua ama umwagiliaji.
βmapambano dhidi ya wadudu magonjwa na magugu.
β usimamizi/mbolea/rutuba ya udongo wako.
Kila mbegu hasa chotara zinakua na kiasi tajwa cha mavuno kwa ekari.
Mf. Gunia 30, 25-30, ama 40 n.k. (gunia tafsiri yake kitaalum ni 100kg.
SOKO LA MAHINDI
Soko utegemea sana wastani ama ungezeko la walimaji na uzalishaji. Soko lake utegemea sana watumiaji wa ndani.
Pia utokea soko katika mkampuni kama wanunuzi wadogo wadogo, kampuni ndogondogo za usagaji mahindi, taasis mbalimbali,Mohamed enterprise, Hifadhi ya taifa ya chakula, n.k na pia soko la nje ya nchi eg Kenya Uganda Sudani Ethiopia n.k
Yafahamu Mambo Mbalimbali ya muhimu kuhusu kilimo cha Mazao ya Mboga Mboga kwa Ku-Download Kitabu cha MBINU ZA KILIMO BORA CHA MBOGA
Ni kitabu kinachotoa elimu ya Kilimo Cha Mboga. Kipo katika Mfumo wa PDF (Soft copy).
Kina kurasa 100 na utaalamu wa mazao zaidi ya 10, ambayo ni nyanya, kabichi, bamia, vitunguu maji, vitunguu twaumu, hoho, matikiti, karoti, uyoga na matango. Bila kusahau kilimo cha mboga kama chainizi na mchicha.
Pia utaweza kufahamu mbinu mbalimbali za kilimo cha mboga kama vile kuandaa shamba na kitalu, udhibiti wa wadudu na magonjwa katika mboga, kuvuna na kuhifadhi mboga, vilevile utajifunza kuhusu kilimo cha matone.
Kitabu hiki ni Soft copy [pdf] kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.
-
Kilimo na Ufugaji
πKitabu cha Mbinu za Kilimo Bora Cha MbogaπΏπ
Original price was: Sh7,500.Sh3,000Current price is: Sh3,000. Download Now
Eti kwa nini Watu hawapostigi hii? Hata selfie sijaonaga
Vijana mkiwa mnaendesha magari mna post mukiwa mpo beach mna post mkiwa kwenye masherehe mna post Lakin mkiwa mmeenda kwa mganga siwaoni kupost mitunguli na vibuyu vya mganga unakuwa je wa zee tena. ππππ
Baada ya walevi wawili kuokota kioo hiki ndicho kilifuata
Angalia kilichotokea
Walevi wawili waliokota kioo, mlevi wa 1 akaangalia muda mrefu kisha akasema “hii sura sio ngeni machoni mwangu sema jina tu silikumbuki..! !!
Mlevi wa pili akamnyang’anya kisha nae akaangalia kioo akasema “wee kweli huna akili, si mimi huyu? halafu unajidai hunikumbuki β¦!!!
SMS ya kumwambia mpenzi wako kuwa haumpendi kwa uzuri wake tuu
Napenda ufahamu kuwa wewe ndiye nikupendae tu
Uzuri wako sio sababu ya mimi kukupenda
Ila nakupenda kwa matendo yako na jinsi ulivyoumbika.
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Kuna watu makauzu ila huyu kazidi.. Soma hii!
Kakubaliana vizuri na msichana fulani hivi kuwa aibuke gheto, mchizi kajipanga vizuri kabisaβ¦. mara saa nne hivi mdada kasema hana nauli.
Mshkaji kajikunja kamtumia Elfu tano maana mwenye shida alikuwa ni yeyeβ¦β¦
Baada ya nusu saa yule dada akamtumia meseji.
“Jamani mpenzi, kumbe baba hatoki nilijua atatokaβ¦ sorry bae sitaweza kuja kwa leoβ¦ sooo sorry!”
Mshkaji jiii! hajajibu kituβ¦..
Baada ya muda kidogo meseji ikaingia katika simu ya binti, akajua mchizi kajibu. Mh! kutazama ni meseji kutoka Mpesa.
“CA90F0511 IMETHIBITISHWA Tshs 5000 ILIYOTUMWA KIMAKOSA KATIKA ACCOUNT YAKO IMETOLEWA SALIO LAKO NI Tshs 5”
Halafu ndo ikaingia meseji ya mshkaji.
“BASI POA SIKU NYINGINE KAMA VIPI”
#dada wa watu mashavu yakamshukaβ¦ hakuamini kilichotokeaβ¦. yaani jamaa keshawapigia Voda na pesa fasta imezuiliwaβ¦β¦
Cheki wanachokisema vichaa baada ya kuona ndege inapita angani
Vichaa wawili walikuwa wamekaa sehemu ghafla ikapita ndege angani kichaa mmoja akasema ndege ile hitakua imembeba rais kichaa mwenzake akajibu hapana ile imebeba wazungu kama ingekuwa imembeba rais ungeona mapikipiki mbele
Maneno na matendo
Uwe mzuri kwenye kufanya kama ulivyo kwenye kufikiri. Matendo yako yafanane na maneno na maneno na matendo.
Jinsi ya kutengeneza Biskuti Ya Keki Kavu (Shortcake)
VIAMBAUPISHI
Unga – 2 Magi (vikombe vya chai)
Sukari iliyosagwa – 2/3 Magi (kikombe cha chai)
Siagi – 220Β g
Unga wa mchele – Β½ Magi
Yai -1
Vanilla – 1 kijiko cha chai
MAANDALIZI
Changanya vitu vyote hivyo kwenye bakuli mpaka unga ushikamane.
Paka mafuta treya ya kuchomea kisha utandaze kwenye treya ya 20cm kwa 30Β cm au (8 in kwa 12 in)
Choma kwenye moto 325ΛC kwa muda wa saa nzima au mpaka ibadilike kuwa rangi ya dhahabu.
Epua acha ipoe kisha kata vipande kama mstatili, weak kwenye sahani tayari kunywewa na chai.
NYONGEZA
Kwa unga huo huo unaweza kutengeneza vibiskuti vya duara duara.
Upendo wa Mungu hauna mwisho
Upendo wa Mungu hauna mwisho. Mtu anaweza akaacha kukupenda na kukusahau kabisa lakini kamwe Mungu haachi kumpenda Mtu wala hamsahau Mtu.
Hii ndio maana ya Matatizo, usiombee hili likukute
Matatizo ni nini???
`Matatizo ni pale unapokuwa umefika ukweni usiku na haja kubwa ikakubana na hukuwa unajua choo kilipo, ukatoka nje na kujisaidia kwenye majani kumbe ni mboga asubuhi ukasikia mama mkwe anasema kuna mjinga kajisaidia kwenye mboga na kaangusha pochi yake hapohapo haa! Vile unajisachi pochi hamna na kulikuwa na passport,vitambulisho, kadi ya benki, pesa zaidi ya laki 2 na nusu, funguo za nyumba yako, `
π€π€π€π€π€π€π€π€π€
Walahi haya ndo matatizoπ π π π π π
Maswali na majibu kuhusu Katekesi
1. Makatekista ni Wafanyakazi maalimu
2. Mashahidi wa moja kwa moja, Wainjilishaji wasio na mbadala
2. Kufikisha mafundisho ya Injili na kuhusika kwenye kazi za Ibada za kiliturujia na kazi za Huruma
3. Kuhubiri na kuwafundisha wakatekumeni
4. Kuelimisha vijana na watu wazima kkatika maswala ya Imani
6. Kuwatembelea wagonjwa na kuwasaidia na kuongoza Ibada za Mazishi
7. Kufundisha dini mashuleni na kuwaandaa watoto katika kupokea Sakramenti mbalimbali
8. Kutembelea Jumuiya ndogondogo kuziendeleza na kuziimarisha













































































I’m so happy you’re here! π₯³
Recent Comments