Kurani inamtaja mwanamke mmoja tu, tena mara 34: ni Mariamu, mama wa nabii Isa. Akichanganywa na dada wa Haruni na Musa, aliyekuwa na jina hilohilo, anatajwa kama binti Imrani. Pia habari nyingine kadhaa zinapishana na zile za Injili.
Hata hivyo anapewa heshima ya pekee, kama inavyoonekana katika sura ya 3:43: βNa kumbukeni malaika waliposema, βEwe Mariamu, kwa hakika Mwenyezi Mungu amekuchagua na kukutakasa na kukutukuza kuliko wanawake wa walimwenguβ. Tena katika aya 3:46: βNa kumbukeni waliposema malaika: βEwe Mariamu, bila shaka Mwenyezi Mungu anakupa habari njema za Neno litokalo kwake, jina lake Masihi Isa mwana wa Mariamu, mwenye heshima katika dunia na ahera, na yu miongoni mwa waliokaribishwaββ.
Aliambiwa amefanywa βisharaβ pamoja na mwanae, ingawa haisemwi ni ishara ya nini. Sura ya 19, yenye jina lake, inaeleza kwamba Malaika Jibrili (Gabrieli) akimpasha habari ya mimba alisema, βHakika mimi ni mjumbe wa Mola wako ili nikupe mwana mtakatifuβ. Akasema, βNinawezaje kupata mtoto hali hajanigusa mwanamume yeyote, wala mimi si mwasherati?β Akasema, βNi kama hivyo; Mola wako amesema: Haya ni rahisi kwangu, na ili tukufanya ishara kwa mwanadamu na rehema itokayo kwetu, na ni jambo lililokwisha hukumiwaβ β (19:19-21). βNa mwanamke yule aliyejilinda tupu yake na tukampulizia roho yetu na tukamfanya yeye na mwanawe ishara kwa walimwenguβ (21:91).
Pamoja na kusifiwa kwa usafi wake, anaongezewa sifa za imani na unyenyekevu: βNa Mariamu binti Imrani aliyejilinda uchi wake, na tukampulizia humo Roho yetu na kayasadikisha maneno ya Mola wake, na vitabu vyake; na alikuwa miongoni mwa wanyenyekevuβ (66:12).
References:
Google ScholarResearchGateSemantic ScholarAckySHINE
Upendo wa Mungu haukosei kamwe.
Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu
Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine
Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia
Hata chembe ya haradali ya imani inaweza kusogeza milima