Nukuu za Dini

Upendo mkuu wa Yesu

Fikiria umenunua zawadi nzuri ya gharama sana na unataka kumpa mtu umpendaye sana. Akipokea zawadi yako unafurahi sana, akikataa kuipokea zawadi inaumiza sana, lakini inaumiza zaidi akiipokea kisha akaitupa mbele yako na kuona haina maana. Hiki ndicho kinachotokea kwa Yesu. Yesu yupo kwa ajili ya kutupa zawadi ya Wokovu alyogharamia kwa uhai wake. Tunapoipokea tunamfurahisha sana, tukiikataa tunamhuzunisha na tunapoipokea na kuiacha baadae tunamhuzunisha kwelikweli.

Maana ya kubarikiwa

Kubarikiwa ni Kutokutindikiwa na kuwa na matumaini ya siku zijazo. Kubarikiwa ni kuwa na amani, furaha, na matumaini katika maisha ya sasa na yajayo. Kubarikiwa sio kuwa na mali nyingi. Yesu hajawahi kumwambia mtu kuwa utakua tajiri sana kwa kuwa umebarikiwa wala hajawahi kumuahidi kumpa mtu utajiri. Unaweza ukawa na mali nyingi lakini zikakufanya ukakosa Amani, furaha na matumaini ya siku zijazo. Ndiyo maana Mungu anatupa kulingana na vile tunavyohitaji ili visiwe mtego kwetu.

Mnyororo wa Baraka za Mungu

Usiache kusali na kutenda mema kwa kuwa huwezi jua ni watu wangapi wanategemea sala na matendo yako mema. Kumbuka Mungu alimwambia Abraham kama akikuta Wacha Mungu wengi hataiharibu Sodoma na Gomora. Vivyo hivyo Inawezekana wapo watu wengi wanaonufaika na Sala na matendo yako, hasa watu wako wa karibu uwapendao. Unapokuwa mtu wa Sala na mcha Mungu unabarikiwa wewe na wale wa karibu yako. KAMWE USIACHE KUMCHA MUNGU NA KUSALI. Ukiwa mregevu ni sawa na unakata Mnyororo wa Baraka za Mungu kwako na wenzako.

Toba, msamaha na Baraka

Inashangaza kwa sasa watu wengi hawapendi kuambiwa kuhusu kutubu dhambi zao bali wanataka waambiwe watabarikiwa. Kama vile wewe huwezi kumvika mwanao nguo nzuri kabla ya kumuogesha vivyo hivyo na Mungu hawezi kukubariki kabla ya kukutakasa. Unapotubu unasamehewa na kutakaswa dhambi zako kisha unakua umefungua milango ya baraka. Huwezi kubarikiwa bila kutubu kweli.

Mungu ni zaidi ya Mzazi na upendo wake ni zaidi ya wa Wazazi

Wakati wazazi waliweza kuaamua kuzaa mtoto tuu, Mungu yeye alikuchagua wewe utungwe mimba na kukulinda ungali tumboni mwa mama yakoโ€ฆ.Wakati wazazi wanasubiri kwa shauku kuona muonekano wako wewe, Mungu anawaweka wajukuu wa wazazi wako/ watoto wako ndani mwakoโ€ฆ. Wakati wazazi wakitafuta chakula kwa ajili yako, Mungu yeye aliwawezesha kukipataโ€ฆ. Wakati wazazi wakingoja kuona unavyoendelea kukua huku wakiwaza hatima ya maisha yako Mungu anakuendeleza na alishapanga maisha yako tangu alipokuchagua uwe mtu ukiwa tumboni mwa mama yakoโ€ฆ. Wazazi wanaweza kukuombea kwa Mungu lakini Mungu ndiye anayeamua akufanyie nini maana Wewe ni wa kwakeโ€ฆ.Wewe na wazazi wako ni watoto wa Baba mmoja ambaye ndiye Mungu.

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About