Mafundisho ya Msingi ya Kanisa Katoliki: Makala za Katoliki

MITAGUSO MIKUU YA KANISA KATOLIKI

MITAGUSO MIKUU

Yesu Kristo aliwakabidhi mitume kumi na wawili uongozi wa Kanisa wakiwa kundi moja lenye mkuu wake, yaani Petro. Vilevile waandamizi wao, yaani maaskofu wote, ni kundi moja na Papa wa Roma ndiye mkuu wao. Huyo peke yake, na kundi la maaskofu likiwa pamoja naye na chini yake, ndio wenye mamlaka ya juu katika Kanisa lote. Mamlaka hiyo inatumika kwa namna ya pekee unapofanyika mtaguso mkuu, yaani mkutano maalumu wa maaskofu uliokubaliwa na Papa kuwa unawakilisha kundi hilo lote. Hakuna uamuzi wa kudumu kuhusu ipi ni mikuu kati ya mitaguso yote iliyofanyika katika historia ya Kanisa. Tangu karne XVI Wakatoliki wataalamu wa sheria za Kanisa wanatoa orodha yao, ambayo kwa sasa ni kama ifuatavyo.

ORODHA YA MITAGUSO MIKUU

• Katika milenia ya kwanza ilifanyika mashariki (Uturuki wa leo):
1. Nisea I (mwaka 325)
2. Kostantinopoli I (381)
3. Efeso (431)
4. Kalsedonia (451)
5. Kostantinopoli II (553)
6. Kostantinopoli III (680-681)
7. Nisea II (787)
8. Kostantinopoli IV (869-870)
• Katika milenia ya pili ilifanyika magharibi (Italia, Ufaransa, Ujerumani, Uswisi na Vatikano ya leo):
9. Laterano I (1123)
10. Laterano II (1139)
11. Laterano III (1179)
12. Laterano IV (1215)
13. Lyon I (1245)
14. Lyon II (1274)
15. Vienne (1311-1312)
16. Konstanz (1414-1418)
17. Firenze (1431-1445)
18. Laterano V (1512-1517)
19. Trento (1545-1563)
20. Vatikano I (1869-1870)
21. Vatikano II (1962-1965)

HISTORIA YA MITAGUSO MIKUU

Mitaguso mikuu ya kwanza ilifanyika hasa ili kubainisha katika mafundisho yaliyogongana yapi yanalingana na imani sahihi. Mwisho wake ulikuwa kutangaza dogma fulani na kutenga na Kanisa watakaokataa kuiamini na watakaofundisha tofauti.
Mitaguso iliyofanyika baada ya farakano la mwaka 1054 kati ya Kanisa la mashariki na la magharibi, pamoja na kulenga umoja uliovunjika na kufundisha dogma mpya, ilishughulikia zaidi urekebisho wa Kanisa katika ngazi na nyanja zote. Kwa namna ya pekee Mtaguso II wa Vatikano tangu uitishwe ulijulikana kuwa wa kichungaji, yaani usio na lengo la kufundisha dogma mpya wala kulaani mafundisho mengine.

Mtaguso I wa Nisea (325)

Mtaguso I wa Nisea ndio mtaguso wa kwanza kuitwa (tangu mwaka 338) mtaguso wa kiekumeni, yaani mtaguso wa dunia yote au mtaguso mkuu. Ndiyo sababu inashika nafasi ya pekee kati ya mitaguso yote.
Uliitishwa na kusimamiwa na kaisari Konstantino Mkuu, aliyehofia mabishano kati ya raia wake Wakristo kuhusu Yesu Kristo, ambayo yalihatarisha umoja na usalama wa Dola la Roma lililoanza kuelekea kusambaratika. Yeye aliwaalika maaskofu wote wa dola, waliokuwa kama 1000 mashariki na kama 800 magharibi. Washiriki walitokea hata nje ya dola hilo, kama vile Persia na Armenia. 2
Katika hali hiyo mtaguso ulianza tarehe 20 Mei 325; washiriki walikuwa kama 318, wengi wao wakitokea upande wa mashariki wa dola hilo. Upande wa magharibi uliwakilishwa na watu 4 kutoka Ulaya na 1 kutoka Afrika. Papa Silvesta I (314-335) aliwakilishwa na mapadri wawili.
Asili ya mabishano ilitokea katika Kanisa la Aleksandria (Misri), ambapo kasisi Arios alikuwa amekanusha umungu wa Yesu, na hivyo alihukumiwa na Sinodi ya Aleksandria ya mwaka 321, iliyoitishwa na askofu Aleksanda wa Aleksandria. Hata hivyo Arios hakuacha mafundisho yake, akakimbilia Palestina kwa rafiki yake Eusebio wa Nikomedia.
Basi, mtaguso ulikiri karibu kwa kauli moja kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu kwa maana ana ousìa (yaani dhati) ileile ya Kimungu aliyonayo Baba. Ndiyo kiini cha Kanuni ya imani ya Nisea iliyopitishwa na mtaguso.
Uamuzi mwingine wa mtaguso ulikuwa kupanga siku ya Pasaka, sherehe kuu ya Kanisa, iwe Jumapili inayofuata mbalamwezi ya kwanza ya majira ya Springi, tofauti na kalenda ya Kiyahudi. Pia zilitungwa kanuni 20 kuratibu mambo mbalimbali.
Mtaguso ulipomalizika tarehe 25 Julai 325, Konstantino alifikiri uamuzi juu ya dogma utamaliza mabishano, lakini haikuwa hivyo, kwa sababu Wagiriki wengi, ingawa hawakukubaliana na Arios, hawakuridhika na msamiati uliotumika kuelezea uhusiano wa Baba na Mwana.

Mtaguso I wa Konstantinopoli (381)

Mtaguso I wa Konstantinopoli ndio wa pili kati ya mitaguso ya kiekumene yaliyofanyika wakati wa mababu wa Kanisa. Uliitishwa na kaisari Theodosius I ukafanyika Konstantinopoli mwaka 381.
Maaskofu 150 waliohudhuria walilaani aina mbalimbali za uzushi, hasa ule wa Masedoni wa Konstantinopoli aliyekanusha umungu wa Roho Mtakatifu, wakathibitisha maamuzi ya mtaguso mkuu wa kwanza (Mtaguso I wa Nisea), uliofanyika mwaka 325.
Hivyo walikiri kwamba Roho Mtakatifu pia, kama vile Yesu Mwana wa Mungu, anachanga dhati ileile ya Baba.
Pamoja na hayo, walikamilisha kanuni ya imani ya Nisea ambayo kwa sababu hiyo inaitwa sasa kanuni ya imani ya Nisea-Konstantinopoli na ambayo inatumika sana hata leo katika madhehebu mbalimbali ya Ukristo, hasa katika liturujia.

Mtaguso wa Efeso (431)

Mtaguso wa Efeso unahesabiwa na Wakristo walio wengi kama mtaguso mkuu wa tatu. Ulifanyika Efeso katika mkoa wa Asia Ndogo, kwa amri ya kaisari Theodosi II; Papa Selestini I (422-432) alimteua Sirili wa Aleksandria kuuendesha; washiriki walikuwa zaidi ya 150 na kujadili vikali hasa uzushi wa Nestori wa Konstantinopoli.
Patriarki huyo alikuwa anasisitiza ubinadamu wa Yesu Kristo kuliko umungu wake, akisema Bikira Maria alimzaa mtu Yesu, si Mungu, wala si Neno wa Mungu aliyehifadhiwa ndani ya nafsi ya Kristo kama hekaluni. Kwa hiyo Kristo alikuwa Theophoros, yaani “mbeba Mungu”, na Maria Christotokos, “Mama wa Kristo” si Theotokos, “Mama wa Mungu”.
Mtaguso huo ulilaani haraka mafundisho hayo ukikiri kwamba nafsi ya Yesu Kristo ni moja tu, ile ya milele ya Mwana wa Mungu, na kwamba nafsi hiyo ilitwaa ubinadamu kamili wenye mwili na roho. Hivyo Maria ni Theotokos kwa kuwa alimzaa Mungu kama binadamu.
Wajumbe wa Papa walipofika walithibitisha uamuzi huo, lakini maaskofu kutoka Antiokia hawakuridhika, na uzushi huo uliendelea Mesopotamia na kuenea hata Asia mashariki.
Mtaguso ulitangaza kuwa Kanuni ya Imani ya Nisea-Konstantinopoli ni kamili ukakataza isibadilishwe kwa namna yoyote. Pia ulilaani Upelaji, uzushi kutoka Ulaya magharibi kuhusu uwezo wa binadamu kutenda mema bila kusaidiwa na neema ya Mungu.

Mtaguso wa Kalsedonia (451)

Mtaguso wa Kalsedonia (leo katika nchi ya Uturuki) unahesabiwa na Wakristo wengi kuwa wa nne kati ya mitaguso ya kiekumeni iliyofanyika katika historia ya Kanisa.
Mtaguso huo uliitishwa na kaisari Marcianus wa Dola la Roma Mashariki pamoja na mke wake Pulkeria wa Bizanti miaka 20 baada ya Mtaguso wa Efeso.
Hao waliona haja ya kudumisha umoja wa Wakristo, uliokuwa msingi wa uimara wa dola hilo, hasa wakati huo ambapo makabila yasiyo na ustaarabu kutoka Asia yalikuwa yanajaribu kuteka Ulaya.
Umoja huo uliingia hatari ya kuvunjika kutokana na uamuzi wa mtaguso mkuu wa Efeso kuhusu imani sahihi juu ya Yesu Kristo kutoeleweka kwa namna moja.
Hasa baadhi ya walioshinda mtaguso huo walionekana kusisitiza mno umungu wake hata kutia shaka kama wanaamini sawasawa ubinadamu wake.
Vikao vilianza tarehe 8 Oktoba 451 vikiwa na washiriki zaidi ya 350: mara nyingi inatajwa idadi ya 600 hivi. Hatimaye mafundisho ya Eutike na Dioskoro wa Aleksandria yalilaaniwa.
Ufanisi wa mtaguso ulichangiwa na msimamo wa kaisari Valentiniano III wa Dola la Roma Magharibi, binamu wa Pulkeria. Kaisari huyo alimuunga mkono Papa Leo I (440-461) aliyekuwa ametoa msimamo wake na wa Kanisa la Roma tangu mwaka 449 katika Tomus ad Flavianum, yaani Waraka kwa Flaviano, Patriarki wa Konstantinopoli aliyeuawa na wafuasi wa Eutike. 3
Ingawa msimamo huo wa kati ulikubaliwa na wengi, wengine waliuona ni kinyume cha uamuzi wa Efeso, hivyo walishikilia sana mtazamo hao hata walipodhulumiwa na serikali. Ndiyo asili ya farakano la Misri, Syria, Armenia n.k. linalodumu hata leo.
Mtaguso huo ulitunga pia kanuni mbalimbali, kama vile kwa kumpatia Patriarki wa Konstantinopoli nafasi ya pili kati ya maaskofu wote.

Mtaguso II wa Konstantinopoli (553)

Mtaguso II wa Konstantinopoli uliitishwa na kaisari Justiniani I mwaka 553 kwa lengo la kupatanisha tena na Kanisa Katoliki Wakristo wote wa Misri, Syria n.k. waliojitenga miaka 100 iliyopita kufuatana na Mtaguso wa Kalsedonia.
Kwa ajili hiyo kaisari huyo alifanya yalaaniwe maandishi ya Wanestori watatu (Teodoro wa Mopsuestia, Teodoreto wa Kiro na Iba wa Edesa) yaliyochukiwa sana na Wamisri.
Pia mtaguso mkuu huo ulilaani baadhi ya mafundisho wa Origene.
Walihudhuria maaskofu 168; kati yao 11 walitokea magharibi. Kumbe Papa Vigili (537-555) na maaskofu wengine 12 wa magharibi walikataa kuhudhuria ingawa walikuwepo Konstantinopoli, ila mwaka uliofuata alikubali maamuzi ya mtaguso.
Hatimaye Papa Gregori I (590-604) aliutambua kama mtaguso mkuu kwa sababu haukuharibu kitu. Hivyo Wakristo wengi wanauhesabu kuwa wa tano kati ya mitaguso ya kiekumeni, ingawa lengo halikufikiwa, kwa kuwa Wamisri waliendelea kukataa Mtaguso wa Kalsedonia.

Mtaguso III wa Konstantinopoli (680-681)

Mtaguso III wa Konstantinopoli unahesabiwa na Wakristo wengi kuwa wa sita kati ya Mitaguso ya kiekumeni.
Kaisari Konstantino IV wa Konstantinopoli ndiye aliyeuitisha na kuuendesha kuanzia tarehe 7 Novemba 680 hadi tarehe 16 Septemba 681.
Suala kuu lililosumbua Wakristo wa karne VII lilimhusu Yesu Kristo upande wa utashi. Ulikuwa unaenea mtazamo wa kwamba hakuwa na utashi wa kibinadamu, bali ule wa Kimungu tu.
Lakini wamonaki Sofronio wa Yerusalemu na Maksimo Muungamadini walipinga vikali jaribio hilo la kuleta upatanisho wa Waorthodoksi wa Mashariki (Wamisri n.k.) kwa kumpunguza Yesu katika ubinadamu wake kamili uliosisitizwa na Mtaguso wa Kalsedonia (451).
Vilevile Papa Martin I (649-655), katika mtaguso uliofanyika Laterani, alilaani mtazamo huo, kinyume cha Kaisari na Patriarki wa Konstantinopoli.
Konstantino IV alikubaliana na Papa Agatoni (678-681), na hivyo Mtaguso III wa Konstantinopoli ulilaani rasmi mtazamo wa kwamba Yesu hakuwa na utashi wa kibinadamu.

Mtaguso II wa Nisea (787)

Mtaguso II wa Nisea uliitishwa na malkia Irene wa Bizanti mwaka 787 ili kujadili matumizi ya sanamu katika Ukristo, kutokana na ombi la Papa Adrian I (772-795).
Wakristo wengi wanauhesabu kuwa wa saba kati ya Mitaguso ya kiekumeni. Ni wa mwisho kufanyika wakati wa mababu wa Kanisa.
Mtaguso mkuu huo ulihitajika ili kumaliza mabishano makali kuhusu sanamu za Kikristo yaliyochukua zaidi ya miaka 100 hasa katika Dola la Roma Mashariki yakimalizika mwaka 843 tu.
Chanzo ni uamuzi wa kaisari Leo III wa Konstantinopoli (717-741) wa kuteketeza sanamu zote ili kujilinganisha na Waislamu waliotishia utawala wake.
Patriarki wa Konstantinopoli alilazimika kujiuzulu, lakini uamuzi wa kaisari ulizidi kupingwa hasa na wamonaki na mwanateolojia Yohane wa Damasko. Mapapa wa Roma pia walipinga uamuzi huo.
Sera ya dola ilibadilika aliposhika uongozi Irene kwa niaba ya mtoto wake mdogo Konstantino VI.
Mtaguso ulianza Konstantinopoli mwaka 786, lakini ulipoingiliwa na jeshi waliowaunga mkono maaskofu wengi waliopinga sanamu, Irene aliuhamishia Nisea ambapo vilifanyika vikao 7 kuanzia tarehe 28 Septemba 787. Cha mwisho kilifanyika katika ikulu tarehe 23 Oktoba 787.
Pamoja na maaskofu 300 hivi wa dola hilo, walihudhuria wamonaki wengi. Papa alituma mabalozi wake wawili na barua moja.
Mtaguso ulitofautisha heshima inayokubalika kwa sanamu na ibada isiyovumilika. Hoja kuu ni kwamba sanamu si kitu, ila inamwakilisha yule aliyechorwa ndani yake. Kimsingi sanamu zinakubalika kutokana na umwilisho wa Mwana wa Mungu uliomfanya atwae sura na kuonekana.
Mtaguso ulichukua pia maamuzi mbalimbali ili kurekebisha Kanisa.

Mtaguso IV wa Konstantinopoli (869-870)

Mtaguso IV wa Konstantinopoli ni jina linalotumiwa na Wakristo kwa namna tofauti, kadiri wanavyokubali au kukataa uhalali na uekumeni wa mitaguso fulanifulani.
Kanisa Katoliki linahesabu kuwa Mtaguso Mkuu IV wa Konstantinopoli ule uliofanyika tangu tarehe 5 Oktoba 869 hadi 28 Februari 870.
Uliitishwa na Kaisari Basili I wa Konstantinopoli na Papa Adrian II (867-872), kwa sababu mwisho wa ikonoklastia katika sinodi ya mwaka 843 ulikuwa umeacha athari kubwa katika Kanisa la Mashariki. 4
Patriarki Metodi wa Konstantinopoli (843-847) alijitahidi kutuliza pande zote, lakini hakufaulu.
Alipofariki, malkia Teodora, akitawala kwa niaba ya mtoto Mikaeli III, alilazimisha nafasi yake ishikwe na Ignas I, mmonaki mwenye msimamo mkali, ambaye hatimaye aliondoshwa.
Badala yake alichaguliwa mlei msomi Fosyo ambaye kwa siku chache alipewa daraja na kutawazwa, lakini kufikia Februari 859 lililotea farakano kati ya waliomkubali yeye na waliomkubali Ignas I.
Ndipo Fosyo alipojitahidi kuungwa mkono na Papa Nikolaus I (858-867), ambaye kwanza alimkubali pamoja na pendekezo la Kaisari Mikaeli III la kuitisha mtaguso uliofanyika Konstantinopoli kati ya Aprili na Agosti 861 wakihudhuria maaskofu zaidi ya 300.
Papa hakupendezwa na maamuzi ya mtaguso huo, akashindana na Kaisari kimaandishi kwa sababu za kiutamaduni na za kisiasa pia.
Hapo Fosyo alipata nguvu dhidi ya Papa akaitisha mtaguso uliovunja umoja kati ya Makanisa ya Mashariki na yale ya Magharibi mwaka 867, akithubutu kwa mara ya kwanza kumhukumu Papa kama mzushi na kutaka kumuondoa madarakani.
Kumbe Kaisari mpya alimrudisha Ignas I kuwa Patriarki na pamoja naye akamuomba Papa atume mabalozi kwa mtaguso mwingine wa kufanyika Konstantinopoli.
Mtaguso ulipoanza tarehe 5 Oktoba 869 walikuwepo tu maaskofu wakuu 5 na maaskofu wengine 7, lakini walikuwepo mabalozi wa Mapatriarki wa Antiokia na Yerusalemu (wale wa Aleksandria walifika baadaye).
Waliokuwa upande wa Fosyo walikubaliwa kuhudhuria kuanzia tarehe 7 Oktoba wakamtetea sana dhidi ya msimamo wa Papa, lakini wakashindwa na kutengwa (29 Oktoba).
Baada ya miezi mitatu mtaguso uliendelea tarehe 12 Februari 870, wakiwepo maaskofu 67 walioongezeka tena hadi kufikia 103 siku ya mwisho (28 Februari), lilipotolewa tamko la imani pamoja na kanuni 26 kuhusu teolojia na sheria, bila kutoa mafundisho mapya. Pamoja na idadi yenyewe kutokuwa kubwa sana, ni muhimu kwamba walikuwepo maaskofu wakuu 37 kati ya 40.
Kwa kuwa mtaguso huu haukukubaliwa sana huko Konstantinopoli (hasa baada ya Fosyo kurudia Upatriarki mwaka 877), na pande mbili zilishindwa zaidi na zaidi kuelewana, uliitishwa mtaguso mwingine, ambapo wafuasi wa Fosyo walikuwa ndio wengi.
Baadhi ya Waorthodoksi wanahesabu mtaguso huo mpya (879-880), uliofuta maamuzi dhidi ya Fosyo, kuwa wa kiekumeni na kuukataa ule wa miaka 10 ya nyuma. Lakini wengine hawakubali kuwa wa kiekumeni kwa sababu haukutoa mafundisho ya imani.
Ingawa wajumbe wa Papa Yohane VIII (872-882) walikubali kwanza maamuzi wa mtaguso huo ili kudumisha amani, na labda hata yeye mwenyewe, waandamizi wake waliukataa, na Fosyo mwenyewe aliondoshwa tena mwaka 886.

Mtaguso I wa Laterano (1123)

Mtaguso I wa Laterano unahesabiwa na Kanisa Katoliki mtaguso mkuu wa tisa katika historia yake, wa kwanza kufanyika Magharibi. Ulianza tarehe 18 Machi ukamalizika tarehe 11 Aprili 1123.
Mahali pake ni kwenye Kanisa Kuu la Roma (Italia) katika mtaa wa Laterano, alipokuwa anaishi askofu wake. Hukohuko baadaye ilifanyika mitaguso mingine minne ya Karne za Kati, halafu umuhimu wake ukapungua Papa alipohamia Vatikano.
Mtaguso uliitishwa na Papa Kalisti II (1119-1124) mnamo Desemba 1122, mara baada ya Mapatano ya Worms, ya kwanza kufanyika kati ya Papa na Dola Takatifu la Kirumi, iliyofurahisha sana wanakanisa, hata mwaka huo ulitajwa kuwa mwanzo wa kipindi kipya.
Mapatano hayo yalikomesha desturi ya walei kuteua viongozi wa Kanisa na wa utawa, yakitenganisha shughuli za kiserikali na zile za kidini, na kukubali kwamba mamlaka ya kiroho inatokana na daraja takatifu.
Ili kuthibitisha mapatano hayo, Papa alialika Roma maaskofu wote wa Magharibi. Waliohudhuria kweli walikuwa zaidi ya 900 kati ya maaskofu zaidi ya 300 na maabati 600 hivi). Papa mwenyewe aliendesha vikao.
Hakuna hati za mtaguso, ila matunda yake. Tunachojua ni kwamba Mapatano hayo yalisomwa yakapitishwa rasmi, pamoja na kanuni 22 au 25, ambazo nyingi zilikuwa zimeshapitishwa zamani.

Mtaguso II wa Laterano (1139)

Mtaguso II wa Laterano, uliofanyika kuanzia tarehe 4 hadi 11 Aprili 1139 chini ya Papa Inosenti II (1130-1143), unahesabiwa na Kanisa Katoliki kuwa mtaguso mkuu wa kumi. Ni wa pili kufanyika Magharibi, kwenye Kanisa kuu la Roma (Italia).
Mtaguso ulihitajika kutokana na farakano lililotokea mwaka 1130 alipofariki Papa Honori II (1124-1130): hapo makardinali waligawanyika kuhusu Mapatano ya Worms, ambayo mwaka 1122 yalikuwa yamekomesha mashindano kuhusu uteuzi wa maaskofu.
Isitoshe, kulikuwa na ushindani kati ya koo mbili za Roma, yaani Frangipane na Pierleoni.
Tarehe 14 Februari 1130, makardinali 16 waliosimama upande wa familia ya Frangipane walimchagua Gregorio Papareschi, aliyejiita Papa Inosenti II. Saa chache baadaye, Pietro Pierleoni alichaguliwa na makardinali wengine na kujiita Anakleti II.
Hatimaye, kwa msaada wa Bernardo wa Clairvaux, Inosenti II alishinda na kukubaliwa na wengi, ingawa hakuweza kuhamia Roma mpaka baada ya mpinzani wake kufa (1138). 5
Mtaguso ulipaswa kurekebisha matokeo ya farakano hilo. Basi, Inosenti II alifungua kikao na kuondoa madarakani maaskofu waliomfuata mpinzani wake.
Halafu papa alikusudia kuendeleza juhudi za urekebisho za Mtaguso I wa Laterano. Hivyo zikapitishwa kanuni 30, ambazo nyingi kati yake zilikuwa za kurudia zile za zamani kuhusu usimoni, mapadri wenye wake n.k.

Mtaguso III wa Laterano (1179)

Mtaguso III wa Laterano uliitishwa na Papa Aleksanda III (1159-1181) ufanyike huko Roma mwaka 1179, kutokana na Amani ya Venezia kati ya Kaisari Federiko I wa Ujerumani na Lega Lombarda ya Italia kaskazini.
Unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na moja. Ulijadili masuala mbalimbali na kuyatungia kanuni. Kati ya maamuzi muhimu zaidi, mmojawapo ulihusu uchaguzi wa Papa, ukidai thuluthi mbili za kura za makardinali wote, bila kutofautisha haki za makundi yao matatu.

Mtaguso IV wa Laterano (1215)

Mtaguso IV wa Laterano unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na mbili.
Uliitishwa na Papa Inosenti III (1198-1216) kama kilele cha kazi yake.
Ulihudhuriwa na maaskofu zaidi ya 400 (wakiwemo mapatriarki wa Kilatini wa Konstantinopoli na Yerusalemu na wawakilishi wa wale wa Antiokia na Aleksandria), na wakuu wa watawa zaidi ya 800, mbali na mabalozi wa watawala wa nchi mbalimbali.
Mada kuu zilikuwa Vita vya msalaba, Mashindano kuhusu uteuzi wa viongozi wa Kanisa, mamlaka ya Papa, mwenendo wa makleri, mashirika ya kitawa, imani (kuhusu ekaristi n.k.) na wajibu wa Wakristo wote kupokea sakramenti ya kitubio walau mara moja kwa mwaka.
Kutokana na wingi na umuhimu wa mafundisho na maamuzi yaliyotolewa, mtaguso huo unahesabiwa kuwa kati ya ile iliyoathiri zaidi Kanisa hadi leo.

Mtaguso I wa Lyon (1245)

Mtaguso I wa Lyon uliitishwa na Papa Inosenti IV (1243-1254) tarehe 24 Juni 1245 akiwa huko Lyon (Ufaransa), alipokimbilia usalama. Waliushiriki karibu viongozi 150 wa Kanisa Katoliki, ambalo linauhesabu kuwa mtaguso mkuu wa kumi na tatu.
Baada ya mashindano makali kati ya mamlaka ya kiroho ya Papa na ile ya kisiasa ya kaisari huko Ulaya, mtaguso huo uliitishwa ili kumhukumu moja kwa moja kaisari Federiko II kuwa Mpinga Kristo.
Mtaguso ulianza tarehe 28 Juni 1245 wakiwepo maaskofu 144, halafu ukawa na vikao viwili vingine tena tarehe 5 Julai na 17 Julai. Hatimaye maaskofu walikuwa 225.
Mwanzoni papa alitangaza matatizo 5 yanayotesa Kanisa:
• kuharibika kwa imani na maadili;
• kushindwa kuikomboa Nchi takatifu (Yerusalemu ulitekwa tena na Waturuki mwaka 1244);
• kudumu kwa farakano la Waorthodoksi;
• kujitokeza hatari ya kuvamiwa na Watartari;
• kupambana na Federiko II.
Maamuzi yalitangazwa tarehe 25 Agosti tu, baada ya papa na wasaidizi wake kurekebisha miswada, yakapokewa na kufafanuliwa na vyuo vikuu. Lakini uamuzi wa kumuondoa madarakani kaisari haukuweza kutekelezwa hata kwa vita.

Mtaguso II wa Lyon (1274)

Mtaguso II wa Lyon unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na nne. Ulikusudiwa hasa kurudisha umoja kamili kati ya Wakatoliki na Waorthodoksi, uliotafutwa katika karne XIII yote.
Mnamo Februari 1274, katika ikulu ya Konstantinopoli, kaisari Mikaeli VIII ilifaulu kufanya maaskofu wengi wakiri ungamo la imani lililodaiwa na Papa Klementi IV (1265-1268).
Ndipo Papa Gregori X (1271-1276) alipoitisha mtaguso huko Lyon, ambao uhudhuriwe na wawakilishi wa Waorthodoksi ili kukamilisha umoja.
Papa Gregori X alifungua mtaguso tarehe 7 Mei 1274 akitangaza tena malengo yake matatu:
• kusaidia Wakristo wa Nchi takatifu,
• kuungana tena na Waorthodoksi,
• kurekebisha maadili ndani ya Kanisa.
Vilifuata vikao viwili tarehe 18 Mei na 4 Juni. Halafu tarehe 24 Juni ulifika na kupokewa kwa shangwe ujumbe kutoka Ugiriki, ukiundwa na maaskofu 2 na katibu wa kaisari.
Tarehe 6 Julai kilifanyika kikao cha nne kwa ajili ya muungano na hatimaye tarehe 16 Julai kile cha mwisho kilichopitisha hati mbalimbali za urekebisho. Kesho yake mtaguso ulifungwa.
Muungano haukuweza kudumu, kwa sababu, alivyoandika Papa Paulo VI (1963-1978) tarehe 19 Oktoba 1974, ulifanyika «bila kulipatia Kanisa la Kigiriki nafasi ya kutokeza kwa hiari mtazamo wake kuhusu jambo hilo. Wakristo wa Kilatini ndio waliotunga hati na matamko kufuatana na mafundisho juu ya Kanisa yaliyofafanuliwa na kupangwa magharibi». 6
Mikaeli VIII alijaribu kulazimisha raia zake wapokee mambo wasiyoyakubali kwa moyo, hata akatumia nguvu kuwadhulumu waliokataa; akilaumiwa na watu wa Roma kwa kushindwa kufanikisha muungano, akaja kutengwa na Kanisa. Alipokufa (1282), mwanae Androniko II aliyemrithi, alifuta maamuzi ya baba yake kwa ajili ya muungano.
Vilevile mipango kwa ajili ya vita vya msalaba haikutekelezwa, na hatimaye (1291) Waturuki waliteka Akri, mji wa mwisho kubaki mikononi mwa Wakristo huko Mashariki ya Kati.
Maamuzi mengine yalihusu utaratibu mpya wa kumchagua Papa kwa lengo la kuzuia uchelewaji uliojitokeza hapo nyuma, na katazo la mashirika mapya ya kitawa.

Mtaguso wa Vienne (1311-1312)

Mtaguso wa Vienne unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na tano.
Mtaguso huu ulifanyika Vienne (Ufaransa) baada ya mashindano kati ya Papa Bonifas VIII (1294-1303) na mfalme wa Ufaransa Filipo IV.
Hatimaye mwaka 1309 mwandamizi wake, Papa Klementi V (1305-1314) alikubali kubaki Avignon (leo nchini Ufaransa), karibu na himaya ya mfalme huyo.
Mapapa walibaki huko hadi mwaka 1377, waliporudi Roma.
Kwa shinikizo la mfalme, Papa alitoa hati Regnans in excelsis (12 Agosti 1308) ili kuitisha mtaguso mkuu huko Vienne tarehe 1 Novemba 1310, kwa lengo la kujadili mada 4:
• suala la Wahekalu;
• vita vya msalaba;
• hali ya imani na Kanisa kwa jumla;
• urekebisho wa Kanisa.
Mtaguso ulichelewa kuanza hadi tarehe 16 Oktoba 1311, walipokuwepo washiriki 170 hivi, ambao kati yao Wafaransa walikuwa zaidi ya thuluthi moja. Wengine walizuiwa na mfalme wa Ufaransa.
Vikao rasmi vikawa vitatu hadi Machi 1312.
Kuhusu Wahekalu, mtaguso uliamua kufuta shirika lao kama alivyopenda mfalme, bila kulifanyia utafiti wala kulitolea hukumu.
Kuhusu Vita vya Msalaba, uliamua kuvianza upya na kwa ajili hiyo kutoza zaka kwa miaka sita, lakini mfalme alijitwalia hizo pesa bila kutekeleza ahadi yake ya kuongoza vita hivyo.
Kuhusu imani, ulijadili baadhi ya mafundisho hasa ya makundi kadhaa ya watawa, lakini uamuzi ulichukuliwa baadaye tu.
Kuhusu urekebisho, ulidai haki za Kanisa ziheshimiwe na serikali za nchi. Pia ulijadili kirefu mahusiano ya ndani, hasa kati ya maaskofu, maparoko na watawa.

Mtaguso wa Konstanz (1414-1418)

Mtaguso wa Konstanz (Ujerumani) unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na sita. Uliitishwa na antipapa Yohane XXIII kwa ombi la kaisari Sigismund wa Ujerumani ukathibitishwa na Papa Gregori XII (1406-1415).
Lengo kuu lilikuwa kumaliza Farakano la Magharibi lililofikia hatua ya kuona maaskofu watatu kujidai Papa kwa wakati mmoja. Malengo mengine yalikuwa kung’oa uzushi na kurekebisha Kanisa “katika kichwa na viungo vyake”.
Hatimaye Papa Gregori XII alikubali kujiuzulu, wapinzani wake wawili waliondolewa, na Papa Martin V akachaguliwa.
Ulikuwa mtaguso muhimu kwa wingi wa waliohudhuria (makardinali 29, maaskofu 186, maabati zaidi ya 100 na wataalamu 300 hivi), muda (vikao 55) na mafanikio, ingawa majaribio yake ya mapinduzi yalishindikana, hasa ulipodai kuwa na mamlaka ya juu kuliko Papa.
Kati ya maamuzi mengine kuna hukumu dhidi ya John Wyclif na Jan Hus kama wazushi.

Mtaguso wa Firenze (1431-1445)

Mtaguso wa Firenze uliitishwa na Papa Martin V (1417-1431) mwaka wa mwisho wa uongozi wake ili kutekeleza shingo upande agizo la Mtaguso wa Konstanz la kwamba mtaguso ufanyike mara kwa mara.
Mtaguso ulianza Basel (Uswisi) chini ya Papa Eugenio IV (1431-1447), ukiwa na maaskofu wachache kulingana na mapadri na walei wenye haki ya kupiga kura.
Ingawa mtaguso ulifaulu kupatanisha wafuasi wa Hus na Kanisa, na kutoa sheria kadhaa za urekebisho kwa kibali cha Papa, baadaye ulianza kumshambulia yeye pamoja na makardinali, ukionyesha wazi wengi waliuona una mamlaka ya juu kuliko Papa, kinyume cha mapokeo.
Hapo Eugenio IV aliuvunja halafu akauhamishia Ferrara (Italia), ulipokutanika tarehe 8-1-1438, bila kujali upinzani wa wale ambao walibaki Basel na kumchagua antipapa wa mwisho, Felix V.
Huko Italia ulifika ujumbe mkubwa kutoka Konstantinopoli kwa ajili ya kurudisha umoja kati ya Kanisa Katoliki na Waorthodoksi. Kati ya wajumbe 700 kulikuwa na kaisari na patriarki wa Konstantinopoli, walioogopa Waturuki watateka mji wao (kama ilivyotokea kweli tarehe 29 Mei 1453); hivyo walihitaji msaada wa Wakristo wenzao wa magharibi.
Ferrara iliachwa kutokana na uhaba wa majengo na hofu ya tauni. 7
Mwaka 1439 mtaguso ulihamia Firenze ukafikia makubaliano ya kurudisha umoja (6-7-1439), ingawa uamuzi ukashindwa kutekelezwa kwa kiasi kikubwa kutokana na upinzani wa waumini wa Konstantinopoli.
Vilevile tarehe 22-11-1439 yalifikiwa makubaliano na Waarmenia na tarehe 4-2-1440 yale na Wamisri.
Hatimaye tarehe 24-9-1443 mtaguso ulihamia Roma kwenye Laterano. Huko yalifikiwa makubaliano ya kurudisha umoja na Wasiria kadhaa (30-4-1444) na Wakaldayo na Wamaroni wa Kupro (7-8-1445).
Hakuna hati kuhusu mwisho wa mtaguso. Lakini waliobaki Basel na kujitenga na Papa, kufikia tarehe 19-4-1449 walimkubali Nikolaus V na siku sita baadaye walifunga mkutano wao.
Mtaguso huo ulichochea Wakristo wa magharibi kutamani mawasiliano na wenzao wa Ethiopia na India, jambo lililowafanya waanze zile safari za mbali kupitia baharini zilizowafikisha Afrika Kusini na Mashariki, China na Amerika.

Mtaguso V wa Laterano (1512-1517)

Mtaguso V wa Laterano ulifanyika kuanzia mwaka 1512 hadi 1517 huko Roma. Kanisa Katoliki linauhesabu kama mtaguso mkuu wa kumi na nane.
Uliitishwa na Papa Julius II (1503-1513) ambaye alianza kuusimamia tarehe 3 Mei 1512. Baada ya kifo chake, uliendelezwa na Papa Leo X (1513-1521) hadi kikao cha 12 na cha mwisho kilichofanyika tarehe 16 Machi 1517.
Ulihudhuriwa na maaskofu 100 hivi, wengi wao wakitokea Italia. Kutofika kwa wajumbe kutoka nchi nyingine, pamoja na wengi kukosa nia ya kujirekebisha, kulichangia kufanya utekelezaji wa maamuzi ya mtaguso ushindikane.
Maamuzi hayo yalitolewa kwa hati za Papa. Mengine yanahusu mafundisho ya imani, mengine maagizo ya urekebisho wa Kanisa.
Kabla yake kilifanyika “Kitaguso” cha Pisa: kwa kuwa Papa Julius II alikuwa hatekelezi kiapo chake cha kuitisha mtaguso kwa ajili ya urekebisho, baadhi ya makardinali, wakihimizwa na watawala wa Ujerumani na Ufaransa, waliuitisha huko Pisa (Italia) kuanzia tarehe 1 Septemba 1511. Walikusanyika wachache tarehe 1 Oktoba, halafu katika kikao cha nane walimsimamisha Papa wakahamia Lyon (Ufaransa).
Papa aliitikia “kitaguso” hicho kwa hati ya tarehe 18 Julai 1511, ambayo pamoja na kukipinga na kujitetea aliitisha mtaguso mkuu ukusanyike tarehe 19 Aprili 1512 huko Laterano.
Vita vilichelewesha mwanzo wa mtaguso wenyewe hadi tarehe 3 Mei 1512, walipokusanyika katika basilika la Laterano makardinali 15, mapatriarki 2, maaskofu wakuu 10, maaskofu 56, maabati na wakuu wa mashirika ya kitawa wachache pamoja na mabalozi wa nchi 3. Mwisho walikuwepo makardinali 23 na maaskofu 122.
Upande wa matokeo, utekelezaji wa maagizo ya mtaguso ulikuwa mdogo sana, la sivyo pengine Matengenezo ya Kiprotestanti yasingetokea. Ukweli ni kwamba Martin Luther aliyaanzisha miezi sita tu baada ya mtaguso kwisha.

Mtaguso wa Trento (1545-1563)

Mtaguso wa Trento (uliofanyika kwa kwikwi kuanzia mwaka 1545 hadi 1563), unahesabiwa na Kanisa Katoliki kuwa mtaguso mkuu wa kumi na tisa.
Mtaguso huo, uliochukua muda mrefu kuliko yote ya historia, ulieneza urekebisho wa Kanisa na kuchukua msimamo kuhusu mafundisho ya Waprotestanti waliojitokeza katika hiyo karne XVI.
Mtu wa kwanza kulilia mtaguso ambao uamue kati yake na papa alikuwa Martin Luther (1517): huko Ujerumani ombi lake liliungwa mkono na wengi, pamoja na kaisari Karolo V aliyeuona kuwa njia ya kurekebisha Kanisa lakini pia ya kujiimarisha kimamlaka. Ndiyo sababu kuu iliyomfanya Papa Klementi VII (1523-1534), aliyesimama upande wa Ufaransa, kukataa kabisa kuuitisha.
Wazo hilo lilipata nguvu tena chini ya mwandamizi wake, Papa Paulo III (1534-1549), ambaye mwaka 1536 aliitia kwanza Mantova halafu Vicenza maaskofu na maabati wote, pamoja na wafalme wadogo wengi wa Dola takatifu la Kijerumani.
Baada ya juhudi mbalimbali kushindikana, mwaka 1542 uamuzi ulifikiwa wa kuitisha mtaguso huko Trento kwa sababu ni mji wa Italia lakini ulikuwa ndani ya mipaka ya dola hilo. Hatimaye (Novemba 1544) papa aliweza kutoa hati ya kuitisha mtaguso inayoitwa Laetare Jerusalem.
Mtaguso ulifunguliwa rasmi tarehe 13 Desemba 1545 katika kanisa kuu la Mt. Vigilio.
Mwanzoni mtaguso ulikuwa na maaskofu wachache, karibu wote kutoka Italia, ukatawaliwa na wajumbe wa papa. Kati ya makardinali wapya (Contarini, Sadoleto, Carafa, Fisher na huyo Pole) wengi walipenda urekebisho.
Zilijadiliwa na kupitishwa hasa dogma dhidi ya mafundisho ya Waprotestanti, kama vile kuhusu utakaso na wokovu. Pamoja na kupitisha tafsiri rasmi ya Biblia katika Kilatini iliyo maarufu kwa jina la Vulgata, kati ya maamuzi muhimu zaidi upo ule wa kudai maaskofu waishi katika majimbo yao ili kufanya uchungaji uliowapasa.
Baada ya mtaguso kuhamishiwa Bologna, Papa Paulo III aliusimamisha mnamo Septemba 1549.
Papa Julius III (1550-1555) aliuitisha tena kuanzia tarehe 1 Mei 1551 na zikatolewa hati juu ya sakramenti za Ekaristi, Kitubio na Mpako wa wagonjwa. Polepole waliohudhuria waliongozeka, 8
wakiwemo Waprotestanti wengi pia, wakidai wanateolojia wao wawe na haki ya kupiga kura na hati zilizokwishatolewa zifutwe. Ndipo ilipoonekana wazi kwamba tofauti katika imani ni kubwa mno.
Majeshi ya Kiprotestanti yalipokaribia Trento, Papa alikubali kusimamisha tena mtaguso tarehe 28 Aprili 1552.
Sehemu ya mwisho ya mtaguso baada ya kuitishwa ilichelewa kuanza hadi tarehe 18 Januari 1562, tena ilikabili matatizo mengi, lakini iliokolewa na kutawaliwa na askofu wa Milano Karolo Borromeo, mpwa wa Papa Pius IV (1559-1565) aliyemalizia haraka mtaguso wakiwemo wajumbe 255.
Katika sehemu hiyo yalitolewa mafundisho rasmi kuhusu Misa, Daraja takatifu na Ndoa, Toharani, sala kwa watakatifu, heshima kwa masalia na rehema. Pia Kanisa la Roma lilikubaliwa kama mama na mwalimu wa makanisa yote. Maaskofu wote walitakiwa kuahidia utiifu kwa Papa, ambaye peke yake ana haki ya kuitisha mtaguso mkuu. Kwa msingi huo, mtaguso ulimuachia Papa kuthibitisha maamuzi yote, naye alifanya hivyo bila kujali upinzani wa maofisa wake huko Roma.
Isitoshe, mwishoni, maamuzi mbalimbali yaliachwa mikononi mwa Papa na ofisi zake, yakachukuliwa miaka iliyofuata; kati yake, urekebisho wa Breviari na Misale, kwa kusawazisha liturujia za majimbo ya magharibi (isipokuwa chache, kama ya Milano na Lyon) kulingana na mapokeo ya Roma. Halafu ikatolewa Katekisimu ya Trento na Orodha ya vitabu vilivyokatazwa (Index librorum prohibitorum).

Mtaguso I wa Vatikano (1869-1870)

Mtaguso I wa Vatikano unatazamwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa ishirini katika historia yake.
Uliitishwa rasmi na Papa Pius IX (1846-1878) mnamo 29 Juni 1867 na vikao vyake viliendelea katika Basilika la Mt. Petro huko Vatikano mjini Roma kuanzia tarehe 8 Desemba 1869 hadi vilipokatika mnamo 1870, kutokana na jeshi la Italia kuteka Roma tarehe 20 Septemba.
Walishiriki maaskofu na mapadri 774 (kati ya 1050 wenye haki ya kuhudhuria), ambao kwa mara ya kwanza walitokea mabara yote. Pia ilikuwa mara ya kwanza ya kutokuwepo wawakilishi wa serikali. Kumbe wajumbe wa Waorthodoksi na wa Waprotestanti walialikwa pia, lakini hawakufika.
Tarehe 24 Aprili 1870, baada ya majadiliano mengi, ilipitishwa hati Dei Filius juu ya Mungu, ufunuo, imani, na uhusiano kati ya imani na akili.
Ingawa lengo halikuwa hilo, tokeo kuu la kazi ya mtaguso huo ni tangazo la dogma ya Papa kuwa na karama ya kutokosea katika mafundisho ya imani na maadili anayoyatoa ili yadumu moja kwa moja pale anapotimiza masharti fulani (kwa kifupi: akisema “ex cathedra”, yaani “kutoka ukulu).
Dogma hiyo iliimarisha mamlaka ya Papa na umoja wa Kanisa dhidi ya maelekeo ya kitaifa ambayo yalitawala karne zilizotangulia yakisababisha matatizo mengi.

Mtaguso II wa Vatikano (1962-1965)

Malengo ya Mtaguso II wa Vatikano

Muda mfupi baada ya kuchaguliwa Papa, mwenye heri Yohane XXIII alitangaza uamuzi wake wa kuitisha mtaguso mkuu akiamini kwamba utaweza kuandaa na kusababisha ustawi mpya wa maisha ya Kanisa. Lengo kuu la mtaguso lilikuwa kuliamsha Kanisa likumbuke wito wake na kwa kujifanya upya kwa ndani lipate msukumo mpya wa kimisionari ili kuwatangazia watu wote ujumbe wa milele wa wokovu, amani na umoja.
Tangazo hilo lilitolewa tarehe 25-1-1959. Baada ya maandalizi, Mtaguso II wa Vatikano ulifunguliwa tarehe 11-10-1962. Vikao vinne vikafanyika mpaka ulipofungwa tarehe 8-12-1965. Kila kikao kilianza Oktoba na kumalizika Desemba ya miaka hiyo.
Kwa kuwa Yohane XXIII alifariki tarehe 2-6-1963, vikao vitatu vya mwisho viliongozwa na mwandamizi wake, Paulo VI, na hati zote kumi na sita zikatolewa chini yake pia kwa kupigiwa kura ya ndiyo karibu kwa kauli moja. Maaskofu na wakuu wa mashirika kadhaa wenye haki ya kupiga kura walikuwa kama elfu tatu, wakiwakilisha karibu Kanisa lote duniani, isipokuwa nchi zile zenye kuwadhulumu Wakristo.

Heshima za Liturujia kwa Bikira Maria

Kuna ibada za Mama Bikira Maria zinazoadhimishwa katika liturujia ya Kiroma. Hapa zimepangwa kulingana na heshima zinavyozidiana:
Sherehe
8 Desemba – Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili 1 Januari – Bikira Maria Mama wa Mungu 25 Machi – Bikira Maria Kupashwa Habari 15 Agosti – Bikira Maria Kupalizwa Mbinguni

Sikukuu

31 Mei – Maamkio ya Bikira Maria 8 Septemba – Kuzaliwa kwa Bikira Maria

Kumbukumbu

Juni – Moyo Safi wa Maria 15 Septemba – Mama Yetu wa Huzuni 22 Agosti – Bikira Maria Malkia 7 Oktoba – Bikira Maria wa Rozari 21 Novemba – Bikira Maria Kutolewa Hekaluni

Kumbukumbu za Hiari

11 Februari – Bikira Maria wa Lurdi 13 Mei – Bikira Maria wa Fatima 16 Julai – Bikira Maria wa Mlima Karmeli 5 Agosti – Kutabaruku Kanisa la Bikira Maria 12 Septemba – Jina takatifu la Maria 12 Desemba – Bikira Maria wa Guadalupe
Tena kila Jumamosi isiyo na adhimisho maalumu, Kanisa huadhimisha kumbukumbu ya Mama wa Mungu.
Pia zipo heshima za binafsi kwa Bikira Maria: mashariki zinatumika tenzi na nyimbo mbalimbali, k.mf. Akatistos inayomuita “daraja linalounganisha dunia na mbingu”, “ngazi aliyoiona Yakobo” “kina kisichochunguzika kwa macho ya malaika” (Mwa 28:12); magharibi]] anaheshimiwa kwa rozari.
Wakristo wanaomheshimu Bikira Maria hawamuabudu hata kidogo, lakini wanamtolea heshima ya juu kuliko watakatifu wengine. Tofauti ni kwamba Mungu tu anastahili kuabudiwa (kwa Kigiriki, ‘latria’) watakatifu wanapewa heshima (‘dulia’) na Bikira Maria heshima zaidi (‘yuper-dulia’). Kanisa Katoliki linakiri neema zote za Mungu zinampitia Maria.

Unayopaswa kujua Kuhusu Kipindi cha Majilio

Majilio (pia: Adventi ) ni kipindi cha liturujia ya
madhehebu mbalimbali ya Ukristo (kama vile
Kanisa Katoliki, ya Waorthodoksi , Waanglikana
na Walutheri ) kinatangulia sherehe ya Noeli na
kuanza mwaka wa liturujia. Kinaweza kudumu
kati ya siku 22 na 40.
Jina lake kwa Kilatini ni adventus maana yake
ujio (wa Yesu Kristo ), lakini jina la Kiswahili ni
sahihi zaidi kwa sababu linadokeza kuwa ujio
wa Yesu ni kwa ajili yetu na kuwa alikuja
zamani, anakuja kila siku na atakuja kwa
utukufu mwisho wa dunia.
Maana ya Majilio katika
maisha ya binadamu
Sisi binadamu hatuwezi kuishi daima katika
hali ileile bila ya matazamio. Hasa kijana
anatarajia mambo mapya tena mema. Hivyo
tunajitahidi kuyapata. Asiyetazamia chochote
amevunjika moyo, hana hamu ya kuishi. Lakini
matazamio ya kibinadamu yakimfikia mtu
hayamridhishi moja kwa moja. Kristo tu
anatimiza hamu zote kwa kumkomboa kutoka
unyonge. Majilio yanatukumbusha kila mwaka
matarajio ya kweli na hivyo yanaamsha hamu
ya kuishi kwa bidii ya kiroho.
MAJILIO: Katika Kanisa la Roma.
Katika mwaka wa liturujia ya Kanisa la Roma ,
sherehe ya Noeli inaandaliwa na kipindi cha
Majilio ambacho kina mambo mawili:
kinakumbusha Mwana wa Mungu alivyotujilia
mara ya kwanza, na papo hapo kinatuandaa
kumpokea atakapotujilia tena siku ya mwisho .
Kufuatana na hayo kina sehemu mbili: hadi
tarehe 16 Desemba kinahusu zaidi kurudi kwa
Bwana; siku nane za mwisho kinatuelekeza
moja kwa moja kuadhimisha kuzaliwa kwake.
Urefu wa Majilio unategemea siku
inayoangukia Noeli, kwa kuwa ni lazima yawe
na Jumapili nne. Hivyo basi yanaanza kwa
Masifu ya Jioni ya kwanza ya Jumapili
inayoangukia tarehe 30 Novemba au tarehe ya
jirani zaidi; yanakwisha kabla ya Masifu ya
Jioni ya kwanza ya Noeli.
Kwa jumla ni kipindi cha toba: rangi yenyewe
ni zambarau; haziruhusiwi sherehe za fahari;
ala za muziki na maua vinaweza kutumika
kwa kiasi tu. Masharti hayo yanalegezwa
katika Jumapili ya tatu kwa sababu ya furaha
ya kuona tunakaribia sherehe yenyewe.
Katika kipindi hicho tunaadhimisha tumaini la
Israeli lililotimizwa Yesu alipokuja katika
unyenyekevu wa umbile letu; pia tunangojea
arudi kwa utukufu. Kama alivyotekeleza ahadi
mara ya kwanza, atazitekeleza pia mara ya
pili, ingawa kwake miaka elfu ni kama siku
moja tu. Kati ya majilio hayo mawili, Bwana
anatujilia mfululizo kifumbo katika sakramenti
(hasa ekaristi ) na katika maisha ya kila siku
kwa njia ya matukio na watu (hasa maskini ).
Basi tunapaswa kuwa tayari daima kumpokea
ili siku ya mwisho tukamlaki, naye
atukaribishe kwenye uzima wa milele. Pia
tunapaswa kumuomba aje kutukomboa, yeye
aliye tumaini letu.
Katika safari ya Majilio watu watatu
wanatuongoza tukutane na Yesu:
1. Isaya
nabii wa tumaini, mwenye kipaji cha kutokeza
matazamio ya binadamu na kumhakikishia
atatimiziwa na Mwokozi
. 2. Yohane Mbatizaji ,
mwenye kuhimiza toba kwa kuwa tunapaswa
kupindua maisha yetu ili tukutane vema na
Kristo.
3. Maria , bikira aliyekuwa tayari
kumpokea Masiya kwa upendo na kushirikiana
naye katika kutimiza mpango wa wokovu .
Tukiwafuata hao watatu tunaweza kujipatia
maadili yale yanayotuandaa kumpokea
Mwokozi anapotujilia: ndiyo matunda maalumu
tunayotarajiwa kuyachuma wakati wa Majilio:
1. Kukesha katika imani, sala na kutambua
ishara za Bwana kutujilia katika nafasi yoyote
ya maisha na mwishoni mwa nyakati.
2.Kuongoka kwa kufuata njia nyofu.
3.Kushuhudia furaha inayoletwa na Yesu kwa
kuwa na upole na uvumilivu kwa wenzetu, kwa
tumaini la kuwa bidii zetu zinawahisha ufalme
wa Mungu wenye heri isiyo na mwisho.
4. Kutunza unyenyekevu kwa kufuata mifano ya
maskini wa Injili ambao ndio waliompokea
Mkombozi .
kwa mambo mengi mengine ya dini tembelea
https://ludovicktmedia.blogspot.com/

Ni nini maana ya Ekaristi Takatifu katika imani ya Kanisa Katoliki?

Ekaristi Takatifu ni moja ya Sakramenti muhimu katika imani ya Kanisa Katoliki. Sakramenti hii huadhimishwa kwa kutumia mkate na divai, ambavyo vinageuka kuwa mwili na damu ya Yesu Kristo. Ni matukio muhimu sana katika ibada za Kanisa Katoliki, kwa sababu Ekaristi Takatifu ni chakula cha kiroho ambacho kinawapa waumini nguvu na neema ya kumtumikia Mungu.

Kanisa Katoliki linatambua Ekaristi Takatifu kama Sakramenti, ambayo ni ishara ya uwepo wa Yesu Kristo. Kwa njia hii, mtu anayepokea Ekaristi Takatifu anakuwa na umoja na Yesu Kristo, ambaye ni Bwana wa maisha yote. Kwa hiyo, Ekaristi Takatifu ni chanzo cha maisha ya kiroho ya kila Mkristo.

Ekaristi Takatifu pia ina maana ya kumbukumbu ya kifo cha Yesu Kristo msalabani. Kristo alitia damu yake kwa ajili ya wokovu wa wanadamu wote. Kwa hiyo, kila tunapoadhimisha Ekaristi Takatifu, tunakumbuka dhabihu ya Kristo na tunashukuru kwa ajili ya upendo wake kwetu sisi.

Kwa mujibu wa Kitabu cha Matendo ya Mitume 2:42, Kanisa la mwanzo lilikuwa likifanya mkutano kila siku "kwa kula chakula chao pamoja kwa furaha na kwa unyofu wa moyo, wakimsifu Mungu". Kanisa Katoliki linatambua Ekaristi Takatifu kama chanzo cha umoja na mshikamano wa waumini. Katika Ekaristi Takatifu, waumini huwa na uzoefu wa kuwa sehemu ya familia ya Mungu.

Kanisa Katoliki linatambua umuhimu wa kuenenda kwa uungwana wakati wa maadhimisho ya Ekaristi Takatifu. Kwa sababu Ekaristi Takatifu ni Sakramenti ya uwepo wa Kristo, ni muhimu kuheshimu Sakramenti hii kwa kutumia vitu vizuri, kama vile chombo cha kuwekea Ekaristi Takatifu.

Kwa kumalizia, Ekaristi Takatifu ni Sakramenti muhimu katika imani ya Kanisa Katoliki. Ni ishara ya uwepo na upendo wa Yesu Kristo, na inatupa neema ya kuwa sehemu ya familia ya Mungu. Kwa hiyo, tunapaswa kuheshimu na kuenenda kwa uungwana katika maadhimisho ya Ekaristi Takatifu. Kama inavyoelezwa katika KKK 1324, "Ekaristi ni chanzo na kilele cha maisha ya Kikristo".

Ni nini imani ya Kanisa Katoliki kuhusu sakramenti ya Kipaimara?

Sakramenti ya Kipaimara ni sakramenti ya tatu katika Kanisa Katoliki baada ya Sakramenti ya Ubatizo na Ekaristi. Ni sakramenti muhimu sana katika maisha ya Mkristo, kwa sababu inaweka muhuri wa Roho Mtakatifu na inapeana nguvu ya kushuhudia imani yetu kwa Yesu Kristo. Kwa hivyo, ni muhimu kujua imani ya Kanisa Katoliki kuhusu sakramenti hii.

Kanisa Katoliki linaamini kwamba sakramenti ya Kipaimara inaweka muhuri wa Roho Mtakatifu kwa Mkristo na inawapa nguvu kushuhudia imani yao kwa Kristo. Inafuatilia mfano wa Yesu mwenyewe aliyehitimu huduma yake kwa ubatizo wa Roho Mtakatifu (Mathayo 3:16, Marko 1:10, Luka 3:22).

Kupitia sakramenti ya Kipaimara, Mkristo anapokea nguvu ya kushuhudia imani yake kwa Kristo. Roho Mtakatifu anamwongoza, kumtia nguvu na kumwimarisha katika imani yake. Hii inampa Mkristo uwezo wa kuwa shahidi wa Kristo katika maisha yake na miongoni mwa watu wake.

Kufuatia mfano wa Yesu, Kanisa Katoliki linatambua sakramenti ya Kipaimara kama sehemu muhimu ya kujiunga na Kanisa. Ni kielelezo cha uhusiano wa kina wa Mkristo na Kristo, na pia ni kielelezo cha uhusiano wake na Kanisa.

Sakramenti ya Kipaimara pia inaunganishwa na Sakramenti ya Ubatizo kwa sababu inaendeleza kazi ya Roho Mtakatifu ambayo ilianza katika ubatizo. Kwa hivyo, Kanisa Katoliki linahimiza watu kukamilisha ubatizo wao kwa kupokea sakramenti ya Kipaimara.

Katika Catechism ya Kanisa Katoliki, tunaona kwamba sakramenti ya Kipaimara inathibitisha imani ya Mkristo na inaimarisha uhusiano wake na Kanisa. (CCC 1285). Ni sakramenti ya kudumu ambayo inatukumbusha jukumu letu la kushuhudia imani yetu kwa Kristo na kuhudumia Kanisa.

Kanisa Katoliki pia linatambua kuwa sakramenti ya Kipaimara inaunganisha Mkristo na washiriki wengine wa Kanisa. Ni kielelezo cha umoja wa kanisa na inawawezesha Wakristo kushiriki katika huduma ya Kanisa la Kristo.

Kwa kumalizia, Kanisa Katoliki linathamini sana sakramenti ya Kipaimara kama sehemu muhimu ya maisha ya Mkristo. Ni sakramenti ambayo inaweka muhuri wa Roho Mtakatifu na inawapa nguvu kushuhudia imani yao kwa Kristo. Kama Mkristo, ni muhimu kushiriki katika sakramenti hii na kuzingatia yale inayofundisha ili kuimarisha imani yetu.

Ni nini imani ya Kanisa Katoliki kuhusu sakramenti ya Upatanisho?

Kanisa Katoliki linayo imani thabiti kuhusu sakramenti ya Upatanisho. Ni sakramenti ambayo inakubaliwa na kanisa zote duniani kama njia ya kupata msamaha wa dhambi. Upatanisho unawakilisha neema kubwa ya Mungu kwa wapenzi wake, ambao wanaamua kuungana tena na Mungu kwa dhati ya mioyo yao.

Kulingana na Katekismu ya Kanisa Katoliki (CCC 1424), "Upatanisho ni sakramenti ya toba, ambayo inaruhusu waamini kupata msamaha wa dhambi zao kutoka kwa Mungu na Kanisa, na kurejeshwa katika neema ya wokovu." Kwa hivyo, sakramenti hii inawakilisha upatanisho kati ya Mungu na mwanadamu.

Waamini wa Kanisa Katoliki wanaamini kuwa sakramenti ya Upatanisho inakuja na namna tatu za toba ambazo ni: kutubu kwa kinywa, kufanya matendo ya toba na kukiri dhambi zetu kwa kuhani. Kutubu kwa kinywa ni kwa kusema au kuomba msamaha kutoka kwa Mungu, wakati kufanya matendo ya toba ni kubadili tabia zetu na kuacha kufanya mambo ambayo sio sawa. Kukiri dhambi zetu kwa kuhani ni hatua ya mwisho ya sakramenti ya Upatanisho.

Katika Biblia, Yesu alitoa mamlaka ya kufanya upatanisho kwa wafuasi wake wakati alisema: "Kama mkisamehe dhambi za mtu yeyote, zitasamehewa; na kama mkihifadhi dhambi za mtu yeyote, zitahifadhiwa " (Yohana 20:23). Kwa hivyo, Kanisa linajua kuwa kuhani ana mamlaka ya kusamehe dhambi zetu kwa jina la Yesu Kristo.

Kuna faida nyingi za kupokea sakramenti ya Upatanisho. Kwanza kabisa, inatupa upya wa maisha yetu ya kiroho na kumweka Mungu kwa nafasi yake sahihi katika maisha yetu. Pia, inasaidia katika kujenga uhusiano na wengine kwa kufanya matendo mema, badala ya kushikilia chuki au kukasirika. Kupokea sakramenti ya Upatanisho husaidia katika kufanya maisha yetu kuwa ya amani na ya furaha.

Kwa hiyo, ni muhimu kwa wapenzi wa Kanisa Katoliki kupokea sakramenti ya Upatanisho mara kwa mara, kama njia ya kudumisha uhusiano wao na Mungu na kusafisha maisha yao ya kiroho. Kwa kufanya hivi, tunaweza kukua katika imani yetu na kuwa wapenzi wazuri wa Yesu Kristo.

Ibada ya Chaplet ya Huruma ya Mungu: Sala ya Upatanisho na Ukombozi

Ibada ya Chaplet ya Huruma ya Mungu: Sala ya Upatanisho na Ukombozi

Sala ni njia ya kuwasiliana na Mungu. Kuna aina nyingi za sala ambazo zinaweza kuwasilishwa kwa Mungu. Mojawapo ya sala hizi ni Ibada ya Chaplet ya Huruma ya Mungu. Sala hii inakujia kwa ajili ya kupata upatanisho na ukombozi kutoka kwa Mungu. Katika makala hii, nitazungumzia Ibada ya Chaplet ya Huruma ya Mungu.

  1. Ibada ya Chaplet ya Huruma ya Mungu ni sala inayotumika kwa ajili ya kutafuta upatanisho na ukombozi kutoka kwa Mungu. Sala hii inaundwa na sala ya Moyo Mtakatifu wa Yesu, sala ya huruma kwa mioyo iliyokufa, na sala ya utukufu kwa Baba.

  2. Ibada hii ilianzishwa na Mtakatifu Faustina Kowalska, ambaye alikuwa mtawa wa Kanisa Katoliki. Kati ya maono yake, alipokea maono kutoka kwa Yesu kumwambia kuhusu huruma na upendo wa Mungu kwa wanadamu.

  3. Maono haya yalimwezesha kuanzisha Ibada ya Chaplet ya Huruma ya Mungu. Kwa njia hii, Mtakatifu Faustina alipata ujumbe kutoka kwa Yesu kwamba kuna uwezo wa kupata upatanisho na ukombozi kwa Mungu kupitia ibada hii.

  4. Ibada hii ni rahisi sana kufuata. Unahitaji kuanza kwa kusali sala ya Baba Yetu, sala ya Moyo Mtakatifu wa Yesu, na sala ya huruma kwa mioyo iliyokufa. Baada ya hapo, unafanya sala ya Chaplet, ambayo ni sala ya kujibu kwa huruma ya Mungu.

  5. Katika Ibada hii, Yesu anafundisha kwamba sala ya huruma ya Mungu inaweza kuwakomboa wote. Unapotafuta huruma ya Mungu, unashirikiana na Yesu katika kazi yake ya upatanisho na ukombozi.

  6. Katika Biblia, tunaona jinsi Mungu alivyotenda kwa kutoa upatanisho kwa wanadamu wote. Yohana 3:16 inasema, "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele."

  7. Kwa mujibu wa Catechism ya Kanisa Katoliki, sala ni njia ya kuwasiliana na Mungu. Sala ya Ibada ya Chaplet ya Huruma ya Mungu inakupa fursa ya kufanya mazungumzo na Mungu na kupata upatanisho na ukombozi.

  8. Katika "Diary of Saint Maria Faustina Kowalska," Mtakatifu Faustina alielezea jinsi huruma ya Mungu ilivyomkomboa kutoka kwa dhambi na upendo wa Mungu ulimkomboa kutoka kwa mtego wa shetani.

  9. Katika historia ya Kanisa Katoliki, tunaweza kuona jinsi watakatifu walivyotumia sala kama njia ya kuwasiliana na Mungu na kupata upatanisho na ukombozi. Kwa mfano, Mtakatifu Padre Pio alikuwa mkubwa katika sala na alitumia sala kama njia ya kupata upatanisho na ukombozi kwa watu.

  10. Ibada ya Chaplet ya Huruma ya Mungu ni njia rahisi ya kupata upatanisho na ukombozi kutoka kwa Mungu. Ni njia ya kuwasiliana na Mungu na kumpa nafasi ya kuonyesha huruma yake. Ikiwa unataka kupata upatanisho na ukombozi kutoka kwa Mungu, jaribu Ibada ya Chaplet ya Huruma ya Mungu.

Je, umewahi kusali Ibada ya Chaplet ya Huruma ya Mungu? Je, imekuwa njia ya kutafuta upatanisho na ukombozi kutoka kwa Mungu? Shiriki mawazo yako kwenye sehemu ya maoni.

Ibada ya Novena ya Huruma ya Mungu: Kupokea Neema na Baraka

Ibada ya Novena ya Huruma ya Mungu: Kupokea Neema na Baraka

Karibu kwa Ibada ya Novena ya Huruma ya Mungu! Hii ni Ibada maalum ambayo inatufundisha kumwomba Mungu Huruma yake na kumpenda kama vile Yeye anavyotupenda. Kwa kuwa wewe ni Mkristo wa Kanisa Katoliki, unaweza kujifunza mengi kutoka kwa Novena hii kuhusu jinsi ya kuchangamana na Mungu na kupata neema na baraka zake.

  1. Ibada ya Novena ya Huruma ya Mungu ni nini?

Ibada ya Novena ya Huruma ya Mungu ni mfululizo wa sala za siku tisa ambazo zinatakiwa kusaliwa kwa ajili ya kuomba Huruma ya Mungu. Novena hii inaanza siku ya Ijumaa ya Kwanza baada ya Pasaka na inamalizika siku ya Jumapili ya Huruma ya Mungu. Kwa njia hii, tunajifunza kumwomba Mungu Huruma yake na kupokea neema na baraka zake.

  1. Kwa nini tunapaswa kumwomba Mungu Huruma yake?

Tunapaswa kumwomba Mungu Huruma yake kwa sababu sisi ni watu wa dhambi ambao hatustahili kupokea baraka zake. Kama inavyosema katika Zaburi 51:3, "Nimekiri dhambi zangu, sitaificha maovu yangu; Nitajitangaza kwa Bwana dhambi zangu." Lakini Mungu anatupenda sana na anataka tufurahie maisha yetu na kupokea neema na baraka zake.

  1. Je! Tunawezaje kupata Huruma ya Mungu?

Tunaweza kupata Huruma ya Mungu kwa kumwomba kwa dhati na kwa imani. Kama inavyosema katika Mathayo 7:7, "Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata; bisheni, nanyi mtafunguliwa." Tunapaswa kuomba Mungu kwa moyo wote wetu na kumwomba Huruma yake kwa imani.

  1. Tunawezaje kupokea neema na baraka za Mungu?

Tunaweza kupokea neema na baraka za Mungu kwa kumwomba kwa imani na kufuata amri zake. Kama inavyosema katika Yohana 15:10, "Mkiyashika maagizo yangu, mtakaa katika upendo wangu, kama vile mimi nilivyoyashika maagizo ya Baba yangu, nami nimekaa katika upendo wake." Tunapaswa kufuata amri za Mungu na kufanya yaliyo mema ili kupokea neema na baraka zake.

  1. Je! Ni nini kinachotokea tunapomwomba Mungu kwa dhati?

Tunapomwomba Mungu kwa dhati, tunapata Huruma yake na kupokea neema na baraka zake. Kama inavyosema katika Mathayo 7:8, "Kwa maana kila aombaye hupokea, naye atafutaye hupata, na bisheni mtafunguliwa." Tunapaswa kuwa na imani thabiti kwamba Mungu atatupatia yale tunayomwomba.

  1. Je! Tunaweza kuwa na uhakika wa kupokea neema na baraka za Mungu?

Tunaweza kuwa na uhakika wa kupokea neema na baraka za Mungu ikiwa tutamwomba kwa moyo wote na kufuata amri zake. Kama inavyosema katika 1 Yohana 3:22, "Nasi twapokea kutoka kwake lo lote tuombalo, kwa kuwa twatunza amri zake, na kufanya yaliyo yapendezayo mbele yake."

  1. Kwa nini ni muhimu kuomba kwa imani?

Ni muhimu kuomba kwa imani kwa sababu imani yetu ndiyo inayotutambulisha kama wana wa Mungu. Kama inavyosema katika Waebrania 11:6, "Bila imani haiwezekani kumpendeza; maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini ya kuwa yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao kwa bidii." Tunapaswa kuwa na imani thabiti ili kupata neema na baraka za Mungu.

  1. Ni nini tunaambatanisha na huruma ya Mungu?

Tunaambatanisha na Huruma ya Mungu katika Ibada ya Novena ya Huruma ya Mungu. Kama inavyosema katika Catechism ya Kanisa Katoliki, "Katika Ibada hiyo, tunaomba kwa ajili ya huruma ya Mungu kwa ajili ya kuokoa ulimwengu na kwa ajili ya ukombozi wetu wenyewe." Tunaomba kwa ajili ya ulimwengu mzima na kwa ajili ya wokovu wetu wenyewe.

  1. Ni nini kinachofuatia baada ya Ibada ya Novena ya Huruma ya Mungu?

Baada ya Ibada ya Novena ya Huruma ya Mungu, tunapaswa kuendelea kuomba kwa ajili ya Huruma ya Mungu na kufuata amri zake. Kama inavyosema katika Yohana 14:15, "Mkinipenda, mtazishika amri zangu." Tunapaswa kufuata amri za Mungu na kuishi maisha yenye haki ili kupata neema na baraka zake.

  1. Je! Unafikiri Ibada ya Novena ya Huruma ya Mungu itakusaidiaje katika maisha yako ya kiroho?

Ibada ya Novena ya Huruma ya Mungu inaweza kuwa muhimu sana katika maisha yetu ya kiroho. Kwa kumwomba Mungu kwa dhati na kufuata amri zake, tunaweza kupata neema na baraka za Mungu. Je! Unafikiri Ibada ya Novena ya Huruma ya Mungu itakusaidiaje katika maisha yako ya kiroho? Tafadhali shiriki maoni yako katika maoni ya chini. Mungu akubariki!

Thamani ya Kazi ya Upadre

UPADRE NI KAZI YA PEKEE YA HEKIMA, UWEZO NA MAPENDO YA UMUNGU WA KRISTU. KAMWE USIMSHAMBULIE PADRE. “Yesu Maria na Yosefu nawapenda, ziokoeni Roho. KUMTETA PADRE [Haya ni maelezo ya Bwana wetu kwa Mutter Vogel.] ” Kamwe mtu asimshambulie Padre hata anapokuwa katika makosa badala yake umwombee na fanya toba ili niweze kumpa tena NEEMA.
Ni yeye peke yake anaye niwakilisha mimi hata awe haishi kulingana na mimi. Endapo Padre anaanguka tumnyoshee mkono wa msaada kwa njia ya SALA na sio KUMSHAMBULIA. Ni mimi pekee nitakuwa HAKIMU wake si mwingine ila mimi”. “Mtu yeyote anapotamka HUKUMU dhidi ya padre ananihukumu mimi”. 
Mwanangu kamwe usiruhusu padre ashambuliwe, jitahidi kuwa upande wake na umtetee”. Mwanangu kamwe usimhukumu mwungamishi wako bali umwombee sana na tolea KOMUNIO TAKATIFU kwa ajili yake, kila siku ya ALHAMISI kupitia MIKONO au MAMA YANGU MTUKUFU. 
Tena kamwe usikubali neno lolote la kumdhalilisha Padre na kusema neno baya dhidi yake (yao), HATA KAMA INGELIKUWA NI KWELI! Kila Padre ni WAKILI wangu na moyo wangu utahuzunika na kusikia uchungu kwa ajili hiyo. Usikiapo HUKUMU dhidi ya Padre, sali SALAMU MARIA. Umwonapo Padre anayeadhimisha MISA TAKATIFU akiwa katika halo isiyostahili, usiongee nae lolote kumhusu yeye bali nieleze mimi tu! Huyo huwa nasimama naye ALTERANI”. ” Oh waombeeni mapadre wangu ili watamani USAFI NA WEUPE WA ROHO kuliko jambo lolote ili waweze kutolea sadaka TAKATIFU kwa moyo na mikono iliyotakata. Ni ukweli kwamba Misa ni ile ile hata ikiadhimishwa na Padre mwenye hali isiyostahiki lakini NEEMA zinazowashukia watu sio zile zile. [MARIA, MALKIA WA MAPADRE UWAOMBEE.]

Je, Kanisa Katoliki linahubiri na kufundisha umuhimu wa sala katika maisha ya Kikristo?

Sala ni sehemu muhimu katika maisha ya Kikristo. Kanisa Katoliki linahubiri na kufundisha umuhimu wake katika maisha ya waumini. Kupitia sala, tunaweza kuwasiliana na Mungu na kumwomba msaada katika maisha yetu. Sala inatusaidia kupata amani ya nafsi na kuimarisha imani yetu. Ni kwa sababu hii Kanisa Katoliki linahimiza waumini wake kusali mara kwa mara.

Katika Biblia, tunasoma maneno ya Yesu yaliyosema, “Omba na utapewa; tafuta na utapata, piga hodi na mlango utafunguliwa” (Mathayo 7:7). Hii inaonyesha kuwa sala ni njia ya kuomba msaada kutoka kwa Mungu. Pia, Biblia inatueleza kuwa Yesu mwenyewe alikuwa akipenda kwenda peke yake kusali. Kwa hivyo, kama wafuasi wa Yesu tunapaswa kufanya hivyo pia.

Kanisa Katoliki linatumia sala kama sehemu ya ibada. Sala ni sehemu ya liturujia, ambayo ni ibada ya Kanisa Katoliki. Liturujia inajumuisha sala, nyimbo, na maandiko kutoka kwa Biblia. Kupitia sala, waumini wanashiriki katika ibada ya Kanisa na wanapata baraka kutoka kwa Mungu.

Kanisa Katoliki pia linatumia sala kama njia ya kutubu dhambi zetu. Katika sala ya kitubio, waumini wanakiri dhambi zao kwa padri na kupata msamaha wa Mungu. Kwa kufanya hivyo, tunaweza kusafisha roho zetu na kuanza upya.

Kanisa Katoliki linatufundisha kuwa sala ni zaidi ya kuomba msaada kutoka kwa Mungu. Sala ni njia ya kuimarisha uhusiano wetu na Mungu. Kupitia sala, tunaweza kumjua Mungu vizuri zaidi na kupata ufahamu wa mapenzi yake. Sala inatuwezesha kusikiliza sauti ya Mungu na kufuata njia yake.

Kanisa Katoliki linatufundisha sala za kawaida kama vile Sala ya Bwana, Salamu Maria, na Tafakari ya Rozari. Sala hizi zinahimizwa kwa waumini ili kusali mara kwa mara na kuimarisha uhusiano wao na Mungu. Sala za kawaida pia zinafaa kama njia ya kufundisha watoto wetu umuhimu wa sala na kujifunza Biblia.

Kwa ujumla, sala ni sehemu muhimu ya maisha ya Kikristo. Kanisa Katoliki linahubiri na kufundisha umuhimu wake kwa waumini wake. Kupitia sala, tunaweza kuwasiliana na Mungu, kusafisha roho zetu, na kuimarisha uhusiano wetu na Mungu. Kwa hivyo, tunahimizwa kusali mara kwa mara na kufuata mafundisho ya Kanisa Katoliki kuhusu sala. Kama Catechism ya Kanisa Katoliki inasema, “Sala ni moyo wa maisha ya kiroho; ni sehemu muhimu ya uhusiano wetu na Mungu” (CCC 2558).

AHADI 15 ZA ROZARI TAKATIFU

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.

1. Yeyote yule atakayesali kwa imani rozari hii takatifu atapokea neema kuu zenye nguvu
2. Naahidi ulinzi wa kipekee na neema za kipekee kwa yule atakayesali rozari hii
3. Rozari itakuwa silaha kubwa dhidi ya nguvu za kuzimu, itaharibu maovu, itapunguza dhambi na kushinda kutofautiana
4. Itafanya fadhila kukua, kazi nzuri kuongezeka, itapatia roho huruma tele toka kwa MUNGU, itaondoa hamu ya wanadamu kupenda mambo ya dunia na majivuno yake na kufanya wapende zaidi mambo ya mbinguni. Ooh, ni kwa namna gani roho hizo zitajifurahisha na kubarikiwa kwa namna hii.
5. Roho zitakazojikabidhi kwangu kwa njia ya kusali rozari, kamwe hazitapotea.
6. Yeyote atakayesali rozari kwa uaminifu huku akiyatafakari matendo makuu ya rozari, kamwe hatashindwa na ubaya. MUNGU hatamwadhibu katika hukumu yake, hatapotea katika kifo asichopangiwa na atabaki katika neema za MUNGU na kustahili kupata uzima wa milele.
7. Yeyote atakayekuwa mwaminifu katika kusali rozari, kamwe hatakufa bila ya kupokea Sakramenti takatifu za Kanisa.
8. Wote watakaokuwa waaminifu katika kusali rozari watadumu katika mwanga wa MUNGU katika maisha yao na saa yao ya kufa na kupata neema zake tele; katika saa yao ya kufa watashiriki fadhila za watakatifu waliopo peponi
9. Nitawatoa toharani wale wote waliokuwa waaminifu katika kusali rozari
10. Watoto wangu waaminifu katika kusali rozari watapata fadhila kuu ya utukufu Mbinguni.
11. Utapata yale yote unayoniomba kwa kusali rozari
12. Wote wale wanaoeneza rozari hii takatifu nitawasaidia katika mahitaji yao
13. Nimepata toka kwa mwanangu Mtukufu kuwa mawakili wote wa rozari takatifu watapata
waombezi toka baraza lote kuu la Mbinguni wakati wa maisha yao na wakati wa saa yao ya kufa.
14. Wote wanaosali rozari hii takatifu ni wanangu, na kaka na dada wa mwanangu wa pekee YESU KRISTO
15. Ibada kwa rozari takatifu ni ishara kuu ya kuelekea ukombozi

Namna Biblia inavyomueleza Bikira Maria

Biblia inashuhudia kuwa watu wanatofautiana

Maandiko matakatifu yanawasifu watu mbalimbali kutokana na jinsi walivyomuamini Mungu na kutenda makuu kwa ajili ya taifa lake.
Abrahamu alimuamini Mungu akawa tayari kumtolea sadaka mwanae Isaka, tukio lililomfanya apate baraka ya pekee ya kuwa baba wa waamini (Mwa 22:15-18).
Yosefu, mwana mpenzi wa Yakobo, alikuwa mwaminifu hata akaliokoa taifa lisiangamie kwa njaa (Mwa 50:20).
Musa ndiye mkombozi wa taifa la Mungu katika Agano la Kale: aliongoza Israeli kutoka [[utumwani Misri akalipatia sheria kutoka kwa Mungu katika mlima Sinai. Maandiko ya Agano la Kale yanakiri, “Wala hajainuka kiongozi kama alivyokuwa Musa” (Kumb 34:10-12).
Waliofuata ni Yoshua, Debora, Gideoni, Ruthu, Samweli, wafalme Daudi na Solomoni, manabii Eliya, Isaya, Yeremia, Ezekieli na wengineo.
Mwishoni Yesu Kristo akamsifu Yohane Mbatizaji akisema, “Ni mkuu kati ya uzao wa wanawake” (Lk 7:24-28).
Elizabeti, mama wa Yohane, alijiona hastahili kutembelewa na Bikira Maria, Mama wa Yesu, akamuita, “Mama wa Bwana wangu” (Lk 1:43).
Bikira Maria si mtu wa ziada katika mpango wa Mungu bali ni mshiriki mkuu wa ukombozi wa binadamu. Maria amechangia wokovu kwa kukubali mpango wote wa Mungu aliyetaka amzae Mwanae, amlee na kumfuata kiaminifu hadi msalabani, aliposhiriki kumtoa kama sadaka ya kutuokoa. Msimamo wake ulikuwa mmoja tu: “Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema” (Lk 1:38).
Tukichunguza nafasi yake katika fumbo hilo, tunaweza kukiri pamoja naye kuwa ni Mwenyezi Mungu aliyemtendea makuu (Lk 1:49), kwa kuwa, “Mtu hawezi kuwa na kitu asipopewa na Mungu” (Yoh 3:27).
Yale yote ambayo Wakristo wengi wanayasadiki kuhusu Bikira Maria, hakujipatia bali alijaliwa na Mwenyezi Mungu huku akiitikia kwa hiari fumbo la mpango wake.

Utabiri kuhusu Bikira Maria kwenye Biblia

Biblia inatupatia utabiri uliotolewa na Mungu mwanzoni mwa historia kuhusu mwanamke atakayemshinda nyoka wa kale (Shetani): “Nitaweka uadui kati yako na huyu mwanamke, kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa chako” (Mwa 3:15). Juu ya [[Eva wa kale, ambaye alidanganywa na kuangushwa na Shetani atende dhambi, imesemwa: “Adamu akamwita mkewe jina lake Hawa, kwa kuwa ndiye aliye Mama wa walio hai” (Mwa 3:20). Hata hivyo Adamu na Eva wa kale wametuletea kifo (Rom 5:12). Mababu wa Kanisa wanamtazama Bikira Maria kama Eva mpya aliyemshinda Ibilisi na kuwa mama wa wote walio hai. Yesu, aliye Adamu mpya, alipokuwa anakamilisha sadaka ya ukombozi pale msalabani alimfanya Mama yake awe Mama wa waliokombolewa kwa kumkabidhi mwanafunzi, tena yule aliyempenda zaidi. “Penye msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mamaye, na umbu la mamaye, Mariamu wa Kleopa, na Mariamu Magdalene. Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, “Mama, tazama, mwanao”. Kisha akamwambia yule mwanafunzi, “Tazama, mama yako”. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake. (Yoh 19:26-27).
Utabiri mwingine ulisema, “Tazama Bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamuita jina lake Emanueli, yaani Mungu pamoja nasi” (Isa 7:14). Dondoo hilo linalinganishwa na Lk 1:34-35, “Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume? Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu akakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli. Kwa sababu hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu”. “Imba, ee binti Sion, piga kelele, ee Israeli, furahi na kushangilia kwa moyo wako wote, ee binti Yerusalemu. Mfalme wa Israeli, naam, yeye Bwana yu katikati yako” (Sef 3:14-15). Dondoo hilo linalinganishwa na Lk 1:28: “Malaika akaingia nyumbani mwake akamwambia, ‘Furahi Maria, umejaliwa neema kubwa, Bwana yu pamoja nawe’”. “Umebarikiwa wewe katika kila hema la Yuda na katika kila taifa, nao wanaposikia jina lako watafadhaika. Imani yako haitatoka mioyoni mwa watu wanaoukumbuka uweza wa Mungu milele” (Yudithi 14:7; 15:9). Dondoo hilo linalinganishwa na Lk 1:42, “Akapaza sauti kwa nguvu akasema, ‘Umebarikiwa wewe kuliko wanawake wote, na yeye utakayemzaa amebarikiwa’”.
Bikira Maria ni fumbo la ajabu alilolifanya Mungu katika mpango wa wokovu kwa ajili yake na kwa ajili yetu. Jamaa yake Elizabeti alimpongeza tena akiongozwa na Roho Mtakatifu, “Heri yako wewe uliyesadiki kwamba yatatimia yale uliyoambiwa na Bwana” (Lk 1:45).
Hivyo manabii mbalimbali kwa mwanga wa Roho Mtakatifu walimuagua Maria kwa heshima. Mambo yaliyotabiriwa katika Agano la Kale yalitimia katika Agano Jipya: ukombozi ulianza Bikira Maria alipokubali kwa imani fumbo la umwilisho wa Mwana wa Mungu. Bikira Maria hakuwa “chombo” tu kilichotumika bila ya kuelewa, bali alikuwa mshiriki huru wa kazi ya ukombozi ya Mwanae, kwa kuwa alipopashwa habari na malaika alikubali kwa hiari mpango wa Mungu akisema, “Mimi ni mtumishi wa Bwana, na iwe kwangu kama ulivyonena” (Lk 1:38).

Bikira Maria katika maisha ya Yesu

Yesu, kama mtu yeyote mcha Mungu, aliwaheshimu na kuwatii wazee wake: “Basi, akarudi pamoja nao Nazareti, akawa anawatii” (Lk 2:51).
Ishara ya kwanza kwenye maisha ya hadhara ya Yesu iliongozwa na Bikira Maria katika arusi ya Kana ya Galilaya, akisukumwa na huruma kwa wenye shida: kwa ombi lake Yesu aligeuza maji kuwa divai, na wanafunzi wake wakamwamini. Yohane alisimulia hivi, “Siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo. Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake. Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, ‘Hawana divai’. Yesu akamwambia, ‘Mama tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia’. Mamaye akawaambia watumishi, ‘Lo lote atakalowaambia, fanyeni’. Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu. Yesu akawaambia, ‘Jalizeni mabalasi maji’. Nao wakayajaliza hata juu. Akawaambia, ‘Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa meza’. Wakapelekea. Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maj), yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi, akamwambia, ‘Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa’. Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini. (Yoh 2:1-12).
Bikira Maria anasifiwa kwanza kwa imani yake kuu kabisa, kuliko kwa kumchukua Yesu tumboni tu. Yesu alitaka kuwainua wasikilizaji wake wafuate mambo ya roho kuliko ya mwili. “Basi, mtu mmoja akamwambia, ‘Mama yako na ndugu zako wako nje, wataka kusema nawe’. Lakini Yesu akamjibu huyo mtu aliyemwambia hivyo, ‘Mama yangu ni nani, na ndugu zangu ni akina nani?’ Kisha akanyosha mkono wake juu ya wanafunzi wake akasema, ‘Hawa ndio Mama yangu na ndugu zangu, maana yeyote anayefanya anavyotaka Baba yangu aliye mbinguni, huyo ndiye kaka yangu na dada yangu na mama yangu’” (Math 12:46-50). Vilevile, wakati wa utume wake, alimsikia “mwanamke mmoja katika lile kundi la watu akisema, ‘Hongera kwa mwanamke aliyekuzaa na kukunyonyesha’. Yesu akamjibu, ‘Barabara, lakini heri yake zaidi yule anayelisikia Neno la Mungu na kulishika’” (Mk 11:27-28).

Bikira Maria alivyoshiriki Mateso ya Yesu

Katika kumfuata Mwanae Bikira Maria alitabiriwa wazi na mzee Simeoni uchungu kama upanga utakaopenya moyo wake, “Tazama huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa. Nawe mwenyewe uchungu ulio kama upanga utauchoma moyo wako” (Lk 2:34-35).
Bikira Maria alishiriki kwanza mateso ya ukimbizi huko Misri kwa lengo la kumficha Mwanae asiuawe na Herode Mkuu, “Hivyo Yosefu aliamka akamchukua mtoto pamoja na Mama yake akaondoka usiku akaenda Misri akakaa huko mpaka Herode alipokufa” (Math 2:14-15).
Bikira Maria alishuhudia hatua kwa hatua kuteswa kwa Yesu; wanafunzi walipokimbia au kumtazama kwa mbali, yeye alikuwa karibu akaona vema kila teso lililompata Mwanae. Kutokana na fungamano la upendo wa ajabu lililokuwepo kati ya Yesu na Mamaye, alipoyashuhudia yote aliteseka sana katika moyo wake safi, kiasi kwamba Bernardo wa Klervoo akasema, “Msalaba wa Yesu uliwasulubisha wote wawili, Yesu mwilini na Mama yake moyoni”. Uaguzi wa mzee Simeoni ulitimia hivyo.
Kadiri ya mtume Paulo kuteseka ni kutimiliza yaliyopungua katika mateso ya Kristo kwa ajili ya Kanisa, “Na sasa nafurahi kuteseka kwa ajili yenu, maana kwa mateso yangu hapa duniani nasaidia kukamilisha kile kilichopungua bado katika mateso ya Kristo” (Kol 1:24). “… maana tukiyashiriki mateso yake Kristo, tutaushiriki pia utukufu wake” (Rom 8:17b).
Pale msalabani Bikira Maria, kwa njia ya mtume Yohane alifanywa Mama wa wote wanaompenda Mwanae; kisha kumzaa pasipo uchungu Bwana wa uzima, pale alituzaa sisi kwa uchungu wa kutisha uliotokana na kumuona Mwanae akifa msalabani. Hata hivyo Bikira Maria aliendelea kumuamini Mwanae aliyeonekana ameshindwa.

Bikira Maria baada ya kifo cha Yesu

Bikira Maria alikuwepo hapo mwanzo wa Kanisa, akilivutia zaidi Roho Mtakatifu kwa sala yake. “Hao wote walikusanyika pamoja kusali, pamoja na wanawake kadha wa kadha, na Maria Mama yake Yesu na ndugu zake” (Mdo 1:14).
Yesu alisema, “Ninayo bado mengi ya kuwaambieni, ila kwa sasa hamwezi kuyastahimili, lakini atakapokuja huyo Roho wa ukweli atawaongoza kwenye ukweli wote” (Yoh 16:12-13). Kwa msaada wa Roho Mtakatifu heshima kwa Bikira Maria ilienea katika Kanisa lote tangu zamani kabisa kadiri ya utabiri wake kuwa ataheshimiwa na vizazi vyote, “Kwa kuwa amemwangalia kwa huruma mtumishi wake mdogo, hivyo tangu sasa vizazi vyote wataniita mwenye heri” (Lk 1:48).

Uelewa wa namba katika Biblia

Biblia imeandikwa na Mungu kupitia waandishi wanadamu kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu. Hivyo Biblia ni Neno la Mungu. Hivyo mwandishi wa Biblia ni Mungu kupitia wanadamu (God is the primary author of the Bible while human authors are secondary authors). Mungu aliwavuvia (inspiration by the Holy Spirit) waandishi wanadamu ili waweze kuandika kile tu ambacho Yeye (Mungu) alitaka kiandikwe kwa ajili ya wokovu wa wanadamu. Kusema kuwa Biblia imeandikwa na Mungu kupitia wanadamu haina maana ya kuandikwa kwa njia ya imla (dictation), kana kwamba Mungu anataja sentensi au neno na wao wanaandika. Hapana, pamoja na kuwavuvia Roho Mtakatifu, waandishi wanadamu walikuwa huru kutumia vipawa mbalimbali vya uandishi na mazingira yao ili kufikisha ujumbe ambao Mungu amewavuvia. Hivyo walikuwa “active writers of the Bible, and not passive writers.” Walitumia akili (reason), utashi (will), ujengaji picha (imagination) na vipawa vingine. Lakini vipawa hivi vyote vilikuwa chini ya maongozi ya Roho Mtakatifu ili kuwawezesha waandishi wa Biblia kufikisha ujumbe kwa ufasaha bila makosa.

Hivyo kuelewa kifungu au ujumbe wa Biblia ni lazima kujua yafuatayo:
Maana aliyokusudia mwandishi (the meaning of the human author)
Kusudi/malengo ya Roho Mtakatifu

Na kwa kuwa kwa mara ya kwanza Biblia waliandikiwa Wayahudi na waandishi wengi walikuwa Wayahudi, hivyo tunapaswa kujua yafuatayo ili kufasiri Biblia vizuri:

Tamaduni za Wayahudi
Historia ya Wayahudi
Mambo ya Kijografia
Namna yao ya uandishi n.k

Jambo muhimu kuelewa
Namba, wanyama, rangi, vitu, watu, maeneo, shughuli mbalimbali n.k vilikuwa na maana sana kwa Wayahudi na kwa Wakristo wa kwanza. Hivyo si ajabu kuona vimetajwa au kutumika katika Biblia.

ISHARA NYINGINE TOFAUTI NA NAMBA

Kabla ya kuzungumzia namba tuzungumzie baadhi ya vitu, rangi, watu au mahali kama vinavyoongelewa kwenye kitabu cha Ufunuo na sehemu nyingine za Biblia:

Mwanamke:

kwenye Ufu.12:1+ anamaanisha taifa au mji, na siyo mwanamke kama tunavyojua

Pembe:

neno pembe kwenye Ufu. 5:6; 12:3 linamaanisha “mamlaka”. Hata kwenye kiswahili mtu akiambiwa kuwa “ameota pembe” maana yake anajifanya kuwa ana mamlaka fulani na hivyo ana kiburi.

Mabawa:

kwenye Ufu. 4:8; 12:14 linamaanisha uwezo wa kufika mahali pote (mobility).

Upanga mkali:

kwenye Ufu. 1:16; 2:12,16) linamaanisha Neno la Mungu, ambalo lina hukumu na kuadhibu.

Matawi ya mtende:

kwenye Ufu. 7:9 ni ishara ya ushindi.

Taji:

kwenye Ufu. 2:10; 3:11 ni ishara ya utawala na ufalme.

Bahari:

kama lilivyotumika kwenye Ufu. 13:1; 21:1 linamaanisha sehemu ya uovu, chanzo cha machafuko na kifo.

Nyeupe:

rangi nyeupe inamaanisha furaha ya ushindi (Ufu. 1:14; 2:17)

Zambarau:

rangi ya zambarau huashiria anasa, utajiri na ufalme (Ufu. 17:4; 18:12,16). Kwenye Yohane 19:2,5; Mk. 15:17 vazi la zambarau huashiria “ufalme”. Kwenye Lk. 16:19 vazi la zambarau la yule tajiri liliashiria “maisha ya anasa”.

Nyeusi:

rangi nyeusi iliashiria kifo (Ufu. 6:5,12).

NAMBA KATIKA BIBLIA

Namba zilikuwa na maana sana kwa Wayahudi kwa sababu za kimazingira, kiuandishi na kilugha. Kila namba ilikuwa na maana. Hebu tutazame baadhi tu ya namba hizo:

Namba 3 na7

Namba hizi kwa Wayahudi (kwenye Biblia) zinamaanisha ukamilifu au utimilifu wa jambo (perfection or completion). Kwa mfano katika Kiebrania (lugha ya Wayahudi) hakuna “superlative” (kulinganisha kwa kutumia sifa ya juu kabisa) mfano “the tallest, the youngest, the holiest” kama kwenye Kiingereza. Hivyo Myahudi kwa upande wake atatamka neno husika mara tatu kuonesha ukamilifu: God is holy, holy, holy (ambapo kwenye Kiingereza tungesema tu “God is the holiest”). Kwa hiyo akitaja neno mara tatu alimaanisha ukamilifu wa jambo(perfection). Anaposema Mungu ni Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu ana maana kwamba Mungu ana ukamilifu wa utakatifu, yaani ni Mtakatifu kupita viumbe au vitu vyote. Mfano mwingine: Myahudi akisema kwamba nilipigwa viboko vitatu haina maana kuwa lazima vilikuwa vitatu tu. Hapa ina maana kwamba alipigwa katika ukamilifu wake yaani alipigwa barabara, sawia, alipigwa mno,
alipigwa mpaka basi. Hata kwenye Biblia ni vivyo hivyo. Yesu alimuuliza Petro mara tatu kama anampenda (Yohane 21:15-19). Hapa Yesu alitaka kujua kama Petro alimpenda katika ukamilifu wa upendo. Namba 7 imetumika mara 42 kwenye kitabu cha Daniel na Ufunuo: mfano “roho saba” ilimaanisha “ukamilifu wa roho” yaani Roho Mtakatifu. Kwa hiyo namba 3 na7 ni namba za ukamilifu. Yesu anapomwambia Petro asamehe “saba mara sabini” (Mt. 18:21-22) anamaanisha kuwa Petro asamehe “kwa ukamilifu, pasipo kukoma”.

Namba 4

Namba 4 kwenye Biblia inamaanisha “ulimwengu mzima” (universality of the visible world). Kwa hiyo aya isemayo “malaika wanne waliokuwa wamesimama katika pembe nne za dunia” (Ufu.7:1; 21:16; Rejea pia Is.11:12) ulimaanisha malaika walikuwa wameenea katika ulimwengu mzima. Pia aya hiyo hiyo inamaanisha kuwa jukumu lao lilikuwa ni kwa ulimwengu mzima.

Namba 6

Hii namba inasimama kumaanisha “mapungufu, isiyo kamilifu”. Namba hii ilihusianishwa na maadui wa Mungu kwenye Biblia. Kitendo cha mtu kuwa adui wa Mungu kilimaanisha mtu huyo si mkamilifu na ana mapungufu (Rejea 1 Nyakati 20:6; Daniel 3:1; Ufu.13:18).

Namba 12, 24

Hizi mara nyingi kwenye Biblia zinawakilisha kabila kumi na mbili za Israeli. Wapo wataalam wa Maandiko wanaosema kuwa Mitume 12 waliwakilisha makabila 12 ya Israel, yaani kila mmoja alitoka miongoni mwa makabila 12 ya Israel. Pia namba 12 inawakilisha Kanisa zima. Lakini pia 12 ni namba ya ukamilifu. Kwa hiyo Mitume 12 walikamilisha taifa zima la Israeli.

Namba 40, 175

Namba hizi kwenye Biblia zinamaanisha “urefu wa jambo” (longevity). Mfano wakisema fulani amekuwa mgonjwa kwa siku 40 ina maana amekuwa mgonjwa kwa kipindi kirefu, haina maana kuwa ni lazima zilikuwa 40 (huenda hata zilizidi). Kusema kuwa gharika ilidumu siku 40 mchana na usiku, ni kusema kuwa gharika ilidumu kwa kipindi kirefu; kusema kuwa Yesu alifunga siku 40 ni kumaanisha kuwa alifunga kwa muda au kipindi kirefu, yawezekana hata zaidi ya siku hizo 40. Kusema kuwa Waisraeli walikaa jangwani miaka 40 ni kusema kuwa walikaa jangwani kwa kipindi kirefu. Kusema kuwa Ibrahimu aliishi miaka 175 ina maana aliishi miaka mingi au kipindi kirefu, si lazima kwamba alifikisha miaka 175 lakini kwamba aliishi miaka ya kutosha, aliishi kipindi kirefu. Haya yote Wayahudi walielewa vizuri, hawakuhitaji kuuliza.

Kuanzia maelfu

Kwenye Biblia ikitajwa namba ya maelfu inamaanisha “umati mkubwa” wa watu. Yohane anaposema “…na watu mia na arobaini na nne elfu pamoja naye..” (Ufunuo 14: 1) anamaanisha kuwa aliona umati mkubwa wa watu wasio na idadi. Hivyo Ufunuo 14:1 haimaanishi watu 144,000 tu bali umati mkubwa wa watu wasio na idadi. Hata kwa Kiswahili kuna wakati tunasema “akihubutia maelfu ya watu” tukiwa na maana kwamba alihutubia umati mkubwa wa watu.

N.B. Hapa nimeeleza baadhi ya namba tu. Zipo nyingine nyingi sana na zina maana yake. Hivyo tusitafsiri Biblia kwa maana sisisi tu (Literal interpretation), yaani kile kilichoandikwa tu. Twende zaidi ya hapo.

UFAFANUZI WA NAMBA 666 (Ufu.13:11-18)

Kuelewa maana ya namba hii ni lazima kuelewa mazingira na sababu za kuandikwa kitabu cha Ufunuo. Kitabu cha Ufunuo kiliandikwa karne ya kwanza (kati ya 90-96 AD) ambapo dini ya Ukristo ilianza kuenea kwa kasi. Hivyo tawala za Warumi na Wayahudi ziliona Ukristo kama dini mpya na tishio kwa imani, siasa na tamaduni zao. Ili kuifutilia mbali Warumi na hata Wayahudi waliendesha madhulumu (persecutions) dhidi ya Wakristo: kuwaua, kuwafunga, kuwatesa na kuwalazimisha wakane Ukristo. Yohane mwenyewe anaandika kitabu cha Ufunuo akiwa gerezani (uhamishoni) katika kisiwa cha Patmos kama matokeo ya madhulumu. Yohane anaandika kitabu cha Ufunuo kuwatia moyo Wakristo katika madhulumu wanayopata, wasikate tamaa, wasikane imani kwa kuwa baada ya madhulumu watapata utukufu katika Yerusalem mpya (mbinguni) na damu watakayomwaga katika madhulumu ndiyo itawatakasa (Ufu. 7:14).

Kwa kuwa madhulumu yalikuwepo ilikuwa ni vigumu Wakristo kuwasiliana kwa lugha ya wazi ili kuepuka kuuawa au kufungwa. Hivyo Wakristo walitumia lugha ya namba na mafumbo kufikishiana ujumbe kwa waandishi (they used coded language). Kumtaja mfalme wa dola ya Kirumi kwa jina ilikuwa ni dharau na hivyo sababu tosha ya kuuawa. Yohane anatumia lugha ya namba kumtaja mmoja wa wafalme wakatili wa dola ya Kirumi aitwaye NERO kwa kutumia namba 666. Wakristo na wataalamu wa Maandiko Matakatifu walijuaje kuwa 666 inamwakilisha mfalme NERO? Mpaka leo kwa Warumi na Wagiriki kila herufi imepewa thamani ya namba. Walipojumlisha herufi zinazounda jina “NERO” walipata jumla ya 666. Kwa Warumi jina la NERO liliandikwa NERON (likiwa na “N” mwishoni). Walijumlisha herufi za jina NERON na kupata 666 na hivyo kugundua kuwa mnyama aliyetajwa kwenye Ufu. 13:11-18 alikuwa NERO. Kwa nini amezungumziwa mnyama halafu sisi tunazungumzia mtu? Ni kwa sababu Yohane mwenyewe anasema: “Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu [for it is man’s number]. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita” (Ufu. 13:18).

Utaalamu wa kuzipa herufi thamani ya namba unaitwa “gematria”. Mfumo wa kuzipa herufi thamani ya namba unafanana na kutofautiana kwa kiasi fulani kwa Warumi na Wagiriki. Utaratibu wa kuthaminisha herufi na namba upo bado. Ndiyo maana tukiwa shule ya msingi tulifundishwa “Namba za Kirumi”. Tunajuaje kuwa MM ni 2000 au MMIX ni 2009. Ni kwa sababu kwa Warumi kila herufi ina thamani ya namba: M ni 1000, hivyo M+M ni sawa na kusema 1000+1000, na hivyo 2000. Tuone sasa kwa jina NERO na thamani ya kila herufi.

Gematria kwa Kirumi: NERON
N = 50
E = 6
R = 500
O = 60
N = 50
neron (50 + 6 + 500 + 60 + 50) = 666

Gematria kwa Wayunani (Waebrania): KAISER NERON

Wayunani walitamka jina ya mfalme kwa kuanza na jina la heshima “title” yaani Kaisari (Ceaser). Hivyo NERO aliitwa qsr nrwn (Kaiser Neron, kwa Kigiriki). Mwanzoni Kiebrania (Kiyunani) hakikuwa na irabu (vowels). Herufi zilizounda neno qsr nrwn (Kaiser Neron) zilipewa thamani ya namba kama ifuatavyo:
q = 60
s = 100
r = 200
n = 50
w = 6
Hivyo basi neno qsr nrwn (60 + 100 + 200 + 50 + 200 + 6 + 50) = 666.

Na Fr. Kelvin O. Mkama

Mafundisho (Dogma) ya Kanisa Katoliki kuhusu Bikira Maria

Kuna mafundisho makuu manne kumhusu Bikira Maria ambayo ni lazima kila Mkatoliki ayasadiki kutokana na ufunuo wa Mungu: 1. B. Maria mkingiwa dhambi ya asili 2. B. Maria Mama wa Mungu 3. B. Maria Bikira daima 4. B. Maria kupalizwa mbinguni mwili na roho

Mkingiwa Dhambi ya Asili

Malaika alimsalimia Maria “umejaa neema” (Lk 1:28) maana ndiye tunda bora la ukombozi ulioletwa na Yesu. Ni imani ya Wakatoliki kwamba kwa stahili za Mwanae alikingiwa asirithi kwa wazazi dhambi ya asili na madonda yanayotokana nayo, wala asitende dhambi maisha yake yote. Kwa maneno mengine, Bikira Maria tangu atungwe mimba Mungu alimkinga na kila doa la dhambi kwa kutazamia stahili za Yesu Kristo aliye Mkombozi wa binadamu wote. Ndiye aliyekombolewa kwa namna bora kushinda viungo vyote vya Kanisa. Maisha yake yote hakutenda dhambi hata moja. Mapokeo ya mashariki yanamuita “A Panagia” = “Mtakatifu tu”. Dogma hiyo ilitangazwa na papa Pius IX mwaka 1854, halafu mwaka 1858 Bikira Maria alijitambulisha kama Mkingiwa kwa Bernadeta Soubirous huko Lurdi (Ufaransa). Tena mwaka 1917 huko Fatima (Ureno) aliwafunulia Lusia, Fransisko na Yasinta Marto moyo wake safi usio na doa.

Mama wa Mungu

Injili ya Yohane inaanza kwa kishindo, “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu” (Yoh 1:1). Huyo Mungu Mwana alitwaa ubinadamu katika Bikira Maria akazaliwa mtoto, jina lake Yesu, maana yake Mungu Mwokozi. Huyo ni binadamu kama sisi katika yote isipokuwa dhambi. Ubinadamu wa Yesu unategemea Nafsi yake ya Kimungu: akisema, ‘Mimi’, ni kwa Nafsi yake hiyo. Ndiyo maana aliwaambia Wayahudi, “Kweli nawaambia, kabla Abrahamu hajazaliwa, nalikuwepo” (Yoh 8:50). “Kama vile Baba alivyo asili ya uhai, ndivyo alivyomjalia Mwanae kuwa asili ya uhai” (Yoh 5:26).
Mtume Paulo akaeleza, “Wakati maalumu ulipotimia Mungu alimtuma Mwanae aliyezaliwa na mwanamke” (Gal 4:4). Bikira Maria ni Mama wa Mungu kwanzia wakati huo: tangu Bikira Maria alipojaliwa kumchukua mimba, kumzaa, kumnyonyesha na kumlea mtu ambaye kwa asili ni Mungu. Cheo hicho kimemuinua juu kuliko hata malaika. “Malaika alimwambia, ‘Hicho kitakachozaliwa kitaitwa Kitakatifu, Mwana wa Mungu’” (Lk 1:35).
Dogma ilitangazwa mwaka 431 kwenye Mtaguso wa Efeso uliomuita “Mzazi wa Mungu”, ukisema Maria anastahili kuitwa hivyo kwa sababu Mwana wa milele wa Mungu, ambaye ni Mungu sawa na Baba, alifanyika mtu toka kwake. Akiwa mja mzito alishangiliwa: “Umebarikiwa wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Limenitokeaje neno hili, hata mama wa Bwana wangu anijilie mimi?” (Lk 1:42-43). Ungamo hilo la Elizabeti likakamilishwa na Mtume Thoma aliyemuambia Yesu mfufuka: “Bwana wangu na Mungu wangu!” (Yoh 20:28).

Bikira na Mama

Wakristo na Waislamu wote wanakiri kuwa Yesu alitungwa bila ya mchango wa mwanamume. La ajabu zaidi katika imani hiyo ni kwamba hata uzazi wenyewe haukuondoa ubikira wake, bali uliutakasa: ni Bikira daima. Ingawa akili inasita, ni lazima kukiri na malaika, “Hakuna lisilowezekana kwa Mungu” (Lk 1:38). Yosefu, ingawa kisheria alikuwa mume wake, hakutenda naye tendo la ndoa.
Ni imani ya Wakatoliki na Waorthodoksi kuwa Mama wa Yesu anastahili kuitwa “Bikira daima” kwa sababu alimchukua mimba akiwa bikira, akamzaa bila ya kupotewa na ubikira, akabaki bikira hadi mwisho wa maisha yake. Hamu yake ya kuwa bikira hata kisha kuchumbiwa inajitokeza katika jibu alilompa malaika aliyemtabiria mimba: “Litakuwaje neno hili, maana sijui mume?” (Lk 1:35). Ni kielelezo cha Wakristo ambao Mtume Paulo aliwaandikia: “Nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi” (2Kor 11:2), “mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine” (1Kor 7:35).
Wanaosemwa katika Injili “ndugu zake Yesu” si watoto wa Bikira Maria, bali ndugu wa ukoo waliokuwa jirani sana na familia hiyo takatifu. Kama Bikira Maria angekuwa na watoto wengine, Yesu angekuwa amefanya kosa la kuwanyang’anya Mama yao na kumfanya awe Mama wa mtume Yohane alipomkabidhi msalabani, “‘Mwana, tazama Mama yako’. Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake” (Yoh 19:27).
Katika Agano Jipya yupo Yakobo anayeitwa na mtume Paulo “ndugu yake Bwana” (Gal 1:19): Yakobo huyo alikuwa maarufu katika Kanisa la Yerusalemu (Mdo 12:7; 15:13-21; 21:18-20; Gal 2:9). Yakobo huyo si mtume Yakobo kaka yake Yohane (Lk 6:12-16), bali ni Yakobo ndugu yake Yose na mama yao kwenye Injili anaitwa “Maria mwingine”, si Maria Mama wa Yesu. “Walikuwepo pia wanawake waliotazama kwa mbali. Miongoni mwao akiwa Maria Magdalena, Salome na Maria mama wa akina Yakobo mdogo na Yose” (Mk 15:40). Maria lilikuwa jina la kawaida kwa Wayahudi: akina Maria wakiwa wengi hivyo, tujue kuwatofautisha kwenye Injili, ambazo zinamtaja Bikira Maria kama “Mama wa Yesu”.

Kupalizwa Mbinguni mwili na roho

Baada ya maisha haya ya duniani Bikira Maria alipalizwa mbinguni mwili na roho, ishara ya mwanamke mshindi. “Ishara kubwa ikaonekana mbinguni, ambapo mwanamke aliyevikwa jua, pia na mwezi chini ya miguu yake, na taji la nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake” (Ufu 12:1). Maneno ya shangilio lake yametimia: Mungu “amewaangusha wakuu katika viti vyao vya enzi; na wanyonge amewakweza” (Lk 1:52).
Imani hiyo ya mapokeo ya kale, yanavyoshuhudiwa na Mababu wa Kanisa, ilitangazwa rasmi na Papa Pius XII kwa niaba ya maaskofu wote mwaka 1950.

Je, Bikira Maria ni Bikira Daima au alizaa watoto wengine?

Jibu fupi ni kwamba Bikira Maria hakuzaa watoto wengine na hakuwa na watoto wengine zaidi ya Yesu
Hapo zamani hakuna mkristu au dehebu lolote lililokuwa linapinga kuwa Bikira Maria sio Bikira Daima hata Waprotestanti/walokole waliamini Bikira Maria ni Bikira Hata Baada ya Kumzaa Yesu. Kwenye Miaka ya 1400-1600 Watu wote wakwanza waliopinga Kanisa Katoliki walikubali kuwa Bikira Maria ni Bikira daima wakiwemo Martin Lutha aliyeanzisha kanisa la Lutheran, John Calvin aliyeanzisha Ulokole/Protestanti, Mchungaji Ulrich Zwingli, Heinrich Bullinger, and Thomas Cranmer. Kwa miaka zaidi ya 350 Waprotestant/walokole waliendelea kuamini kuwa Bikira Maria ni Bikira Daima.
Lakini baadae wakristo wengi walianza kupinga kuwa Bikira Maria ni Bikira Daima.

Tunaweza kuthibitisha kuwa Bikira Maria hakuzaa watoto wengine kwa kunukuu Biblia Kama ifuatavyo;

1. Bikira Maria Alikuwa Bikira Kabla ya kumzaa Yesu

Biblia inatuambia wazi kwamba Bikira Maria alikuwa Bikira Kabla ya kumzaa Yesu Kama tunavyosoma katika Luka 1:26-35
26 Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya, 27 kwa msichana mmoja aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi. 28 Malaika akamwendea, akamwambia, “Salamu Maria! Umejaliwa neema nyingi! Bwana yu pamoja nawe.” 29 Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: maneno haya yanamaanisha nini? 30 Malaika akamwambia, “Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema. 31 Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume na utampa jina Yesu. 32 Yeye atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake. 33 Kwa hivyo atautawala ukoo wa Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho.” 34 Maria akamjibu, “Yatawezekanaje hayo, hali mimi ni bikira?” 35 Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakushukia, na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu. (Luka 1:26-35)

2. Biblia Haiwataji ndugu wa Yesu wakati Yosefu na Maria walipokimbilia Misri kumficha Yesu na wakati waliporudi

19 Baada ya kifo cha Herode, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto kule Misri, 20 akamwambia, “Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, urudi tena katika nchi ya Israeli, maana wale waliotaka kumwua mtoto huyo wamekwisha kufa.” 21 Basi, Yosefu aliamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, akarejea katika nchi ya Israeli. 22 Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao mwanawe Herode alikuwa mfalme wa Yudea mahali pa baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye baada ya kuonywa katika ndoto, alikwenda katika mkoa wa Galilaya, 23 akahamia katika mji uitwao Nazareti. Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyonenwa kwa njia ya manabii: “Ataitwa Mnazare.” Matayo 2:19-23
Kama wangekuwepo wadogo zake Yesu Biblia ingetuambia kwamba walikuwa wapi wakati huo na walikuwa na Yesu au la.

3. Biblia haituambii kuwa Yesu alikua na wadogo zake alipokuwa na miaka 12

Wakati wa Maria, Yoseph na Yesu walipoenda Yerusalemu Yesu akiwa na miaka 12 Biblia haituambii kuwa Yesu alikuwa na wadogo zake na walikuwa wapi. Kumbuka walikuwa na Desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka kwa ajili ya Pasaka familia nzima kama familia. Je hao watoto wengine walikuwa wapi. Kwa nini walikuwa na Yesu Mwenyewe? Maana yake ni kwamba Yesu hakuwa na Wadogo zake.
41 Wazazi wa Yesu walikuwa na desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka wakati wa sikukuu ya Pasaka. 42 Mtoto alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, wote walikwenda kwenye sikukuu hiyo kama ilivyokuwa desturi. 43 Baada ya sikukuu, walianza safari ya kurudi makwao, lakini Yesu alibaki Yerusalemu bila wazazi wake kuwa na habari. 44 Walidhani alikuwa pamoja na kundi la wasafiri, wakaenda mwendo wa kutwa, halafu wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa na marafiki. 45 Kwa kuwa hawakumwona, walirudi Yerusalemu wakimtafuta. 46 Siku ya tatu walimkuta Hekaluni kati ya walimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. 47 Wote waliosikia maneno yake walistaajabia akili yake na majibu yake ya hekima. 48 Wazazi wake walipomwona walishangaa. Maria, mama yake, akamwuliza, “Mwanangu, kwa nini umetutenda hivyo? Baba yako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwa huzuni.” 49 Yeye akawajibu, “Kwa nini mlinitafuta? Hamkujua kwamba inanipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu?” 50 Lakini wazazi wake hawakuelewa maana ya maneno aliyowaambia. 51 Basi, akarudi pamoja nao hadi Nazareti, akawa anawatii. Mama yake akaweka mambo hayo yote moyoni mwake. 52 Naye Yesu akaendelea kukua katika hekima na kimo; akazidi kupendwa na Mungu na watu. (Luka 2:41-52).
Kwa hiyo Biblia haionyeshi kuwa Yesu alikuwa na kaka na dada wakati akiwa na miaka 12. Kama wangekuwepo wangetajwa hapa kuwa walikuwa pamoja na Wazazi wao kama Yesu au walikuwa na Yesu wakati anapotea. Biblia haituambii chochote kwa hiyo wakati huo hapakuwa na wadogo zake Yesu.

4. Kukosekana kwa neneo “Binamu” kwenye lugha ya Yesu

Wakristu wa kwanza pamoja na Yesu aliongea Kiaramaiki au Kiebrania. Katika lugha zote hizo hakuna neno “Binamu” kwa hiyo mabinamu walijulikana kama dada na kaka wa mtu. Kwenye Agano jipya Neno kaka na Dada lilitumika pia kuwakilisha binamu.
Biblia inapotuambia kuwa Kaka na dada zake Yesu haimaanishi kaka wa kuzaliwa bali ndugu au Binamu
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
Kwa hiyo wanaotajwa hapa ni ndugu wa Yesu kwa maana maneno kama; ndugu, kaka au dada lilitumika badala ya Binamu yaani mtoto wa shangazi au mjomba. Hapa juu Yosefu ametajwa kama kaka yake Yesu lakini tunajua kuwa Yosefu ni Baba yake Yesu. Baba na mwana hawawezi kuwa na jina sawa.

5. Biblia haitumii neno Ndugu, kaka au dada ikimaanisha ndugu wa kuzaliwa mama mmoja na baba mmoja

Sio mara zote Biblia imetumia neno Ndugu kumaanisha ndugu (Dada na Kaka) wa kuzaliwa yaani kaka na dada kwa mfano
Kwa kuangalia lugha ya Kiswahili na Kiingereza 1 Wakorintho 15:6 tunaona tafsiri tofauti.
KISWAHILI 6 Kisha aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano kwa mara moja; wengi wao wanaishi bado, lakini baadhi yao wamekwisha kufa.
ENGLISH 6 After that, he appeared to more than five hundred of the brothers and sisters at the same time, most of whom are still living, though some have fallen asleep.
Kwa hiyo hapa neno kaka dada na ndugu linaonekana wazi halikumaanisha ndugu au kaka wa damu.

6. Undugu wa Yakobo, Simoni, Yosefu na Yuda kwa Yesu Sio wa mtu na kaka zake

Wasemao kuwa Bikira maria alikuwa na wana zaidi ya Yesu wananukuu kifungu hiki;
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
Kumbuka kulikuwa na Yakobo wawili wakati wa Yesu, Vifungu vifuatavyo yunaweza kuona kuwa kulikuwa na yakobo wawili ambao walikuwa ndugu za Yesu lakini sio kaka wa kuzaliwa kwa mama.
35 Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo, walimwendea Yesu wakamwambia, “Mwalimu, tunataka utufanyie kitu tutakachokuomba.” (Marko 10:35)
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56)
Tunaweza kuona Undugu huu na Yesu kwa kusoma;
19 Lakini sikuwaona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana. (Wagalatia 1:19)
Lakini Yuda anasema;
1 Mimi Yuda, mtumishi wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, nawaandikia ninyi mlioitwa na Mungu na ambao mnaishi katika upendo wa Mungu Baba, na katika ulinzi wa Yesu Kristo. (Yuda 1:1)
Kwa hiyo Yakobo na Yohane walikuwa watoto wa Mama mwingine ambao baba yao ni Zebedayo. Na Yakobo na Yosefu walikuwa watoto wa Maria Mwingine. Kwa hiyo ni Yakobo wa wili wa Mama wengine Tofauti na Maria. Yuda alikuwa ni ndugu yake Yakobo. Yakobo vilevile alikuwa ndugu yake Yesu.
Kuthibitisha kuwa Hawa kina Mama ndio waliokuwa Mama zao kina Yakobo wote hao wawili na wengine tunaweza kusoma;
25 Karibu na msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mama yake, na dada ya mama yake, Maria mke wa Kleopa, na Maria Magdalene. (Yohana 19:25)
Kwa hiyo kwenye (Yohana 19:25) tunaona Kuwa ni kwenye Msalaba wa Yesu alikuwepo Mama yake Yesu (Bikira Maria), Dada yake Bikira Maria, Mke wa Cleopa na Maria Magdalena. Na kwenye (Matayo 27:55-56) wamwtajwa ni Mama za kina nani kama inavyoonekana kwenye kifungu kifuatachi;.
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56).
Kwa hiyo hii ina maanisha kulikua na wanawake watatu wenye majina sawa ya Maria waliokuwa chini ya Msalaba. Yakobo na Yuda walikuwa watoto wa Maria Mke wa Cleofasi, na sio Mama wa Yesu, na hivyo sio kaka za Yesu.

7. Yesu alimwacha Mama yake kwa Yohane kwa kuwa hakuwa na Kaka na dada wakumwachia mamaye

26 Yesu alipomwona mama yake, na karibu naye amesimama yule mwanafunzi aliyempenda, akamwambia mama yake: “Mama! Tazama, huyo ndiye mwanao.” 27 Halafu akamwambia yule mwanafunzi: “Tazama, huyo ndiye mama yako.” Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake.
Ndiyo maana Bikira Maria tangu siku ile alihamia kwa Yohani kwa kuwa hakuwa na watoto wengine.

Huruma ya Mungu: Nguvu ya Kufufua na Kurejesha

Huruma ya Mungu: Nguvu ya Kufufua na Kurejesha

Ni kweli kwamba maisha yetu yanapitia changamoto kubwa, kukataliwa, msiba, na hata kifo. Lakini kama wakristo, tunajua kwamba kuna nguvu kubwa ya Mungu inayoweza kutufufua na kuturejesha kutoka kwa hali mbaya. Nguvu hii ni Huruma ya Mungu.

  1. Huruma ya Mungu ni zawadi kwa wanadamu. Mungu alitupenda tangu mwanzo wa ulimwengu, na kila wakati tunapojisikia wenye dhambi au kupotea, tunaweza kumgeukia na kumwomba Huruma yake. "Neno la Bwana hukaa milele." (1 Petro 1:25)

  2. Huruma ya Mungu inajirudisha kwetu hata katika maisha yetu ya kila siku. Tunapokabiliwa na changamoto, tunaweza kuomba msaada wake, na Mungu atatupatia nguvu na amani ya akili. "Tazama, namna alivyo mwema Mungu, ni neno lake ndilo linaodumu milele." (Zaburi 100:5)

  3. Huruma ya Mungu inatupatia msamaha wa Mungu. Tunapokuwa wenye dhambi, tunaweza kumwomba Mungu msamaha. Msamaha wake ni wa kweli na wa milele, na anaturudisha kwake kama watoto wake wapenzi. "Kama tukiungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote." (1 Yohana 1:9)

  4. Huruma ya Mungu inatufufua kutoka kwa hali mbaya. Katika maisha yetu, tunaweza kuanguka na kukata tamaa. Lakini Huruma ya Mungu inatufufua na kutufufua kwa nguvu zake. "Naamini ya kuwa utafufuka katika ufufuo wa wafu." (Yohana 11:25)

  5. Huruma ya Mungu inatupatia nguvu za kufanya mapenzi ya Mungu. Tunapokabiliwa na changamoto, tunaweza kumwomba Mungu atusaidie kufanya mapenzi yake. Tunajua kwamba nguvu zake zinatosha na atatupa nguvu za kufanya kile alichoamuru. "Kwa maana ni Mungu atendaye kazi ndani yenu kwa kutaka kwake kwa vyovyote." (Wafilipi 2:13)

  6. Huruma ya Mungu inatufufua kutoka kwa dhambi zetu. Dhambi zetu zinaweza kutufanya tuonekane kuwa dhaifu na wenye hofu. Lakini tunapomwomba Mungu msamaha na kumkiri kama Bwana wetu, atatubadilisha na kutufanya kuwa wapya. "Kwa maana atakayekuwa ndani ya Kristo amepata kuwa kiumbe kipya." (2 Wakorintho 5:17)

  7. Huruma ya Mungu inatupatia upendo wa kweli. Mungu anatupenda hata tunapokuwa wenye dhambi. Kupitia Huruma yake, tunapata upendo wake wa daima na wa kweli. "Nami nimesema, rehema yake itadumu milele." (Zaburi 89:2)

  8. Huruma ya Mungu inatupatia amani ya akili. Tunapokabiliwa na hali ngumu, tunaweza kuomba Huruma ya Mungu na kupata amani. "Amkeni, amkeni, valeni nguvu, enyi mkono wa Bwana; amkeni kama siku za kale, kama vizazi vya zamani." (Isaya 51:9)

  9. Huruma ya Mungu inatupatia tumaini. Kupitia Huruma yake, tunaweza kuwa na matumaini hata tunapokabiliwa na changamoto kubwa. "Kwa maana mimi najua fikira nilizo nazo kwenu, asema Bwana, fikira za amani wala si za mabaya, kuwapa matumaini katika mwisho wenu." (Yeremia 29:11)

  10. Huruma ya Mungu inatupatia wokovu. Kupitia Huruma ya Mungu, tunapata wokovu na tumaini la maisha ya milele. "Na hii ndiyo ahadi aliyotuahidia, yaani, uzima wa milele." (1 Yohana 2:25)

Kama wakristo, tunapaswa kuomba Huruma ya Mungu kila siku na kuamini katika nguvu zake za kutufufua na kuturejesha kutoka kwa hali mbaya. Kwa maombi yetu, tunaweza kutafakari juu ya Huruma ya Mungu na kuishi kwa furaha na amani. Kama alivyosema mtakatifu Faustina, "Huruma yako, Mungu, ni kubwa kuliko dhambi zangu zote."

Je, unafikiriaje kuhusu Huruma ya Mungu? Je, imekuwa nguvu kwako katika maisha yako?

Mbinu 4 anazotumia Shetani kuteka na kurubuni Watu

1. Kutushawishi tuache kusali maaana njia kuu ya mawasiliano kati yetu na MUNGU.Hivyo akifanikiwa hapo kwisha habari yako

2. Kufanya umwogope shetani na nguvu zake kuliko unavyompenda MUNGU. Wakristo wengi leo hii husali na kuomba kwa nguvu mno siyo sababu wanampenda MUNGU mno hapana ni sababu wanamwogopa shetani na majeshi yake na muda mwingine hata watumishi wa MUNGU wanamsaidia kwa kuhubiri mno na muda mwingine kuongeza jumvi juu ya nguvu za giza kuna wahubiri huambatanisha kila kitu na vifungo vya nguvu za giza na kusahau kuhubiri uzuri na wema wa MUNGU kwetu.

3.Kutufanya tusahau uwepo wake au kuupuzia. pale tunapokuwa hatupay attention existance ya shetani yeye ndio hupata wakati mzuri wa kutupiga ,sababu ni rahisi mno kutouutambua ubaya wa dhambi kama hatutaamini uwepo wa shetani ktk uovu…hii hutupelekea kutenda dhambi na kuziona siyo dhambi mfano kwa wasomi wengi hupuuzia baadhi ya mambo kama kujilinda na zinaa wakiamini ni kupitwa na wkt kama utakuwa hauna mahusiano ya kingono mpaka umefika chuo kikuu tena huchukulia wasiokuwa hivyo ni wagonjwa.hapo ni kuwa wengi wameignore uwepo wa shetani “no devil no evil” hivyo watu ndio hupotea.

4.KUTUTIA MOYO WAKATI WA KUTENDA DHAMBI NA KUTUKATISHA TAMAA YA KUSAMEHEWA. nitatoa mfano huu mtu ambaaye anataka kufanya uzinzi shetani humtia moyo kuwa MUNGU anajua kuwa sisi ni binadamu dhaifu na yeye husamehe dhambi zetu daima lakini ifikiapo wakati ukataka kutubu hafanya kila njia kukukatisha tamaa ya kusamehewa na hututia aibu hata kutsmka kwa padri kuwa nimedhini maana huanza kufikiria padre atanionaje mimi.

BASI NDUGU TUSISINZIE BALI TUWE MACHO DAIMA MSHITAKI WETU YU MACHO KUTUJARIBU.

Ufafanuzi wa Sala ya Baba yetu

Baba Yetu uliye mbinguni,
jina lako litukuzwe;
ufalme wako ufike,
utakalo lifanyike
duniani kama mbinguni.
Utupe leo mkate wetu wa kila siku,
utusamehe makosa yetu,
kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea.
Usitutie katika kishawishi,
lakini utuopoe maovuni.
Amina

Ufafanuzi wake uliotumiwa na Fransisko wa Asizi

BABA YETU mtakatifu kabisa: muumba, mkombozi, mfariji na mwokozi wetu.
ULIYE MBINGUNI: katika malaika na katika watakatifu, ukiwaangazia wawe na ufahamu, kwa sababu wewe Bwana ni mwanga; ukiwawasha wawe na upendo, kwa sababu wewe Bwana ni upendo; ukikaa ndani mwao na kuwajaza furaha, kwa sababu wewe Bwana ni wema mkuu kabisa, wema wa milele, ambaye kwako hutoka mema yote, na bila yako hakuna jema.
JINA LAKO LITUKUZWE: ujuzi wetu juu yako uwe wazi zaidi na zaidi, tuweze kujua upana wa baraka zako, urefu wa ahadi zako, kimo cha ukuu wako, kina cha hukumu zako.
UFALME WAKO UFIKE: utawale ndani yetu kwa njia ya neema yako na kutuwezesha kuingia katika ufalme wako ambapo unaonekana kama ulivyo, unapendwa kikamilifu, unatia heri ya kukaa nawe, unatia raha ya kukufurahia milele.
UTAKALO LIFANYIKE DUNIANI KAMA MBINGUNI: tuweze kukupenda kwa moyo wetu wote, kwa kukuwaza wewe daima; kwa roho yetu yote, kwa kukutamani wewe daima; kwa akili yetu yote, kwa kuelekeza nia zetu zote kwako na kwa kutafuta utukufu wako katika yote; kwa nguvu zetu zote pia, kwa kutumia uwezo na hisia zote za roho na mwili katika kuhudumia upendo wako na si chochote kingine; na tuweze kuwapenda majirani wetu kama tunavyojipenda, kwa kuwavuta wote kwa nguvu zetu zote kwenye upendo wako, tukifurahia mema ya wengine kama tunavyofurahia ya kwetu, na tukihuzunika pamoja na wengine kwa mabaya yanayowafikia, bila ya kumuudhi yeyote.
MKATE WETU WA KILA SIKU: Mwanao mpendwa Bwana wetu Yesu Kristo.
UTUPE LEO: kwa ukumbusho, ufahamu na heshima ya upendo ule aliokuwanao kwetu sisi na ya mambo yale ambayo alisema na kutenda na kuteseka kwa ajili yetu.
UTUSAMEHE MAKOSA YETU: kwa huruma yako isiyosemeka, kwa nguvu ya mateso ya Mwanao mpendwa, pamoja na stahili na maombezi ya Bikira mbarikiwa daima na ya wateule wako wote.
KAMA TUNAVYOWASAMEHE NA SISI WALIOTUKOSEA: na lolote tusilosamehe kikamilifu, wewe Bwana utuwezeshe kulisamehe kabisa, tuwapende kweli maadui wetu kwa ajili yako, na tuwaombee kwa bidii mbele zako, bila ya kumlipa yeyote ovu kwa ovu, bali tukijitahidi kumsaidia kila mmoja katika wewe.
NA USITUTIE KATIKA VISHAWISHI: kilichofichika au cha wazi, cha ghafla au cha muda mrefu.
LAKINI UTUOPOE MAOVUNI: yaliyopita, ya sasa na yajayo.
ATUKUZWE BABA NA MWANA NA ROHO MTAKATIFU KAMA MWANZO, NA SASA NA MILELEAMINA.

Ibada ya Huruma ya Mungu: Njia ya Ukarabati na Uongofu

Ibada ya huruma ya Mungu ni njia ya ukarabati na uongofu kwa kila mtu. Inatupa fursa ya kupitia maisha yetu, kujitambua na kuomba msamaha kwa makosa yetu. Kupitia ibada hii, tunaweza kupata uponyaji na kusafisha roho zetu.

Hapa kuna mambo muhimu ya kuzingatia katika Ibada ya huruma ya Mungu:

  1. Kuanza na toba: Kabla ya kuanza ibada ya huruma ya Mungu, ni muhimu kufanya toba kwa makosa yetu na kuomba msamaha kutoka kwa Mungu. Kwa sababu "Bwana hupenda toba ya kweli" (Zaburi 51:17).

  2. Tengeneza mioyo yetu: Ibada ya huruma ya Mungu inahitaji mioyo yetu iwe wazi, safi na tayari kupokea upendo wa Mungu. Tunaombwa kujitakasa dhidi ya dhambi, tamaa, na ubinafsi. Kama ilivyoelezwa katika kitabu cha Waebrania 12:14, "Tafuteni kila mmoja kuwa na amani na watu wote na utakatifu, bila huo hakuna mtu atakayemwona Bwana."

  3. Kuomba kwa moyo wote: Ibada ya huruma ya Mungu inahitaji kuongea na Mungu kwa moyo wote na kuomba kwa imani. Lazima tukiri makosa yetu na kumwomba Mungu atusamehe. Kama ilivyoandikwa katika 1 Yohana 1:9, "Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote."

  4. Kuwa na imani: Ni muhimu kuwa na imani katika Mungu na huruma yake. Ibada ya huruma ya Mungu ni nafasi ya kumwomba Mungu atutolee rehema na huruma yake. Kama ilivyoelezwa katika kitabu cha Waebrania 11:6, "Bila imani haiwezekani kumpendeza Mungu; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yupo, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao."

  5. Kujikabidhi kwa Mungu: Ibada ya huruma ya Mungu ni nafasi ya kumwomba Mungu atupe nguvu, ujasiri na utulivu. Ni nafasi ya kufungua mioyo yetu na kumruhusu Mungu atusaidie kuwa bora zaidi. Kama ilivyoelezwa katika kitabu cha Zaburi 55:22, "Mtu yeyote atupaye mzigo wake kwa Bwana, yeye atamtegemeza."

  6. Kutumia sakramenti ya kitubio: Ibada ya huruma ya Mungu ni nafasi nzuri ya kutubu na kusamehewa dhambi zetu. Lakini pia ni muhimu kushiriki sakramenti ya kitubio kwa mara kwa mara. Kama ilivyoelezwa katika Katekisimu ya Kanisa Katoliki, "sakramenti ya kitubio ni njia ya uhakika ya kusamehewa dhambi zetu na kupata amani na Mungu na kanisa."

  7. Kuonyesha huruma kwa wengine: Ibada ya huruma ya Mungu inahitaji pia kuonyesha huruma kwa wengine. Kama ilivyoelezwa katika Mathayo 25:40, "Na mfalme atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi."

  8. Kuwa na nguvu ya kuwa na wema: Ibada ya huruma ya Mungu inatupa nguvu ya kutenda mema na kujitahidi kuwa na wema. Kama ilivyoelezwa katika kitabu cha Wakolosai 3:12, "Basi, kama watu wa Mungu wateule, watakatifu na kupendwa, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu."

  9. Njia ya uponyaji: Ibada ya huruma ya Mungu ni njia ya uponyaji wa kiroho na kinga dhidi ya dhambi. Kwa kushiriki katika ibada hii, tunaweza kupata baraka, rehema na uponyaji kutoka kwa Mungu. Kama ilivyoelezwa katika kitabu cha Yeremia 17:14, "Uniponye, Ee Bwana, nami nitaponywa, niokoe, nami nitaaokoka, kwa maana wewe ndiwe sababu ya sifa yangu."

  10. Ibada ya huruma ya Mungu inatufundisha kuwa na shukrani na kuwa wastahiki: Tunaposhiriki katika Ibada ya huruma ya Mungu, tunakumbushwa kuwa na shukrani kwa Mungu kwa yote aliyotupatia. Tunatambua kuwa sisi si wa kustahili kupata upendo wa Mungu, lakini ni kwa rehema yake tu tunaweza kupata uponyaji na uongofu wetu.

Kwa hiyo, Ibada ya huruma ya Mungu ni njia ya ukarabati na uongofu kwa kila mmoja wetu. Inatupa nafasi ya kujitakasa, kuomba msamaha na kuwa karibu na Mungu wetu. Ni nafasi ya kupata uponyaji na kusafisha roho zetu. Shukrani kwa huruma ya Mungu, tunaweza kuwa na matumaini na kuwa na uhakika wa kuelekea kwenye uzima wa milele. Je, wewe ni mmoja wa wale wanaotamani uponyaji na uongofu katika maisha yako? Njoo basi, kwa Ibada ya huruma ya Mungu, ukapate uponyaji wa kiroho na baraka kutoka kwa Mungu wetu mwenye huruma.

Ni nini imani ya Kanisa Katoliki kuhusu maisha ya kuwa mtakatifu?

Ni nini imani ya Kanisa Katoliki kuhusu maisha ya kuwa mtakatifu? Hili ni swali muhimu sana kwa wakristo wote. Kuwa mtakatifu ni kielelezo cha maisha ya kujitolea kwa Mungu, kuishi katika mapenzi yake na kufuata maagizo yake yote. Ni kuitikia wito wa Mungu kwetu sisi wote kuishi maisha ya utakatifu.

Kanisa Katoliki linatufundisha kuwa kila mmoja wetu ameitwa kuwa mtakatifu. Katika barua ya kwanza ya Mtume Petro, anasema "Muwe watakatifu, kwa kuwa mimi ni mtakatifu" (1 Petro 1:16). Lakini ni vipi tunaweza kuwa watakatifu? Kanisa Katoliki linatufundisha kuwa njia pekee ya kuwa mtakatifu ni kwa kufuata maagizo ya Mungu, kuishi maisha ya sala, na kumtumikia Mungu na wenzetu.

Kanisa Katoliki linatufundisha kuwa kuwa mtakatifu ni jambo linalowezekana kwa kila mmoja wetu. Kwa mfano, tunaweza kuwa watakatifu kwa kuishi maisha ya kuwajali wengine, kwa kusameheana, kuwapenda na kuwatumikia wengine. Kanisa linatufundisha kuwa kuwa mtakatifu ni kumfuata Yesu kwa karibu, kufuata maagizo yake na kuwa na imani thabiti kwa Mungu.

Kanisa Katoliki linatukumbusha kuwa tunapokuwa watakatifu, sisi ni sehemu ya jumuiya ya watakatifu na kwamba utakatifu ni karama inayotolewa na Mungu. Utakatifu unatokana na neema ya Mungu na hakuna mtu anayeweza kuwa mtakatifu kwa nguvu zake mwenyewe. Kwa kufanya hivyo, Kanisa linatufundisha kuwa tunahitaji kudumisha maisha yetu ya kiroho, kwa kuishi maisha ya sala, kuwahi sakramenti na kufanya kazi ya kiroho.

Kanisa Katoliki linatufundisha kwamba kila mtu ana wajibu wa kutafuta utakatifu. Hii ina maana kuwa tunapaswa kutafuta kumjua Mungu zaidi, kumtii na kumtumikia. Katika Catechism ya Kanisa Katoliki, tunasomwa kwamba "Mtakatifu ni mtu aliyejisalimisha kikamilifu kwa Mungu. Kwa hiyo, kuishi maisha ya utakatifu ni kuwa na urafiki wa karibu na Mungu" (CCC 2013).

Kanisa Katoliki linatufundisha kuwa ili kuwa mtakatifu lazima tujifunze kutawala tamaa zetu, kutetea ukweli, kusamehe, kuwa na msamaha na kujitolea kwa kazi ya Mungu. Tunahitaji kuwa jasiri na kuwa na nguvu za kiroho ili kupambana na ulimwengu wa dhambi na uovu.

Katika hitimisho, Kanisa Katoliki linatufundisha kuwa kila mmoja wetu ana wajibu wa kuitikia wito wa Mungu wa kuwa mtakatifu. Kwa kufanya hivyo, tunahitaji kuwa karibu na Mungu, kuishi maisha ya sala na kutumia maisha yetu kujitolea kwa kazi ya Mungu. Tunahitaji kuwa na imani thabiti katika Mungu na kujitahidi kutimiza mapenzi yake. Kwa kufanya hivyo, tutaweza kufikia utakatifu wa kumjua Mungu na kuishi maisha ya utakatifu.

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About