Mafundisho ya Msingi ya Kanisa Katoliki: Makala za Katoliki

Maana ya siku ya Jumatano ya Majivu

Utangulizi

Wakati umetimia na ufalme wa Mungu umekaribia, tubuni na kuiamini Injili, (Mk 1:15), haya ndiyo maneno ya kwanza ya Yesu ambayo kadri ya Mwinjili Marko yanafungua kazi ya hadhara ya Yesu, kwa maana hiyo kazi ya Yesu inaanza kwa kuwaandaa watu katika toba ili hatimaye, wapate kuukaribia au kuingia katika ufalme wa Mungu.
Na wakati ndiyo sasa. Wakati ni sasa, Yesu anatuhubiria na Kwaresima imewadia, na ndiyo maana siku ya Jumatano ya majivu, kwa kuitikia mwito wa maneno ya Yesu kanisa linatualika kuingia katika kipindi cha Kwaresma, ambacho ni kipindi cha kujikusanya, kujitayarisha, kijitengeneza na kujikarabati hasa kwa toba, kufunga, kusali na kujitoa sadaka zaidi mambo yanayorutubishwa kwa tafakari ya kina ya Neno la Mungu.

Nini maana ya Jumatano ya majivu?

Jumatano ya majivu ni mwanzo wa kipindi cha kwaresima katika kanisa, Ni mwanzo wa siku arobaini za kutafakari kwa undani fumbo kuu la upendo wa Mungu linalofunuliwa kwa kujitoa kwake na kufa msalabani, kifo cha aibu cha Msalaba ili kuichukua aibu yetu au dhambi zetu.

Kwaresma ni nini?

Kwaresma ni kipindi cha siku 40 cha kujiandaa kuadhimisha Sherehe kuu ya PASAKA yaani kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Tunajiandaa kwa Kufunga Kusali, Kutubu, na Matendo mema.
Mama kanisa anatupatia kipindi hiki ili tuweze kutafakari njia na mienendo yetu na kubadilika kama haimpendezi Mungu
Tunapofunga tunatakiwa kuzuia vilema vyetu na kuviacha kabisa, tunaomba kujaliwa moyo wa toba, tunainua mioyo yetu na tunaomba Mungu atujalie nguvu na tuzo. Haitoshi tu kukiri makosa yetu bali tunahimizwa kuungama na kutubu hayo makosa na kuwa tayari kuanza upya. Kipindi cha Kwaresima huanza tangu Jumatano ya majivu. Mwanzoni mwa kazi yake ya kuhubiri Habari njema Yesu anaanza kwa kusema tubuni na kuiamini Injili – Mk 1,15. Maneno haya haya tunayasikia/tumeyasikia kila tunapopakwa majivu. Mwaliko huu wa Yesu unatuingiza katika kipindi cha toba – tubuni na kuiamini Injili. Huu ni mwaliko wa uzima. Ni mwaliko ili tuongoke, tuanze maisha mapya, maisha ya sala, kufunga na kutoa sadaka.

Kwa nini ikaitwa Jumatano ya majivu?

Jina linatokana na desturi ya kumpaka mtu majivu kichwani pamoja na kumtamkia maneno ya kumhimiza afanye toba inavyotakiwa na kipindi hicho cha liturujia kinachoandaa Pasaka.
Kwa kawaida siku ya Jumatano ya majivu unaanza mfungo unaofuata kielelezo cha Yesu kufunga chakula siku arubaini jangwani baada ya kubatizwa na Yohane Mbatizaji na kabla ya kuanza utume wake mwenyewe.

Nini maana ya majivu tunayopaka?

Majivu ni ishara ya majuto, nayo hufanywa visakramenti kwa kubarikiwa na kanisa. Tunapopakwa majivu katika paji la uso hutusaidia kutafakari na kutukumbusha kuwa wanadamu sisi tu mavumbi na mavumbini tutarudi. Hutukumbusha zaidi kuwa maisha ya hapa duniani tunapita na safari yetu itakamilika pale tutakapoungana na Bwana na mwokozi wetu katika ufalme wako.
Angalia; Isaya 61:3, Ester 4:1-3, Yeremia 6:26, Ezekieli 27:30, Mathayo 11:21 na Luka 10:13.

Kwa nini majivu yanapakwa kwenye paji la uso na si vinginevyo?

Ishara yoyote iwekwayo katika paji la uso huonesha umiliki (soma Ufunuo 7:3, Ufunuo 9:4, Ufunuo 14:1, Ezekieli 9:4-6, ). Tunapochorwa ishara ya msalaba katika paji la uso ni ishara kwamba sisi tupo chini yake yeye aliyekufa msalabani kwa ajili yetu.
Hali kadhalika hutukumbusha ishara ya msalaba tuliyochorwa na mafuta matakatifu siku ya ubatizo wetu, hutukumbusha ahadi tuliyoiweka siku hiyo ya ubatizo na kutuita tuishi maisha ya utakatifu

Padri hutamka maneno gani wakati anapaka majivu?

Tunapopakwa majivu Padre husema; Mwanadamu kumbuka u mavumbi na mavumbini utarudi AU Tubuni na kuiamini Injili.

Maneno anayosema padre yana maana gani?

Maneno haya kwa upande mmoja hutukumbusha tunapoelekea, tusisikitike kwamba siku moja tutarudi mavumbini bali tuwe na furaha kwani wakati miili yetu unarudi mavumbini roho zetu zitakwenda kuungana na Mungu Baba mbinguni.
Hivyo maandalizi tunayoalikwa kuyafanaya si maandalizi ya kuelekea mavumbini bali maandalizi ya kuelekeza roho zetu mbinguni. Ndio maana pia twaambiwa tubuni na kuiamini Injili.

Majivu tunayopakwa yanatoka wapi?

Majivu tunayopakwa hutoka katika matawi yaliyotumika katika jumapili ya matawi ya mwaka jana. Majivu haya hubarikiwa na kuwa visakramenti. Hivyo majivu yanapoashiria toba na majuto pia hutukumbusha wema wa Mungu na utayari wake wa kutusamehe.

Kwa nini unatumia matawi ya Jumapili ya Matawi?

Matawi haya yalimkaribisha Yesu Yerusalemu akiwa tayari kufa kwa ajili ya dhambi zetu, yalimpokea mfalme kwa furaha na shangwe kuu. Matawi haya yanapochomwa na sisi kupakwa majivu yetu yanatukumbusha kuwa ni kwa ajili ya dhambi zetu Mungu alimtoa mwanae wa pekee kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu sisi wanaadamu. Hivyo hututafakarisha kuacha dhambi.

Kanisa limekataza nini siku ya Jumatano ya majivu?

Tumekatazwa kula chakula siku ya Jumatano ya Majivu na kula nyama siku ya Ijumaa Kuu katika Amri ya Pili ya Kanisa.

Nani analazima kufunga siku ya Jumatano ya majivu na Kwaresma?

Kila Mkristo aliyetimiza miaka 14 na zaidi anapaswa kufunga kula nyama (Ijumaa kuu) na mwenye miaka zaidi ya 21 kufunga chakula Jumatano ya Majivu

Tunaposema kujinyima wakati wa Kwaresma tunamaana gani?

Kujinyima ni kujikatalia kitu ukipendacho mfano nyama, pombe, sigara, muziki, safari, maongezi n.k.

Mwisho

Wakati wa Kwaresma Waamini wanapaswa kujitakasa zaidi kwa kusali, kufunga, toba na matendo mema
Kipindi cha Kwaresima ni fursa makini ya kumkimbilia Mwenyezi Mungu, kwani kwa njia ya dhambi wamejikuta wakiwa mbali na Uso wa huruma ya Mungu, kiasi hata cha kupoteza imani na matumaini kwa Mwenyezi Mungu. Hii ni changamoto ya kumpenda Mungu na jirani badala ya kukumbatia malimwengu yanayoendelea kuwatumbukiza katika utupu wa maisha ya kiroho. Kwaresima ni kipindi cha waamini kukimbilia na kuambata huruma ya Mungu inayoganga na kuponya dhambi. Ni wakati wa sala, upendo na kufunga.

Huruma ya Mungu: Chemchemi ya Upendo Usiokwisha

Huruma ya Mungu ni chemchemi ya upendo usiokwisha. Tunaishi katika dunia ambayo imejaa shida na mateso, lakini tunapaswa kukumbuka kwamba Mungu daima yuko nasi. Uaminifu wetu kwake unatupa nguvu ya kuvumilia na kushinda majaribu. Katika makala hii, tutaangazia zaidi juu ya huruma ya Mungu na jinsi inavyotusaidia katika safari yetu ya kiroho.

  1. Huruma ya Mungu ni upendo wake usiokwisha. Yeye daima anatupenda, hata katika nyakati ngumu zaidi. Kwa mujibu wa Zaburi 103:8, "Bwana ni mwenye huruma na neema, si mwepesi wa hasira, naye ni mwingi wa rehema." Kwa hiyo, tunaweza kutegemea upendo wake daima.

  2. Huruma ya Mungu inatupatia msamaha wa dhambi zetu. Kwa mujibu wa Kitabu cha Isaya 43:25, "Mimi, naam, mimi ndimi yeye anayefuta makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitakumbuka dhambi zako." Kupitia msamaha wa dhambi, tunaweza kuwa huru kutoka kwa mzigo wa hatia na kuanza upya.

  3. Huruma ya Mungu inatupatia faraja. Katika Warumi 8:28, tunasoma, "Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao ili mema yote yawasaidie, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake." Kwa hiyo, tunapaswa kuwa na imani kwamba Mungu anatenda kazi katika hali zetu zote na kwa hivyo tunapaswa kupata faraja.

  4. Huruma ya Mungu inatupatia nguvu ya kutenda mema. Kwa mujibu wa Wafilipi 4:13, "Naweza kufanya mambo yote katika yeye anitiaye nguvu." Bila huruma ya Mungu, tungekuwa hafifu na hatuna nguvu ya kutenda mema. Lakini kwa sababu ya upendo wake, tunaweza kupata nguvu zote tunazohitaji.

  5. Huruma ya Mungu inatupatia tumaini. Kama ilivyoelezwa katika 1 Petro 1:3, "Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema yake yenye wingi ametuletea uzima wa milele kupitia kwa ufufuo wa Yesu Kristo kutoka kwa wafu." Huruma ya Mungu inatuonesha kwamba ana mpango mzuri kwa ajili yetu, na kwamba tunaweza kuwa na tumaini kwa ajili ya siku zijazo.

  6. Huruma ya Mungu inatupatia uwezo wa kusamehe wengine. Tunapaswa kuwa na huruma kwa wengine kama vile Mungu anavyokuwa na huruma kwetu. Kama tunavyojifunza katika Mathayo 18:21-22, "Kisha Petro akamwendea, akamwuliza, Bwana, ndugu yangu atanikosea mara ngapi niweze kumsamehe? Kwa kuwa mara saba?" Yesu akamjibu, "Sikuambii hata mara saba, bali hata mara sabini mara saba."

  7. Huruma ya Mungu inatupatia amani ya ndani. Katika Yohana 14:27 Yesu alisema, "Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; nawaambia si kama ulimwengu unavyowapa mimi nawapa." Huruma ya Mungu inatupa amani ya ndani ya kuwa tunaweza kuwa na uhakika wa upendo wake na wokovu wetu.

  8. Huruma ya Mungu inatupa msukumo wa kuwahudumia wengine. Kama ilivyoelezwa katika 1 Yohana 3:17-18, "Lakini yeye mwenye mali ya dunia, akimwona ndugu yake akiteswa na kuufumba moyo wake kwake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake? Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa kazi na kweli." Tunaweza kumwonyesha Mungu tunampenda kwa kuwahudumia wengine.

  9. Huruma ya Mungu inatupa msamaha wa kila siku. Kama ilivyoelezwa katika Zaburi 103:12, "Kama mbali sana alivyo kuondosha makosa yetu na kututupa mbali na maovu yetu." Huruma ya Mungu inatupa msamaha kila siku, tunapoomba msamaha wa dhambi zetu.

  10. Huruma ya Mungu inakuja kwa njia ya sakramenti. Kama ilivyoelezwa katika Katekisimu ya Kanisa Katoliki, "Sakramenti ya kitubio haiwezi kukosekana kwa kila mmoja anayetaka kuishi kadiri ya mapenzi ya Mungu.. Katika sakramenti ya kitubio, tunapokea msamaha wa Mungu kwa dhambi zetu na tunapata nguvu ya kutenda mema.

Kwa hiyo, huruma ya Mungu ni muhimu sana katika safari yetu ya kiroho. Tunahitaji kuiweka imani yetu katika upendo wake usiokwisha na kuwa na tumaini la uzima wa milele. Tunapaswa kusamehe wengine na kuwahudumia kama Mungu anavyofanya kwetu. Na wakati tunapotenda dhambi, tunapaswa kutubu na kutafuta msamaha kupitia kwa sakramenti ya kitubio. Je, nini maoni yako juu ya huruma ya Mungu? Unafanya nini ili kuwa na huruma kwa wengine katika maisha yako ya kila siku?

Shopping Cart
33
    33
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About