Mafundisho ya Msingi ya Kanisa Katoliki: Makala za Katoliki

Uzinzi na Uasherati ndio mtego wa kizazi hiki

Uzinzi na uasherati wakati huu umekuwa ndio sumaku kuu ya kuwanasa watu ili waende jehanamu.

Sumaki hii imewanasa hata ambao hawakutegemewa wala kutarajiwa.

Uzinzi uzinzi uzinzi umekuwa kama perfume ya kujipulizia kila Mara mtu akipenda.

Uasherati umekuwa kama heshima ya kibinadamu kwa vijana wengi.

Mbingu zimenyamaza kwa sababu iko jehanamu inawangoja wazinzi na waasherati.

Dhambi hii imekuwa sumaku kubwa ya shetani ya kukamata wanadamu ili waende jehanamu.

Wanadamu wa Leo ukimwambia kwamba aache uzinifu maana wazinzi na waasherati hawataenda uzima wa milele, mtu huyo anakuambia unamhukumu.

Ni Neno la MUNGU ndile limesema katika maandiko mengi tu kwamba wazinzi na waasherati sehemu yako itakuwa katika ziwa la moto.

Hata makanisani baadhi ya watu wamenasa kwenye sumaku hii.

Dada mmoja ambaye kila wiki anasimama na kushika mic kanisani kwao siku moja aliniambia kwamba hawezi kumaliza wiki bila kufanya ngono, na hajaolewa. Niliumia sana rohoni nikamwambia aache kutumika madhabahuni, yeye akasema itakuaje maana yeye ndiye tegemeo.

Mama mmoja alisema yeye ana mume mema sana na mume wake ni mwaminifu sana katika ndoa yao lakini yeye huyo mama ndio hutoka nje ya ndoa Mara kwa Mara, ni hatari inayohitaji neema ya MUNGU tu ili kutubu na kuacha.

Mama mmoja yeye ana watoto zaidi ya wawili na yuko katika ndoa lakini hana uhakika kama watoto wale ni wa mume wake wa ndoa, ni hatari sana.

Baba mmoja akiwa ndani ya ndoa amezaa watoto zaidi ya watatu nje ya ndoa tena wanawake zaidi ya wanne(4) tofauti tofauti.

Mwanaume moja ambaye husimama madhabahuni yeye kila Mara humdanganya mkewe kwamba anaenda safari kumbe ana mahawara karibia kila mkoa, ni hatari sana.

Watu wengi sasa wanaona uzinzi na uasherati ndio fashion nzuri ya wakati kuu.

Kila kijana ana girlfriend kwa lengo la ngono tu na sio vinginevyo.

Kila binti ana boyfriend kwa ajili ya uasherati.

Ukitaka watu wakuchukie basi kemea uzinzi na uasherati.

Watu wengi wamekuwa vipofu wa kiroho kwa sababu ya uzinzi na uasherati.

Lakini upo mwisho mmoja kwa watenda dhambi wote ambayo ni jehanamu.

Ndugu unahitaji kutubu Leo na kuacha dhambi.

Ndugu mmoja akasema yeye anaishi maisha matakatifu ila dhambi moja tu yaani uzinifu ndio imemshinda, hiyo ni hatari.

Leo hata ndoa takatifu zimeadimika maana wahusika huanza kwanza uzinzi na uasherati ndio baadae ndoa, ndugu mnahitaji kutubu.

Ndugu yangu unayenisikiliza kwa njia ya ujumbe huu nakuomba tubu na acha dhambi hiyo.

Amua kuiacha.

Mwisho wa uzinzi na uasherati ni kifo(Mauti) na baada ya kifo ni hukumu(Waebrania 10:27)

Nimekuonya wewe Leo ili ukishupasa shingo usije ukalaumu siku ile ukiwa katikati ya bahari ya moto huku kifo kimezuiliwa ili uteseke milele.

Mimi naamini utatengeneza ndugu baada ya kuusoma ujumbe huu.

Mimi naamini utaachana na mahawara na kuanza kuiheshimu ndoa yako.

Mimi naamini hutamsaliti tena mkeo/Mumeo.

Mimi naamini utaachana na huyo girlfriend/Boyfriend, wengine wanao zaidi ya mmoja, nakuomba ndugu achana nao.

Kijana au binti kaa tulia hadi wakati wako wa ndoa.

Uliyenisikia na utatubu na kuacha dhambi hiyo, MUNGU akubariki sana.“`

ALIYE NA AKILI AWEKE MOYONI MANENO HAYA. AMINA

Ishi kama Penseli ili uwe mtu bora

Muumbaji wa penseli alipomaliza kuiumba penseli yake aliiambia mambo muhimu ya kuzingatia ili iweze kuwa penseli bora kabla hajaituma kuingia kazini kwa matumizi.

โ€œKuna vitu sita unatakiwa uvitambue, โ€œ Aliiambia penseli,

โ€œKabla sijakutuma kwenda kutumika, unatakiwa uviweke akilini vitu hivyo na usivisahau kamwe. Vitakusaidia siku zote na utakuwa penseli bora maisha yako yote.โ€

Alisema muumbaji wa penseli.

โ€œMoja,โ€ alianza kuvitaja,โ€utakuwa na uwezo wa kufanya vitu vingi, lakini kama utakubali na utaruhusu kuongozwa na mkono wa mtumiaji wakoโ€

โ€œMbiliโ€ aliendelea kutoa nasaha, โ€œutapata maumivu makali kutokana na kuchongwa mara kwa mara. Lakini vumilia kwani itakusaidia kuwa penseli bora na kuandika vizuri.โ€

โ€œTatu, utakuwa na uwezo wa kusahihisha makosa utakayo yafanya.โ€

โ€œNne, kitu pekee cha muhimu katika maisha yako ni kile kilicho ndani yako kwa sababu ndicho chenye uwezo wa kuandika.โ€

โ€œTanoโ€ alisisitiza mtengenezaji penseli, โ€œkwenye kila sehemu utakayotumika, utaacha alama yako. Hata ikiwa ni kwenye sehemu ngumu au mbaya kiasi gani, ni lazima alama yako ibaki.

โ€œNa sitaโ€, alimalizia muumbaji yule wa penseli, โ€œipo siku utaisha na kupotea. Hivyo usiwe na hofu wala woga wala hudhuni uikaribiapo siku hiyo na ukaogopa kutimiza wajibu wako kwa kuhofia kuisha. Ukiogopa kuisha hautotumika na umuhimu wako hautonekana kwani hautatimiza wajibu uliombiwa kuufanyaโ€

Penseli ilielewa na kuahidi kukumbuka na ikaingia sokoni ikiwa na dhamira yake moyoni.

Sasa tutumie mfano huo wa penseli katika maisha yetu halisi. Ukivikumbuka vitu hivyo sita ilivyopewa penseli, utaweza kuwa mtu bora kabisa kwenye maisha yako yote.

Moja, una uwezo wa kufanya mambo mengi na makubwa, kama utajiweka kwenye mikono ya Mungu.

Mbili, utakutana na magumu mengi ya kuumiza, lakini hayo ndiyo yatakufanya uwe mtu imara na bora, usiyakimbie.

Tatu, una uwezo wa kurekebisha makosa yote uliyoyafanya. Usijilaumu.

Nne, sehemu yako ya muhimu ni ile iliyo ndani yako kwani ndiyo inayoandika maisha yako. Ilinde.

Tano, kila sehemu utakayopita, acha alama yako kwa kufanya mazuri yatakayokufanya ukumbukwe daima, bila kujali mazingira. Timiza wajibu wako kwa kiwango cha juu.

Sita, tambua kuwa ipo siku utakufa. Usiwe na hofu yoyote juu ya kifo kwani ukiogopa kifo hutafanya lolote hapa duniani.

Tumia mfano huu wa penseli upate ujasiri wa kutambua kuwa wewe ni mtu muhimu hapa duniani na umeumbwa kwa madhumuni maalumu na umepewa uwezo mkubwa sana na Muumba wako! Ni wewe pekee mwenye uwezo wa kutimiza dhamira uliyotumwa na Muumba.

UBARIKIWE SANA.

Shopping Cart
29
    29
    Your Cart
    ๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About