Vituko Vya Wikiendi
KICHEKESHO: Ajira ngumu!! Cheki hawa walivyoamua kujiajiri
Jamaa mmoja alienda kuomba kazi Mbuga ya Wanyama, akaambiwa nafasi ya Kazi ipo ila hakuna Sokwe, “hivyo utajifanya Sokwe na tutakupa ngozi utavaa”
Jamaa siku ya kwanza akavaa, walipokuja watalii mambo yalienda vizuri, Siku iliyofuata Banda lake liliwekwa juu ya Banda la Simba, Jamaa ktk kuongeza mbwembwe akawa anarukaruka, kwa bahati mbaya si akaangukia ndani ya Banda la Simba, akawa anapiga kelele “Mama nakufaaa!”
Mara yule Simba akamwambia “Acha Ufala ww kelele za nini sasa, mimi mwenyewe Binadamu! rudi kwenye Banda lako kabla watalii hawajaja watatushtukia! chezea ajira ww”………!!
😂😂😂😂😂😂😂😂👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻
Angalia alichojibu huyu mwanafunzi, Ungekua wewe ni mwalimu wake ungemfanyaje?
Mwanafunz alikuwa kila siku anachelewa shule, na kila siku alikuwa anachapwa, basi siku moja mwalimu akaona ngoja amuulize.
Mwalimu: Mbona unachelewa kila siku?
Mwanafunzi: Nakaa mbali mwalimu
Mwalimu: (huku ana hasira akauliza)Mbali mbinguni?
Mwanafunzi: Mbinguni kwa mbele😂😂😂😂😂
Kuna watu makauzu ila huyu kazidi.. Soma hii!
Kakubaliana vizuri na msichana fulani hivi kuwa aibuke gheto, mchizi kajipanga vizuri kabisa…. mara saa nne hivi mdada kasema hana nauli.
Mshkaji kajikunja kamtumia Elfu tano maana mwenye shida alikuwa ni yeye……
Baada ya nusu saa yule dada akamtumia meseji.
“Jamani mpenzi, kumbe baba hatoki nilijua atatoka… sorry bae sitaweza kuja kwa leo… sooo sorry!”
Mshkaji jiii! hajajibu kitu…..
Baada ya muda kidogo meseji ikaingia katika simu ya binti, akajua mchizi kajibu. Mh! kutazama ni meseji kutoka Mpesa.
“CA90F0511 IMETHIBITISHWA Tshs 5000 ILIYOTUMWA KIMAKOSA KATIKA ACCOUNT YAKO IMETOLEWA SALIO LAKO NI Tshs 5”
Halafu ndo ikaingia meseji ya mshkaji.
“BASI POA SIKU NYINGINE KAMA VIPI”
#dada wa watu mashavu yakamshuka… hakuamini kilichotokea…. yaani jamaa keshawapigia Voda na pesa fasta imezuiliwa……
Jinsi ya Kubana matumizi X-mass
Badala yakupika PILAU tutapika TAMBI kwenye Xmas maana tutakua tumeokoa sh.15,000/= Vitunguu swaumu 2000, Vitunguu maji 1000, hiliki 1000, Magome 1000, Michele wa 2000, Soda 3000, Nyama 5000 . Fedha hizi zitatumika kununua mfuko wa cement ili tuanze kujaza kibubu cha ujenzi wa nyumba badala ya kupanga. Karibuni saana maji ya kunywa tumechemsha ndoo nzima.
🎀✨Marry Xmas & Happy new year.✨🎀
Alichofanya maasai baada ya kupanda Tax
Baada ya kupanda daladala aina ya DSM kutoka Mbagala chalambe mpaka Mwenge na kulipa sh 500.Masai akachukua tax wakati wa kurudi.walipofika sasa shughuli ilikuwa hivi.
Masai: we dureva? Naulisa Ng’ombe na mbusi ipi ngali?
Dereva: Ni ng’ombe ghali Masai.
Masai: kwanini Ng’ombe ngali?
Dereva: kwa sababu ni mkubwa zaidi ya mbuzi
Masai: umepata..na mbusi na kuku ipi ngali
Dereva: ni mbuzi kwa sababu nae ni mkubwa kuliko kuku.
Masai: Umepata..
Masai: sasa me nimekwenda kule mwenge kwa ngali kubwa nikalitoa sh. 500 hii yko ndogo unasema nikupe 40,000 wewe acha wizi.. Nitakupa 250 Tu..wee acha lbia morani…!!!
Eti kupooza chai kwa kizungu inaitwaje?
Kuishi kijijini kunahitaji moyo sana
..unaenda kuoga, unakumbuka kuwa umesahau sabuni…unaenda kuchukua sabuni kurudi bafuni, unakuta ng’ombe amekunywa maji yote..unaamua kufuata mengne,unarudi unakuta mbuzi kala sabuni…😂😂😂😂
Angalia anachojibu huyu babu. Wazee wengine bwana
Babu: Mjukuu wangu ngoja nikusimulie hadithi ya mimi babu yako kwenye vita ya kagera
Mjukuu: Niambie babu
Babu: Kwenye vita ya kagera tulienda sehemu tukakamatwa wote askari na maadui wakatuambia chagueni kuuliwa au kubakwa.
Mjukuu: Sasa babu wewe ulichagua nn?
Babu: Niliuliwa!!!
Utoto bwana. Raha sana!
Utoto buana! eti mnacheza mpira wa makaratasi(chandimu) unapiga chenga kibao afu ukifika golini ufunge unakuta goli hamna kumbe mwenye ndala zake ameitwa kwao😆
Cheki kilichotokea baada ya kufumaniwa
Nimefumaniwa hapa na jamaa ameniambia nitulie tuyamalize kishikaji, yaani nisijali sasa ametoka nje nasikia ananoa kisu nadhani anataka anichinjie kuku!
WATU WENGINE WANA ROHO NZURI!😋😋😋😋
Eti kwani wewe ni turubali?
Unakuta MTU mwaka Mzima
Umehudhuria, birthday parties 20 , misiba 30,
Mikutano kanisani 40, Ndoa 80 na bado uko Single Kwani wewe ni turubai jaman??
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Madogo wa sikuizi ni kiboko, cheki huyu alichokifanya akiwa darasani na mwalimu wake
Muda wa kwenda nyumbani ulikuwa umefika, mwalimu
akasema: yeyote atakaye jibu swali langu lolote kwa usahìhi ataondoka asiye jibu atabaki.
Dogo mmoja akatupa begi nje ya dirisha.
Mwalimu akauliza nani katupa ilo begi nje?
Dogo akajibu fasta mimi. Akafungua mlango akaenda kwao.
neno moja kwa dogo
Utoto raha..! Angalia hawa watoto wanachokifanya sasa
Leo nimepulizia Air Fresh yenye Harufu ya Pilau nyumbani kwangu sasa watoto wa Jirani wamehamia Mlangoni kwangu ndio wanacheza hapo. Kila nikitoka wananisalimia. Mama yao ndio kanimaliza kabisa nimetoka akaniambia
“Kumbe wewe ni Mpishi mzuri, Hongera”
Imebidi nisirudi nyumbani maana wale watoto wanaweza kuingia ndani kabisa na pilau hakuna.
#UTOTO RAHA 😂
😂😂😂😂👆🏻👆🏻👆🏻
Ameniomba nimfungulie akaunt facebook cheki nilichomjibu
Leo nimechoka zangu alafu shangazi amekuja anataka nimuunganishe facebook. Imebidi nimwambie
lazima awe na picha passport size 4 kwaajili ya kuweka profile picture, barua kutoka kwa afisa mtendaji na Atm card ya nmb bank. Alafu awe na marefa wanne ambao wamekuwa facebook for more than 3 years. Amesema
hataki tena kujiunga fb!
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Saa ivi niko zangu nimelala naendelea kupunguza uchovu
Ikitokea hii kwenye chumba cha mtihani
Upo kwenye chumba cha mtihani,
maswalii yamekupiga kinyama
Unaamua kuchukua smartphone ugoogle kisha ucopy na kupaste kwenye booklet yako,
Ghagfla lecturer aningia na wewe kwa woga wako unaficha calculator na kuweka simu mezani,
Hapo ndo utajua shetani naye alikua anasimamia paper.
😂😂😂😂😂
Utani wa wahindi, cheka kidogo
Mhindi afaulu mtihani wa Kiswahili
(1) Mfa maji ?……………….. Tampa life jacket.
(2) Mwenda pole?………… Tachelewa fika.
(3) Usipoziba ufa ?……….. Mizi taona mpaka dani.
(4) Usilolijua ?……………… Uliza google.
(5) Mbio za utelezini ?……. Chafua guo yako.
(6) Ukipenda boga ?……… Ngoja mezi ya ramzani tapata.
(7) Ukiona vinaelea ?…….. iko nyepesi hiyo.
(8) Maji yakimwagika ?…… Mambie dada tapiga deki.
(9) Chelewa chelewa ?……… Takosa guo ya sikukuu…
(10) Kila ndege ?………….. …Hutua Airport
(11) Bandu bandu ?….. …….Rafiki yake Jecha
(12) Mtaka cha Mvunguni ?… Ondoa tanda
(13) Simba mwenda kimya?….Kama sio gonjwa basi haina njaa.
(14) Aisifuye mvua ?………. Najua iko Mkulima hiyo
(15) Barabara ndefu ?…….. Ongeza mwendo au tachelewa fika.
(16) Mlanawe hafi nawe ila?…. Takimbia
(17) Asie sikia la mkuu ? …….. Tapeleka jela
(18) Hasira za mkizi ? …………..Tatafuna veve
(19) Mchamba wima ?…….. Karibu ya Hurumzi
(20) Akumurikae mchana ?….Kipofu hiyo
(21) Mficha maradhi ?…….. Taenda Loliondo
(22) Mkataa wingi ? ……….Taenda Chadema
(23) Bendera ?……………. Kama sio ya CCM, ya CUF
(24) Baniani mbaya ?……. Peleka Bombay Lakini sio HB kweli, naonea tu
(25) Akili nyingi ?………. Tapasi mtihani yote
(26) Penye kuku wengi ? …….. Chija bili tatu ivi, hapana mtu najua.
Wale wa kupenda kupewa pewa namba za simu soma hii
Unaomba namba ya simu ya mdada af anakunyima ila unalazimisha akupe anaona kuliko muendelee kuongea bora tu akupe anakutajia 071112016 unafuraahi unaondoka unafika nyumbani unajaribu kuipiga but kabla hujapiga unagundua alikutajia tarehe ya leo Wadada acheni hizo 😝😝😝😝🏃�🏃�🏃�🏃
Huyu bibi kweli kiboko, cheki alichofanya akiwa na babu
Bibi na Babu walisafiri wakielekea kwa mtoto wao ambae hawajamuona zamani.
Walipofika njiani wakawa wamechoka Sanaa. Wakaamua kutafuta hotel ili walale.
Wakakubaliana walale kwa masaa 4. Wakalala, Walipoamka, mfanyakazi wa Hotel akawatoza Tsh. 500,000/=
Wale wazee wakashangaa hata kama ni hotel ya kisasa lakini sio laki tano kwa masaa 4.
Babu akagoma kulipa akasema aitiwe meneja.
Meneja akaja kuwasikiliza
Babu: ” Kwanini bili ni kubwa hata kama ni hotel ya kisasa?”
Manager;“kuna maswiming puli, ya kisasa “
Babu; “Lakini hatukuyatumia”
Manager; “Ah ah ah. Lakini mungeweza kama mngetaka”
Babu: “Hata hivo bado haithamini kuwa laki 5”
meneja: “Pia Kuna waimbaji kutoka sauzi, Uganda , Congo”
Babu: “Lakini sisi hatukuwasikiliza”
Meneja: “Ndiooo. Lakini mngeweza kama mngetaka”
Babu; aka give up na kumwambia mkewe andika cheki uwape,,
Bibi akaandika akampa meneja.
Meneja anaangalia anaona sh. 50,000
Akashangaa na kusema. “VP mbona hamsini'”
Bibi akajibu “450,000 ya kulala na mimi”
Meneja akajibu; “Lakini sijalala”
Bibi :“ungeweza kama ungetaka”
Huyu Baba ni noma, Cheki anachomjibu huyu mtoto wake
Mtoto: baba eti Botwasna ipo wap?
Baba: angalia itakuwa humo humo kabatini maana mama yako nae kwa kuficha kuficha vitu hajambo…
Kilichotokea wakati mchungaji akifungisha ndoa ya Mashoga
Mchungaji mmoja baada ya kuwafungisha ndoa “MASHOGA” wawili alipata wakati mgumu kutamka kuwa “sasa ninyi ni MKE na MUME”
atafanyaje wakati wote ni wanaume? mchungaji akapiga moyo konde na kusema “tangu sasa ninyi ni MAN UNITED”
Recent Comments