Vituko Vya Mchana Huu
Wachaga wana mambo mbele ya hela, angalia hii bili ilivyomchanganya MASSAWE
MASSAWE alienda na marafiki zake bar kunywa, baada ya kumaliza kutumia akaletewa bili kama ifuatavyo:
Manka 35,000
Marieta 20,000
Kekuu 30,000
Kitime 15,000
Kinabo 10,000
TOTAL 110,000/=
MASSAWE akaicheki akasema “Wote nitawalipia lakini huyo “TOTAL” Yesuu simlipii.
Kwansa anamiliki sheli kibao sa mafuta hapa bongo. Shensi taip ! Na amekunywa nyingi kuliko wote alipe mwenyeweβ¦
Kingereza sio mchezo, angalia huyu anavyojichanganya
Jamaa fulani alikuwa ame2lia beach mzungu akapita akamuliza “Are u relax ? Jamaa akawa hamuelewi akamjibu No! Mzungu mwengine akapita akamuliza vilevile akajibu No!
Akaona hapa anasumbuliwa akasogea mbele kidogo ya maji akamuona mzungu mmoja alikuwa ame2lia. Akamuliza “are u relax? Mzungu akajibu yes jamaa akamkata makofi mawili na kumwambia kumbe we ndo relax inuka unatafutwa na wenzakoβ¦..Shenz mkubwa mie nasumbuliwa na wenzako kule we umejikausha!!
Tofauti kati ya Binti wa Kizungu na Binti wa Kibongo mwanamme anapotoka kuoga
Tofauti ya Binti wa Kizungu na Binti wa Kibongo pale ambapo Mwanaume wake atokapo kuoga.
Binti wa Kizungu:Β Baby you look nice and fresh.Β
Binti wa Kibongo:Β Naona safari imeiva, Mwanaume hupumziki kama nesi wa zamuΒ
ππππ
Hakuna siku mbaya maishani kama hii
Hakuna siku mbaya maishan kuona mtu uliyesoma naye darasa moja, anakupita na private car,, afu we umeninginia kwenye daladala,,, tena ulikua unamzid akili πππhapo Ndo utajua kwann gunia na dunia vinatofautiana neno moja
Soma alichokisema mlevi baada ya kukuta watu wakimpiga mwizi
Mlevi mmoja aliona wananchi wakipiga mwizi akawaambia “mwacheni msimpige, hii tabia yenu ya kupiga wezi mtakuja shtukia mnampiga Yesu, maana imeandikwa atakuja kama mwizi!”
Huyu traffic noma, kweli ulevi mbaya
Trafik mlevi alisimamisha gari Mama akapaki pembeni akaona trafik anakuja akiwa anayumba! Alipofika akasema, “naomba leseni yako.”
Mama akasachi mkoba Wake akatoa kioo kidogo cha kujtazama akampatia! Trafik akakiangalia kwa dakika 2
Akasema sasa si ungesema kama wewe ni trafik mwenzangu!
Haya nenda
Ulevi sio mzuri
ππππ
Angalia nilichomfanyia huyu mwizi
Et jana usiku mwiz kavunja mlango kwangu
akaanza kutafuta kitu kila kona ikabid
na mie niamke namuuliza unatafuta nini ananijibu hela ndipo nilipoanza na mie kutafuta nae
maana hta hela ya kula Jana sikua
nayo alichoka zaid nilipomuliza una uhakika uliweka humu?
*sipendagi ujinga
Duh. mjamzito ana kazi
ππππukimuona mjamzito katema mate ujue mtoto kajamba
Cheka kidogo: Majibu ya mhindi kwenye mtihani wa Kiswahili alipoambiwa ajibu methali
Mhindi kwenye mtihani wa kiswahili anaambiwa amalizie methali:
(a)Nyani haoniβ¦..valisa miwani!
(B)Debe tupuβ¦.weka dengu!
(c)Masikini akipataβ¦.iko acha iba!
(d)Penye kuku wengiβ¦chinja bili,tatu!
(e)Asiyesikia la mkuuuβ¦.peleka yeye polisi!
(f)Penye wengiβ¦β¦iko kutano ya chadema!
Duh! Wanaume jamaniβ¦
Lakini sisi wanaume hatuko fair β¦ Yani demu anang’ng’ana kujipodoa uso na sisi tunaangalia matako. πππmungu anatuona jamanππππππMakeup ya matako iletwe
Soma alichojibiwa huyu mzee baada ya kudai kutaka kumsikiliza Nyerere
Mzee: Dereva ongeza sauti tumsikilize Mwalimu Nyerere!!
Dereva: ungemsikiliza mwalimu wako miaka iyo saivi ungekua na gari yako
π π π π π π π π π
Tofauti ya mwanamke wa Kizaramo, Kitanga, Kihaya, na wa Kichaga
Mwanamke wakizaramo: Unampa hela ana nunua dela anaenda ana msutia jirani, analivaa dela bila nguo ya ndani mbele yako, unazidiwa anakupa kitu fresh unatoka unatabasamu.π€π½ππ½
Mwanamke wa kitanga:
Unampa hela anapika vitu mtaa mzima unasikia harufu ya chakula, chenji inayo baki ananunua kinga ukirudi unakula afu unakula..ππΌππΌπ€π½ππ½
Mwanamke wa kihaya:
Unampa hela ukirudi unakuta majirani wote wanataarifa kuwa wew uliacha hela, anakupkia vitu vzuri, usiku anakuhudumia ukimsifia anakuhudumia tena hata mara nne kwa usiku mmoja..we mle sifa tuππ½ππ½π€ΈπΎββππ½.
Mwanamke wa kichaga:
Unampa hela anaenda ananunua dagaa anapika na michuzi mingi mpaka dagaa wanafufuka unakula kwa shida, dagaa wanakula utumbo wako unakufa.. Madaktari wanajitahidi wanakutibu unafufuka. Ukiwa hujapata akili vizuri anakuletea bili ya umeme, anakukumbusha deni la kwa Massawe, anakukumbusha kodi ya nyumba.. *Unashikwa na presha unakufa moja kwa moja*ππ½πππΌββππΎπ€ΈπΎββ
Mvua zazua kasheshe! Soma hii..
Baba- : Halloo mke wangu.. yaani ni shida sitaweza kurudi nyumban, daraja limevunjika na kutoka morogoro kurudi dar haiwezekani
MAMA:- Mme wangu morogoro ulienda bila kuniaga! ?
BABA:- Ilikuwa ni ghafla sana mke wangu sikuweza kukwambia
MAMA:- kha! Sasa watoto nani atawaangalia
BABA:- Unasemaje! We uko wapi kwan
MAMA:- Niko bagamoyo na daraja limeondolewa na maji sitaweza kurudi.
BABA:- Unasemaje we mwanamke.. nakwambia nikukute nyumban ndani ya dk 15
Baada ya dk 15 Baba kafika nyumban.
MAMA:- Haya umefkaje kutoka morogoro?
BABA:- Nimepewa lift na helkopta ya Mbowe..
Kama umeipenda shea na rfiki zakoooβ¦..
Hii ndiyo sababu ya kumfanya huyu jamaa kujiita fara
MZEE:”sasa huyu mgeni sijui alale wap?”
MKE:”saa hizi ni usiku akalale na Bebi.”
jamaa akaona huyo Bebi pengne mtoto anakojoa kitandani au akalia asije msumbua usiku
JAMAA:”msipate tabu mi ntalala hapa kwenye kochi” akalala
asubh wanakunywa chai akaibuka mrembo,jamaa akapigwa bumbuwazi almanusra ajimwagie chai.
BINTI:”Naitwa BEBI,we unaitwa nani?”
Jamaa akasema mimi naitwa Faraβ¦..!
Hii dunia kweli haina haki, soma hii
Unapiga kilimo chako unamsomesha girlfriend anafika chuo anakutana na msomi mwenzake anarudi anakwambia unanidai shilingi ngapi..,,?
Hapo ndo utatambua kwann kinyesi hakina mwiba ila ukikanyaga lazima uchechemee..πππππππππππ€
Hizi swaga za huyu jamaa ni shida, Google!
Jamaa alikuwa kwenye daladala pembeni kuna
dada mrembo kakaa. Kamlia timing kwa muda
kisha halafu akamuuliza “Samahani dada
unaitwa Google?”.
Dada: “hapana, kwanini umedhani naitwa
hivyo?”. Jamaa: “Una kila kitu nnachokitafuta
“π
πππππππππ
Kilichotokea baada ya kuzamia sherehe
Pale unapozamia kwenye Dinner Party ya Jumuiya Fulani, sasa Lengo la Jumuiya hiyo ni kupata Fedha za kutunisha Mfuko wa Jumuiyaβ¦sasa unakakaa mbele kabisa ili Muda wa Msosi usichelewe na kukuta kwenye Buffee yamebaki maharage!
MC : “Papai zuri kabisa kutoka Newala, Papai Mwendokasi, hili ni Shilingi laki 1..jamani Papai,nipeni ofa!”
MOSHA : “Laki 3 hapaaa!”
“Jamani laki 3 pale kwa Mosha, Papai linaondoka jamani, papai hili ni self contained kabisaβ¦.papai jamani”
KIBOLIBO: “Milioni 1 hapaaa”
“Jamani Mambo yanazidi kunoga hapa!β¦Benedict Kibolibo anataka papai kwa milioni 1 jamani, linaondoka papai!”
RWEYEMAMU : “nitanunua Papai hilo kwa Milioni 5”
Haya sasa jamani Rweyemamu ametoa ofa ya Milioni 5 Jamani, nani mweingineee?”
Kimyaaaβ¦
Haya jamani Papai kama hakuna Ofa basi Papai linakwenda kwa Rweyemamu!β¦β¦..haya sasa Kuna Kuku hapa Jogoo kabisa, bei yake ni laki 6 jamani Jogoo twitter huyu!”
WEWE “Milioni Mojaaa!”( hapa umejiwahi wa kwanza na wewe uonekane upo huku ukijua kabisa Wakina Mosha na Rweyemamu lazima watampandia Dau Jogoo, tena dau kubwa”
MC: ee sasa Kumekucha Jamani, Kabasele anamtaka Jogoo kwa Milioni 1 jamani!β¦.ofa nyingineeee!”
Kimyaaaβ¦
Jamani Jogoo anakwenda kwa Kabasele jamani!β¦ofa nyinginee!
Kimyaaaβ¦.
Kimyaaaβ¦.
πππβ¦hapa sasa ndio mfukoni kuna Buku jero,..huko kwengineko NMB nill balanceβ¦sasa unageuza mimacho kumtazama Mosha kama atapanda dau kwa jogooπ(mama wee Mosha anachezea Simu!)β¦..unamtazama Rweyemamu (teh anatafuna Kuku)β¦..mama weeeπ
MC: Haya jamani kama hakuna Mwingine basi zoezi letu liishie hapa na limekwenda kwa Mafanikio, Mpatieni Kabasele Jogoo wake!
Hapa sasa unapokea jogoo wako wa MILIONI kwa Tabasamu la Maitiβ¦.kule nyumbani Jogoo wako Mkubwa unauza elfu 20 lakini sasa haka kajogoo kapya Mkononi kanakuwa kazito utadhani umembeba John Cenaπβ¦Mama weee hapa sasa vidari ulivyotafuna unaviona kama vimerudi kwenye Ulimiβ¦.Chicken wings zinataka kutokea Masikioniβ¦..Uuuuwiiiii,πππ
Na hapa sasa kabla Dinner haijaisha ndipo unapojikuta Umebuni Cocktail ya Sparetta na Tomatoπππππ.
chiel wie okee
Kilichotokea Leo mahakamani
Leo nimeenda mahakamani, mara judge akasema..
Order! Orderβ¦
Mimi na kiherehere changu nikasema.. Chapati .. Maziwa na ovacado tatu β¦
Nimewekwa kwa karoom kengine hapa kanagiza..
i think wananiandalia chapati
πππππππππ
Recent Comments