Sipendi ujinga. Cheki nilichokifanya
Nimeingia chumban nikakuta panya wamekula dawa yangu ya minyoo,
Na mimi nimechukua yakwao nikanywa.
Sipendagi ujinga mm!!
πππ
Nimeingia chumban nikakuta panya wamekula dawa yangu ya minyoo,
Na mimi nimechukua yakwao nikanywa.
Sipendagi ujinga mm!!
πππ
Dalali aliwatafutia jamaa chumba Buguruni karibu na reli, nyumba nzuri sana. Jamaa na mkewe wakahamia kwa furaha, lakini furaha yao iliisha walipokuja gudundua nyumba ile iko karibu mno na reli treni ikipita mpaka kitanda kinacheza.
Siku hiyo dalali akapita mke akamwita na kumwambia tatizo wakati treni inapita, wakaanza kubishana, yule mama akamwambia dalali kwa kuwa kuna treni itapita sasa hivi⦠njoo ndani uone mwenyewe.
Bahati mbaya wakiwa wamejilaza kitandani ili dalali aone adhabu wanayopata, Mzee mwenye mali alirudi ghafla, akauliza,
‘Nyie mnafanya nini hapa?’
Masikini dalali kwa woga mkubwa akajibu’ Tunangoja treni’
Ndoto zingine bwana usiombe zikupate
Mimi usiku wa kuamkia Leo nikiwa nimelala nimeota naendesha gari Yangu aina ya BMW mpya Mara gafla ikakwama kwenye tope .hivyo ikabidi nishuke ili kuisukuma loh! Yani kudadeki ile kuamka nikakuta nimesukuma kitanda hadi sebleni Daaa ilinisikitisha sana jiangalie sana sese hivi ndio narudisha kitanda chumbani .angalizo angalia ndoto unazo ota unaweza kuota upo baharini ukaamka unajikukuta unaogelea kwenye Jaba la Maji shauri yako.
1. Mwanaume hata awe bahili vipi, hawezi kumpa mwanamke mimba nusu.
2. Hata uwe na magari mangapi chooni utaenda kwa miguu.
3. Kama ubinadamu kazi mbona hatupewi mishahara?
4. Ukichanganya wali na choroko unapata mseto, lakini hautibu malaria.
5. Hata njiwa nae ana makinda, lakini hawezi kuwa spika wa Bunge.
6. Hata uwe na haraka vipi kwenda Zenj, huwezi kupanda Jahazi ya Yusuph Mzee.
7. Umeme hauna kiuno lakini unaongoza kwa kukatika.
8. Hata uwe kauzu vipi, huwezi kujamba wakati unatongoza.
9. Hata uwe na imani kali vipi, huwezi kusali wakati unafanya mapenzi.
10. Hata kizibo ni mfuniko lakini hauwezi kufunika sufuria.
1. Awe na pesa nyingi
2.Siyo lazima awe mzuri wa sura
3. Ajenge ukweni
4.Awe mpole
5.Asimuonee wivu mke wake
6.Awe mwenye upendo wa dhati
7.Asishike simu ya mke wake.
8.Akimkuta na mwanaume apite tu, akitaka kujua ni nani asubiri nyumbani
9.Awe anamskiliza mke wake kwa kika kitu.
10.Asipende mwanamke mwingine zaid yake
UKIMPATA MWANAUME MWENYE SIFA HIZO KAPIME DNA LAZIMA ATAKUWA NI BABA AKO.
ππππππππ
Mngojwa: daktari Nina tatizo la kusahausahau kila dakika.
Daktari: hilo tatizo lilianza lini?
Mngojwa:tatizo lipi?
πππππππ
Mzee mmoja alipanda Gari Stend;
Wakati wa kugombania Siti,
Akaibiwa Nauli.
Akasimama katikati ya Gari-Akasema; “Jamani Naomba Aliyeniibia Pesa yangu Arudishe Haraka,
Tena Fasta kabla Sijafanya Tukio kama Nililofanya 1977″
Abiria kuskia hivyo wakaogopa.
Ikabidi Mwizi Ajitokeze,
Akarudisha Pesa na Kuomba Msamaha! Mtu Mmoja akauliza,
Mzee,
Kwani 1977 Ulifanya nn?
Si nilienda kwa Miguu mpaka Nyumbani!
Uscheke Peke Yako, wa2mie na wengine ili nao wacheke!
Jay akaruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospital ya Vichaa, akapakiwa ktk ambulance hadi karibu na nyumbani kwake, akaulizwa unapakumbuka? akajibu ndio nyumba yangu ileee, mara wakatoka watoto wawili wamevaa uniform akasema watoto wangu walee wanakwenda shule.. akatoka mwanamke akasema na mke wangu yulee, ghafla akatoka mwanaume Jay akasema na mimi yule naenda kazini. hivi Jay kweli kapona?
MUME: “Mke wangu nasikia John katembea na wake za watu wooote hapa mtaani kasoro mmoja tu!”
MKE: “Mmmh! basi huyo aliebaki atakuwa MAMA MBILINGE KISIKI, maana yule mama ndo ANAJIFANYAGA MGUMU sanaaa.!!”
Je, huyu mama angekuwa mkeo ungekuwa na swali lingine la kumuuliza?
Teacher: Who is a pharmacist?
Shemdoe raised up his hand.
Teacher: So itβs only Shemdoe that can tell who a pharmacist is in this class? So there is no body else to answer the question except Shemdoe? (There was no reply from the students)
Teacher: Ok now Shemdoe, chukua hii fimbo, charaza vilaza hawa wote kila mmoja viboko kumiβ¦. Shemdoe akiwa amevimba kichwa, akawatwanga viboko kumi kumi vya kushiba darasa nzima
Teacher: Now, my dear Shemdoe tell this dumb students who a pharmacist isβ¦
Shemdoe: Yes, sir. A Pharmacist is a farmer who assists people. Shemdoe saiv amelazwa MOI kwa wataalam wa mifupa π
Mama mkwe alimuuliza mkwewe “binti” samahani mbona mtoto hajafanana na mwanangu kabisa?
Binti akajibu, “bila samahani mama huku chini nina njia ya uzazi sio mashine ya photocopy”
mama mkwe hoii!! Chezea Wakwe Wa Bongo wewe.
CHEKA KIDOGO
Wachungaji watatu walikutana kwa siri na kuelezana matatizo yao ili waweze kuombeana.
MCHUNGAJI WA KWANZA: mimi tatizo langu ni wizi, kila nikimaliza ibada lazima niibe pesa za sadaka.
WA PILI: Mimi tatizo langu ni wanawake yani nimeshalala na wana kwaya wote pamoja na mke wa ASKOF.
WA TATU akaanza kulia badala ya kuongea.WENZAKE:
We vp unatatizo gani mbona unalia???
AKAJIBU: jamani mimi tatizo langu ni “umbea” haya yote tuliyoongea lazima nikaseme!
πππππππ»ππ
Mfugaji mmoja alikwenda kwa mfugaji mwenzake (ambae pia ni bwana mifugo wa eneo lao) asubuhi moja. Alipobisha hodi mtoto wa kiume wa umri upatao miaka 12 akamfungulia mlango. Mazungumzo yafuatayo yakafuatia:
Mkulima: Baba yako yupo?
Mtoto: Hapana Mzee, amekwenda mjini.
Mkulima: Mama yako?
Mtoto: Nae kaenda mjini na baba.
Mkulima: Kaka yako Howard yupo?
Mtoto: Nae hayupo, wote yeye, baba na mama wamekwenda mjini. Kwani una shida gani? Kama kuna kitu unahitaji niambie maana nimeachiwa funguo na najua vifaa vinapowekwa.
Mzee akawaza kidogo halafu akasema: Kwa kweli nilitaka kuongea na baba, mama au kaka yako kwa kuwa kaka yako amempa mimba binti yangu.
Mtoto akafikiria kidogo halafu akasema: Kusema ukweli itabidi umsubirie baba, ila kwa kukusaidia ni kuwa baba hulipisha shilingi laki moja kwa kupandisha dume la ng’ombe na elfu hamsini kwa beberu. Ila sijui baba hutoza shilingi ngapi kwa Howard akifanikiwa kutia mimba.
UTOFAUTI KATI YA MWANAMKE NA MWANAUME
1. Kwenye mshituko; mwanaume hushituka halafu huangalia nini kimemshitua, mwanamke hushituka halafu huzimia hivyo ataambiwa na mwanaume kilichomshituaππ
2. Kwenye kupenda; mwanaume huanza kutamani alafu hupenda, mwanamke huanza kupenda moja kwa moja bila kumjua vizuri huyo ampendaeπππ
3.Kwenye kusaidia; mwanaume hutoa msaada alafu uhuzunika, mwanamke huuzunika badae ndo anakumbuka km msaada unahitajikaπππ
4.Kwenye maamuzi; mwanaume hufikiri ndipo hutenda, mwanamke hutenda halafu hufikiriπππ
5.Kwenye kudanganya; Mwanaume hudanganya ili kumlinda mwanamke, mwanamke hudanganya ili kumkomoa mwanaumeπππ
6.Kwenye ugomvi; wanaume hupigana halafu hueshimiana, wanawake hupiga mikelele alafu kila mmoja hurud kwake, kexho tenaπππ
7.Kwenye ndoa; mwanaume hutafuta maixha ndipo huoa, mwanamke huolewa ndipo atafute maishaπππ
8.Kwenye kukata tamaa; mwanaume hukata tamaa mapema ili jambo lisimsumbue, mwanamke hajui kukata tamaa hadi aumizweπππ
9.Kwenye kula;Mwanaume hushiba alafu huanza madoido, mwanamke huanza na madoido alafu badae hujilaumu hakushibaππ
10.Kwenye siri; Mwanaume hutunza siri hasa za aibu, mwanamke humueleza shoga yake badae hugombana nae baada ya kumrudia mwenyewe kwa siku 2 tuπππ
Hizi ni baadhi tu ya sifa tofauti kati ya mwanaume na mwanamkeβ¦.. VIVA GENTLEMENππ½π
πππππ
ππ ππππππ Jamaa kagombana na mkewe, akasusa kulaπ½π¨ kurudi kazini kamkuta mkewe amevaa kanga imeandikwaΒ ukisusa wenzio walaΒ ilipofika asubuhi mke akavaa kanga imeandikwaΒ ukitoka πΆπΆmwenzio anaingiaππ
jamaa akagoma kwenda kazini π¬π¬ mke akabadili kanga na kuvaa iloandikwaΒ nimemdhibiti ndo mana hatokiπ· jamaa akaenda kuomba ushauri kwa rafiki yake akaambiwa twende nyumbsni kwako, walipofika walimkuta mke kavaa kanga imeandikwaΒ ulidhani rafiki yako kumbe adui yakoπ€π€ jamaa akaamua kusafiri siku tano ili kupunguza hasira. Aliporudi akamkuta mke amevaa kanga imeandikwaΒ ni bora nimpe jirani kuliko kiozee ndani
ππππππππππ
hata kama hupendagi ujinga kwa maneno ya kwenye kanga utasanda tu
Hili nalo neneo.
Ukimuona mbwaπΆ harusini usimpige mawe wala kumfukuza inawezekana kilichomleta pale ndicho kilichokupeleka na wewe hapo
Kuna mdada nilimkopesha pesa kwa ahadi kuwa baada ya wiki moja atanirejeshea pesa zangu.
Baada ya wiki moja nampigia simu hapokei simu zangu, nimempigia zaidi ya mara kumi (10) bila ya mafanikio!
Kila nikimpigia simu hajibu simu zangu, nikahamua kumwandikia message kwa WhatsAppβ¦!
_Hello Mamu, Nakupigia simu sio kukudai pesa zangu, ila nataka kukwambia kuwa hapa Ubungo Plaza kuna wadada wawili walikuwa wanapigana kumgombea Mumeo (Baba Nang’oto). Ilikuwa vuta nikuvute na mumeo alikuwa kasimama tu anawaangalia akitabasamu. Baada ugomvi kwisha akaondoka na mmoja wao na kumwacha yule mwingine akitukana matusi kama ana akili nzuri._
β
_*Kisha nikaituma ile message*_
Baada ya dakika kama mbili hivi, akanipigia simu nami wala sikupokea simu yake⦠Akapiga tena na tena kama mara ishirini hivi wala sikupokea.
*Akatuma message akiniulizaβ¦*
_Hao wanawake unawajuwa, β¦mume wangu na huyo mwanamke wameelekea wapi, wewe unawajuwa hao wanawake waliopigana, yaani hapa nimechanganyikiwa kwa kweliβ¦!_
Nikaisoma message yake wala sikuijibu, nikamchunia kimyaaaβ¦!
Akanipigia tena simu mara tano, sikupokea simu zake, kimyaaaβ¦! Akaniandikia message nyingineβ¦.
*β¦Nakupigia jamani pokea simu basi nina pesa zako nataka nikupeβ¦ Naomba basi tukutane mjini unihadithie vizuriβ¦!*
Nami nikamjibuβ¦
_Nitumie hizo pesa kwenye Namba yangu ya Mpesa, ili nipitie sheli kujaza mafuta nije mjini kukupitia nikupeleke mahala walipoβ¦!_
Baada ya dakika 2 message ikaingia, kuangalia balance yangu ya Mpesa, nikakuta kaingiza pesa zangu zote ninazo mdaiβ¦!
Nikazima simu nikajilalia zangu kimyaaaβ¦. Kama sio mie!
Recent Comments