Vituko Vya Kushangaza

Baadhi ya misemo mikali ya leo

1. Mwanaume hata awe bahili vipi, hawezi kumpa mwanamke mimba nusu.

2. Hata uwe na magari mangapi chooni utaenda kwa miguu.

3. Kama ubinadamu kazi mbona hatupewi mishahara?

4. Ukichanganya wali na choroko unapata mseto, lakini hautibu malaria.

5. Hata njiwa nae ana makinda, lakini hawezi kuwa spika wa Bunge.

6. Hata uwe na haraka vipi kwenda Zenj, huwezi kupanda Jahazi ya Yusuph Mzee.

7. Umeme hauna kiuno lakini unaongoza kwa kukatika.

8. Hata uwe kauzu vipi, huwezi kujamba wakati unatongoza.

9. Hata uwe na imani kali vipi, huwezi kusali wakati unafanya mapenzi.

10. Hata kizibo ni mfuniko lakini hauwezi kufunika sufuria.

Kwa nini vitu vunavyoanza na “K” ni vitamu sana?

Zuzu kaniuliza, “Anko, unajua vitu vinavyoanzia na K ni vitamu sana.”
Nikashtuka, “Astaghafilulah we mtoto! Niondolee wehu wako hapa!”

Zuzu akatabasamu. Akaendelea kuongea kabla sijafanikiwa kumzuia. “Kweli kabisa anko. Vitu vinavyoanza na K ni vitamu sana kwa mfano kuku, kalimati, keki, kabab, katleti, kashata, kisheti na karoti.”
Nikashusha pumzi. “Ahaa! Kumbe ndo hivyo, ni kweli!”

Zuzu akanitupia swali. “Kwani we anko ulidhani nini?”

Alichojibu dalali baada ya kufumwa na mke wa mtu ndani ya nyumba ya kupanga

Dalali aliwatafutia jamaa chumba Buguruni karibu na reli, nyumba nzuri sana. Jamaa na mkewe wakahamia kwa furaha, lakini furaha yao iliisha walipokuja gudundua nyumba ile iko karibu mno na reli treni ikipita mpaka kitanda kinacheza.

Siku hiyo dalali akapita mke akamwita na kumwambia tatizo wakati treni inapita, wakaanza kubishana, yule mama akamwambia dalali kwa kuwa kuna treni itapita sasa hivi… njoo ndani uone mwenyewe.

Bahati mbaya wakiwa wamejilaza kitandani ili dalali aone adhabu wanayopata, Mzee mwenye mali alirudi ghafla, akauliza,

‘Nyie mnafanya nini hapa?’

Masikini dalali kwa woga mkubwa akajibu’ Tunangoja treni’

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About