Vituko Vya Kukuchangamsha
Je, hili nalo ulilipitia ulipokua Shuleni?
Hakuna Kitu Kilikua Kinaniumizaga Kipindi Nipo Shuleni.
Time Mmetoka Kwenye Mitihani Wa Mathematics Halafu Mpo Kikundi Fulani Either Mnarudi Nyumbani Au Mnapumzika Kwa Ajili Ya Next Exam.
Unasikia Jamaa Wanabishana Pale Jibu Lilikua 4 Mwingine Anasema 5, Na Wewe Ulijaza 80.
Angalia anachokisema Madenge sasa
MWALIMU kaingia darasani na kusema. “Wanaojijua wajinga wasimame”.
MADENGE akasimama peke yake.
MWALIMU: Wewe ndio mjinga?
MADENGE: Hapana, ila nimeona umesimama peke yako nikaona usijisikie vibaya angalau tuwe wawili.
Angalia kilichonikuta nilipoenda kwa mganga
Usije ukaenda kwa mganga, mwenzako yamenikuta, yani masharti niliyopewa, acha tu,
yalikua hivi:-
1.Jasho la nyoka.
2.Manyoya ya mende.
3.Sisimizi Shoga.
4.Mbwa mjane.
5.Kuku aliye single.
6.Samaki mwenye miaka miwili bila kuoga
7.Mti wenye ujauzito.
8.Mbavu za Nzi.
9.Nywele za Kiroboto.
10.Mwanya wa Mbu.
Duuh..!! mwanangu kwa hali hii mbona itakula kwako.
Wengine wanasemaga
IGA UFE! Rizik anagawa Mungu tu shetan simuelew!
Jinsi ya Kubana matumizi X-mass
Badala yakupika PILAU tutapika TAMBI kwenye Xmas maana tutakua tumeokoa sh.15,000/= Vitunguu swaumu 2000, Vitunguu maji 1000, hiliki 1000, Magome 1000, Michele wa 2000, Soda 3000, Nyama 5000 . Fedha hizi zitatumika kununua mfuko wa cement ili tuanze kujaza kibubu cha ujenzi wa nyumba badala ya kupanga. Karibuni saana maji ya kunywa tumechemsha ndoo nzima.
๐โจMarry Xmas & Happy new year.โจ๐
Madenge hakosi visa. Soma hii
MADENGE
HAKOSI
VISA
baada ya kumaliza form four baba akamwambia achague zawadi yoyote aipendayo
MADENGE: naomba pesa nikamuoe bibi maana siku nyingi amekuwa akiniita mchumba wake.
BABA: Shenzi, yule ni mama yangu mzazi huwezi kumuoa.
MADENGE: Mbona wewe umemuoa mama yangu mzazi sijasema kitu ww inakuuma? lazima nilipize kisasi ikikuuma muache mama yangu kila mtu akae na mamayake. ๐๐๐
Kilichompata huyu anayependa kusoma SMS za watu kwenye daladala
Jana nilipanda daladala nikapata seat nikaketi, nikawa nimejiachia ninachati kwenye simu yangu(Smart phone), kukawa na jamaa kasimama pembeni yangu, ye hakupata seat. Sasa akawa anasoma message zangu bila aibu yani anafutilia ninavyochatiโฆ
Basi nikasema ngoja nimtie Adabu mshenzi huyuโฆ. Nikacheck saa yangu yamkononi kisha nikatext:ย “Oya Ben Kwaheri bwana, zimebaki sekunde 30 tu hili bomu๐ฃ lilipukeโฆ najua hatutaonana tena, nitunzie Familia yangu, wambie nawapenda sanaโฆ”ย Yule jamaa akajirusha dirishaniโฆโฆ๐๐
โkwani mi napenda ujinga xx ๐๐๐๐๐๐๐
Baada ya walevi wawili kuokota kioo hiki ndicho kilifuata
Angalia kilichotokea
Walevi wawili waliokota kioo, mlevi wa 1 akaangalia muda mrefu kisha akasema “hii sura sio ngeni machoni mwangu sema jina tu silikumbuki..! !!
Mlevi wa pili akamnyang’anya kisha nae akaangalia kioo akasema “wee kweli huna akili, si mimi huyu? halafu unajidai hunikumbuki โฆ!!!
Hawa ndio wanaume wanaoweza kushinda vishawishi
Wanaume wenye kushinda vishawishi ni;
Wanaume ambao mnaweza kula wali hadi mwisho bila kugusa nyama nyie ndio mnaweza kushinda vishawishi๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ
๐โโ๐โโ๐โโ๐โโ๐โโ๐โโ
Duh! Hiki nacho chombo cha moto?
_Sheria inasema kila anaetembea na chombo cha moto barabarani sharti awe na leseni._
_Sasa hawa wauza kahawa mbona wanatembea na chombo cha moto lakini hawakamatwi ๐ก._
_Hizi sheria zinapendelea._
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Recent Comments