Huyu mwanafunzi kweli kiboko
Ticha: Wa kwanza kujibu swali langu ataenda Home mapema..
John kusikia hivyo….Karusha begi la daftari nje…..`Β
`Ticha akauliza: Nani karusha begi nje!?!`*
`John: Mimi….. Kwa herii Mwalimu……` ππ,ππ
Ticha: Wa kwanza kujibu swali langu ataenda Home mapema..
John kusikia hivyo….Karusha begi la daftari nje…..`Β
`Ticha akauliza: Nani karusha begi nje!?!`*
`John: Mimi….. Kwa herii Mwalimu……` ππ,ππ
MCHUNGAJI; “Unakunywa bia!?
MLEVI; “Ndio.
MCHUNGAJI; “Kwa siku unakunywa bia ngapi!?
MLEVI; “Nakunywa bia tano!
MCHUNGAJI; “Bia moja bei gani!?
MLEVU; “2500/
MCHUNGAJI; “Ulianza lini kunywa bia!?
MLEVI; “Miaka 18 iliyopita!
MCHUNGAJI; “Kwa hiyo kwa siku unatumia zaidi ya 10,000??
MLEVI; “Ndio!
MCHUNGAJI; “Kama u gekuwa unatunza hiyo pesa 10,000 kwa siku leo hii si ungekuwa na Range Rover!?
MLEVI; “Samahani, naweza kukuuliza swali!?
MCHUNGAJI; “Uliza!
MLEVI; “Unakunywa bia!?
MCHUNGAJI; “Hapana!
MLEVI; “Nionyeshe Range Rover yako!
MCHUNGAJI; “akasepa”
{ NGOMA DROO}
Sikuizi utawasikia wadada wakisema kuachwa na mwanaume asie na pesa nisawa na kuluhusiwa hospital
{Sasa na sisi} wanaume tunasema
Kuachwa na demu mpenda pesa nisawa na kumaliza mkopo benk ππππππ
Wanaume atutakagi ujinga!!!! Wanaume heeeeeeππΎββππΎββππΎββππΎββ
Jay akaruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospital ya Vichaa, akapakiwa ktk ambulance hadi karibu na nyumbani kwake, akaulizwa unapakumbuka? akajibu ndio nyumba yangu ileee, mara wakatoka watoto wawili wamevaa uniform akasema watoto wangu walee wanakwenda shule.. akatoka mwanamke akasema na mke wangu yulee, ghafla akatoka mwanaume Jay akasema na mimi yule naenda kazini. hivi Jay kweli kapona?
Jamani punguzeni pombe,kuna jirani yangu amerudi amelewa sasa nachungulia dirishani naona anagonga mlango wake takribani masaa mawili,wakati hapa anaishi peke yake, kwakuwa sipendagi ujinga nimetoka nikamwambia mwenyewe kasafiri.Nae kaondoka.
GARI YA MILIONI 50
UNALAZA NJEβ¦
mke wa laki sita
unalala nae ndaniβ¦.
BANGI SI NZURI JAMAN
ππππππππ
Ticha katangaza test , Akatoa Masharti; Ukiandika jibu hamna kufuta au kukata.
Swali la kwanza,
Taja vyakula vi3 ambavyo ukienda hotelini umelipiwa utapenda kula (marks 1)
WAVULANA wakajaza; wali, ugali, mihogo.
WADADA wakajaza; burger, pizza, egg chop. Swali la
2: Eleza jinsi ya kupika kila chakula ulichotaja hapo juu. (marks 99)
wacha wadada waanze kuhangaika kukata majibu ya mwanzo!
Β
Mume kaingia duka la nguo na kamnunulia mke wake chupi dazeni moja zote za rangi nyeusi, akaenda kumzawadia. Mpenzi akashukuru lakini alipogundua kuwa zote ni nyeusi si akaropoka.
MY HONEY: Sasa umeninunulia chupi zote nyeusi, sasa watu si watadhani nina chupi moja tu sibadili,
Jamaa alifura akawa kama mbogo na hapo ndipo zogo kuu lilipoanza
MUME:Watu gani hao watakaokuambia unachupi moje, inamaana unawaonyesha kitumbua changu? Leo utanambia’
Ungekuwa wewe ungefanya nini?
Jamaa karudi toka kazini mpole na hana furaha!
MKE; Vipi leo mbona mpole?
MUME; Ofisi yetu imeungua na watu wote waliokuwemo wamekufa.
MKE; Ilikuaje wewe ukapona?
MUME; Nilikua chooni jirani na ofisi najisaidia.
MKE; Loh maskini, familia zao itakuaje?
MUME; Watalipwa million 100 kila mfiwa.
MKE; KWA HASIRA, Ona sasa na wewe kunya kunya kwako umetukosesha mihela.. Ungeenda kunya akhera.
Kuishi kijijini kunahitaji moyo sana
..unaenda kuoga, unakumbuka kuwa umesahau sabuniβ¦unaenda kuchukua sabuni kurudi bafuni, unakuta ng’ombe amekunywa maji yote..unaamua kufuata mengne,unarudi unakuta mbuzi kala sabuniβ¦ππππ
Marafiki wawiliΒ (Jose na Ben)Β walikuwa wanatembea mtaani akatokea mwanamke akarusha busu kwa mmojawapo kupitia dirishani katika jengo la ghorofa tatu.
Wakaanza kujadiliana kama ifuatavyo:
Ben:Β Muone yule mrembo amenirushia busu
Jose:Β tafadhali achana na huyo mwanamke, usimjali..
(baadae yule mwanamke akamuashiria aende)
Ben:Β yule mwanamke ameniita!
Jose:Β Rafiki yangu, usiende. Nakutafadhalisha.
Ben:Β Kwa nini unaniambia nisiende Wakati mrembo kama yule ananiita? Huo ni wivu
Jose:Β Ben, Ninakutafadhalisha tena, usiende, tafadhali usiende kuleΒ (akihisi kutotiliwa maanani)
(Rafiki yake alimpuuza na alienda kwa yule mwanamke, mwanamke alishuka kukutana naye na wakapanda juu. Ghafla wakiwa wanataka kuanza taratibu za kula uroda, wakasikia mlio WA gari getini).. ππ
Lady:Β _(akiangalia kupitia dirishani)_
Oooh! Yule ni mume wangu!!
Ben:Β Mama yangu !
Nipo matatani, kweli ? ..!!
Lady:Β Usiwe na khofu, jifanye kuwa Dobi na anza kupiga pasi hizo nguo
(akimuonyesha lundo la nguo)
(Ben alitumia masaa matano kukamilisha kunyoosha zile nguo kwa sababu yule mume hakutoka tena siku ile)
(Siku iliyofuatia Ben alikwenda kwa Rafiki yake)
Ben:Β Kaka, unaweza kuamini Jana nimepiga pasi nguo kwa masaa matano???
Jose:Β Lakini nilikwambia usiende. Nguo zote hizo ulizonyoosha,Β Nilizifua Mimi Juzi!!
πππππππππ
When an experienced person speaks β¦ πyou must listen..!
High school Flashback!!
.
Watchman : Amkeni muende morning preps.
Allan : Mimi ni mgonjwa.
Watchman : Unaumwa na nini hiyo?
Allan : Bionomial Nomenclature.
Watchman : Eeh, lala tu kijana. Hiyo kitu ni
mbaya. Imeuwa watu South Africa.
ππππππππππ
#_Sipendagii ujinga kabisaa mimi
Zuzu kaniuliza, “Anko, unajua vitu vinavyoanzia na K ni vitamu sana.”
Nikashtuka, “Astaghafilulah we mtoto! Niondolee wehu wako hapa!”
Zuzu akatabasamu. Akaendelea kuongea kabla sijafanikiwa kumzuia. “Kweli kabisa anko. Vitu vinavyoanza na K ni vitamu sana kwa mfano kuku, kalimati, keki, kabab, katleti, kashata, kisheti na karoti.”
Nikashusha pumzi. “Ahaa! Kumbe ndo hivyo, ni kweli!”
Zuzu akanitupia swali. “Kwani we anko ulidhani nini?”
Binti: Hallow mpenzi, Mambo
Jamaa: Poa baby
Binti:Uko wapi?
Jamaa: Niko town napata lunch
Binti: Wow unarudi saa ngap? Nina njaa dear naomba uniletee msosi
Jamaa: Narudi baada ya nusu saa nikuletee nini?
Binti: Niletee chipsi kuku, soseji, mayai manne ya kukaangwa pembeni, baga, piza, coke take away baridi, mkate wa moto kwenye ile bekari ya wapemba na maji ya kunywa ya kiimanjaro.
Jamaa:Umesahau viti, meza, masufuria, sahani na beseni na vijiko.
Binti: Kwanini dear?
Jamaa: Naona hutaki kula unataka kufungua hoteli!
Kuishi kijijini kunahitaji moyo sana
..unaenda kuoga, unakumbuka kuwa umesahau sabuniβ¦unaenda kuchukua sabuni kurudi bafuni, unakuta ng’ombe amekunywa maji yote..unaamua kufuata mengne,unarudi unakuta mbuzi kala sabuniβ¦ππππ
Bakari ni house boy mara nyingi huiba wine ya boss wake na kisha kuongeza maji kwenye chupa ili boss asigundue. Mara kadhaa boss alihisi ladha tofauti anapokunywa wine hivyo kuhisi kuna mchezo mchafu alihisi tu Bakari anahusika. Ilikua ni bahati tu alimvizia na kumbamba Bakari akichakachua wine, kwa kuwa mkewe alikua anamtetea Bakari, ili kumthibitishia mkewe kuwa Bakari ndo culprit,
boss alianza kwa kumuuliza Bakari maswali. Siku hiyo Bakari alikua jikoni,boss na mkewe walikua sebuleni.
Boss:- Bakariiii!
Bakari:- Naam baba!
Boss:- Nani anakunywa wine yangu?
Bakari:- Kimyaaaa hajibu kitu! Boss:- Bakariiiii !
Bakari:- naam baba! Boss:- nauliza nani anakunywa wine yangu halafu anajazia majiii!
Bakari:- kimyaaaaa!
Boss akaamua amfuate hukohuko jikoni.
Boss: Kwanini nikikuita unaitikia, nikikuuliza unanyamaza?
Bakari: Baba huku jikoni ndo kulivyo, unasikia jina tu likiitwa lakini maneno menginehusikii, na kama huamini baki jikoni mi niende sebuleni.
Bakari akaenda sebuleni akaanza kuita.
Bakari:Babaa!
Boss: Naam Bakari!
Bakari: Saa sita usiku huwa unaenda kufanya nini chumba cha house girl?
Boss:- kimyaaaa!
Bakari:- Baba babaa!
Boss:- Ndio Bakari!
Bakari:- Nauliza hivii, chumbani kwa house girl saa sita za usiku huwa wafuata nini?
Boss:- kimyaaaaaaa!
Boss akatoka nje: Bakari huku jikoni ni kweli husikii kitu zaidi ya jina!.
Mama akasema msinizingue nyieβ¦Mbona siwaelewi..
Bakar: mama kama uamini na ww nenda uone.
Mama akaenda jikoni..
Bakari: akaita mamaa
Mama : bee bakari
Bakari: eti hiyo mimba niya baba au yangu.?
Mama kimya
Bakari; mama nakauliza tena hiyo mimba niyababa au yangu.
Mama akatoka aisee kweli humu unasikia jina tuβ¦..πππππ
MUME wakati anakata roho huku mkewe akiwa amemshikilia alisema mke wangu, mi natubu kwako, kwani nilifanya mapenzi na dada yako, mdogo wako, rafiki yako na mama yako
MKE akamnong’oneza mume wake na kumwambia mbona mimi nayafahamu yote, ndio maana nimekupa sumu ili na wewe ujue uchungu wake. JE NANI ZAIDI?
Juzi nikitoka church nilipanda kihiace na kulikuwa na mrembo mkali hujawahi kuona,kila kijana alikuwa akimtupia macho,so me nilikuwa na wepesi wa kuongea naye kirahisi coz nilikuwa kando yake,,, Sasa kama unavyojuwa wanaume kwa kujikosha Nikaimigine mtto ananiangalia so nikaamuwa kupiga fake phone
“Hello Mr. Supervisor,nitachalewa kidogo coz kuna mahali nitapitia, so nipelekee tu hyo Ferrari yangu nyumbani”
Nikaona mrembo ameniangalia kwa macho ya husda apo nkajua nimeuwa ndege kwa jiwe moja, nkaamua kujikosha mtt wa kiume , “niaje mrembo”, akanikazia macho kisha akaniambia,
“Shika battery yako uliangusha ukitoa simu”
Icho kicheko watu walicheka hujawahi ona jooo adi ikabidi dereva aegeshe gari watu wacheke kwanza ππππππππππππππππ
Nikaona isiwe tabu nikashukia pale paleπΆπΏπΆπΏπΆπΏ
Tujifunze kusema ukweli kwani uongo sio mzuri hata kwa Munguβ¦ πππππ
Recent Comments