Visa Vya Wazee

Tofauti ya ukopaji wa mzungu na mswahili

MZUNGU: Hi, I need $100, will pay back on Monday

MSWAHILI: Kaka vipi, shwari? Dah.. hatuonani mzee, mishe vipi, mnatunyima nini? Juzi nimekuona kwa mbaaali… mzee shavu dodo, full kipupwe! Sie tupo bwana, shida tu, afu misiba mingi tu, wife nae kajifungua ghafla. Sasa, kuna cheque naisubiri haijatoka hadi leo, wanasema itatoka next week, hapa nimekwama kweli. Naweza pata ‘Laki Moja’ ya karibu hapo nitarudisha mwisho wa mwezi…?😂😂😂😂😂

Utoto raha..! Angalia hawa watoto wanachokifanya sasa

Leo nimepulizia Air Fresh yenye Harufu ya Pilau nyumbani kwangu sasa watoto wa Jirani wamehamia Mlangoni kwangu ndio wanacheza hapo. Kila nikitoka wananisalimia. Mama yao ndio kanimaliza kabisa nimetoka akaniambia

“Kumbe wewe ni Mpishi mzuri, Hongera”

Imebidi nisirudi nyumbani maana wale watoto wanaweza kuingia ndani kabisa na pilau hakuna.

#UTOTO RAHA 😂

😂😂😂😂👆🏻👆🏻👆🏻

Wadada acheni hizo

Mfalme Sulemani alikuwa na wake 700 na alichepuka(cheated)na vimada 300 . Mpenzi wako/Mume wako unamfumania na kimada mmoja tu ugomvi na amani imapotea ndani ya nyumba,unasimulia kuanzia padri,mchungaji,ukoo wako mzima,mashoga, stress,vidonda vya tumbo,inapelekea mpaka unaokoka,eti kisa kamuonjesha mmoja☝ sasa akionjesha 700 si utakutwa Mirembe�

Wadada acheni HIZO
😂😂😂😂😂😂.

Hapo sasa patamu, cheki jamaa alivyowezwa na huyu dogo

Mfugaji mmoja alikwenda kwa mfugaji mwenzake (ambae pia ni bwana mifugo wa eneo lao) asubuhi moja. Alipobisha hodi mtoto wa kiume wa umri upatao miaka 12 akamfungulia mlango. Mazungumzo yafuatayo yakafuatia:

Mkulima: Baba yako yupo?

Mtoto: Hapana Mzee, amekwenda mjini.

Mkulima: Mama yako?

Mtoto: Nae kaenda mjini na baba.

Mkulima: Kaka yako Howard yupo?

Mtoto: Nae hayupo, wote yeye, baba na mama wamekwenda mjini. Kwani una shida gani? Kama kuna kitu unahitaji niambie maana nimeachiwa funguo na najua vifaa vinapowekwa.
Mzee akawaza kidogo halafu akasema: Kwa kweli nilitaka kuongea na baba, mama au kaka yako kwa kuwa kaka yako amempa mimba binti yangu.

Mtoto akafikiria kidogo halafu akasema: Kusema ukweli itabidi umsubirie baba, ila kwa kukusaidia ni kuwa baba hulipisha shilingi laki moja kwa kupandisha dume la ng’ombe na elfu hamsini kwa beberu. Ila sijui baba hutoza shilingi ngapi kwa Howard akifanikiwa kutia mimba.

Baadhi ya misemo mikali ya leo

1. Mwanaume hata awe bahili vipi, hawezi kumpa mwanamke mimba nusu.

2. Hata uwe na magari mangapi chooni utaenda kwa miguu.

3. Kama ubinadamu kazi mbona hatupewi mishahara?

4. Ukichanganya wali na choroko unapata mseto, lakini hautibu malaria.

5. Hata njiwa nae ana makinda, lakini hawezi kuwa spika wa Bunge.

6. Hata uwe na haraka vipi kwenda Zenj, huwezi kupanda Jahazi ya Yusuph Mzee.

7. Umeme hauna kiuno lakini unaongoza kwa kukatika.

8. Hata uwe kauzu vipi, huwezi kujamba wakati unatongoza.

9. Hata uwe na imani kali vipi, huwezi kusali wakati unafanya mapenzi.

10. Hata kizibo ni mfuniko lakini hauwezi kufunika sufuria.

Shopping Cart
23
    23
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About