Visa Vya Wazee

Mipango ya mke na mume ya pasaka

Mke: Unampango gani na pasaka hii mmewangu..
Mume: Nitafanya kama yesu..
Mke: Unamaanisha Nini?

Mume: Nitaondoka ijumaa na Kurudi j3..
Mke: Unanishangaza, kama utafanya hivi nami nitafanya kama Maria..
Mume: Unamaanisha Nini?
Mke: Nitapata mimba bila ya kuingingiliwa na wewe mume wangu..
Mume: ๐Ÿ˜ณ๐Ÿ˜ณ๐Ÿ˜ณ

๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Alichojibu dalali baada ya kufumwa na mke wa mtu ndani ya nyumba ya kupanga

Dalali aliwatafutia jamaa chumba Buguruni karibu na reli, nyumba nzuri sana. Jamaa na mkewe wakahamia kwa furaha, lakini furaha yao iliisha walipokuja gudundua nyumba ile iko karibu mno na reli treni ikipita mpaka kitanda kinacheza.

Siku hiyo dalali akapita mke akamwita na kumwambia tatizo wakati treni inapita, wakaanza kubishana, yule mama akamwambia dalali kwa kuwa kuna treni itapita sasa hiviโ€ฆ njoo ndani uone mwenyewe.

Bahati mbaya wakiwa wamejilaza kitandani ili dalali aone adhabu wanayopata, Mzee mwenye mali alirudi ghafla, akauliza,

‘Nyie mnafanya nini hapa?’

Masikini dalali kwa woga mkubwa akajibu’ Tunangoja treni’

Baada ya kumkuta mwanamme mwingine chumbani kwake na mke wake cheki huyu anachokifanya

NAKUA(BABA) karudi kazini mwanae mdogo akamuwahi,
DOGO: Baba usiingie ndani kina jini chumbani kwenu
NAKUA: Hakuna kitu kama hicho
DOGO: Kweli baba kuna jini liko kwenye kabati lenu la nguoโ€ฆ.

NAKUA kaingia ndani kamkuta mkewe kalala kitandani kajifunika shuka gubigubi hadi kichwani. Kaenda kwenye kabati kufungua mlango , akamkuta rafiki yake wa miaka mingi yuko uchi ndani ya kabati
NAKUA: Aise unajua we fala sana, we rafiki yangu miaka yote hiyo halafu unamtisha mwanangu eti wewe jini, hebu toka huko nenda kwenu kacheze michezo hiyo na mwanao.

Cheka na methali

1.Simba mwendapole =Huyo ni Sharobaro
2.Asiyefunzwa na Mamae= Ujue Mama hajapitia Ualimu
3.Zimwi likujualo= Lilikuona Sehemu.
4.Chelewa Chelewa= Ukizikusanya utapata Ufagio.
5.Hakuna Masika= Wakati wa Kiangazi.
6.Mpanda Ngazi= Asiwe Mwoga kuanguka
7.Dua la kuku=
Bismilah rahman rahim
11.Penye wengi= Pana Ajali au Tukio
12.Ukiona vyaelea= Ujue ni vyepesi.
13.Mwenye nguvu= amekula ugal wa dona(โ€ฆ..)

Jamaa mpenda michepuko kapatikana

โ€ฆUpo kazini umeacha familia yako nyumbani mara ghafla unapigiwa simu kutazama unakutana na no ngeni na kuamua kuipokea ndipo unakutana na Sauti ya msichana ya kuvutia lakin kabla hajasema shida yake anaamua kukata simu. Unashikwa na hamu ya kujua ni nani. Tamaa ya mchepuko inakujia ghafla na kuamua kuipiga ile no tena kwa mara nyingine inakuwa haipatikani.

Siku hiyo hiyo usiku ukiwa umelala chumba kimoja na mkeo meseji inaingia tena kwenye cm yako kwa ile namba iliyokupigia mchana ikikuomba umpigie kwa mida ule na kusisitiza kuwa ana hamu ya kukufahamu. kila ukimtumia meseji ya kumdanganya upo sehemu mbaya hasikii anakubipu mara nyingi. Uzalendo unakushinda, unamuangalia pembeni mkeo kalala fofofo kajifunika shuka hadi usoni. Unaamua kuondoka kwa kunyata mpaka sebuleni kwenda kuipiga Ile namba kwa lengo la Kumwambia kesho mkutane. Ile unafika sebuleni na kuanza kuipiga ile cm ndipo unakutana na sauti hii:-ย MUME WANGU ACHA MCHEPUKO, NILIKUWA NAKUPIMA TU RUDI TU CHUMBANI TULALEย ๐Ÿ˜‹๐Ÿ˜‹๐Ÿ˜‹๐Ÿ˜‹๐Ÿ˜‹๐Ÿ˜‹๐Ÿ˜‹๐Ÿ˜‹ Hapo ndo utajua kwann bata hata ale kokoto anaharisha ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Angalia nilivyoingizwa mjini na ujanja wangu wote

Ndio nilikuwa nimeshuka kwenye basi la SAI BABA pale Ubungo, nina Begi kubwa Mgongoni na begi Dogo la Lap Top mkononi, sura inatazama Mbele Very Serious kama nipo kwenye Gwaride la Uhuru!..Mabega juu yanafanya Cheers na Mawingu!, natembea kwa madoidoโ€ฆ..leo nimetoka Likizo Moshi,

“Brother Simu ya ukweli hii..kitu cha Tecno C9 bei poa” hii ilikuwa sauti ya Teja mmoja hivi!

Yaani huyu Teja Bwege kweli,anataka kumuuzia nani sabuni? mimi sio wa kuja!โ€ฆkamwe Siwezi kuibiwa hapa Town,hakuna wizi au utapeli nisioujua!, Mimi nimezaliwa Mwananyamala kwa Manjunju, nikalelewa Tandale kwa Mtogole, Shule ya msingi nimesoma Turiani Magomeni, Hivi Mbwa gani aniibie?โ€ฆkwa Style ipi?

Sipendi kabisa Upuuzi!, Wajinga ndio wataibiwa, sio Mimi!โ€ฆsasa Kwa mwendo wa haraka nikatoka nje kabisa ya Stendi ya Ubungo straight mpaka Stendi ya dala dala za Kariakoo, hapo ndipo nikakutana na Vijana wawili wadogo wakiwa na mzani wa kupimia uzito,โ€ฆhakika napenda sana vijana wanaojituma kama hawa na sio ile Mijizi ya kule ndani Stendi!!,โ€ฆ.hapa sasa nikapata wazo!

“Dogo mnapima uzito kwa shilingi ngapi?”

“Mia mbili tu Kaka!”

”Ok”

Kwa mwendo wa kikakamavu nikapanda juu ya mzani,lengo hapa ni kujua uzito wangu, Mtori niliokula mwezi mzima kule kwa Mshekuu sio mchezo, hapa nahisi nacheza kwenye kg za John Cena,

“Mama wee! Dogo mzani mzima huu kweli? Mbona nina kilo 134?” (Nilihamaki)

“Aaah! Brother huoni umepanda na Mabegi juu ya mzani?”’

Hahaha! kweli nimechanganyikiwa!โ€ฆSasa nikatoa mabegi yote mawili na kurudi juu ya Mzani, hapa ndipo Uzito ukashuka kutoka kg 134 mpaka kg 56!โ€ฆMy God kweli Body la “One Pack ” haliongopi! thats means mabegi yaliniongezea kg 78! duh hii ni hatari!

“Yaani we Dogo kitambi chote hiki kg 56? huu Mzani Mzima kweli?”

Kimyaโ€ฆ

“Dogo huu Mzani vipi?”

Kimyaโ€ฆ

Dogo ana dharau huyu!โ€ฆSasa ndio nikabandua macho yangu toka kwenye kioo cha mzani ili nimtazame huyu dogo asiyejibu!โ€ฆ.ndipo macho yangu yakakutana na Kigoda tupu kilichochongwa Mvomero!โ€ฆDogo hakuwepo!โ€ฆ.na Mabegi pia hayapo!โ€ฆlap top haipo!โ€ฆ.NIMEPIGWA!

Ni dhahiri watoto wa Mjini walikuwa wameniacha juu ya Mzani, wamechukua Lap top ya Milioni na wameniachia Mzani chakavu wa elfu 40, what a stress!โ€ฆ.sasa nilirudisha macho kwenye kioo cha uzito na sasa kilisoma KG 38!โ€ฆyaani dakika hii hii nimepungua kilo zingine 18, Hakiyamama nahisi hata utumbo wangu wamebeba!โ€ฆniitieni Ambulance!

๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ

Shopping Cart
17
    17
    Your Cart
    ๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About