Visa Vya Kileo Tuu

Angalia huyu jamaa alivyoachika na msichana wake kwa kujidai kuongea kingereza na mwishowe kuchanganya maneno

MSICHANA: Mbona jana nimekupigia simu hujapokea?
JAMAA: please beby forget me.
MSichAnA: eeeh unaniambia hivo mimi?
JAMAA: nakuomba sana forget me.
MSICHANA: aya bwana poa maisha mema.

Msichana anakata simu jamaa ndo ananiuliza.”sasa
sijui amekasirikia lipi?” Mi nikamwambia we zuzu
umemwambia AKUSAHAU, dah, kumbe
ningemwambiaje? hahaha, ungemwambia
ForgivE me! au Ungesema Tu NaombA nSameHe.

Padri Akimbia wakati wa kuungamisha, chanzo ni hiki

Padri alikuwa amekaa katika confession booth kanisani
peke yake.
Mara kukaingia jamaa mmoja akapiga magoti upande wa
pili, akafanya ishara ya msalaba kisha akaanza kuungama
{confess}
“Padri nimekuja kuungama dhambi zangu, leo nimefanya
dhambi kubwa sana.”
Padri, “Endeleaโ€ฆ”

“Bosi wangu aliniita nyumbani kwake, akaniambia
amegundua nimeiba shilingi millioni 100 kazini. Akasema
nisipozitoa atanipeleka polisi, sa kwa ukweli mi naogopa
kufungwa.
Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu,nikatoa bastola nikamuuaโ€ฆ.. Yesu atanisamehe?”

Padri: “Utasamehewa.”
“Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango
unafunguliwa kutazama, Loh! Mke wa bosi, alipoona
kilichotokea akasema anapiga polisi simu.
Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu, nikamuua na yeye piaโ€ฆ Yesu atanisamehe hilo?”
Padri: “Utasamehewa.”

Nikatoka nje, nikawasha gari niondoke, lakini mlinzi
akakataa kunifungulia, ati amesikia mlio wa
bastola. Nikaona ataniletea kizuizi huyu.
Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu, nikamuuaโ€ฆ.. Yesu atanisamehe?”
Padri:”Utasamehewa.”

“Nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda
nyumbani, wakati napanga kuja kuungama mtoto wa bosi
akabisha hodi, nikawaza mambo gani tena, akasema alirudi
nyumbani na kukuta yaliyotokea akanionesha diary ya
babake, inayoonesha nilikuwa na appointment naye
wakati nilipomuua. Nikamuuliza nani mwingine anayejua?
Akasema ameanzia kwangu kisha anaenda polisi.

Nikatazama huku na huku nikakuta tuko wawili peke
yetu, nikamuuaโ€ฆ.. Yesu atanisamehe na hilo?”

Kimyaaโ€ฆ.
“Padri yesu atanisamehe?”
kimyaโ€ฆ.

Jamaa akatazama kwenye confession booth padri
hayupo, lakini kwenye kona moja akaona kabati la nguo
za mapadri linatikisika. Kufungua akaona padri kajificha ndani anatetemeka huku akitokwa na jasho.

Jamaa, “Sasa baba mbona umekimbia?”
Padri kwa taabu akajibu, “Nilitazama huku na huku
nikagundua tuko wawili peke yetuโ€ฆโ€ฆ.”

Jinsi ya Kubana matumizi X-mass

Badala yakupika PILAU tutapika TAMBI kwenye Xmas maana tutakua tumeokoa sh.15,000/= Vitunguu swaumu 2000, Vitunguu maji 1000, hiliki 1000, Magome 1000, Michele wa 2000, Soda 3000, Nyama 5000 . Fedha hizi zitatumika kununua mfuko wa cement ili tuanze kujaza kibubu cha ujenzi wa nyumba badala ya kupanga. Karibuni saana maji ya kunywa tumechemsha ndoo nzima.

๐ŸŽ€โœจMarry Xmas & Happy new year.โœจ๐ŸŽ€

Cheka na methali

1.Simba mwendapole =Huyo ni Sharobaro
2.Asiyefunzwa na Mamae= Ujue Mama hajapitia Ualimu
3.Zimwi likujualo= Lilikuona Sehemu.
4.Chelewa Chelewa= Ukizikusanya utapata Ufagio.
5.Hakuna Masika= Wakati wa Kiangazi.
6.Mpanda Ngazi= Asiwe Mwoga kuanguka
7.Dua la kuku=
Bismilah rahman rahim
11.Penye wengi= Pana Ajali au Tukio
12.Ukiona vyaelea= Ujue ni vyepesi.
13.Mwenye nguvu= amekula ugal wa dona(โ€ฆ..)

Mjini shule. Soma hii

Kuna mdada nilimkopesha pesa kwa ahadi kuwa baada ya wiki moja atanirejeshea pesa zangu.

Baada ya wiki moja nampigia simu hapokei simu zangu, nimempigia zaidi ya mara kumi (10) bila ya mafanikio!

Kila nikimpigia simu hajibu simu zangu, nikahamua kumwandikia message kwa WhatsAppโ€ฆ!

_Hello Mamu, Nakupigia simu sio kukudai pesa zangu, ila nataka kukwambia kuwa hapa Ubungo Plaza kuna wadada wawili walikuwa wanapigana kumgombea Mumeo (Baba Nang’oto). Ilikuwa vuta nikuvute na mumeo alikuwa kasimama tu anawaangalia akitabasamu. Baada ugomvi kwisha akaondoka na mmoja wao na kumwacha yule mwingine akitukana matusi kama ana akili nzuri._

โ€”
_*Kisha nikaituma ile message*_

Baada ya dakika kama mbili hivi, akanipigia simu nami wala sikupokea simu yakeโ€ฆ Akapiga tena na tena kama mara ishirini hivi wala sikupokea.

*Akatuma message akiniulizaโ€ฆ*

_Hao wanawake unawajuwa, โ€ฆmume wangu na huyo mwanamke wameelekea wapi, wewe unawajuwa hao wanawake waliopigana, yaani hapa nimechanganyikiwa kwa kweliโ€ฆ!_

Nikaisoma message yake wala sikuijibu, nikamchunia kimyaaaโ€ฆ!

Akanipigia tena simu mara tano, sikupokea simu zake, kimyaaaโ€ฆ! Akaniandikia message nyingineโ€ฆ.

*โ€ฆNakupigia jamani pokea simu basi nina pesa zako nataka nikupeโ€ฆ Naomba basi tukutane mjini unihadithie vizuriโ€ฆ!*

Nami nikamjibuโ€ฆ

_Nitumie hizo pesa kwenye Namba yangu ya Mpesa, ili nipitie sheli kujaza mafuta nije mjini kukupitia nikupeleke mahala walipoโ€ฆ!_

Baada ya dakika 2 message ikaingia, kuangalia balance yangu ya Mpesa, nikakuta kaingiza pesa zangu zote ninazo mdaiโ€ฆ!

Nikazima simu nikajilalia zangu kimyaaaโ€ฆ. Kama sio mie!

Kilichompata sista duu bishoo wakati akijidai kununua pete

Mwanamke mmoja aliingia duka la vito vya thamani, akaona pete moja ya dhahabu nzuri sana amabayo ilikuwa kwenye shelf ya chini, wakati anainama apate kuitazama vizuri kwa bahati mbaya (au nzuri!), shuzi likamtoka- druuuuuu, soni ikamuingia huku akigeuka haraka kuangalia kama kuna yeyote dukani pale ameliskia shuzi lake, macho yakagongana na mwenye duka ambaye alikuwa karibu huku uso ukiwa umejaa tabasamu zito, mwana mama hakuwa na uhakika kama amesikika au hakusikika, akaona atumie nafasi ile kuyeyushaโ€ฆAkauliza “Hii pete bei gani?” . Jamaa mwenye duka, huku akiangua kicheko, akajibu “Umeiona tu umejamba, je nikikuambia bei yake si utakunya kabisa?”

Kwa nini vitu vunavyoanza na “K” ni vitamu sana?

Zuzu kaniuliza, “Anko, unajua vitu vinavyoanzia na K ni vitamu sana.”
Nikashtuka, “Astaghafilulah we mtoto! Niondolee wehu wako hapa!”

Zuzu akatabasamu. Akaendelea kuongea kabla sijafanikiwa kumzuia. “Kweli kabisa anko. Vitu vinavyoanza na K ni vitamu sana kwa mfano kuku, kalimati, keki, kabab, katleti, kashata, kisheti na karoti.”
Nikashusha pumzi. “Ahaa! Kumbe ndo hivyo, ni kweli!”

Zuzu akanitupia swali. “Kwani we anko ulidhani nini?”

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About