Visa Vya Jumanne
Omba omba sio barabarani tuu
Boy:- baby ivi nikifa utakuja msibani?
Girl:-ntakuja ukinitumia nauli.
Hapo ndo unagundua kuwa sio kila omba omba yuko barabarani.
๐ค๐ค๐ค๐ค๐ค๐ค
Kilichotokea baada ya kuzamia sherehe
Pale unapozamia kwenye Dinner Party ya Jumuiya Fulani, sasa Lengo la Jumuiya hiyo ni kupata Fedha za kutunisha Mfuko wa Jumuiyaโฆsasa unakakaa mbele kabisa ili Muda wa Msosi usichelewe na kukuta kwenye Buffee yamebaki maharage!
MC : “Papai zuri kabisa kutoka Newala, Papai Mwendokasi, hili ni Shilingi laki 1..jamani Papai,nipeni ofa!”
MOSHA : “Laki 3 hapaaa!”
“Jamani laki 3 pale kwa Mosha, Papai linaondoka jamani, papai hili ni self contained kabisaโฆ.papai jamani”
KIBOLIBO: “Milioni 1 hapaaa”
“Jamani Mambo yanazidi kunoga hapa!โฆBenedict Kibolibo anataka papai kwa milioni 1 jamani, linaondoka papai!”
RWEYEMAMU : “nitanunua Papai hilo kwa Milioni 5”
Haya sasa jamani Rweyemamu ametoa ofa ya Milioni 5 Jamani, nani mweingineee?”
Kimyaaaโฆ
Haya jamani Papai kama hakuna Ofa basi Papai linakwenda kwa Rweyemamu!โฆโฆ..haya sasa Kuna Kuku hapa Jogoo kabisa, bei yake ni laki 6 jamani Jogoo twitter huyu!”
WEWE “Milioni Mojaaa!”( hapa umejiwahi wa kwanza na wewe uonekane upo huku ukijua kabisa Wakina Mosha na Rweyemamu lazima watampandia Dau Jogoo, tena dau kubwa”
MC: ee sasa Kumekucha Jamani, Kabasele anamtaka Jogoo kwa Milioni 1 jamani!โฆ.ofa nyingineeee!”
Kimyaaaโฆ
Jamani Jogoo anakwenda kwa Kabasele jamani!โฆofa nyinginee!
Kimyaaaโฆ.
Kimyaaaโฆ.
๐๐๐โฆhapa sasa ndio mfukoni kuna Buku jero,..huko kwengineko NMB nill balanceโฆsasa unageuza mimacho kumtazama Mosha kama atapanda dau kwa jogoo๐(mama wee Mosha anachezea Simu!)โฆ..unamtazama Rweyemamu (teh anatafuna Kuku)โฆ..mama weee๐
MC: Haya jamani kama hakuna Mwingine basi zoezi letu liishie hapa na limekwenda kwa Mafanikio, Mpatieni Kabasele Jogoo wake!
Hapa sasa unapokea jogoo wako wa MILIONI kwa Tabasamu la Maitiโฆ.kule nyumbani Jogoo wako Mkubwa unauza elfu 20 lakini sasa haka kajogoo kapya Mkononi kanakuwa kazito utadhani umembeba John Cena๐โฆMama weee hapa sasa vidari ulivyotafuna unaviona kama vimerudi kwenye Ulimiโฆ.Chicken wings zinataka kutokea Masikioniโฆ..Uuuuwiiiii,๐๐๐
Na hapa sasa kabla Dinner haijaisha ndipo unapojikuta Umebuni Cocktail ya Sparetta na Tomato๐๐๐๐๐.
chiel wie okee
Maisha ya kijijini hadi raha!!
Jamaa alimfumania mtu anazini na mkewe,
Akamtoza Faini ya sh 5000 tu,yule mtu akatoa 10000.
Jamaa akasema lala nae tena sina chenji!๐๐๐๐๐๐๐
Cha kufanya msichana akikukimbia halafu atake kukurudia
โฆโฆโฆ Kama msichana atakutupa kwa sababu huna pesa, na baadaye unapopata pesa akarudi tena kuomba msamahaโฆ Ndugu yanguโฆ.. Msameheโฆ. Mpe ahadi ya ndoa, mwambie utamuoaโฆ. iambie familia yake unataka kufanya ukarabati wa nyumba yaoโฆโฆ Ondoa paa lote la nyumba yao halafu TOWEKAโฆ..
๐โฆโฆโฆ ๐โฆโฆ.. ๐
Kweli mitandao imeharibu watu, angalia huyu anachokisema sasa
๐๐ kweli nimeamin mitandao inahribu watu
Leo kuna jamaa kamuona Dada akipita barabaran kapendeza jamaa kamwendea Dada akamwambia!
Dada nice photoย ๐๐๐๐
Angalia sababu ya mke Mtarajiwa kuzimia kabla ya harusi
*Jihadharini* na wachapaji wa kadi za harusi. Hakikisha unasoma maandishi yaliyochapwa kabla ya kadi kuchapwa na kusambazwa!
Mchapaji aliombwa aweke 1 Yohana 4:18 katika kadi ya harusi lakini mchapaji kwa makosa aliweka Yohana 4:18.
1 Yohana 4:18 panasema, “Katika pendo hakuna hofu, lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofuโฆ”
Lakini Yohana 4:18 tunasoma, “Kwa maana umekuwa na waume watano, naye uliye naye sasa siye mume wako.”
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐_MKE MTARAJIWA AKAZIMIA HAPA, TUNAMPEPEA_
KICHEKESHO: Ajira ngumu!! Cheki hawa walivyoamua kujiajiri
Jamaa mmoja alienda kuomba kazi Mbuga ya Wanyama, akaambiwa nafasi ya Kazi ipo ila hakuna Sokwe, “hivyo utajifanya Sokwe na tutakupa ngozi utavaa”
Jamaa siku ya kwanza akavaa, walipokuja watalii mambo yalienda vizuri, Siku iliyofuata Banda lake liliwekwa juu ya Banda la Simba, Jamaa ktk kuongeza mbwembwe akawa anarukaruka, kwa bahati mbaya si akaangukia ndani ya Banda la Simba, akawa anapiga kelele “Mama nakufaaa!”
Mara yule Simba akamwambia “Acha Ufala ww kelele za nini sasa, mimi mwenyewe Binadamu! rudi kwenye Banda lako kabla watalii hawajaja watatushtukia! chezea ajira ww”โฆโฆโฆ!!
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐ป๐๐ป๐๐ป๐๐ป
Njia nne za kufikisha Habari kwa haraka
Kuishi kijijini kunahitaji moyo sana
..unaenda kuoga, unakumbuka kuwa umesahau sabuniโฆunaenda kuchukua sabuni kurudi bafuni, unakuta ng’ombe amekunywa maji yote..unaamua kufuata mengne,unarudi unakuta mbuzi kala sabuniโฆ๐๐๐๐
Angalia hawa vichaa walichokifanya, Vichaa bwana, ni noma!
Vichaa walipanga kutoroka, wakakubaliana wamnyonge mlinzi watoroke!
Walipofika getini wakakuta geti lipo wazi na hakuna mlinzi, wakasema “Turudi mipango yote imevurugikaโฆ
Utani kwa wadada wembamba
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Wadada wembamba hebu nenepeni basi mnatupa tabu kusoma maneno ya kwenye kanga jamanii โฆโฆโฆmnaviringisha kanga mwili mara 3 mpaka maandishii hayaonekanii
๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ
Recent Comments