Vihoja Vya Kuwaadisia

Angalia huyu jamaa anavyojiona msomi, huyu kamuotea, hapa amekwama

USIJIONE MJUAJI SAAAA…NA.
Jamaa kamaliza chuo anarudi nyumbani kwa wazee, kufika
nyumbani.

kwa furaha waliopata wazazi, mama aliamua
kurosti kuku WAWILI(2) kwa ajili yao.
Mezani jamaa akataka kuwadhihirishia kuwa yeye ni msomi,
akawaambia “hawa kuku unaona wako wawili ila kwa kutumia
sheria za arthematic na geometric kuna kuku watatu mezani”
mama”hee embu tuoneshe mwanangu”
jamaa akachukua kuku ya kwanza akainua juu “ngapi?”
wazazi”moja” akainua wa pili “ngapi?” wazazi “mbili”
akawarudisha akisema”wazee wangu nadhani japo shule
hamkwenda ila mnajua moja+mbili=tatu so tuna kuku watatu
mezani”
baba”mmh kweli mwanangu umesoma. SASA TUFANYE IVI
MIMI NACHUKUA KUKU MOJA NA MAMA YAKO WA PILI WE
UTAKULA UYO WA TATU ULIYOSEMA”

Cheka kidogo, angalia anachosema huyu mchaga

Mchaga baada ya kufa akaulizwa na malaika anayetoa roho: Mangi hapa ni njiapanda kulia ni Mbinguni na kushoto ni Jehanamu, Je unachagua kwenda wapi?

MANGI: Bwashee, mi nabaki hapa hapa njiapanda aisee.
MALAIKA: Kwa nini?
MANGI: Aisee, nikifungua duka hapa si nitapata wateja wa Mbinguni na Jehanam. Yani patakuwa senta ya hatari, supu na nyama choma muda wote. Hata we utafaidi, unavyoenda kuchukua roho unaniletea stock nakupa hela yako cash mkononi. Na kila ukipita hapa unapiga mchemsho wako wa ulimi na bia mbili chap kabla ya kuingia mbinguni.
Kwanza nashangaa Shirima alipitaje hapa bila kushika ploti, au alikufa amelewa sana?

Unakumbuka haya enzi za shule?

Kama umesoma st Kayumba utakuwa una aidia na haya…

1.Unaenda shule umechelewa unakuta mwalim anakamata wachelewaj unaamua urudi nyumbani
2.unachukua kimbegu cha ubuyu unasugua sakafuni af unamuunguza mwenzio
3.mkiruhusiwa tu unakimbia unataka uwe wa kwanza kwenye njia yenu y kurudia nyumban
4.MTU akikukera unamfungia shule (mnapigana baada ya kufunga shule)
5.MTU akikunyima kitu chake unamwambia “Ahaa eeh utaona sa nne”
6.wadada wembamba ndo wanaongoza kwa kusuta wenzao
7.ukiibiwa daftar jipya unalia kuliko hata uliloandika
8.unajaza mapeni kwenye mkebe(compass) na mengine hayaandiki
9.vifaa vingine kwenye mkebe hujawahi hata kuvitumia mfano bikari labda utolee mwiba😂
10.hakuna habari nzur kama kuambiwa Leo hamna shule mwalim haupo
11.habari mbaya zaidi n kurud nyumban kutoka shule una njaa af unaambiwa chakula mgeni kaja tumempa
12.mtoto wa mwalim utamgundua tu kwanzia sweta begi na viatu vyake
13.usiombee umpige mtoto wa mwalim utataman uache shule
14.unatengeneza kifutio cha ndala af unatishia eti kinafuta hadi peni😂
15.ukaguzi na huna ufagio.. unaomba chelewa kwa watu af unaongeza kijiti katikati
16.siku ukienda na ufagio wanakagua maji, ukienda na naji wanakagua kuni au mbolea😆
😂
Dah shule zetu hizi kiboko!!

Ipi umeipitia wewe
Share na wengine

Kweli shilingi yaua, Huyu jamaa kapatikana, angalia anachomjibu mke wake,

Jamaa alikuwa anagombana na mkewe,hatimae
akamwambia kwa ukali
“Unajua nimechoka sasa, haya kusanya nguo
zako na……..

Kabla hajamalizia sentensi simu
ya mkewe ikaita, kumbe alikuwa ni baba yake.
Basi mzee akaanza kuongea na binti yake huku
jamaa anasikia

“Aisee mwanangu nimebahatika kuuza ile
nyumba yangu sasa nimeona niwatumie milioni
20 mjaribu kuanzisha mradi na mwenzio.
Haya mwambie yeye nitampigia kesho kama
ana mradi mwingine nimpe hela kidogo”.Baada
ya simu kukatwa mke akamgeukia jamaa
akamuuliza,”eeenhee!!! ulikuwa unasema
umenichoka nikusanye nguo zangu halafu
iweje? Jamaa kwa upole akajibu “Nilikuwa
nasema ukusanye nguo zako na unipe nifue”.

Misemo 17 ya kuchekesha

1) gari la kuvutwa halina overtake
2) kisigino hakikakai mbele
3) wimbo wa taifa haupgwi disko
4) feni haiwashwi beach
5) mshkaki hauchomwi kwa jiko la ges
6) mganga haagiz tembele
7) hata bibi alikuwa bint
8) mke wa mtu sumu,mume wamtu maziwa
9) kipara bila pesa ni kovu
10) mbwa hanenepi migiuu
11) picha ya rais haina bodyguard
12) mjini shule kijiji tuition
13) saa ya ukutani haivaliwi mkonon
14) heshima pesa shkamoo makelele
15) ulinz pesa bastora mzgo
16) kuku ni kuku jogoo mbwembwe
17) kusoma kuelewa kukesha mbwembwe

Angalia sababu ya mke Mtarajiwa kuzimia kabla ya harusi

*Jihadharini* na wachapaji wa kadi za harusi. Hakikisha unasoma maandishi yaliyochapwa kabla ya kadi kuchapwa na kusambazwa!

Mchapaji aliombwa aweke 1 Yohana 4:18 katika kadi ya harusi lakini mchapaji kwa makosa aliweka Yohana 4:18.

1 Yohana 4:18 panasema, “Katika pendo hakuna hofu, lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu…”

Lakini Yohana 4:18 tunasoma, “Kwa maana umekuwa na waume watano, naye uliye naye sasa siye mume wako.”

🏃🏃🏃🏃🏃🏃🏃😂😂😂😂_MKE MTARAJIWA AKAZIMIA HAPA, TUNAMPEPEA_

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About