Angalia alichokifanya huyu sharobaro kanisani
Huu usharobaro mwingine uchizi. Jamaa kamzimia demu kanisani,
mara ukafika mda wa kutoa sadaka, eti jamaa akamwambia ”dont worry bby” ntakulipia!!
Huu usharobaro mwingine uchizi. Jamaa kamzimia demu kanisani,
mara ukafika mda wa kutoa sadaka, eti jamaa akamwambia ”dont worry bby” ntakulipia!!
Jambazi mmoja aliingia kanisani na bunduki akapiga risasi juu ya bati akasema “asiyempenda YESU atoke nje” wakatoka wote ispokuwa Mchungaji na Wazee wawili.
Jambazi likamwambia Mchungaji “unaweza kuendelea na ibada, nilikuwa nakuondolea wanafiki”, Mchungaji akasema “ungewaacha kwanza nichukue sadakaβ¦!
Jamaa kaenda kanisani akakaa karibu na mrembo.
Wakati mahubiri yakiendlea jamaa akaanza kuingiza vocal:
Jamaa: dada mi nakupenda saana
Dem: Kaka naomba umsikilize mchungaji
Jamaa: nipe nafasi uwe msimamizi wa serikali ya moyo wanguβ¦
Dem: niacheβ¦
Jamaa: kweli nakupenda mpnz
Dem: (kwa sauti kubwa) nmesema NIACHEEEE!!
Watu wote kanisani wakageuka⦠Jamaa kaona noma na ili atulize msala
Jamaa: sikuachi hadi ukiri YESU kuwa Bwana na mwokozi wa Maisha yako.
Padri alikuwa amekaa katika confession booth kanisani
peke yake.
Mara kukaingia jamaa mmoja akapiga magoti upande wa
pili, akafanya ishara ya msalaba kisha akaanza kuungama
{confess}
“Padri nimekuja kuungama dhambi zangu, leo nimefanya
dhambi kubwa sana.”
Padri, “Endelea⦔
“Bosi wangu aliniita nyumbani kwake, akaniambia
amegundua nimeiba shilingi millioni 100 kazini. Akasema
nisipozitoa atanipeleka polisi, sa kwa ukweli mi naogopa
kufungwa.
Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu,nikatoa bastola nikamuuaβ¦.. Yesu atanisamehe?”
Padri: “Utasamehewa.”
“Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango
unafunguliwa kutazama, Loh! Mke wa bosi, alipoona
kilichotokea akasema anapiga polisi simu.
Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu, nikamuua na yeye piaβ¦ Yesu atanisamehe hilo?”
Padri: “Utasamehewa.”
Nikatoka nje, nikawasha gari niondoke, lakini mlinzi
akakataa kunifungulia, ati amesikia mlio wa
bastola. Nikaona ataniletea kizuizi huyu.
Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu, nikamuuaβ¦.. Yesu atanisamehe?”
Padri:”Utasamehewa.”
“Nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda
nyumbani, wakati napanga kuja kuungama mtoto wa bosi
akabisha hodi, nikawaza mambo gani tena, akasema alirudi
nyumbani na kukuta yaliyotokea akanionesha diary ya
babake, inayoonesha nilikuwa na appointment naye
wakati nilipomuua. Nikamuuliza nani mwingine anayejua?
Akasema ameanzia kwangu kisha anaenda polisi.
Nikatazama huku na huku nikakuta tuko wawili peke
yetu, nikamuuaβ¦.. Yesu atanisamehe na hilo?”
Kimyaaβ¦.
“Padri yesu atanisamehe?”
kimyaβ¦.
Jamaa akatazama kwenye confession booth padri
hayupo, lakini kwenye kona moja akaona kabati la nguo
za mapadri linatikisika. Kufungua akaona padri kajificha ndani anatetemeka huku akitokwa na jasho.
Jamaa, “Sasa baba mbona umekimbia?”
Padri kwa taabu akajibu, “Nilitazama huku na huku
nikagundua tuko wawili peke yetuβ¦β¦.”
Recent Comments