Vichekesho Vya Asubuhi Hii

Mzunguko wa elimu kiafrikaafrika

01.๐Ÿ‘‰ Wale wanafunzi walioongoza Mashuleni, wanaenda kwenye Engineering na Medical school.

02.๐Ÿ‘‰ Wale waliokuwa wa pili, wanachukua MBA na LLB na kuja kuwa Mameneja wa wanafunzi walioshika nafasi ya kwanza.
03.๐Ÿ‘‰ Wale waliokuwa wa tatu, wanageukia Siasa na kuwaongoza wote hapo juu. Yaani wa kwanza na wa pili.
04.๐Ÿ‘‰ Wale waliofeli, wanaenda Jeshi, hawa wakigoma, basi hao wa juu wote hawana raha.
05.๐Ÿ‘‰ Wale waliopata Zero na waliokataa shule wanakuwa waganga wa kienyeji, wote hapo juu watamtafuta huyu, pale mambo yao yanapokwenda kombo. Tuache kudharauliana, kila mtu ni boss akiwa kwenye nafasi yake. ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‰๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿƒ๐Ÿƒ๐Ÿ˜œ๐Ÿ˜œ๐Ÿ˜œ๐Ÿ˜œ๐Ÿ˜œ

Ungekua wewe ni mwalimu ungemshauri nini huyu mwanafunzi?

Mwalimu aliingia darasani na kuwauliza wanafunzi juu ya ndoto zao za baadae.

MWAL: John we unataka ukiwa mkubwa uwe nani?

JOHN: Nataka niwe daktari wa moyo niwasaidie watanzania wanaougua magonjwa ya moyo.

MWAL: vizuri. Na wewe Rose unataka kuwa nani?

ROSE: Nataka kuwa rubani, niweze kusaidia watu wanapenda kusafiri kw anga.

MWAL: Safi sana Rose. Utakua utakua mfano kwa wasichana wenzio kuwa na bidii kwenye masomo ya sayansi.

MWAL: Na wewe James??

JAMES: mimi nataka kuwa tajiri mkubwa sana. Niwe na nyumba Tanzania, S.Africa, Marekani na Dubai. Niwe na gari 7 za kutembelea. Kila siku nabadilisha. Leo nikipanda hii, siirudii hadi week iishe. Nataka niwe namiliki viwanda, Makampuni, ndege binafsi na mashamba makubwa. Nataka niwe na nguvu serikalini ya kuamua nani awe Rais na nani asiweโ€ฆโ€ฆ”

Akameza mate kisha akaendeleaโ€ฆ.

“Nataka kuwa na walinzi 20 wenye silaha nzito wakinizunguka, na watumishi wakininyenyekea. Nataka kuwa bilionea ninayeogopwa. Lakini pia nataka kuwa na mke mzuuuri sana ambaye nitakuwa natembea nae kila mahali.”

MWAL: ndoto nzuri sn lakini unahitaji bidii sana kutimiza. Haya na wewe Jenny tueleze unataka kuwa nani??

JENNY: Nataka kuwa mke wa James.!!

Ziara za kushtukiza zinachekesha sana

Mimi Nimecheka sana
๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

ZIARA ZA KUSHTUKIZA๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€
Mimi ni msomaji mzuri wa magazeti, na msikilizaji mzuri wa redio, huwa naangalia luninga mara chache sana kama nikibahatika kupita mahala kuna luninga. Sasa wiki hii nimesikia mengi kuhusu hizi ziara za kushtukiza za viongozi wetu, nikaona hili ni jambo zuri tena linafaa kuigwa na sisi wananchi wapenda maendeleo. Nikaona nijipange na mimi nifanye ziara kadhaa za kushtukiza katika sehemu mbalimbali zinazonihusu.

Nikaona nianze na ziara ya kushtukiza pale shuleni kwa huyu mwanangu, maana kila siku anakunywa chai na kuondoka na daftari zake na mie sijawahi kwenda shuleni kwao toka nilipomuandikisha shule mwezi Januari. Nilifika shuleni na kumuona mwalimu mkuu, ambae alianza kutetemeka nilipomuambia kuwa nimekuja pale kwa ziara ya kustukiza, sijui alidhani mi ni mmoja wa Mawaziri wapya, maana nilimuona jasho linamtiririka ghafla. Akanikaribisha ofisi yake iliyokuwa na vitabu kila kona, na kuita waalimu wote na kunitambulisha kuwa ni kiongozi nimekuja kwenye ziara ya kustukiza.

Nilipojitambulisha kuwa ni mzazi, waalimu wote nikawaona waanza kupumua kwa raha. Nikawaambia kuwa mimi nina mwanafunzi pale na nilikuja ziara ya kustukiza kujua maendeleo yake. Baada ya mwalimu mkuu kusaka jina la mwanangu nae akanambia, โ€œMzee huyu mtoto hajaja shule mwezi wa tatu sasa, tulijaribu kukutafuta ikashindikana, hatujui yu wapiโ€ Jasho likaanza kunitoka mimi, yule mtoto kila asubuhi nampa nauli anaenda shule, na mara nyingi ananiomba michango kumbe hata shule haji. Niliondoka bila kuaga presha ikiwa juu.

Nikaona niende kwenye genge la mke wangu nae nikamfanyie ziara ya ghafla nimhadithie mambo ya mwanae, nilipofika pale nikakuta kuna mdada mwingine anauza genge. Nikamsalimu, na kumuuliza mwenye genge ntampataje, jibu lake lingeniua kama ningekuwa si mkakamavu, โ€œMume wake kaja kumchukua na gari wameenda kununua shamba Bagamoyoโ€. Nikaondoka nimechanganyikiwa, nikajuwa hapa dawa yangu moja tu, nayo ni Sabrina, mtoto wa Kinyaturu pale ambapo nikipata maudhi huwa naenda kubembelezwa.

Nikatwanga mguu kwa Sabrina nae nikamfanyie ziara ya ghafla ili anipoze moyo. Nilipogonga mlango wa chumba chake akatoka mbaba wa miraba minne, akanisalimia kwa upole, โ€œSalama kaka unasemaje?โ€ Jibu likanitoka โ€œSamahani mie nilimkopesha huyu dada wa chumba hiki vitenge, nilikuja kuuliza kama ameshapata hela yanguโ€ Ziara za kushtukiza zinataka moyo wa chuma jamani

Sababu ya mwanaume kunya kitandani alipokuwa kalala na mke wake

Jamaa flani alikuwa amelala na mkewe. Mara akamuona mtu amesimama kitandani.

Jamaa akafoka, “Toka hapa, we ni nani mpaka unakuja kitandani mwangu?”

Yule mtu akajibu, “Mi ni malaika na hapa sio kitandani mwako uko mbinguni!”

Jamaa, “Huh! Inamaana nimekufa,mbona mi bado kijanaโ€ฆ naomba nirudishwe!”

Malaika, “Inawezekana lakini siwezi kukurudisha kama mtu labda urudi kama mbwa ama kuku.”

Jamaa akakumbuka mbwa wanavyopata taabu ya kulinda, akaonelea arudi kama kuku.

Malaika akamgeuza kuku, akamwambia ajifunze kutaga kabla hajapelekwa duniani.

Akachuchumaa na kuanza kujikamua; yai la kwanza likatoka. akajikamua tena, yai la pili likatoka. Akajikamua tena mara ya tatu.

Wakati yai la tatu linatokaโ€ฆ akashtukia amepigwa konde ikifuatwa na sauti ya hasira ya mkewe, “Pumbav*! Balaa gani hiiโ€ฆ. unakuny* kitandani!!”

Sababu za kumuacha mke kama umemchoka

Ukimchoka mkeo, waweza kumtaftia sababu za kumuacha kama hizi

_
1. Missed calls 16? Umeua betri la simu yangu. Kwa hiyo hata mimi unaweza kuniuaโ€ฆ It’s Over!!!
_
2. Hata hunieshimu. Mi naongea na wewe lakini we upo bize unavuta pumzi? It’s over!
_
3. Nimekupigia umepokea simu hapohapo. Huna subira. Itโ€™s over!!
_

4. Nilikwambia huwa napenda chakula cha moto lakini hujanipashia ice cream. Hunijali. It’s over!
_
5. Nimekupa mayai mawili, moja uchemshe jingine ukaange. We umekaanga ambalo ulitakiwa kuchemsha na umechemsha ulilotakiwa kukaanga. Huniheshimu, Itโ€™s over!
_
6. Nimekuita DARLING na wewe ukaniita HONEY. Yani kwa maana nyingine unamuita mama yangu NYUKI. Huheshimu wazazi wangu, fungasha kilicho chako. its over.

๐Ÿ˜„๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜„๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜„๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜„๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜„

KICHEKESHO: Ajira ngumu!! Cheki hawa walivyoamua kujiajiri

Jamaa mmoja alienda kuomba kazi Mbuga ya Wanyama, akaambiwa nafasi ya Kazi ipo ila hakuna Sokwe, “hivyo utajifanya Sokwe na tutakupa ngozi utavaa”

Jamaa siku ya kwanza akavaa, walipokuja watalii mambo yalienda vizuri, Siku iliyofuata Banda lake liliwekwa juu ya Banda la Simba, Jamaa ktk kuongeza mbwembwe akawa anarukaruka, kwa bahati mbaya si akaangukia ndani ya Banda la Simba, akawa anapiga kelele “Mama nakufaaa!”

Mara yule Simba akamwambia “Acha Ufala ww kelele za nini sasa, mimi mwenyewe Binadamu! rudi kwenye Banda lako kabla watalii hawajaja watatushtukia! chezea ajira ww”โ€ฆโ€ฆโ€ฆ!!

๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ‘†๐Ÿป๐Ÿ‘†๐Ÿป๐Ÿ‘†๐Ÿป๐Ÿ‘†๐Ÿป

Wachaga wana mambo mbele ya hela, angalia hii bili ilivyomchanganya MASSAWE

MASSAWE alienda na marafiki zake bar kunywa, baada ya kumaliza kutumia akaletewa bili kama ifuatavyo:
Manka 35,000
Marieta 20,000
Kekuu 30,000

Kitime 15,000
Kinabo 10,000
TOTAL 110,000/=
MASSAWE akaicheki akasema “Wote nitawalipia lakini huyo “TOTAL” Yesuu simlipii.
Kwansa anamiliki sheli kibao sa mafuta hapa bongo. Shensi taip ! Na amekunywa nyingi kuliko wote alipe mwenyeweโ€ฆ

Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    ๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About